Menu

Zingatia Uumbaji Wa Mungu–Fikiria Ukuu Wake

Wakristo katika karne ya 21 wanafikiria kidogo kuhusu Uumbaji wa Mungu; halikadhalika tunafikiri kidogo kuhusu Mungu. Tunajipenda sana – ratiba zetu, kazi zetu, tekinolojia yetu, shughuli za mitaala yetu nk., kiasi kwamba tunashindwa kuona nyota, na kunusa harufu nzuri ya maua. Leo, pengine zaidi ya muda mwingi katika historia, binadamu anakosa vitu vyepesi katika maisha ambavyo vinaweza kutusababisha kuendelea kuwaza juu ya ukuu wa Muumba. Naam, hakuna kilicho muhimu sana Wakristo kukiwazia kuliko neno la Mungu (Zaburi 1: 2), lakini pamoja na mafunuo maalum ya Mungu (neno lake), tunapaswa kutafakari sana jinsi ufunuo wa Mungu wa kushangaza wa mazingira – asili ya Mungu, unavyothibitisha nguvu yake isiyo kiasi, akili na kutujali.

Kwa mara nyingine tena, maandiko matakatifu yanaonyesha uumbaji wa Mungu kama kithibitisho cha ukuu wake. Tangu nyakati za Ayubu, Nuhu na kurudi nyuma mpaka Adamu, binadamu amejifunza  vitu vya ajabu kuhusu Mungu kwa kuzingatia uumbaji wake wa kushangaza. Mtume Paulo aliandika “Kwa sababu mambo yake yasiyoonekana tangu kuumbwa ulimwengu yanaonekana na kufahamika kwa kazi zake, yaani uweza wake wa milele na uungu wake; hata wasiwe na udhuru” (Warumi 1: 20).

Pengine hakuna kitabu kingine cha Biblia kinachomuongoza mtu katika kuuwaza ukuu wa Mungu kwa ndani kuliko kitabu cha Zaburi. Lakini cha kufurahisha mara kadhaa, kitabu hiki hiki chenye uvuvio, kinageuza fikra za mtu kuelekeza kwenye uumbaji wa Mungu. Katika Zaburi ya 8, kwa mfano, Mtunga Zaburi anasifia jina bora la Mungu ameweka “utukufu wake juu ya mbingu” Aliyeumba mwezi, nyota, binadamu na hata “wanyama wa mwituni, ndege wa angani, na samaki wa baharini, na kila kipitacho njia za baharini” Mtunga zaburi alihitimishaje? “Wewe Mungu, Bwana wetu, jinsi lilivyo tukufu jina lako, duniani mwote” (Zaburi 8: 9). Na katika Zaburi 19: 1, tunakumbushwa kwamba “Mbigu zahubiri utukufu wa Mungu, na anga laitangaza kazi za mikono yake”. Na pia katika Zaburi ya 33, tunajifunza kuhusu moja ya sababu ambazo binadamu anapaswa kuwa na hofu na kuishi katika kumcha Bwana; (Zaburi 33: 8) – kwa sababu “Kwa neno la bwana mbingu zilifanyika na jeshi lake lote kwa pumzi ya kinywa chake … Maana yeye alisema ikawa; naye aliamuru ikasimama” (Zaburi 33: 6, 9).

Zingatia kilele cha kitabu cha Ayubu, Mungu alipoongea na mababu toka kwenye upepo wa kisulisuli. Badala ya kumwambia Ayubu sababu hasa, kwa madira yake, Mungu aliongea naye kuhusu uumbaji wake. Ukianzia na Ayubu 38: 39 na kuendelea mpaka 39, 40 na 41, Mungu aliongea na Ayubu kuhusu wanyama kadhaa tofauti tofauti, ikiwa ni pamoja na Simba, Mwewe, kiboko. Kati ya vitu vyote ambavyo Mungu angemwambia Ayubu, alitumia mistari 77, akiongea juu ya uumbaji wake wa wanyama. Alichagua kumfundisha Ayubu, kuhusu nguvu zake zisizo na kikomo, kujua vyote na ukuu wake kwa kuelezea baadhi ya uumbaji wake waajabu wa wanyama.

Nabii Isaya aliwahi kuandika juu ya kuruhusiwa kwake kuona maono ya  kiti cha enzi cha Mungu. Mbele ya Mungu kulikuwa na viumbe wa ki-Malaika wakaitana kila mmoja kwa mwenzake, Mtakatifu, Mtakatifu, mtakatifu ni Bwana wa majeshi (Isaya 6: 3). Ni nini msingi wa sifa hizi? Ni sababu ipi moja inayopaswa kutusukuma kumwabudu Mungu? Isaya alifunua moja ya misingi ya sifa za Mungu, katika mstari unaofuata “Dunia yote imejaa utukufu wake (Isaya 6: 3b).

Naam, uzuri, fahari na ubunifu wa uumbaji wa Mungu unapaswa kutusukuma karibu na Muumba. Alama zake za vidole zinapasa kutuweka katika hofu yake. Vitusukume kwenye kupiga magoti katika kumwabudu. Na vituhamasishe kuwaambia wengine habari zake. Kama Mtunga Zaburi alivyoimba, tunapaswa “kuwahubiri mataifa habari za utukufu wake, na watu wote habari za maajabu yake, kwa kuwa Bwana ni mkuu, mwenye kusifiwa sana” (Zaburi 96: 3, 4).


Published

A copied sheet of paper

REPRODUCTION & DISCLAIMERS: We are happy to grant permission for this article to be reproduced in part or in its entirety, as long as our stipulations are observed.

Reproduction Stipulations→