Yesu Kristo – Mtu wa Historia au Muhusika wa Hadithi za Kufikirika?
Watoto na watu wazima wengi wanajua jina Yesu Kristo kwa urahisi. Wengi hata wanaweza kuelezea hadithi ya maisha Yake. Hata hivyo, watu hao hao pia wanajua majina ya Peter Pan, Snow White, na Cinderella. Na wanaweza kuelezea “ukweli” wa hadithi hizi za kufikirika vilevile. Je, Yesu wa Nazareti ni muhusika wa kufikirika ambaye anastahili kujumuishwa katika orodha ya wachawi wa kushangaza, Wanadamu walio na ujasiri, na mashujaa wanaoruka? Au jina Lake linapaswa kuchukua nafasi yake inayostahili katika wigo wa historia ya ukweli?
Baadhi ya watu wanasema kwamba Yesu ni mithili ya hadithi ambayo haikuwahi kutokea hapa Duniani. Pamoja na yote hayo, ni ukweli kwamba hatuna hata kitabu kimoja au barua iliyoandikwa na Yesu Mwenyewe. Na, bila shaka, hakuna mtu yeyote ambaye amewahi kutoa ushahidi wa kimwili (kama vile mwili Wake) kuthibitisha uwepo Wake. Ushahidi gani unapatikana kuthibitisha kwamba Yesu alikuwepo kweli kwenye Dunia hii?
USHUHUDA WA MAADUI
Inafurahisha kwamba, aina ya kwanza ya kumbukumbu, zinatokana na kile kinachojulikana kama vyanzo “vya uhasama”. Vyanzo vya uhasama vilikuwa vimeandikwa na watu ambao hawakumpenda Yesu na wafuasi Wake. Watu hao hakika hawakutaka kuendeleza imani ya Kristo au kuongeza ukweli wa uwepo Wake. Kwa kweli, walikataa mafundisho Yake na mara nyingi waliwalaani Yesu na wafuasi Wake. Kwa hiyo, wakati vyanzo hivi vinapozungumzia Yesu, hakuna mtu anayeweza kuwashutumu kwa kuficha mambo kwa kumpendelea Yesu.
Mtu anayeitwa Tacitus atakuwa shahidi wa kwanza wa uhasama kuitwa kutoa ushahidi. Alizaliwa karibu na mwaka wa A.D. 56 na alikufa karibu na mwaka wa A.D. 117. Alikuwa Mrumi wa daraja la juu mwenye elimu nzuri ambaye alishikilia nafasi za juu za kiserikali chini ya watawala kadhaa wa Kirumi anajulikana zaidi kwa kuandika Taarifa za – kihistoria za Kirumi zilizoandikwa karibu na mwaka wa A.D. 115. Katika Taarifa hizo alieleza kuhusu Moto Mkubwa wa huko Rumi, uliotokea mwaka wa A.D. 64. Nero, Mtawala wa Kirumi, aitembelewa na watu wengi kwa kuwaamuru waukaribie mji. Tacitus aliandika:
“Nero alitengeneza vibwengo, na akawaadhibu kwa njia zote wakristo waovu waliojulikana (kama walivyojulikana). Mwanzilishi wao, Kristo, alikuwa amesulubiwa wakati wa utawala wa Tiberio na gavana wa Yudea, Ponsio Pilato. Lakini licha ya kurudi nyuma kwa muda, imani hii mbaya ilizuka tena, sio tu huko Yudea (ambapo uharibifu ulianza) bali hata huko Rumi.”
Tacitus aliwachukia Wakristo na jina la Kristo. Kwa hiyo, hakuwa na chochote kizuri cha kusema kuhusu kile alichokiita “imani za Kishirikina”. Hata hivyo, alikuwa na kitu cha kusema kuhusu hilo. Ushahidi wake unathibitisha pasipo na mashaka yoyote kwamba, dini ya Kikristo ilikuwa muhimu kihistoria na kwamba mwanzilishi wake alikuwa mtu anayejulikana kihistoria ambaye alivutia hata umakini wa Mtawala wa Kirumi mwenyewe!
Ushahidi mwingine wa uhasama unatoka kwa Suetonius, aliyeandika karibu na mwaka wa A.D. 120. Maandishi ya Suetonius ni ushahidi wa kihistoria unaoaminika. Mara mbili katika kitabu chake cha historia, Suetonius alimtaja Kristo au wafuasi Wake. Aliandika, kwa mfano: “Kwa sababu huko Rumi Wayahudi walileta machafuko ya mara kwa mara kwa uchochezi wa Kristus au Claudius aliwafukuza kutoka mji huo” (kumbuka kwamba katika Matendo 18:2 Luka alitaja kufukuzwa huku na Claudius). Kristus pengine ni makosa ya tahajia ya neno Kristos, neno la Kigiriki kwa Masihi. Suetonius aliendelea kueleza: “Adhabu pia zilitolewa kwa Wakristo, kikundi kinachokiri imani mpya na yenye madhara.” Tena, ni wazi kwamba Suetonius na serikali ya Rumi walikuwa na chuki kwa Kristo na kundi lake la “waasi wenye madhara”. Ni wazi pia kwamba Suetonius (na,kwa kweli, Rumi yote) walimtambua Kristo kama Mwanzilishi mashuhuri wa dini ya kihistoria.
Mrumi mwingine ajulikanaye kwa jila la Pliny Mdogo, pia alitoa ushahidi wa uhasama kuhusu maisha ya Yesu. Katika barua aliyoiandika karibu na mwaka wa A.D. 110, alitumia maneno “Mkristo” au “Wakristo” mara saba, na aliandika jina “Kristo” mara tatu. Ni jambo lisilo na shaka kwamba Wakristo, wakiwa na Kristo kama Mwanzilishi wao, walikuwa wameenea kiasi cha kusababisha hofu kwa Mtawala na maafisa wake hadi wakati Pliny alipoandika hiyo barua. Baada ya kuchunguza aina hii ya ushahidi, haiwezekani kukataa ukweli kwamba Yesu Kristo alitambuliwa kama mtu wa kihistoria, aliye hai.
Hata msomaji wa kawaida anayesoma ushahidi wa mashahidi wa Kirumi wa uhasama ataguswa na ukweli kwamba watu hawa hawakumdhihirisha Kristo kama Mwana wa Mungu au Mwokozi wa ulimwengu. Walimvua maneno Yake ya Uana wa Mungu, walikanusha utukufu Wake, na kudharau ukuu Wake. Walimuelezea kwa watu wa wakati wao, na kwa vizazi vijavyo, kama mtu wa kawaida tu. Hata hivyo, ingawa walikuwa wamekosea sana kuhusu Yeye ni nani, walakini walithibitisha kwamba Alikuwapo. Na kwa hilo, tunawashukuru.
UZALISHAJI & MASHARTI: Tunayo furaha kutoa ruhusa ya makala hii kuzalishwa kwa sehemu au kwa ukamilifu, ili mradi masharti yetu yazingatiwe.
Masharti ya Uzalishaji→
REPRODUCTION & DISCLAIMERS: We are happy to grant permission for this article to be reproduced in part or in its entirety, as long as our stipulations are observed.