Menu

Yesu Alikuwa na Mantiki

Mtazamo wa Yesu unaoenea katika tamaduni maarufu ni ule unaomwonesha Yeye kama asiye jali mantiki na umakini sahihi kwa undani wa mafundisho. Jumuia ya Wakristo iliyochanganyikiwa imemsingizia Yesu ambaye si mgomvi, “sahihi Kisiasa” na hawezi kamwe kuwa “mwenye hukumu” au “asiyevumilia.” Hata hivyo, Agano Jipya-chanzo pekee cha kuthibitisha utambulisho wa Yesu linamwonyesha katika mwanga tofauti kabisa.

Chukulia kwa mfano, tokio katika Yohana 7 wakati Wayahudi walimchambua Yesu kwa kumponya siku ya Sabato mtu aliyekuwa na ugonjwa wa miaka 38 (Yohana 5:2-9). Wengi wangefikiri kwamba Yesu hangejishughulisha na utii wa makini wa sheria. Wangedhani kwamba Yesu angewashutumu Wayahudi kwaajili ya mkabala wao wa kupendelea, wa kufuata sheria ya dini, na kwamba Angekuwa tayari kabisa kutupilia mbali matakwa ya Sheria ili kutoa kipaumbele kwa hitaji la mwanadamu kwa njia la huruma. Kwa bahati mbaya mtazamo huu umejaa makosa, tathmini yake ni kudhalilisha sheria-  ambayo Mungu, Mwenyewe, aliiandika. Sheria kulingana na Mungu, imetolewa kwaajili ya ustawi wa mwanadamu (Kumbukumbu la Torati 6:24; 10:13; Mithali 29:18). “Sheria ya Mungu ni takatifu na ya Haki na njema” (Warumi 7:12), na hutumika kwa makusudio chanya yanayokusudiwa na Mungu (warumi 3:20). Kwa kweli, jinsi Yesu alivyo washughulikia watesi wake katika kipindi hiki huonyesha jinsi alivyokuwa na heshima kubwa kwa sheria, uhitaji wa kupatana nayo kwa uangalifu, na umuhimu mkubwa wa kuitumia kwa usahihi.

Akirejelea Muujiza alioufanya, Yesu alitoa kanusho la kimantiki kwa madai kwamba alivunja Sabato. Hapa kuna hoja hiyo iliyowekwa katika muundo wa (syllogistic):

  1. Ikiwa sharia ya Musa inataka tohara ya mtoto wa kiume siku ya 8 baada ya kuzaliwa-hata siku ya 8 inapoangukia siku ya sabato-basi kumponya mtu siku ya Sabato ni halali vivyo hivyo.
  2. Sheria ya Musa inahitaji tohara ya mtoto wa kiume siku ya 8 baada ya kuzaliwa-hata siku ya 8 inapoadhimishwa siku ya Sabato.
  3. Kwa hiyo, kumponya mtu siku ya Sabato ni halali pia.

Kisha Yesu alitoa onyo la kuhitimisha ambalo lilithibitisha uhalali wa hoja yake: “msihukumu kwa sura tu, bali mhukumuni kwa hukumu ya haki” (mstari 24). Kutumia sheria za Mungu kwa msingi wa “kuonekana” kunarejelea kufanya hivyo kulingana na jinsi mambo yanavyoonekana au kuonekana kwa mtu anayetoa uamuzi, yaani, kutoa maoni yanayotegemea uthibitisho usiotosha. Kinyume chake, “hukumu kwa hukumu ya uadilifu” kunamaanisha kufanya tathmini sahihi kwa kupata tu hitimisho linalikubalika kutokana na uthibitisho, yaani, kufikiri na kutenda kwa njia ya akili.

Tukio hili moja katika maisha ya Kristo ni mfano wa tabia yake katika matukio mengine, kuthibitisha kwamba Yesu alikuwa na mantiki katika mtazamo Wake wa maisha. Inaonyesha heshima kubwa aliyokuwa nayo kwa sheria. Inaangazia wasiwasi wa Uungu kwa kufuata sheria kwa uangalifu. Wote wanaotamani kuwa kama Kristo lazima waige mahangaiko haya haya. Kama Yesu mwenyewe alivyosema: “si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakaye ingia katika ufalme wa mbinguni, bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni” (Mathayo 7:21).


Published

A copied sheet of paper

REPRODUCTION & DISCLAIMERS: We are happy to grant permission for this article to be reproduced in part or in its entirety, as long as our stipulations are observed.

Reproduction Stipulations→