Menu

Wanamageuzi Wana Upofu Wa Imani

Kila mmoja anaamini katika kitu fulani. Upofu wa imani, hata hivyo, ni kuamini katika kitu fulani pasipo ushahidi. Kila mtu duniani ana imani, lakini kuwa kipofu wa imani, kwa tafasiri hakuna sababu; ni  kutoa hitimisho bila uhakiki wa kutosha. Imani niliyo nayo katika sheria za sayansi sio za kiupofu; zimesimamia kwenye mwamba wa ushahidi ambao umeundwa kwa miaka mingi ya kujenga tabia ya imani kwa upande wao. Ukristo haujajengwa kwenye imani tu, bali kwenye imani ambayo imehakikishwa kwa ushahidi, na Mungu anataka imani ya Kikristo iwe hivyo. Waumini wa asili (Wapagani), hata hivyo, wana upofu wa imani katika matukio kadhaa, ambayo ingekuwa lazima kama mageuzi ni kweli.

Kama mfano mmoja tu, fikiria; kama mtu ni muumini wa asili, lazima aamini kwamba, wakati fulani huko nyuma, maisha yalitokea kutoka kwenye vitu visivyo na maisha, (yaani, uzaliwaji wa ghafla wa maisha ulitokea). Majaribio mengi ya kisayansi yamefanyika kwa karne nyingi, wakijaribu hiyo nadharia kwamba “uzaliwaji wa ghafla wa maisha” unaweza kutokea, na kila mmoja wao ametoka na hitimisho lile lile; kwa asili, maisha yanatoka katika maisha tu. Haijalishi kipi wanasayansi wamejaribu kufanya katika maabara, ili kufanya vitu visivyo na uhai vitoe uhai, bado vimebakia kuwa vitu visivyo na uhai. Kama mtu mmoja ni wa kawaida na anafuata ushahidi kufikia suluhisho makini, atahitimisha kwamba katika ulimwengu (kwa asili), maisha hayawezi kuja kuwepo kutoka kwa vitu visivyo hai. Na kama hata hivyo hawezi kumeza ushahidi, na akachagua  badala yake kuamini isivyo kawaida kwamba maisha yanaweza kuwepo kutoka kwenye vitu visivyo hai, licha ya ushahidi, anashikilia upofu wa imani kwa kufanya hivyo. Hakuna hata mfano mmoja katika vitu vya asili, ambao katika huo, maisha yameonyeshwa kuja kutoka kwenye vitu visivyo hai.

Kama maisha yanatoka tu, katika maisha yaliyokuwepo ulimwnguni basi maisha ya mwanzo yalitoka wapi? Lazima yatakuwa yalitokana na chanzo cha ajabu, cha muujiza, Mmoja aliye nje ya ulimwengu. Naam huyo ni Mungu, ambaye “anatoa uhai kwa vyote, pumzi na vitu vyote” (Matendo 17: 25).

Rejea

Lionel Ruby (1960), Logic; An Introduction

Dave Miller (2003), “Blind Faith”

Jeff  Miller (2012), “The Law of Biogenesis (Part 1)


Published

A copied sheet of paper

REPRODUCTION & DISCLAIMERS: We are happy to grant permission for this article to be reproduced in part or in its entirety, as long as our stipulations are observed.

Reproduction Stipulations→