Menu

Wakristo na Nadharia ya Mageuzi

Sio kitu cha ajabu kusikia Wakristo wa karne ya 21 kudai kuamini katika mageuzi. Nimesoma nao majarida, na kukutana na watu wengi katika karne zilizopita ambao walikiri kuamini vyote, uvuvio wa Biblia na katika namna nyingi za mageuzi kidogo kidogo. Baadhi wanaamini kwamba mlipuko (Big Bang) wa mabilioni ya miaka iliyopita ni halisi, lakini kwamba Mungu alishiriki katika hilo. Wengine wanasema kwamba tabaka za dunia zinawakilisha muda wa mamia ya mamilioni ya miaka, na kwamba mabaki yaliyoozeana humo (fossils), yana mamilioni ya miaka umri wake. Sasa hata baadhi ya Wakristo wanafikiri kwamba Mungu aliumba mtu kutoka viumbe jamii ya nyani. Wanaamini kuwa watu wamegeuka-geuka kutoka maisha ya hali ya chini, wakati Mungu akiliongoza zoezi hilo la mageuzi.

Naendelea kushangazwa na madai hayo toka kwa wanaodai ni Wakristo, kwa sababu tofauti tatu; ya kwanza, kama tulivyoelezea mara nyingi muda uliopita, Biblia inatufundisha wazi kwamba Biblia ina umri wa siku tano zaidi ya binadamu, na hata mwanamageuzi wa kipagani, hawaamini kwamba, watu wamekuwepo duniani kwa mabilioni ya miaka (Lyons 2006). Wakristo wanaweza kuchagua kuamini kipimo hicho cha mageuzi ya mabilioni ya miaka, ambacho kinadai kwamba watu wamegeuka-geuka karibu kwa miaka bilioni 13.996 baada ya kuanza kwa ulimwengu, au wanaweza kuamini kile alifundisha Yesu na Mtume Paulo – kwamba wanadamu wamekuwepo duniani tangu kuwekwa misingi ya Ulimwengu (Luka 11: 49-51; Mariko 10: 6; Warumi 1: 20). Huwezi, iwe kwa akili au kwa maandiko, kuamini maoni yote mawili.

Ya Pili, Mageuzi kidogo kidogo hayajawahi kuthibitishwa. Wakristo wamekubali mageuzi ingawa nadharia nzima imeelemea, fikra tu.Wanamageuzi wanafikiri kwamba kwa sababu kuna ufanano kati ya binadamu na wanyama, basi binadamu atakuwa amegeuka-geuka toka kwa wanyama. Ingawa kiukweli huu ufanano hauthibitishi kitu hiki. (Kwa usahihi kabisa wanaelekeza kwa Muumba mmoja, aliyeumba vitu vyenye uhai vyote vikiwa na ufanano mwingi kwa sababu tunaishi katika Sayari moja, tunavuta hewa ya aina moja, tunakula chakula  cha aina moja, na kunywa maji ya aina moja nk). Na zaidi,si elimu ya miamba wala elimu ya uozo miamba zilizothibitisha mageuzi kidogokidogo. Njia zote za kutafuta umri wa miamba, zimeegemea fikra zilizojengeka ndani (Angalia Riddle, 2007). Mwanamageuzi na wasomi wa miamba, na wasomi wa uozo ndani ya miamba, hawajahakikisha kwamba hizi tabaka za dunia na uozo ndani yake zina mamilioni ya miaka, wanafikiria tu kwamba, hizo njia zao za kupanga umri ziko sahihi. Na zaidi hakuna ‘mtiririko maalum wa mageuzi’ katika rekodi ya uozo huo. Lakini tafasiri ya Wanamageuzi ya huo uozo. Kiufupi tuseme tu kwamba, mageuzi kidogo kidogo hayajawahi kuonekana wala kuthibitishwa.

Mwisho, Wakristo wengi wanaoneka wana nia ya kutetea mageuzi kiupofu-upofu, kuliko hata wanamageuzi wapagani. Kwa mfano, ingawa wengi wa wanaojiita Wakristo, wamemeza ndoano na uzi na boya vya hiyo “nadharia ya mlipuko mkubwa” (Big Bang Theory). (Mfano msomi mkuu, anayesomea biolojia, kwenye chuo kikuu cha kikristo, aliwahi kuniambia maprofesa wake wote wa sayansi, wanaamini uwepo wa Mlipuko mkubwa), ambao ni baadhi ya vitu vinavyopambwa duniani ambavyo Wanamageuzi wasomi wa fizikia ya anga, wanaamini kwamba “bado tupo kama tumechanganyikiwa kama mwanzo kuhusu jinsi ulimwengu ulivyoanza” (Cole, 193 [2593]: 37). Kwa ufupi tu, wakati nadharia ya mlipuko mkuu inapitia wakati mgumu ndani ya mduara wa wanamageuzi wapagani (Brook, 2008, 198 [2659]: 31; Coles, 2007, 193 [2593]: 33-37), bado inaenezwa miongoni mwa baadhi wanaoamini Biblia kama ni ukweli. Huwezi kuamini! Wakristo Wanamageuzi wanajulikana kwa kukubali kinachoaminiwa kama “anwani ya mtandao iliyopotea” kama kithibitisha cha jinsi binadamu alivyo geuka-geuka toka kwa Wanyama. Mwanafunzi mwingine wa chuo cha Kikristo, aliwahi kuniambia kuhusu Profesa mmoja, jinsi anavyounga mkono wazo kwamba “Lucy” (mtu wa kufikirika kwenye maigizo ya Kimarekani), anaonekana kama mmoja wa wazazi wetu, mwenye nywele, nusu mtu- nusu nusu nyani, ambaye aliishi miaka milioni kadhaa iliyopita. Ki ukweli wazo la Lucy kuwa mzazi wetu limejulikana kwa mda mrefu sasa kuwa ni kitendawili chenye matatizo, ambacho hata baadhi ya Wanamageuzi wapagani wamekiri (Angalia Harrub na Thompson 2003, uk 41-57).

Mbaya zaidi, wengi wa wanaojiita Wakristo wamejikuta katika mafundisho mabaya na yanayo udhi ya Darwin, licha ya kwamba (1) Hayajawahi kuthibitishwa (2) Wanamageuzi maarufu wa-kipagani, wameitilia shaka, na (3) Maandiko yanafundisha wazi kwamba dunia haina umri mkubwa sana na sio mabilioni ya miaka. Maandiko na Sayansi havipingani, bali neno la Mungu na nadharia jumla ya mageuzi inavyofanya. Mungu na awasaidie watu wake waache kutii usomi huu wa Wanasayansi wa kimageuzi na kuanza kumtii Mungu kwa neno lake.

Rejea

Brooks, Michael (2008), “Inflation Deflated.

Coles, Peter (2007), “Boomtime”

Harrub, Brad and Bert Thompson (2003), The Truth About Human Origins

Lyon, Eric (2006), “Man Has Been on Earth Since …”

Riddle, Mike (2007), “Does Radiometric Dating Prove the Earth is Old?


Published

A copied sheet of paper

REPRODUCTION & DISCLAIMERS: We are happy to grant permission for this article to be reproduced in part or in its entirety, as long as our stipulations are observed.

Reproduction Stipulations→