Uwe Mwenye Haki Unapotafsiri Biblia
Waamerika wa karne ya Ishirini na moja, wanafikiri kidogo sana jinsi mawasiliano yetu yanavyoonekana kujipinga yenyewe. Kwa wale ambao hawana ukaribu na Kingerza cha kisasa cha Amerika. Kuendesha gari sehemu ya maegesho na au kuegesha gari sehemu ya kuendesha, haiingii akilini, na hasa ukizingatia maana ya kuendesha na kuegesha. Kupokea mzigo toka kwenye malori na kupokea shehena toka melini, yana “bizarre” sawasawa ingawa sio kwa Waamerika. Tuna miguu inayonusa na pua zinazokimbia. Tunakula hambagi zilizotengenezwa kwa nyama na hotdog zilizotengenezwa kwa nyama ya nguruwe. Nini zaidi tena, tunaendesha kwenye barabara kuu za majimbo, ambazo haziendi katika majimbo hayo, (mfano barabara ya Hawaii – H 1) na tunataka kusoma kiwango cha juu cha mwendo kasi, huku tukiwa kwenye kiwango cha chini.
Swali moja la kijinga ambalo Waamerika wanauliza, “hukufanya kitu kile, ulifanya? Tunajibuje swali kama hilo? Basi huwa tunasema tu, Hapana huku tukimaanisha Ndiyo. Na kama tuna maanisha ya Hapana, tunasema Ndiyo. Hivi karibuni niliwauliza vijana wangu wawili swali kama hilo. Mmoja alisema Hapana na mwingine akasema Ndiyo. Lakini walimaanisha kitu kimoja wote wawili. Kwa ujumla walichanganyikiwa kwamba watajibuje swali kama hilo. Mtu anapotulia akifikiria aina za hotuba Wamarekani wanazotumia katika mawasiliano, atashangazwa sana na idadi ya kauli pinzani tunazotumia mara kwa mara.
Ni muhimu sana kwa wanafunzi wa Biblia kutambua kwamba waanndishi waliovuviwa pia walitumia aina nyingi za hotuba. Tukishindwa kuzitambua haya maneno yanayojipinga, tunaweza kufikia suluhisho la kijinga, ambalo wachambuzi wengi wa Biblia wamelifikia – kwamba waandishi wa Biblia walifanya makosa. Wakati kimsingi makosa yako upande wa yule anayetafasiri, na sio upande wa Mungu wa waandishi wake. Wasiwasi unapotokea kwamba Yesu alidanganya aliposema “atatoka kaburini “baada ya siku tatu” (Marko 8: 31), kwa sababu katika tukio jingine alionyesha kwamba atafufuka siku ya tatu (Mathayo 16:21; 17:23; 20: 19; rejea Matendo 10: 40), wanashindwa kutambua aina iliyozoeleka ya hotuba kwa nyakati za zamani. “Baada ya siku tatu”, na “siku ya tatu” mara kwa mara vilimanisha kitu kimoja (rejea 2 Nyakati 10: 5, 12; Mwanzo42: 17-18; Esta 4: 16- 5: 1). Hata maadui wa Yesu wa karne ya kwanza walitumia kauli zinazofanana na hizi. (Mathayo27: 63-64;) Kwa maelezo zaidi; www.apologeticspress.org/articles/570
Baadhi ya wachunguzi wa Kristo wanampinga kwa kumwita mama yake “mwanamke” katika Yohana 2: 4. Allegedly, Mwana wa Mungu hawezi kutumia maneno yasiyo ya kiutu katika namna isiyo na heshima kama hiyo. Kwa ukweli, hata kama ingawa kauli hii inaweza kuonekana kali au mbaya, katika karne ya 21, miaka 2,000 iliyopita ilitumika kwa namna ya heshima kabisa (Mathayo 15: 28; Yohana 19 26; 20: 15)
Wachunguzi wa Biblia wangetulia ili kufikiria aina nyingine zaidi za hotuba, tunazotumia kila siku (ambazo kwa wengine ni nzuri na kwa wengine zinajipinga). Pia zipo tofauti chache za kusawazisha dhidi ya Biblia. Kuiendea Biblia kwa usahihi ni kule kufikiria aina nyingi nyingi za hotuba, kuliko kudhania tu, ubaya wa waandishi wake.
REPRODUCTION & DISCLAIMERS: We are happy to grant permission for this article to be reproduced in part or in its entirety, as long as our stipulations are observed.