Uumbaji Na Umri Wa Dunia
Kwa maelfu ya miaka, kitabu cha Mwanzo sura ya I, imeeleweka kama mwanzo wa uumbaji wa mbingu na nchi uliofanyika siku za kawaida sita, lakini kubwa, bora na za kuvutia. Katika karne mbili zilizopita, wengi wamedanganywa kuamini kwamba mabilioni ya miaka yanayotakiwa ili mageuzi (evolution) yafanyike lazima yapate nafasi na yakubalike kwenye sura ya kwanza ya Biblia. Kwa sababu wengi wa “wanaoamini Biblia”, njia zilizoharibiwa za kupanga tarehe za mageuzi zimekuwa zikitawala kwa nguvu tafsiri ya Biblia. Kwa hiyo tunaambiwa kwamba Mungu hakutumia siku sita za kawaida, bali mabilioni ya miaka kuumba mbingu na nchi na kila kilichomo ndani yake. Mara nyingi tunasikia kauli kama hizi; “Mungu hafungwi na wakati” “Mungu angechukua muda mwingi apendavyo wakati wa kuumba mbingu na nchi, na vyote vilivyomo” na “mabilioni ya miaka yanaweza kuwa yalipita ndani ya Mwanzo sura ya I”. Kusema kwamba uumbaji haukuchukua mabilioni ya miaka, ni kumuwekea mipaka Mungu.
Kila Mkristo anakubali kwamba Mungu hafungwi na muda. Yeye hana mwisho wala mwanzo, ni wa milele, ana uwezo wote, Muumba anayejua vyote. Yeye ni wa “Tangu milele na hata milele” (Zaburi 90: 2). Msisitizo hata hivi sio kwamba Mungu ni Muumba wa milele aliyefunuliwa kwetu kuhusu uumbaji wake kwa uwezo wa neno lake. Mungu angeweza kuumba mbingu na nchi kwa njia yoyote aliyoitaka, na kwa mpangilio wowote alioutaka, na kwa muda wowote aliochagua. Angeweza kuumba dunia na vyote vilivyomo kwa saa sita, sekunde sita, au hata katika sehemu ya mia ya sekunde moja – Yeye ni, hata hivyo, Mungu mwenyezi (Mwanzo 17: 1). Lakini swali la msingi sio kile ambacho Mungu angefanya; bali ni kile alichosema alifanya na alisema aliumba kila kitu kwa siku sita (Mwanzo 1). Zaidi sana, Mungu alipowapa Waisraeli amri kumi alisema;
Ikumbuke siku ya saba, uitakase. Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote, lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana Mungu wako. Siku hiyo usifanye kazi yoyote, wewe wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. Maana kwa siku sita Bwana alifanya mbingu na nchi na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba. Kwa hiyo Bwana akaibarikia siku ya sabato na akaitakasa (Kutoka 20: 8-11)
Hii amri ya Sabato inaweza kueleweka vizuri ikiwa tu siku za wiki zinatafasiriwa kama siku za kawaida.
Uumbaji wa Binadamu na Umri wa Dunia.
Kwa mujibu wa nadharia ya mageuzi (theory of evolution), binadamu ni mgeni kwenye sayari ya dunia, akiondolewa mbali kabisa na mwanzo wa mbingu na nchi. Kama mbingu na nchi zilifanywa miaka bilioni 14 iliyopita, kama wanamageuzi wengi, wanamageuzi wa ki-mungu, na wale wanaofuatilia uumbaji wanvyoamini, binadamu “hakutokea” mpaka kama miaka bilioni 13.996 baadaye, kama muda huo ungewakilishwa na siku moja ya masaa 24, na hiyo inayodhaniwa kuwa mlipuko mkuu (Big Bang) ukatokea saa 6 usiku, basi binadamu hakuonekana mpaka Saa 5: 59: 58 usiku. Muda aliopangiwa binadamu katika siku moja ya masaa 24, ungewakilisha muda kidogo wa sekunde mbili tu.
Kama Biblia ilifundisha, iwe waziwazi au kwa kificho, kwamba binadamu aliondolewa mbali sana toka kwenye mwanzo wa mbingu na nchi, Wakristo wanaoamini Biblia wasingekuwa na shaka kukubali muda uliotajwa hapo juu. Kama Mkristo anavyoamini kwamba Mungu aligawanya bahari ya Shamu (Kutoka 14), alifanya shoka la chuma kuelea juu ya maji (II Wafalme 6: 5), na alimfufua Yesu kutoka kwa wafu (Mathayo 28: 1-8), angekubali kwamba binadamu walitokea duniani mabilioni ya miaka baada ya uumbaji – kama hicho ndicho Biblia inafundisha. Tatizo la wanamageuzi wa ki-mungu (theistic evolutionist) na wale wanaofutilia uumbaji, ni kwamba neno la Mungu halikuelezea muda huo. Ukweli ni kwamba, linafanya kinyume chake.
Biblia inatofautisha kwa uwazi kabisa baina ya vitu vilivofanyika kabla ya “kuwekwa msingi wa dunia” na matukio yaliyotokea baada ya “kuwekwa msingi wa dunia” Yesu aliomba kwa Baba usiku ule aliokamatwa na kusalitiwa akisema “ulinipenda kabla ya kuwekwa misingi ya dunia” (Yohana 17: 24). Petro aliweka wazi katika waraka wake wa kwanza jinsi “Yesu alivyojulikana kweli tangu zamani, kabla haujawekwa msingi wa dunia, lakini alifunuliwa mwisho wa zamani kwa ajili yenu” (I Petro 1: 20). Paulo aliwaarifu Wakristo wa huko Efeso jinsi Mungu “alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu ili tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo (Waefeso 1: 4). Kabla hajaumba mbingu na nchi (Mwanzo 1: 1), alikuwepo na alikuwa safi tu.
Kama wanamageuzi wa ki-mungu (theistic evolutionist) na wanaofuatilia uumbaji (progressive cretionists) wako sahihi, basi binadamu alionekana au kutokea, sio kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, au muda mchache baada ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, lakini ni miaka mingi sana baadaye – miaka bilioni 13.996 baadaye kuwa sawasawa zaidi. Hii nadharia hata hivyo, inapingana na maandiko wazi wazi.
Yesu alifundisha kwamba “damu ya manabii wote, iliyomwagika tangu kuwekwa kwa msingi wa ulimwengu, tangu damu ya Habili, hata damu ya Zakaria, aliyeuawa kati ya madhabahu na Hekalu” (Luka 11: 50, 51, Rejea pia Luka 1: 70). Sio tu kwamba maadui wa Yesu wa karne ya kwanza waliwaua Manabii, bali mababu zao ndio waliowachinja pia tangu siku za Habili. Chunguza kwamba Yesu aliunganisha muda wa mmoja wa wana wa Adamu na Eva kwenye “kuwekwa msingi wa ulimwengu”. Muda huu unatofautishwa na muda wa nabii aitwaye Zakaria, ambaye Yesu aliwaambia maadui zake, “mlimuua katikati ya Hekalu na madhabahu” (Mathayo 23: 35). Zakaria alitenganishwa kutoka siku za Habili kwa maelfu ya miaka. Damu yake haikumwagwa karibu na kuwekwa msingi wa ulimwengu; lakini ya Habili iliuawa hivyo. Baadhi ya wafia dini wa mwanzo, akijumuishwa Habili, waliisi karibu sana na uumbaji kwa Yesu kusema kwamba damu zao zilimwagika tangu kuwekwa msingi wa ulimwengu”. Kama binadamu alitokea au kuonekana mabilioni ya miaka, baada ya dunia kuumbwa na mamia ya mamilioni ya miaka baada ya viumbe hai mbali mbali kama vile Samaki, jamii ya vyura na wale watambaao kuwepo (kama kalenda ya wanamageuzi inavyoonyesha), kauli ya Yesu ingewezaje kueleweka? Ukweli ni kwamba binadamu hakuumbwa, miaka mingi sana baada ya kuumbwa kwa ulimwengu. Badala yake, amekuwepo “tangu kuwekwa msingi wa ulimwengu”
Katika tukio jingine, wakati wapinzani wa Yesu walipomkaribia, walimuuliza juu ya uhalali wa talaka. Yesu alijibu kwa kusema “Lakini tangu mwanzo wa uumbaji, Mungu aliwaumba mume na mke” (Marko 10: 6). Kwa mujibu wa Mwanzo 1 na 2, Mungu aliwaumba Adamu na Eva siku ya sita ya uumbaji wake (Mwanzo 1: 26 – 31; 2: 7, 21 – 25). Yesu alirejea kwenye tukio hili hili na akaonyesha kwamba Mungu aliwaumba “tangu mwanzo wa uumbaji”. Sawasawa na alivyohusisha siku za Habili na “kuwekwa msingi wa ulimwengu”, kuumbwa kwa Adam na Eva siku ya sita ya uumbaji kunaweza kuzingatiwa “tangu mwanzo wa uumbaji”.
[Zingatia: Yesu hatoi ushauri kwamba Adamu na Eva waliumbwa, mwanzoni mwa siku ya kwanza ya wiki ya uumbaji. Neno “uumbaji” (kitseos) kama lilivyotumika katika Marko 10: 6, halikutumika kwa kumaanisha wiki ya uumbaji. (Kama ingekuwa hivyo, basi Yesu angesema kwamba wanandoa wa mwanzo waliumbwa ”mwishoni mwa wiki ya uumbaji”) Watalaam wa lugha ya Kigiriki wanaoheshimika, Danker, Arnndt, na Gingrich, walizingatia kwamba Yesu anarejea kwenye “jumla ya vyote viivyoumbwa;” “dunia” (2000 Uk 573). Kwa maneno mengine, Adamu na Eva waliondolewa mbali kabisa kutoka karne ya kwanza BK na wakati ambao Yesu alitoa kauli hii, kwamba mtu angeweza kusema kabisa kwamba, binadamu wa kwanza aliumbwa “tangu mwanzo wa uumbaji, au tangu mwanzo wa ulimwengu, au tangu mwanzo wa mbingu na nchi (Rejea 2Petro 3:4).
Kama ratiba ya miaka bilioni 14 ya mageuzi ilikuwa kweli, kauli ya Yesu katika Marko 10: 6 ingekuwa na makosa; Adamu na Eva wasingekuwa popote, karibu na mwanzo wa mbingu na nchi, lakini wangefika “mwishoni” – miaka bilioni 13.996 baada ya kuanza. Kwa kifupi tunaweza kuiweka hivi, nadharia ya mageuzi na kauli ya Yesu, katika Marko 10: 6 haziwezi kuwa za kweli zote.
Katika waraka wake kwa Wakristo wa Rumi, mtume Paulo pia alidokeza juu ya muda gani binadamu amekuwepo hapa duniani. Aliandika “kwa sababu mambo yale yasiyoonekana tangu kuumbwa ulimwengu yanaonekana na kufahamika kwa kazi zake; yaani uweza wake wa milele na uungu wake, hata wasiwe na udhuru” (Warumi 1: 20). Ni nani hapa duniani anaweza kutambua uweza wa milele na uungu wa Mungu? Ni binadamu. [Zingatia; Ingawa wengine wanaweza kuwafikiria Malaika wanajua sifa zisizoonekana za Mungu, lakini mtazamo wa Warumi 1: 18- 32 unamrejea kwa uwazi Binadamu na sio Malaika]. Binadamu amemjua Mungu na sifa zake zisizoonekana tangu lini? “Tangu kuumbwa kwa ulimwengu”. Inakuwaje basi binadamu “kumjua” au “kumuelewa” Mungu “tangu kuumbwa kwa ulimwengu” kama ametenganishwa na uumbaji wa “mbingu na nchi, bahari” na vingine kama wanyama (dinosaurs, na wanyama wengineo wa mwanzo) kwa mamilioni au mabilioni ya miaka? Hali hii inapingana kabisa na maandiko. Bado kama David Riegle livyoona mwanzo, watu (na hata “Wakristo”) watakubali nadharia ndefu, ngumu, na za kubuni, na kuacha ukweli uliotolewa kwa Musa na Muumba mwenyewe (1962, uk 24).
Ukweli mwepesi ni kwamba, mtu hawezi kuamini kwa akili ya kawaida, katika vyote, mageuzi na Biblia. Lazima kufanya uchaguzi kati ya haya mawili. Mtu mmoja anaweza kuchagua nadharia ya kisayansi, iliyofanywa na binadamu, ya mtu anayebadilika-badilika kila siku (Miller 2013), au anaweza kuamua kuamini “neno la Bwana” ambalo “halinyauki wala halipukutiki” bali “ladumu hata milele (1 Petro 1: 24, 25).
Mtiririko wa Mungu wa Uumbaji na Nadharia ya Mageuzi.
Kwa nyongeza ya nadharia ya Mageuzi kupingana na ratiba au mtiririko wa uumbaji, inapinga zaidi tena mtiririko halisi kama unavyofunuliwa katika Mwanzo 1. Muumba mwenye uwezo wote angeumba kila kitu kwa muda ule ule. Angeumba kila kitu mpangilio maalum ambao wanamageuzi wanadai ulimwengu ulijiendeleza – kwa muda wa miaka bilioni 14. Kuna idadi isiyo kipimo ya namna ambayo Mungu angeweza kufanya kila kitu kuwepo duniani. Hata hivi kuna njia moja tu, ambayo neno la Mungu lenye mamlaka lilisema alifanya mbingu na nchi kuwepo na kwamba njia moja inapingana na nadharia ya mageuzi. Chunguza baadhi ya tofauti kati ya mtiririko wa mageuzi na Mwanzo 1.
Kipi kilikuja Kwanza – Dunia au Jua?
Mageuzi yanadai kwamba jua na vitu vingine vya angani, vilitokea mamilioni ya miaka kabla ya dunia. Hata hivi kwa mujibu wa Mwanzo 1, Mungu aliumba dunia iliyofunikwa na maji siku ya kwanza (Mwanzo 1: 1-5), wakati alileta jua, mwezi na nyota siku ya nne (Mwanzo 1: 14-19). Hivyo ni nini? Je dunia iliumbwa siku tatu kabla ya jua, au dunia ilibadilika-badilika (evolve) kwa mamilioni ya miaka baada ya jua? Mtu hawezi kwa akili ya kawaida kukumbatia yote mawili.
[Zingatia; baadhi ya Wakristo wanatetea Mungu lazima atakuwa aliumba jua, mwezi na nyota katika Mwanzo 1: 1 na baadaye “kuviweka” (Mwanzo 1: 16; Kiebrania nathan) mahali pake maalum huko angani siku ya nne ya uumbaji (Angalia Thurman, 2006 uk 3). Hata hivi ilikuwa ni siku ya nne ya uumbaji ambayo Mungu “aliweka tu” vitu hivyo vya angani mahali pake. Lakini alivifanya kwanza (kiebrania asah) (Mwanzo 1: 16). Sawasawa na jinsi Mungu alivyoziumba mwanzo, nchi na bahari vikiwa ukiwa na utupu (void), bila maisha ya viumbe, (ambavyo baadaye viliumbwa siku ya tano na ya sita ya uumbaji), “Mbingu” ziliumbwa “hapo Mwanzo”, bali jeshi lote la mbinguni, (ambalo sasa lipo huko) viliumbwa katika anga ya mbingu” siku ya nne. Ambayo inafanana zaidi na jinsi Mungu alinena mwanga uwepo katika siku ya kwanza ya uumbaji, akisema “Na iwe nuru” (Mwanzo 1: 3). Katika siku ya nne Mungu alisema “Na iwe mianga katika anga la mbingu … ikawa hivyo (Mwanzo 1: 14, 15). Kama Gary Workman alivyona;
“Na iwe mianga” (mst 14) iko sawasawa katika muundo wa sarufi na kauli nyingine kama hizo za, “Na iwe …” katika sura hiyo. Kwa hiyo amri ile inaweza tu kumaanisha kwamba Mungu alisema mianga kuwepo, siku ya nne, kama ambavyo amefanya mwanga wa mwanzo ile siku ya kwanza na anga katika siku ya pili” (1989 uk 3).
Weka akilini kwamba “Baba wa mianga” (Yakobo 1: 17), ambaye pia ni “mwanga” (1 Yohana 1: 5), anaweza kuumba mwanga kirahisi bila kuumba jua, mwezi na nyota kwanza. Kama ambavyo Mungu angeweza kutoa mti utoao matunda siku ya tatu pasipo mbegu. Angeweza kuumba mwanga kimuujiza siku ya kwanza bila vitoa mwanga vya kawaida, ambavyo viliumbwa siku ya nne (Angalia Miller 2014 kwa maelezo zaidi juu ya somo hili).
Dunia ya Mwanzo – Ilikuwa Kavu au Ilifunikwa na Maji?
Mageuzi wanadai kwamba mabilioni ya miaka baada ya mlipuko mkubwa. Dunia ilitokea kutoka katika wingu kubwa la vumbi ambalo lilikuwa mabilioni ya maili kwa upana. Nini zaidi, kulikuwa hakuna maji kwenye uso wa dunia ya kwanza, kwa sababu maji yote hayakuundwa kwa mamilioni ya miaka.
Je mazingira haya yanasema chochote kinachoeleweka kama simulizi za uumbbaji? Kwa kweli hapana. Mungu alinena dunia iliyofunikwa na maji iwepo siku ya uumbaji (Mwanzo 1: 1-5). Siku ya pili aligawanya maji (Mwanzo 1: 6-8). Haikuwa mpaka siku ya tatu, ambapo Mungu alifanya nchi kavu kutokea (Mwanzo 1: 9-13) kwa mara nyingine tena, mtiririko wa Mungu wa uumbaji na ule wa nadharia za mageuzi vinakataana.
Miti izaayo Matunda – Kabla au Baada ya Samaki na Viroboto.
Angalia tofauti nyingine, ambayo mara nyingi haizingatiwi, kati ya nadharia za Wanamageuzi na Biblia, Inadaiwa “mimea ilitawala nchi kavu kwanza katika kipindi cha Odovician, kama miaka milioni 465 iliyopita” (Donoghue 2007, 196[2631]: 38). Haikuwa mpaka mageuzi ya miti (evolution), miaka milioni 80 baadaye ambapo mimea ingesambaa duniani kote (uk 40). Kulikuwa na samaki ndani ya bahari, ( Evolution …1994 uk 30), na “viumbe wadogo kama wadudu” juu ya nchi (O’ Donoghue, uk 38), lakini kwa mujibu wa Wanamageuzi, miti izaayo mbegu, miti izaayo matunda, ilichanua mamilioni ya miaka baadaye.
Na kwa mujibu wa maandiko, Mungu mwenye uwezo wote, aliyeumba kila kitu kwa “pumzi ya kinywa chake” (Zaburi 33: 6), alisema “ nchi na itoe majani, mche utoao mbegu, na mti wa matunda, uzaao matunda kwa jinsi yake, ambao mbegu zake zimo ndani yake, juu ya nchi (Mwanzo 1: 11). Biblia halafu inaweka wazi, “Na ikawa hivyo. Nchi ikatoa majani, mche utoao mbegu kwa jinsi yake, na mti utoao matunda, ambao mbegu zake zimo ndani yake, kwa jinsi yake; Mungu akaona kuwa ni vyema. Ikawa jioni na ikawa asubuhi, siku ya tatu (Mwanzo 1: 11-13).
Ni rahisi tu, Mungu aliumba majani, miti, mbegu, Spora, na matunda katika siku moja ya uumbaji. Hapakuwa na kipindi kirefu sana kwa ajili ya mchakato uliofanya mimea kuwa vichaka, vichaka kuwa miti kwa miaka milioni nyingi. Mungu alisema aliyafanya kwa siku moja, “Na ikawa hivyo”. Zaidi sana, aliyafanya kabla ya kuumba maisha ya mnyama yeyote. Ingawa Wanamageuzi wanasema kwamba Samaki na wadudu vilikuwepo kabla ya miti izaayo matunda, Biblia inafundisha vinginevyo (Mwanzo 1: 20-25).
Kwa kweli, mtiririko wa uumbaji, kama unavyofunuliwa katika Mwanzo 1, unapingana kabisa na nadharia za Wanamageuzi. Mtu anayeamini Biblia kwelikweli, hawezi kushikilia kabisa nadharia hizo zinazodai, wanyama fulani wamekuwepo, mamilioni ya miaka kabla ya miti, au kwamba dunia ya Mwanzo haikuwa na maji juu ya uso wake. Kadiri Mkristo anavyokubaliana na mageuzi mapema, anakiri upinzani kati ya Mageuzi na simulizi za uumbaji wa Mungu vizuri zaidi. Kama nadharia za mageuzi ni za kweli, basi Biblia ni ya uongo, na kama Biblia ni ya kweli, basi nadharia za mageuzi ni uongo. Ni kwa muda gani utasita sita kati ya fikra mbili tofauti?
Nadharia ya Siku – Enzi.
Wakristo wanaokumbatia umri mrefu wa Wanamageuzi lazima watafute namna ya kupachika hayo mabilioni ya miaka katika rekodi za Biblia. Nadharia moja maarufu sana iliyoundwa ili kuongeza kipindi kirefu kwenye umri wa dunia inajulikana kama “Nadharia ya Siku – Enzi” Nadharia hii inasema kwamba siku za Mwanzo 1, sio za kawaida za masaa 24, bali ni kipindi kirefu cha miaka (mamilioni au mbilioni). Je nadharia hiyo inakaribishwa kwa mikono yote au kuna sababu nzuri ya kuikataa? Ukweli ni kwamba ushahidi uliopo unafunua sababu kadhaa, tunaoweza kujua siku zinazotajwa katika Mwanzo 1, zilikuwa ni aina ya siku, kama tunavyoziona nyakati hizi, na hazikuwa vipindi virefu sana vya muda.
Kutafasiri neno “Siku” sio Sayansi ya roketi.
Umoja na wingi wa neno “siku” kwa Kiebrania (Yom na Yamim) vinatokea katika Agano la Kale zaidi ya mara 2,300 na kulifanya neno la tano kwa umaarufu katika Agano la Kale (Saebo, 1990, 6: 13-14). Neno hili limetumika kwa namna tatu za msingi. Namna mbili za kwanza zinaelezewa kwa ufupi; “Siku” (yom) inaweza ikawa inarejea siku ya masaa 24 (mfano Mwanzo 50: 3), na inaweza ikarejea sehemu tu ya kipindi cha masaa 24, ambacho ni cha mwanga, (tofauti na usiku/au giza; mwanzo 1: 3 – 5). Siku pia inatumika katika namna pana kurejea vipindi virefu, vipindi visivyo na maelezo ya kutosha huko nyuma, sasa na hata vijavyo (mfano “Siku ya Bwana” Zakaria 14: 1).
Hata leo, tunatumia neno “siku” katika namna tofauti tofauti, lakini ni mara chache watu kuwa na wakati mgumu kuelewana juu ya matumizi yake, kwa sababu muktadha na njia ambapo neno limetumika vitalielezea neno kiurahisi. Fikiria juu yake. Ni mara ngapi unalazimika kuingilia na kumuuliza mtu kwa sababu hukuelewa anavyotumia neno “siku”? Maswali kama hayo hutokea mara chache sana, na kama yakiulizwa, zingatia aya inayofuata;
Katika siku za Ibrahimu, Mungu alifanya Agano na Babu mwenye haki na kizazi chake, akisema “… Kila mwanaume wa kwenu atatahiriwa … Mtoto wa kiume wa siku nane atatahiriwa kwenu” (Mwanzo 17: 10, 12). Kwa kuwa ilikuwa ni siku ya nane, isingekuwa shida kama Ibrahimu na uzao wake wangemtahiri kijana wao wakati wa mchana ama usiku. Katika siku za Musa, hata kama siku ya nane iliangukia siku ya saba (Sabato), Waisraeli walitegemewa kutahiri watoto wao kwa siku hiyo, ili kwamba sheria ya Musa isivunjwe (Yohana 7: 23).
Neno “siku’ limetumikaje hapo juu? Limetumika mara mbili kwa kurejea vipindi viwili tofauti ambavyo humo, Ibrahimu na Musa waliishi. Limetumika mara moja kurejea kinyume cha usiku. Limetumika mara sita kurejea siku ya kawaida ya masaa 24.
Wasomaji wengi wa Biblia walio wengi wanaweza kwa urahisi na kwa haraka kuelewa jinsi waandishi waliovuviwa walivyotumia neno siku (yom) kote katika Biblia. Watu wengi wanaelewa vizuri kabisa kama neno “siku” limetumika katika namna inayoelezeka (kama sehemu ya au siku nzima ya masaa 24) au kwa namna isiyoelezeka (mfano “Katika siku ya Bwana”). Baada ya gharika, Bwana alisema “Muda nchi idumupo, majira ya kupanda na mavuno, wakati wa baridi na wakati wa hari … mchana na usiku, havitakoma. (Mwanzo 8: 22). “Mchana” (day) inatumika hapa bila shaka kwa kurejea kipindi maalum, sehemu ya siku ya masaa 24, yaani “mwanga (Mwanzo 7: 4; 29: 7; Kutoka 24: 18). Wakati wa gharika, maji “yalikaa kwenye uso wa nchi siku mia moja na hamsini” (Mwanzo 7: 24). Kwa mara nyingine, “siku” (yamim) imetumika kwa maana iliyofafanuliwa, ingawa badala ya kurejea kwenye kipindi cha siku chenye mwanga, msisitizo uko kwenye masaa yote 24 – hasahasa kipindi cha siku 150 zenye saa 24. Katika Kumbukumbu 31: 17, Mungu alitangulia kusema jinsi Waisraeli watakavyovunja Agano lake, na “katika siku hiyo” matatizo mengi yatawajilia. Msisitizo hapa ni juu ya kipindi maalum cha muda – katika siku zijazo, wakati Waisraeli wangeanza kuabudu sanamu za mataifa ya Wapagani yanayowazunguka.
Siku na Namba.
Moja ya njia rahisi sana (japokuwa sio njia pekee) ya kutambua pale Biblia inapotumia neno siku kwa kumaanisha masaa 24, ni kama neno hilo limeboreshwa na namba. Ni wazi kwamba siku ya nane (katika aya zilizotajwa mwanzoni), inarejelea siku ya nane (sio wiki, wala mwezi, wala mwaka, wala karne nk) katika maisha ya mtoto. Siku ya saba, inarejelea siku ya saba ya wiki ya kawaida – Sabato. Cha kufurahisha, kama Henry Morrison alivyowahi kusema, “pale namber inayopinga inapoambatanishwa kwenye ‘siku’ katika Agano la Kale (na kuna matukio zaidi ya 200 ya hivyo), maana yake ni ile ya siku ya kawaida. (1974 uk 224). Hakika, kama Yona alivyokuwa katika tumbo la samaki mkubwa kwa siku tatu, (na sio miaka 3, 000), na kama Waisraeli walivyoizunguka Yeriko, mara moja kwa siku kwa siku sita (na sio vipindi virefu vya muda), tunaweza kujua sasa kwamba Mungu aliumba kila kitu katika “siku sita” (Kutoka 20: 11; 31: 17), na siyo miaka bilioni sita. Kuhusu kila siku ya uumbaji, Musa aliandika; “ikawa jioni, ikawa asubuhi siku ya kwanza … siku ya pili … siku ya tatu …. Siku ya nne …. Siku ya tano …. Siku ya sita (Mwanzo 1:5, 8, 13, 19, 23, 31).
Siku Zenye Jioni na Asubuhi.
Kigezo kingine kote katika lugha za maandiko zilizo za kawaida, zisizo za kinabii, kwamba yom, inarejea muda maalum, unaoelezeka wa kipindi cha masaa 24, au pungufu [yaani kama imetumika kumaanisha (a) masaa ya mchana ya kipindi cha saa 24 tu (b) kipindi chote cha masaa 24], ni kama maneno “asubuhi” na/au “jioni” yametumika kuielezea siku hiyo. Maneno “asubuhi” (boqer) na “jioni” (erev) yanatokea mara 348 katika Agano la Kale, (Boqer inatokea mara 214, na erev mara 134; Konkel 1997, 1: 711, 716). Tena na tena kote katika Agano la Kale, maneno haya yanatumika kurejea kipindi maalum, kinachoelezeka cha siku zenye masaa 24.
- Nuhu “alingoja kwa siku saba nyingine, katuma nje tena njiwa toka katika safina. Njiwa akamrudia jioni” (Mwanzo 8: 10, 11).
- Musa aliwaamua Israeli, … na siku iliyofuata … na watu wakasimama mbele ya Musa tangu asubuhi mpaka jioni (Kutoka 18: 13).
- Mungu alimwamuru Haruni na wanaye katika kitabu cha Walawi kuhusu matoleo mbalimbali, pamoja na sheria zinazohusu sadaka za amani. Kwa mujibu wa Walawi 7: 15 “Na hiyo nyama ya sadaka zake za amani zilizochinjwa kwa ajili ya shukrani, italiwa siku iyo hiyo ya matoleo yake asisaze yoyote hata asubuhi”
- Kipindi cha Waisraeli kuzunguka jangwani, Mungu alifanya wingu libakie juu ya hema “tangu jioni mpaka asubuhi; na pale wingu lilipochukuliwa asubuhi, walisafiri, ikiwa ni mchana au usiku (Hesabu 9: 21).
Tukio pekee ambapo jioni na asubuhi, vinaweza visirejee muda maalum katika masaa 24, ni mara chache sana, ambapo vimetumika katika lugha za kinabii au za kimafumbo (mfano Mwanzo 49: 27; Habakuki 1: 8). Vinginevyo ushahidi unazidiwa pale “asubuhi” na ama ‘jioni” vimetumika kurejea kipindi cha muda (cha kawaida, kisicho cha kinabii au cha kimafumbo) mara nyingi vinarejea siku za kawaida za masaa 24 (au sehemu zake). [Zingatia; Kwa tofauti ya wazi kati ya lugha ya maandiko, ya kawaida, inayoelezeka, isiyo ya ki-nabii, na lugha Biblia, ya mafumbo, na ya kinabii, linganisha simulizi za Yusufu katika Mwanzo 37 – 48 na kile Yakobo anachotabiri kitamtokea Yusufu, ndugu zake na kizazi chao katika Mwanzo 49: 1 – 27. Kwa habari zaidi juu ya asili, ya kawaida na ya ki-historia ya kitabu cha Mwanzo 1 na 2, angalia Thompson, 2000, uk 133 – 161 na De Young, 2005, uk 157 – 170].
Sasa hii inahusu nini kwenye uumbaji? Ni kuwa tu, kila siku ya uumbaji ilikuwa na jioni moja na asubuhi moja.
“Hivyo jioni hiyo na asubuhi vilikuwa ni siku ya kwanza”(Mwanzo 1: 5).
“Hivyo jioni hiyo na asubuhi vilikuwa siku ya pili”(Mwanzo 1: 8).
“Hivyo jioni hiyo na asubuhi vikawa siku ya tatu” (Mwanzo 1: 13).
“Hivyo jioni hiyo na asubuhi vikawa siku ya nne” (Mwanzo 1: 19).
“Hivyo jioni hiyo na asubuhi vikawa siku ya tano” (Mwanzo 1: 23).
“Hivyo jioni hiyo na asubuhi vikawa siku ya sita” (Mwanzo 1: 31)
Kama Mungu alivyosema juu ya vipindi maalumu na vinavyoelezeka vya siku kwa kutumia maneno “jioni” na “asubuhi” mara mamia kote katika Agano la Kale. Alifanya hivyo mara sita katika simulizi za uumbaji. Kama kila mahali pia, katika lugha za kawaida, zisizo za kinabii katika Agano la Kale, maneno haya yametumika kumaanisha siku za kawaida za masaa 24, kwa nini wengine wanatetea siku za kawaida, zisizo za kinabii, simulizi ya uumbaji katika Mwanzo zilikuwa ni kipindi kisichoelezeka cha muda mrefu wa mageuzi? Inaweza kuonekana ni kwa sababu, utiifu wao kwenye hisia hiyo ya kufikirika, na nadharia isiyothibitishwa ya mageuzi, ina maana kubwa kwao kuliko tafasiri ya Biblia, isiyo na mchezo, isiyopingana, na makini.
Maswali Mengine Wanayopaswa Kuzingatia Waamini wa Siku – Enzi.
Kwa nyongeza kwenye ushuhuda wa nguvu dhidi ya nadharia ya Siku – Enzi uliotolewa na waandishi wa Biblia walivyotumia neno yom wakiunganisha na kivumishi cha namba na neno “jioni” na “asubuhi”, Maswali mengine yanayostahili kukawia kwa Wana-nadharia wa siku – enzi.
- Kama “siku” za uumbaji za Mwanzo 1: 14 zilikuwa “vipindi virefu vya muda” je nini neno “miaka” ilimaanisha? Neno “miaka” linaweza kueleweka vyema katika muktadha huu kama tu neno “siku” lilimaanisha siku za kawaida.
- Kama “siku” za Mwanzo hazikuwa kabisa, bali vipindi virefu vya kimageuzi, basi shida itatokea katika Nyanja za mimea. Uoto ulikuja kuwepo siku ya tatu (Mwanzo 1: 9 – 13). Kama kila siku ya Mwanzo 1, ilikuwa vipindi virefu vikijumuisha kipindi kimoja cha mchana na cha usiku (Mwanzo 1: 4, 5). Maisha ya mimea yameishi vipi mamilioni ya miaka ya giza totoro?
- Ingekuwaje mimea ambayo inategemea wadudu kwa uchavushaji kuishi mabilioni ya miaka kati ya siku ya tatu na siku ya tano na sita, wadudu walipoumbwa?
- Kama Roho Mtakatifu anaweza akawasilisha tofauti kati ya siku ya kawaida na kipindi kirefu kama “miaka elfu kadhaa” (2Petro 3: 8), ni sababu gani, nyeti na inayokubalika, ambayo mtu anaweza kutoa kwa kudhani kwamba siku moja ya Mwanzo lazima itakuwa ilikuwa maelfu, mamilioni, au mabilioni ya miaka?
Ukweli ni kwamba, Nadharia ya siku – enzi inakufa kunapokuwepo usomaji makini wa Mwanzo 1 na sehemu zingine za Maandiko matakatifu.
Hitimisho
Wale wanaopendekeza kwamba mabilioni ya miaka ya mageuzi ilitangulia kuumbwa kwa Adamu na Eva, wanahitaji kutoa wazo makini, kwa aya nyingi za Biblia, zinazofundisha vinginevyo. Biblia haiko kimya kuhusu asili yetu. Mungu mwenyezi aliumba mbingu na nchi (na vyote vilivyomo) kirahisi tu kwa neno vikawepo.
Kwa neno la Bwana mbigu zilifanyika, na jeshi lake lote kwa pumzi ya kinywa chake …. Nchi yote na imwogope Bwana, na wote wakaao duniani na wamche. Maana yeye alisema na ikawa, na yeye aliamuru, ikasimama (Zaburi 33: 6, 8, 9).
Mungu kama angechagua kufanya hivyo angetumia miaka bilioni sita, au milioni sita, au elfu sita akiumba ulimwengu. Kama angetoa ishara yeyote, kwamba alitumia muda mrefu sana ili kwamba michakato ya asili ifanyike wakati wa uumbaji, tungeelewa kwa nini Wakristo wangeshikilia imani kama hiyo. Hata hivyo Mungu amefanya tofauti kabisa. Kwanza alifunua kwamba mbingu na nchi ni matokea ya nguvu za asili (na hivyo kupingana na nadharia jumla ya mageuzi). Pili; Alitupatia mtiririko wa matukio yaliyotukia ambayo yanapingana na nadharia ya mageuzi. Nini zaidi alitwambia kabisa kabisa alitumia muda gani kuumba. Sura ya kwanza ya kitabu cha Mwanzo kinafunua kwamba, tokea kuumbwa kwa mbingu na nchi mpaka kuumbwa kwa binadamu, alitumia siku sita. Katika matukio mawili katika kitabu kinachofuata cha Biblia anatukumbusha kwamba uumbaji ulifanyika sio kwa vipindi sita virefu vya miaka mingi, lakini kwa siku sita (Kutoka 20: 11; 31: 17). Baadaye alisisitiza wasoma Biblia kwamba binadamu hana miaka 14 bilioni mdogo kuliko mwanzo wa mbingu na nchi, kwa kumrejea kama aliyepo duniani (1) “tokea mwanzo wa uumbaji” (Marko 10: 6), (2) “Tangu kuumbwa kwa ulimwengu” (Warumi 1: 20) na (3) “Tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu” (Luka 11: 50).
Kama Mungu aliumba kila kitu kwa siku za kawaida sita, na akategemea tuamini hivyo. Angehitaji kitu gani tena kusema zaidi ya alichosema? Ni kwa uwazi kiasi gani angeyaweka ili tuelewe vizuri? Na kama haijalishi tunawaza juu ya somo hili, kwa nini alitufunulia mtiririko wa matukio ya kuanzia?
Kweli, kama Mungu alivyosema wazi juu idadi ya masomo ambayo waumini mbalimbali wameyaharibu, (kama vile; gharika ya Nuhu, ulazima wa kuzamisha katika ubatizo kwa ondoleo la dhambi, kurudi kwa Kristo nk), Biblia inafundisha wazi wazi kwamba Mungu, kwa neno la kinywa chake, alitamka mbingu na nchi na kila kilichomo ndani yake, vikawepo katika siku sita. Hakuna aya ya Biblia inayotumika kwa halali, itakayomwongoza mtu kwenye hitimisho jingine (2Timotheo 2: 15).
Rejea
Danker, Fredrick William, William Arndt and F. W. Gingrich (2000), Greek – English Lexicon of the New Testament
De Young, Donald (2005), Thousands not billions
Evolution; Changing Over Time (1994)
Konkel, A. H. (1997), boqer, New Internationl Dictionary of Old Testament
Miller, Jeff (2014), “How Could there Be Light Before the Sun?
Morris, Henry M. (1974) Scientific Creationism
O’Donoghue, James (2007), “A Forest is Born
Riegle, David (1992), “Creation or Evolution?
Saebo M (1990), Yom, Theological Dictionary of The Old Testament
Thompson Bert (2000), Creation Compromise?
Thurman, Clem (2006), “How Was LightBefoore the Sun”
Workman, Gary, (1989), “Question From Genesis”
REPRODUCTION & DISCLAIMERS: We are happy to grant permission for this article to be reproduced in part or in its entirety, as long as our stipulations are observed.