Menu

Usahihi Wa Biblia

Mtu anapoanza kusoma Biblia, haichukui mda mrefu, mpaka anapokuja kukutana na kauli kama “Mungu akasema” au “ndivyo asemavyo Bwana” au haya ni “maneno ya Bwana”. Kauli kama hizi zinatokea mara mia kadhaa katika Maagano yote, la Kale na Jipya. Kwa kweli, amri kumi zenyewe zinaanza na sentensi, “Mungu akanena maneno haya yote akasema,” (Kutoka 20: 1). Mara thelathini na tatu katika kitabu cha Walawi pekee, tunasoma maneno, “Bwana akanena na Musa” (4: 1; 5: 14 nk). Katika Zaburi 119 pekee, maandiko yametukuzwa kama ni neno la Mungu mara 175. Katika Agano Jipya, Mtume Paulo alidai kwamba ujumbe wake haukupokelewa toka kwa wanadamu, “bali kwa ufunuo wa Yesu Kristo” (Gal 1: 12). Hali kadhalika, akiwaandikia Kanisa la Thesalonike, alidai kwamba alichokiandika kilikuwa ni “Maneno ya Bwana” (I Thesalonike 4: 15). Kwa kweli waandishi wote wa Agano la kale na hata Jipya, waliweka msisitizo mkubwa, juu ya ukweli kwamba ujumbe wao, ulitoka kwa Mungu – kwamba waliongea sio kwa mapenzi ya wanadamu, bali “kwa Roho Mtakatifu” (II Petro 1: 21).

KUTAFASIRI  UVUVIO

Sio tu kwamba Biblia inadai kwamba imevuviwa, lakini pia inatoa tafasiri na kuelezea maana ya uvuvio. Katika II Timotheo 3: 16, Paulo alidai “Kila andiko lenye pumzi ya Mungu” Neno la Kigiriki ni theopneustos, likimaanisha kutoka mdomoni mwa Mungu au kwa Kiingereza, God breathed. Mungu kimsingi alitoa pumzi ya neno. Biblia ni neno la Mungu, sio la wanadamu. Aya tatu baada ya hiyo, yaani (II Timotheo 4: 2), Paulo aliweka wazi kwamba “Kwa hiyo … lihubiri neno”. Kwa nini? Kwa sababu ni neno la Mungu. Kama hakika yake kwamba pumzi ya Mungu iliufanya ulimwengu kuwepo, (Zaburi 33: 6), basi na Biblia inajiweka wazi kuwa ni matokeo ya pumzi ya Mungu.

Katika waraka wake wa pili, (2 Petro 1: 16-21), Petro alisema kwenye tukio adimu la Kristo kubadilika sura – Pale Mungu alipotamka wazi wazi toka mbinguni moja kwa moja kwa Petro, Yakobo na Yohana. Mungu alishaongea kwa mdomo akisisitiza kwamba Yesu ni mwanae mpendwa, na kwamba binadamu wanaamriwa kumsikiliza (Mathayo 17: 5). Petro baadaye aliweka wazi “Nasi tunalo neno la unabii likithibitishwa … Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu”. Petro alikuwa anasema kwamba maandiko tuliyopewa na manabii ni uhakika na ni ya haki, na yana amri kama sauti ya Mungu iliyoongea wakati wa kubadilika sura.

Mtume alielezea zaidi kwamba maandiko (neno la unabii) hayakutafasiriwa kama apendavyo mtu tu, kwa maana kwamba, hayakutokana na wao, wala katika akili za hao walioandika. Maandiko hayakutokana na “Mapenzi ya wanadamu”. Sio matokeo ya mwisho ya utafiti wa kibinadamu, au uchunguzi wa vitu vya asili. Maandiko sio matokeo ya fikra za waandishi wake. Kinyume chake “Wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu wakiongozwa na Roho Mtakatifu” (II Petro 1: 21). Neno kuongozwa, katika Kigiriki linamaanisha kuletwa. Petro alisema kuwa Roho Mtakatifu aliwachukua waandishi (ambao ni Manabii) na kuwaleta kwenye lengo alilochagua mwenyewe. Hivyo maandiko, ingawa yameandikwa kwa vifaa vya kibinadamu, yalisimamiwa na Mungu, ili kwamba maneno yatakayotoka yawe yake.

Huyu ni Petro yuleyule, ambaye huku akisubiri ujio wa Roho Mtakatifu, katika Matendo 2, siku ya Pentekoste alisimama katikati ya Mitume wenzake na kusema “Ndugu ilipasa andiko litimizwe alilonena Roho Mtakatifu zamani kwa kinywa cha Daudi, katika habari za Yuda” na baadaye akanukuu kutoka katika Zaburi (Matendo 1: 16…). Petro aliamini kwamba Roho Mtakatifu aliongoza kile alichokiandika Daudi, na matokeo ya uandishi ule yanaitwa “maandiko matakatifu”.

Huyu ni Petro yule yule ambaye katika 1 Petro 1: 10-12, alielezea kwamba (1) Wasemaji waliovuviwa wa Agano la Kale hawakuelewa wakati wote habari zilizotolewa na Mungu kupitia wao (2) ilikuwa ni Roho wa Kristo aliyekuwa akifanya kazi ndani yao (3) Habari hii hii iliyovuviwa ilikuwa ikitolewa na Mitume, nyakati za Petro (4) Roho Mtakatifu yule yule alikuwa akiongoza usemaji wao. Hii ina maana kwamba watu waliovuviwa akili zao zilipagawa walipotoa  vitu vilivyovuviwa. Lakini matokeo yalikuwa ni ya Mungu, kwani hawakuelewa umuhimu wa kile walichokitoa.

Huyu ni Petro yuleyule ambaye katika 2 Petro 3: 15, 16 alimrejea “ndugu yetu mpendwa Paulo” kwamba “aliwaandikia” na tena akasema, “vile vie kama katika nyaraka zake zote pia akitoa humo habari za mambo hayo, na mambo hayo watu wasio na elimu huyapotosha, kama wayapotoavyo na maandiko mengine”. Angalia Petro aliweka wazi kwamba (i) Paulo aliandika Nyaraka, na (ii) Nyaraka hizo zinahesabika kama “maandiko matakatifu” – kwa hiyo nyaraka za Paulo ni maandiko matakatifu, hata kale kadogo kabisa, kama ilivyo kwa Agano la Kale na hata Agano Jipya, na (iii) Na maandiko haya yana amri na ni ya ki-Mungu, maana Petro alisema kuyapotoa ni kukaribisha uvunjifu. Ambayo ni ishara ya kuwa mbali na upendeleo wa Mungu, na madhara ya ki-roho, yatokanayo na kutotii maneno ya Mungu

Biblia bila shaka inadai yenyewe hadhi ya “uvuvio”, – ambao umetolewa na Mungu mwenyewe. Uvuvio huo una usimamizi wa Mungu kiasi kwamba hata maneno yenyewe yamekuja kwa uwezo wa Mungu. Mfalme Daudi aliwahi kusema “Roho ya Bwana ilinena ndani yangu, na neno lake likawa ulimini mwangu” (2 Samweli 23: 2). Chunguza kwamba Daudi hakusema, mawazo ya Mungu au fikra za Mungu, zilikuwa ulimini mwake, lakini kwamba neno la Yehova lilikuwa ulimini mwake. Katika I Wakorinto 2, Mtume Paulo aliweka wazi kwamba mambo ya Mungu yalifunuliwa kwa watu kwa Roho wa Mungu. Halafu kuhusu ujumbe wenye uvuvio wa Mungu, aliendelea kusema: “Mambo tunayoyasema, sio katika maneno, yanayofundishwa na hekima ya wanadamu, bali ambayo Roho anayafundisha, tukiyafasiri mambo ya rohoni kwa maneno ya rohoni” (1 Wakorinto 2: 13 pamoja na fafanuzi, angalia pia Yohana 17: 8). Maneno ya ufunuo yanaongozwa na Roho, na sio maneno ya hekima ya kibinadamu tu. Huu ni uvuvio wa mdomo au wa maneno. Hii haimanishi kwamba, waandishi walifanya imla. Bali Biblia inaonyesha kwamba Mungu alifanya kazi hiyo ya uvuvio kwa kila uwezo wa mtu, maneno, mtindo na tabia ya kila mwandishi.

USAHIHI WA BIBLIA NA MAADUI ZAKE

Swali moja ambalo inaonyesha idadi kubwa ya watu wameliuliza hivi karibuni, ni kama “kila neno la maandiko matakatifu “ni ukweli uliovuviwa?” Wapinzani, Wapagani, na Wenye mashaka, wameliponda wazo la usahihi wa Biblia. Yaani kwamba Biblia (iwe katika hali yake ya asili au ya sasa) haina makosa au uongo.

[Angalia neno “errant” linatoka katika Kilatini, ambako linamaanisha kupotelea mbali, na kinyume chake, yaani “inerrant” kinaliweka kinyume yaani kuwa sahihi. Kwa hiyo kukiri usahihi wa Biblia ni kuthibitisha kwamba, maandiko yanaendana na ukweli kuliko kwenda mbali na ukweli au kopotea (angalia Preus 1984 uk 91-93; Parker 1958, uk 95).] Kwa wasioamini, Biblia ni kitabu kingine “kinachoweza kuwa na makosa, kilichoandikwa na watu wasio wakamilifu”. Hoja hizi zinapelekea kwenye aya nyingi ambazo wanasema eti ama zinajipinga au zinapingana na aya nyinginezo za maandiko au zinapinga ukweli wa; historia, jiografia, au sayansi. Bahati mbaya watu maarufu katika shule za umma, katika vyuo vikuu, katika biashara, na hata katika vyombo vya habari. Wanaohoji Biblia wamekuwa na nguvu na ushawishi katika siku za karibuni. Wenye mashaka zaidi na zaidi wanaweza kusikika duniani kote; katika redio, televisheni, mitandao na hata madarasani. Katika kitabu chao kinachofurahisha “Surveying the religious landscape; Trends in U.S. Beliefs,George Gallup Jr na Michael Lindsay walieleza jinsi wa-Amerika wasivyoamini Biblia tena, walisema;

     Wa-Amerika wengi wanaiendea Biblia kama kitabu cha hadithi, historia, au cha kufundisha mila.. Majaribio kadhaa yamefanyika ili kuitafasiri upya na kuitoa katika hali hiyo yanaendelea katika taasisi za elimu kwa miaka kadhaa sasa. Na sasa yanaonekana kutoka kwenye taasisi za elimu na kuhamia mitaani, hivi karibuni, 1963, watu wawili kati ya watatu (2/3) waliiona Biblia kama neno halisi la Mungu linalostahili kuchukuliwa kama lilivyo, neno kwa neno. Leo ni mmoja tu kati ya watatu (1/3) ambaye bado anaamini hivyo (1999 Uk 36).

Hakika kwa miaka  sasa, wenye mashaka wamekuwa wakifanya kazi kwa bidii katika kujaribu kupuuza msingi muhimu wa imani ya Ukristo – kwamba Biblia ni sahihi, ni neno la Bwana lililovuviwa. Jinsi fundisho lao lilivyo la uharibifu, na labda ujumbe unaoharibu zaidi wa makosa ya Biblia unaweza kusikika toka kwa watu kadhaa wanaodai kuwa ni Wakristo.

Tangu kuwepo udhamini wa Waliberali (walegezaji) katika karne ya  18, mashambulizi yamesawazishwa ndani ya “Ukristo” kuhusu kuaminika kwa Biblia. Kama Musa ndiye mwandishi wa Vitabu 5 vya Torati, historia ya kitabu cha Yona na hata miujiza ya Yesu ni baadhi tu ya mada za Biblia ambazo walegezaji (liberals) wamezishambulia bila kuchoka kwa karne tatu zilizopita. Majina kama Karl Graf, Julius Wellhausen, na Rudolf Bultimann yamekuwa yakirejewa na wasomi pale Kuaminika kwa Biblia kunapohojiwa. Mwishoni mwa karne ya 20, mwandishi George Marsden, katika kitabu chenye kichwa, “Reforming Fundamentalism” (1987), aliandika juu ya namna Seminari maarufu ya theolojia  huko Amerika (Fuller Seminary), imeacha kutetea na kuamini usahihi wa maandiko tokea mapema miaka ya 1960. Na mbaya zaidi mwelekeo huu umekuwa na madhara yanayoendelea katika Amerika yote. Kwamba shule zaidi za theolojia hata zile zenye asili ya msimamo mkali kuliko “Fuller” wanakataa imani kwamba Biblia ni sahihi katika yote inayofundisha.

Moto mtakatifu wa Mungu

Katika mwaka 2002, idara ya chapa ya “Abeline Christian University” (ACU) ilichapisha kitabu chenye jina “Holy Fire” au moto mtakatifu, kiliandikwa na maprofesa watatu, kutoka kwenye shule ya juu ya theolojia kwenye chuo hicho. Walichukulia suala la matumizi au uhalali wa neno “usahihi”, Kenneth Cukrowski, Mark Hamilton, na James Thmpson, waliuliza kama “usahihi” huo unahusu hata vitu vidogo vidogo ndani ya Biblia? (Uk 40). Kwa mujibu wa watu hawa, mara kadhaa ndani ya Biblia, mtu  anaweza akaona kupingana katika maelezo (uk 40). Mfano waliotoa (1) Kufufuliwa kwa binti wa Yairo; (2) Yesu aliulaani mtini; (3) kusafisha Hekalu, na (4) Nukuu zinazodaiwa za Mathayo katika Yeremia 27: 9 zinazopingana. Kufuata huku kupingana kwa ndani walisema baadaye kwamba wakati mwingine maelezo hayaendani na rekodi za historia (Uk 40). Ingawa Cukrowsk, Hamilton na Thompson walikiri kwamba “taarifa zaidi zinaweza kusuluhisha nyingi za hizi shida (uk 41).” Baadaye waligundua kwamba “kwa sababu Biblia imetujia kupitia wanadamu, mtazamo wetu juu ya maandiko kutoka kwa Mungu, sio suala la uhakika wa kimahesabu, bali uthibitisho wa imani (uk 45). Mwisho watu hawa walielezea, sio wenye mashaka bali Wakristo wa maana, wanaoshikilia maandiko kama  neno la kweli la Mungu katika yote linalosema, kama hao ambao “katika kujaribu kwao kutoa ukweli halisi, … wametengeneza mgogoro wa imani” kwa sababu  “muda wote wanahisi kuwajibika kutoa jibu kwa kila tofauti kubwa zinayojitokeza(Uk 44). Kwa mujibu wa waanndishi hawa, Wakristo huwa wanadhania tu kwamba, Mungu alihakikisa usahihi wa matoleo ya mwanzo tu (uk 42, pamoja na fafanuzi).

Pengine moja ya misimamo inayochanganya ya wale wanaojifanya ni waamini wa Biblia kuhusu usahihi wa maandiko, unatoka katika kitabu maarufu, ambacho hutumiwa mara nyingi na watetezi wa Ukristo, wanapotetea usahihi wa Biblia. Ujumbe Mgumu wa Biblia ni mkusanyiko  wa makala ya wasomi wanne wa Biblia wanaojulikana sana – Walter Kaiser, Peter Davids, Manfred Brauch na F. F. Bruce – ambao wanapaswa kuwa wanasaidia wanaosoma Biblia kupata majibu ya maswali magumu bila kupatanisha au kuoanisha aya za Biblia. Kwa hiyo inasumbua sana kuona mmoja wa waandishi hawa.

“Akielezea” aya ya Wakorintho wa I sura ya 10. Katika kujibu jinsi Paulo alivyohitimisha kwamba Waisraeli 23, 000, walianguka katika Agano la Kale kama matokeo ya uzinzi (1 Wakorintho 10: 8), kuliko 24,000, ambao Musa alisema katika Hesabu 25: 9 kama hesabu ya waliokufa katika pigo, Peter Davids aliandika.

Inawezekana kwamba Paulo akinukuu Agano la Kale toka kichwani, kama alivyowaandikia Wakorintho alirejea kwenye tukio la Hesabu 25: 9, lakini akili yake iliteleza ikapita sura ile, baadaye katika kukumbuka idadi ile… hatuwezi kuhukumu uwezekano wa kuwepo kwa rejea ya 23 au 23,000 katika mazingira yake alipokuwa anaandika na hiyo ikasababisha kuteleza katika kichwa chake.

Paulo hakuwa anajaribu kuwaelekeza watu juu ya historia ya Agano la Kale, na hakika sio katika vipengele vya historia ya Agano la Kale.

Hivyo tuna suala ambalo Paulo anateleza akilini mwake kwa sababu kadhaa (labda kama alikuwa na ufunuo maalum, ambao hakutujulisha), hata hivyo kosa hilo la kiakili haliathiri mafundisho. Ni mara ngapi tumewasikia wahubiri pamoja na Biblia mbele yao wakifanya makosa kama hayo ya vipengele, ambayo bila shaka yanaathiri ujumbe wao? Kama tuliona, (na baadhi yetu tumeona), huwa tuna tabasamu tu na kuangalia juu ya kile kinachozungumzwa. Kama ilivyoonyeshwa hapo juu, Paulo pengine hakuwa na Biblia yenye maandishi kuweza kuthibitisha (Ingawa wakati mwingine alikuwa na fursa ya kuwa na gombo au chuo) vya Agano la Kale. Lakini kiujumla wa mazungumzo yake alinukuu mfano toka kichwani na akakosea vipengele (uk.598, 599 pamoja na fafanuzi).

Fikiria Paulo alifanya makosa, alikosea tu kama mhubiri wa siku hizi, anaweza akanukuu vibaya aya katika maanndiko. Kwa mujibu wa   shuhuda zilizojirudia za Daudi, Paulo alikuwa tu na “kuteleza kwa akili” (na hivyo kukumbana na hicho ambacho wengine wanakiita “kupitiwa” kwa sababu ya utu uzima – senior moment) na tunachofanya sisi pamoja na wenye mashaka ni kutabasamu tu na kuangalia kile kinachozungumzwa.

Huwezi kuamini, Walter Kaiser, Peter Davids, Manfred Brauch na F.F. Bruce, waliandika kitabu cha kurasa 800 katika kujaribu kujibu kinachodhaniwa ni Biblia kujipinga na hivyo kutetea “kuaminika kwa Biblia” na bado Davids akawa na ujasiri kutoa wazo kwamba Paulo alinukuu mfano toka akilini na akakosea baadhi ya vipengele. Kwa nini duniani Davids alitumia muda mwingi (na nafasi) kujiu maswali mbalimbali, ambayo wenye mashaka waliuliza mara nyingi na akahitimisha kwamba mtu aliyeandika karibu nusu ya vitabu vya Agano Jipya alifanya makosa katika uandishi wake? Amehitimisha kile wenye mzaha wanachofundisha, – waandishi wa biblia walifanya makosa! Zaidi sana, kama Paulo alifanya kosa moja katika uandiishi wake,  tunawezaje kusema kuwa Petro, Yohana, Isaya, na wengine hawakuteleza? Kwa kweli kwa nini tusielezee tofauti zote kama matokeo ya kuteleza kwa muda kwa akili ya waandishi?

Ukweli ni kwamba kama Paulo, au yeyote katika watu hawa, alifaya makosa katika uandishi wake, basi hawakuwa wamevuviwa na Mungu (rejea 2 Timotheo 3: 16, 17; 2Petro 1: 20, 21), kwa sababu Mungu hakosei (Tito 1: 2; Zburi139: 1-6). Na kama maandiko hayakutolewa kwa uvuvio wa Mungu, basi Biblia haikutolewa kwa pumzi ya Mungu. Na Hivyo Biblia haikutoka kwa Mungu, na kama ndivyo basi wenye mashaka wako sahihi. Lakini wenye mashaka (skeptics) hawako sahihi!.Aya katika  Wakorintho I, sura ya 10: 8, inaweza kuelezewa kwa akili bila kudhani kwamba maandishi ya Paulo hayako saihi. Jibu liko katika ukweli kwamba Paulo alisema kwamba 23,000 walianguka kwa siku moja, wakati katika Hesabu 25: 9, ambayo huenda ni aya dada na hiyo ya Wakorinto, Musa aliandika kwamba jumla ya waliokufa katika pigo lile walikuwa 24, 000. Musa hakuandika ilichukua muda gani kwa watu 24,000 kufa, bali tu alionyesha idadi ya waliokufa katika pigo lile. Hivyo rekodi ya Wakorintho I, inatupa ufahamu zaidi juu ya kilichotokea katika Hesabu 25; kwamba 23, 000 kati ya 24,000 waliokufa katika pigo lile walikufa “Katika siku moja

Mbaya zaidi Peter Davids anaondoa kabisa sehemu nyingi ambazo Paulo anadai maandiko yake yametoka kwa Mungu. Paulo alipoyaandikia makanisa ya Galatia, aliwaambia kwamba mafundisho yake  yalimjia “kupitia ufunuo wa Yesu Kristo” (Galatia 1: 12). Pia katika waraka wake wa kwanza kwa Wakristo wa Thesalonike, alidai maneno aliyoandika yalikuwa ni “kwa neno la Bwana” (I Wathesalonike 4: 15). Na kwa Kanisa la Efeso, Paulo aliandika kwamba ujumbe wa Mungu “ulifunuliwa na Roho kwa mitume wake watakatifu na Manabii (Waefeso 3:5). Na waraka huo huo ambao Davids anadai “Paulo aliteleza akilini” Paulo alisema, mambo ninayowaandikia ni amri za Bwana (I Wakorintho 14: 37). Paulo hakuanzisha ukweli kuhusu simulizi za Agano la Kale, wala hakuegemea kumbukumbu zake zenye kuweza kukosea, kukumbuka majina au idadi fulani. Maandishi yake yalikuwa ni “Maandiko matakatifu (2Petro 3: 16). Roho mtakatifu alimfunulia ukweli – ukweli wote (Yohana 14: 26; Yohana 16: 13). Kama waandishi wengine wa Agano la Kale, Paulo alikuwa na uvuvio kamili wa Roho mtakatifu (2 Samweli 23; 2; Matendo 1: 16; 2 Petro 1: 20, 21; 3: 15, 16; 2 Timotheo 3: 16, 17).

UPI ULIKUWA MTAZAMO WA YESU NA WAANDISHI WA BIBLIA JUU YA MAANDIKO?

Kile ambacho wanatheolojia waliberali (walegezaji) hawawaambii wasomaji wao ni kwamba Biblia yenyewe inatoa uthibitisho wa kutosheleza juu ya hali ya uvuvio wake. Labda uhakika mkubwa ni ukweli kwamba si Yesu wala mwandishi yoyote wa Biblia, aliyethubutu kuwekea shaka hata aya moja ya maandiko. Yesu na waandishi wa Biblia waliamini katika ukweli na kuaminika kihistoria kwa hata ile sehemu yenye mashaka katika Agano la Kale. Angalia hii mifano michache;

Akiongea na Mafarisayo, katika mkoa wa Yudea, ng’ambo ya Yordani Yesu alithibitisha imani yake juu ya kuwepo kwa Wanandoa walioumbwa  katika wiki ya uumbaji (Mathayo 19: 4, rejea Mwanzo 2: 24).

Akiliandikia Kanisa la Korintho Paulo alithibitisha imani yake kwa Adamu kama binadamu wa kwanza (1 Wakorintho 15: 45). Na baadaye katika waraka wake wa kwanza kwa Timotheo alithibitisha ukweli kwamba Eva aliumbwa baada ya Adamu (1 Timotheo 2: 13 rejea Mwanzo 3).

Wote Yesu na Mtume Petro waliamini kwamba Nuhu alikuwa mtu halisi, na kwamba ile gharika ilikuwa ni tukio la ki-historia (Mathayo 24: 37-39; 2Petro 2: 5 rejea Mwanzo 6 – 8).

Yesu na Petro pia walithibitisha imani yao katika uhistoria wa Lutu na katika uharibifu wa Sodoma (Luka 17: 28-32; 2Petro 2:6,7 rejea Mwanzo 19).

Paulo alithibitisha kuvuka kwa Waisraeli bahari ya Shamu, na pia akahakikisha imani yake katika kunywa kwao maji ya mwamba (1 Wakorintho 10: 1-4 rejea Waebrania 11: 29, rejea pia Kutoka 14). Wakati Yesu alithibitisha imani yake kuponywa kimiujiza kwa Waisraeli walioangalia nyoka wa shaba aliyetundikwa na Musa huko jangwani (Yohana 3: 14 rejea Hesabu 21: 4-9).

Hatimaye, tofauti na watu wengi leo, ikiwa ni pamoja na wale wanaojifanya wanaamini Biblia kuwa neno la Mungu lililovuviwa, Yesu aliihesabu habari ya siku tatu mchana na usiku za Yona katika tumbo la samaki kama tukio la kihistoria (Mathayo 12: 39, 40).

Mifano mingine kama hii ipo, na inaelezea kuaminika kwa maandiko. Waandishi wa Agano la Kale waliokuja baada ya Musa walielezea imani kamili katika vitabu vya Musa na pia katika maandiko ya kila mmoja wao. Na zaidi pia Yesu na waandishi wa Agano jipya, mara kwa mara waliziona kauli za kila mmoja wao pamoja na waandishi wa Agano la Kale kama ukweli, bila kujali, somo husika.

Ingawa leo sio kawaida kwa mwandishi wa kidini kuchukua suala na mwingine, hata kama wanachangia mtazamo wa kidini au wanachama wa kundi moja la imani. Waandishi wa Biblia hawakupinga maanndiko ya kila mmoja wao, hata pale ilipotegemewa hivyo. Kwa mfano Paulo alimkemea Petro waziwazi kwa unafiki (Wagalatia 2: 11…). Na bado Petro hakulipiza kisasi kwa kupinga au kudharau maanndiko ya Paulo. Kiukweli, kama tulivyoona mwanzo Petro alisema kwamba maandiko ya Paulo yalikuwa na mamlaka kama “mandiko mengine” (2 Petro 3: 15, 16). Kwa nyongeza, katika kutetea haki ya Maaskofu (Wazee) kupokea malipo kutoka mfuko wa Kanisa kwa kazi yao, Paulo alinukuu Kumbukumbu 25: 4 na Luka 10: 7 na akaelezea vyote kama “maandiko” (1 Timotheo 5: 18). Ni wazi kwamba waandishi wa Biblia mara kwa mara walichukulia kazi ya kila mmoja wao kuwa ya kweli. Inakuwaje mtu yeyote anayedai kuwa Mkristo, kushikilia mtazamo kwamba maandiko yana makosa? Yesu na waandishi wa Biblia mara kwa mara walikiri kwamba Mungu alihakikisha usahihi wa toleo la mwanzo (Cukrowski na wenzake 2002 uk 42), kwa nini sisi tuwe tofauti?

USAHIHI KWENYE “T”

Yesu aliliunga mkono Agano la Kale angalau kama mara 12 akitumia neno kama, Maandiko (Yohana 5: 39); Torati (Yohana 10: 34); Torati na Manabii (Mathayo 5: 17); Torati, Manabii na Zaburi (Luka 24: 44); au Musa na Manabii (Luka 16: 29). Kwa nyongeza mwana wa Mungu alinukuu, alirejea na au alitaja matukio karibu katika vitabu tofauti 18 vya Agano la Kale. Lakini ni kwa kiwango gani Kristo aliamini katika uvuvio? Nyaraka zifuatazo zimerejewa pasipo shaka kwamba Bwana alithibitisha uvuvio wa maneno kwa kila herufi ya maandiko. Katika Mathayo 5: 17, 18, Kristo alisema;

Msidhani ya kuwa nilikuja kutangua Torati au Manabii, la, sikuja kutangua, bali kutimiliza. Kwa maana amini nawaambia, mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya Torati haitaondoka, hata yote yatimie.

Yodi (jot) ilikuwa ni herufi ndogo kabisa ya Kiebrania, na nukta (tittle) ilikuwa mkato mdogu juu ya baadhi ya herufi za Kiebrania. Ni sawasawa na kusema kwamba hata ka “nukta” kwenye “i” au ka-mkato kwenye “t” vitabakia, havitabadilika. Yesu alipotumia kauli hizi kama mifano, alithibitisha usahihi hata wa kale ka-sehemu kadogo katika Agano la Kale.

Katika Yohana 10: 34, 35, Yesu alijihusisha katika kubadilishana pamoja na Wayahudi waliomtuhumu kwa kujifanya Mungu. Alikwepa tuhuma zile kwa kunukuu Zaburi 82: 6, akirejea aya ile kama “sheria”. Yesu alirejea kwenye Zaburi kama “Sheria” kwa fikra kwamba Zaburi ni sehemu ya maandiko matakatifu. Kwa hiyo Yesu alikuwa akiyapa mamlaka maandiko yote. Alifanya kitu kama hicho, katika Yohana 15: 25. Vilevile Mtume Paulo alinukuu kutoka katika Zaburi, Isaya, na Ufunuo na akarejea kwa kila moja kama ni “Sheria” (1 Wakorintho 14: 21; Warumi3: 19; Wagalatia 4: 21). Baada ya Yesu kunukuu katika Zaburi na kuiita “sheria”, aliongeza kwa kusema “na maandiko hayawezi kutanguliwa”. Ni azimio kubwa kiasi gani! Angalia kwamba Kristo alilinganisha “Sheria” na “Maandiko” – akiyatumia maneno hayo, kila moja mahali pa jingine (yana maana moja), alipoweka wazi kwamba, “Torati” au “Maandiko” haviwezi kutanguliwa, alikuwa akitilia mkazo kwamba haiwezekani maandiko kupuuzwa, kwa mamlaka yake kukataliwa au ukweli wake kuondolewa (Angalia Warfield, 1970 uk 138 – 140). “Nguvu yake haiwezi kuondolewa kwa kuonyesha kuwa ina makosa” (Morris 1995 uk 468).

Yesu alinukuu aya isiyojulikana katika Agano la Kale, na akaithibitisha kuwa na mamlaka, kwa sababu “Maandiko hayaweza kutanguliwa” Wasikilizaji wake wa Kiyahudi walielewa ukweli huu. Kama walikuwa na fikra kwamba walegezaji (liberals) wengi leo, wanaweza wakawa wameitoa aya hii pembeni, kwa kusema kwamba Mwandishi wa Zaburi alikosea, au kwamba kipande hiki cha maandiko, kina makosa. Wangejibu kwa kumuuliza Yesu, unajuaje kama kipande hiki cha maandiko ni cha kweli, kama mengine sio kweli? Angalia kwamba, ingawa hili halikuwa jibu lao. Wote Yesu na hadhira yake walielewa kwamba Zaburi ambamo ndimo alinukuu ilikuwa ni ya kweli – kwa sababu ni sehemu ya Maandiko matakatifu. Kiukweli Yesu alichukulia kila sehemu ya maandiko, hata ile kauli ya chini kuwa ni neno la Mungu lenye mamlaka.

Muda fulani Yesu alipowauliza Mafarisayo kuelezea Masihi ni nani, (Mathayo 22: 41-45), aliangalia matumizi ya Daudi ya neno moja “Bwana” katika Zaburi 110: 1, aliwauliza Mafarisayo akisema”kama Daudi anamwita Bwana, anakuwaje tena awe mwanaye? (Mathayo 22: 45). Pointi nzima ya Yesu ilitegemea uvuvio wa maneno au wa mdomo.

Baada ya Yesu kufufuka, Luka alirekodi jinsi Yesu alivyotokea kwa watu wawili, wakisafiri kwenda Emaus waliokuwa wameshtushwa na kushangazwa na kusulubiwa hivi karibuni kwa mtu mmoja ambaye walikuwa wakimtegemea “atawakomboa Israeli” (Luka 24: 21), macho yao yakiwa yamefumbwa “ili kwamba wasiweze kumtambua” walimwambia Yesu yaliyotokea  siku chache zilizopita juu ya kifo chake, na maziko na sasa kaburi wazi. Andiko linaonyesha kwamba Yesu aliwakemea hawa watu wawili, akisema, Enyi msiofahamu, na wenye mioyo mizito kuamini, yote waliyosema Manabii! Je haikumpasa Kristo kupata mateso haya na kuingia katika utukufu wake? (Luka 24: 25, 26 pamoja na fafanuzi). Angalia kwamba Yesu hakuwashutumu kwa kuwa wazito kuamini baadhi ya yaliyosemwa na Manabii, bali aliwashutumu kwa kutoamini yote waliyosema kuhusu Kristo. Kwa sababu hii Yesu akaanza kutoka kwa Musa na Manabii wote, akawaeleza katika maanndiko yote, mambo yaliyomhusu yeye mwenyewe (Luka 24: 27).

Haishangazi kwamba Yesu angewakemea wapinzani wake wa kiimani, kwa kauli kama hizo, “hamkusoma hata andiko hili?” (Marko 12: 10, rejea Mathayo 21: 42); “Mwapotea kwa kuwa hayajui maandiko wala uweza wa Mungu” (Mathayo 22: 29); au “Lakini nendeni mkajifunze maana yake maneno haya” (Mathayo 9: 13); Wazo la msingi katika kauli zote hizi ni kwamba “ukweli wa Mungu uko katika maandiko, na kama wewe hujui maandiko, una uwezekano wa kukosa”

UTHIBITISHO HASA, KWAMBA UVUVIO UNAMAANISHA USAHIHI.

Katikati ya mazungumzo yake na Masadukayo kuhusu kukataa kwao ufufuo wa wafu (Mathayo 22: 23-33), Yesu alirejea Kutoka 3: 6, ambamo Mungu alimwambia Musa, “Mimi ni Mungu wa Ibrahimu, na Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo” Yehova aliposema maneno haya, Ibrahimu alishakufa karibu miaka 400 nyuma, lakini Bwana bado anasema “Mimi ni Mungu wa Ibrahimu” kama Yesu alivyoonyesha kwa usahihi kwa Mafarisayo “Mungu si Mungu wa waliokufa bali wa walio hai” (Mathayo22: 32). Hivyo Ibrahimu, Isaka na Yakobo, watakuwa wanaishi, wako hai. Lakini njia pekee ya wao kuwa hai ni kama roho iliendelea kuishi licha ya miili yao kufa. Aina hii ya nafsi kuwepo inamaanisha ufufuo ujao wa mwili – pointi ile ile ambayo Kristo alikazia. Kinachofurahisha hata hivi ni ukweli kwamba, mazungumzo yake yote yalisimamia kwenye wakati wa tendo! Angalia;  madai kwamba Yesu alijenga hoja juu ya hata wakati wa tendo ni kweli. Hata hivi kauli kama hiyo inahitaji maelezo zaidi, Kiebrania hakina, wakati uliopita, uliopo wala ujao, badala yake tendo linachukuliwa kama lililokamilika au lisilokamilika. Na hivyo tendo hutokea katika Kiebrania kama lililokamilika au lisilokamilika. Hakuna tendo linalotokea katika kauli ya Mungu Kutoka 3: 6. Kufuatia hilo, wakati unamaanishwa na sio kuonyeshwa. Katika hali hii, kiebrania kinaruhusu wakati wowote wa neno “kuwa”. Yesu hata hivyo alielezea mchanganyiko uliomo katika aya ile kwa kuthibitisha hasa nini Mungu alichomaanisha, ambacho ndicho sababu ya Mathayo kutunza matumizi ya Yesu ya wakati uliopo katika Kigiriki(ego eimi).

Wakati huo huo, katika tukio jingine, akiwa anajaribiwa na kundi la Wayahudi juu ya kama amemuona baba yao Ibrahimu au la, Yesu alijibu kwa kusema “Amini, amini nawaambia, yeye Ibrahimu asijakuwapo, mimi nipo” (Yohana 8: 58 pamoja na fafanuzi). Kama katika wakati ambapo Mungu alitaka Musa kuishawishi Misri juu ya asili yake ya milele, akijiita “mimi ndimi” (I am who I am). – (Kutoka 3: 14). Kristo aliwaza kushawishi wayahudi wa karne ya kwanza, juu ya umilele wake. Yesu sio “aliyekuwa” au “atakayekuwa” yeye ndiye, tangu milele na milele (Zaburi 90: 2). Mara nyingine tena aliweka hoja yake katika wakati wa tendo.

Aina ile ile ya kutegemea neno moja, inaonyeshwa na Paulo (kama alivyorejea Mwanzo 22: 18) katika Wagalatia 3: 16, “Basi ahadi zilinenwa kwa Ibrahimu na kwa mzao wake, hasemi kwa wazao kana kwamba ni wengi, bali kana kwamba ni mmoja, kwa mzao wako yaani Kristo” (pamoja na fafanuzi). Nguvu ya hoja yake ilielemea kwenye idadi ya jina (umoja na sio wingi)

Katika ukweli kwamba Yesu na waandishi wa Biblia wanayatazama maneno ya maanndiko kama yamevuviwa (na ndio ukweli), mpaka chini kwenye wakati wa tendo na idadi ya majina, ndivyo inavyotakiwa kwa Wakristo wote. Kweli kama alivyoandika mtunga Zaburi, “Jumla ya neno lako ni kweli, na kila hukumu ya haki yako ni ya milele” (Zaburi 119: 60 ASV). Au kama aya inavyotafasiriwa katika toleo la NKJV “ Jumla kabisa ya maneno yako ni kweli”, yote ni kweli, na yote yanatoka kwa Mungu, yako sahihi katika sehemu zote. Biblia nzima ina asili ya Mungu na kwa hiyo ina aminika na kutegemewa. Naam, Mungu aliwatumia watu kuandika Biblia, na kwa kufanya hivyo aliwaruhusu kuweka alama zao humo (Mfano; aina ya lugha, hofu inayoonyeshwa, maombi yanayotolewa, mapenzi binafsi, hamasa ya kielimu etc). Lakini waliandika pasipo kufanya makosa ya kawaida, ambayo watu wengine wanaweza kuyafanya katika mazingira ya kawaida. Mungu alihakikisha kwamba maneno yatakayotolewa na waandishi-wanadamu aliowavuvia hayatakuwa na makosa, wala kasoro, ambazo ni sifa za waandishi wasiovuviwa. Kihalisia, mamia ya aya za Biblia, zinawahimiza watu wa Mungu kuamini maandiko kabisa, lakini hakuna aya inayohamasisha mashaka au kukosa imani katika maandiko. Kutegemea usahihi wa kila kipengele cha historia kilichothibitishwa katika Maandiko ni kufuata mafundisho na matendo ya waandishi wa Biblia wenyewe.

MAANDIKO YANAPOSEMA, MUNGU AMESEMA.

Kwa mara nyingine tena, Yesu na waandishi wa Biblia wanathibitisha kwamba, “Mungu ndiye chanzo cha maandiko” Angalia katika Mathayo 19: 4-6, Jinsi Yesu alivyoelezea maneno ya Mwanzo 2: 24  kama Mungu ndiye chanzo cha hayo maneno. Aliwauliza Mafarisayo waliokuja kumjaribu “hamkusoma kwamba aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mwanamke na mwanamume na akasema “Kwa sababu hii mwanamume atamwacha baba yake na mama yake, naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja. Inafurahisha zaidi kwamba katika Mwanzo 2: 24 hakuna, ishara inayoonyesha kwamba Mungu ndiye aliyekuwa anaongea badala yake maneno kama maoni tu yaliyoandikwa na mwandishi-mwanadamu Musa. Kwa kule Yesu kuyaita maneno ya Mungu, aliweka wazi kwamba Maandiko Matakatifu yote, yametoka kwa Mungu (2 Timotheo 3: 16). Akiwaandikia Wakristo wa Korintho, Paulo aliichukulia mada hii katika hali ile ile (1 Wakorinto 6: 16).

Katika matukio kadhaa katika maandiko, Mungu alisema, kusema vitu kadhaa ambavyo viko katika hali yake ya awali, maneno ya maandiko tu.  Kwa Mfano; Waebrania 3: 7 inasoma; “Kwa hiyo kama  anenavyo Roho Mtakatifu…” na tena Zaburi 95: 7, imenukuliwa. Katika Matendo 4: 25, Mungu inasemekana aliongea kwa Roho Mtakatifu kupitia kinywa cha Daudi, maneno ya Zaburi 2: 1. Katika Matendo 13: 34, Mungu amewakilishwa kama aliongea maneno ya  Isaya 55: 3 na Zaburi 16: 10. Katika kila moja ya mambo haya, maneno yanayoonekana ni ya Mungu sio ya kwake hasa, katika uasili wake, ila ni maneno tu ya maandiko yenyewe. Waandishi wa Agano Jipya wakati mwingine walirejea Maandiko kama yalikuwa Mungu (Warumi (9: 17; Wagalatia 3: 8); na wakati mwingine walimrejea Mungu kama vile alikuwa ni maandiko. Biblia kwa hiyo inajionyesha yenyewe kama maneno ya Mungu hasa.

Katika Waebrania 1: 5-13, mwandishi alinukuu, kutoka Zaburi 2: 7, 2 Samweli 7: 14, Kumbukumbu 32: 43, Zaburi 104: 4, Zaburi 45: 6-7 Zaburi 102: 25-27 na Zaburi 110: 1. Mwandishi wa Waebrania alisema kila moja ya aya hizi, msemaji ni Mungu. Na bado katika hali yake ya awali katika Agano la Kale, wakati mwingine Mungu ndiye msemaji wake, na wakati mwingine yeye sio msemaji, na kiukweli yeye ndiye anayezungumwa au anayeambiwa. Kwa nini mwandishi wa Waebrania amekurupuka tu na kumpa Mungu aya  hizi? Ni kwa sababu zote zinafanana kwa ukweli kwamba ni maneno ya maandiko, na kwa njia hiyo ni maneno ya Mungu. Hivyo kila neno la Biblia, ni neno la Mungu! Na kama Yesu alivyoomba usiku ule wa kusalitiwa kwake, “neno la Mungu ndiyo kweli” (Yohana 17: 17)

MUNGU HAWEZI KUSEMA UONGO

Tangu mwanzo mpaka mwisho, Biblia inaweka wazi kwamba, huyu wa milele na asiye na mwisho, aliyeumba kila kitu na kila kitu vilivyopo ulimwenguni (tukimuacha Yeye mwenyewe), ni kweli. “Roho ndiye kweli” (1 Yohana 5: 7), maneno yake ni kweli (2 Samweli 7: 28), Sheria yake ni ya kweli (Zaburi 119: 14), Amri zake ni kweli (Zaburi 119: 151), hukumu zake ni za kweli (Zaburi 19: 9) na matendo yake ni ya kweli (Daniel 4: 37). Kwa kawaida amejivika ukweli. Mwana wa Mungu alipokuwa duniani alidai kuwa kweli (Yohana 14: 6). Hakuna kitu uongo kwa Mungu. Paulo alipomwaandikia Tito, alimuelezea Mungu kama ambaye “hawezi kusema uongo” (Tito 1: 2), vile vile mwandishi wa Waebrania aliweka wazi kwamba “Haiwezekani kwa Mungu kusema Uongo” (Waebrania 6: 18).

Kama Mungu ni mkamilifu, na kama Biblia ni neno la Mungu (ambavyo inadai kuwa, kama kipengele kilichopita kinavyoelezea), basi inafuatia kwamba, katika hali yake ya asili, kama ilivyotoka kwa Mungu, Biblia lazima itakuwa imekamilika. Maandiko hayawezi kukosea kama yametokana na Mungu. Jaribu kadiri mtu anavyoweza, kwa akili Kabisa mtu hawezi kuwa navyo vyote; yaani Biblia; ama imetoka kwa Mungu (na hivyo haina makosa katika hali yake ya mwanzo), au ina makosa na hivyo haikutoka kwa Mungu wa kweli. Huwezi kuwa katikati ya haya mawili.

Baadhi wanabisha “Lakini Biblia iliandikwa na binadamu. Na kukosea ni ubinadamu; hivyo Biblia isingekuwa kamili kabisa tangu mwanzo” Zingatia uwongo wa kufikiria hivyo. Kama mtu atahitimisha kwamba watu wote wanakosea – bila kujali mazingira – Basi Yesu lazima alifanya dhambi. (1) Yesu alikuwa ni binadamu (Wagalatia 4: 4). (2) Wanadamu wanafanya dhambi (Isaya 53; 6). (3) Kwa hiyo Yesu alifanya dhambi. Lakini wanafunzi wa Biblia walio wengi, wanajua kwamba Yesu hakufanya dhambi. Agano Jipya linasema kwamba alikuwa “Safi” na “Mwenye haki” (1 Yohana 3: 3; 2; 1), na “hakufanya dhambi wala hila haikuonekana kinywani mwake” (1 Petro 2: 22). Alikuwa ni kondoo asiyekuwa na ila asiyekuwa na waa (1 Petro 1: 19), “yeye asiyejua dhambi” (2 Wakorintho 5: 21). Kwa kuwa tunajua kwamba Yesu hakufanya dhambi, kitu fulani kitakuwa sio sahihi mahali, kwa hoja hiyo hapo juu. Lakini kitu hicho ni nini?

Kosa ni kudhania kwamba Yesu ni kama binadamu yeyote. Ni kweli binadamu wa kawaida anafanya dhambi. Lakini Yesu hakuwa binadamu wa kawaida, bali pia Mungu. Hali kadhalika, Biblia sio kitabu cha kibinadmu tu, pia ni neno la Mungu. Kama ilivyo kwa Yesu, kiko kote kote, kibinadamu na ki-Mungu. Na kama Yesu alivyokuwa binadamu lakini hakufanya dhambi, hivyo pia na Biblia ni kitabu cha kibinadamu lakini hakina makosa. Vyote, neno la Mungu lililo hai (Kristo), na neno lililo katika maandishi (Maandiko matakatifu) ni ya kibinadamu lakini hayana makosa. Ni ya Mungu hivyo hayawezi kuwa na makosa. Hakuwezi kuwepo makosa tena katika neno la Mungu lililoandikwa kama kusivyokuwa na dhambi katika neno la Mungu lililo hai (Kristo). Mungu hawezi kukosea, kituo (Geisler na Howe, 1992 uk 14, 15).

Tunakiri, ni kawaida kukosea. (kiukweli makala hii hii ina uwezekano wa kuwa na kosa moja au zaidi ndani yake). Lakini, mazingira ambayo kwayo waandishi wa Biblia waliandika yalikuwa ya kawaida kabisa. Waliwezeshwa na waliongozwa katika kweli yote na Roho wa Mungu (Yohana 16: 13; 2 Petro 1: 21).

SABABU ZA USAHIHI WA BIBLIA.

Bahati mbaya, ni kawaida kusikia wanatheolojia waliberali (walegezaji), na wale wanaokubaliana nao, wanawaza kwambasehemu ya kiroho ya maandiko imevuviwa, lakini sehemu zile zinazohusika na mambo ya historia, jiografia, mambo ya anga, Udaktari, na vingine vinavyofanana, hazijavuviwa. Wazo hilo linajulikana kama “Fundisho la uvuvio kwa Sehemu” (Partial Inspiration). Fundisho hilo ni makosa kwa sababu kama tatu hivi;

Kwanza; Hakuna kauli katika maandiko, inayomuongoza mtu kuamini hii namna ya kutafasiri Biblia inayokubalika. Kinyume chake, kama ilivyokwisha onyeshwa, wote Yesu na waandishi wa Biblia mara kwa mara walifanya kazi kutokea mahali ambapo Ulimwengu wa Mungu  ni kweli kabisa (Zaburi 119: 160), na sio kweli kwa sehemu.

Pili; ingekuwa kweli kwamba sehemu ya kiroho tu ya Biblia ndiyo iliyo sahihi, kila anayesoma maandiko angekuwa na wajibu binafsi wa kutembea katika makala za Biblia ili kuamua hasa ni jambo gani la kiroho (na hivyo lililovuviwa) na lipi sio la kiroho (na hivyo halijavuviwa). Tafasiri kama hiyo ya maandiko, hata hivyo inazitania mamlaka za Biblia.

Biblia inaweza kuwa na mamlaka kama, na kama tu, ni kweli na imethibitishwa kama neno la Mungu. Kwamba neno lake limepita kwa watu, haipingi mamlaka yake maadam, amewaongoza dhidi ya makosa yote. Kama mamlaka yake kwa waandishi wa Biblia haikuwa kamili, hatuwezi kuwa na uhakika kama wandishi walikuwa makini (na hivyo kuaminika) na au kama walikosea (na hivyo kustahili kukataliwa). Katika hali kama hiyo, biblia itakuwa na mamlaka pale tu tutakaposema na kuweka wazi kwamba iko hivyo. Hivyo duara limekamilika, na binadamu ana mamlaka juu ya Biblia, badala ya kuwa chini ya maelekezo ya Biblia (Shelly, 1990, uk 152).

Kama Wakristo wataacha mafundisho ya usahihi wa Biblia, basi kuwa na kipimo ambacho watu wote wataishi maisha yao kwa hicho isingewezekana. Kama mtoto anayemheshimu baba yake, pale tu anapokubaliana na mamlaka yake, Mkristo angekuwa na kipimo chake cha mamlaka kwa sababu Biblia  ingekuwa na mamlaka, kama tu ataamua iwe muongozo wa kuaminika. Kirahisi, maandiko hayawezi kuelezwa kuwa na mamlaka ya ki-Mungu, kama Biblia (tena katika toleo lake la mwanzo) lilikuwa na makosa

Mwisho, kama Mkriso anaamini kwamba Biblia ina makosa, basi mtu analazimika kukubali, hitimisho lisilokwepeka kwamba, katika matukio kadhaa, Mungu alitoa pumzi ya ukweli, na katika tukio jingine alitoa pumzi (neno) ya uongo (rejea 2 Timotheo 3: 16). Kama maandiko yote yameorodheshwa kama yametoka kwa Mungu – hata zile kauli na maoni toka kwa wasioamini – basi mashambulizi juu ya kuaminika kwa aya yoyote ni mashambulizi dhidi ya Mwenyezi Mungu. Kama Mungu anaweza kumvuvia mtu kuandika ukweli wa kitheolojia na kimafundisho, anaweza pia kumvuvia mtu huyo kuandika historia na sayansi vizuri. Kama Biblia haiaminiki na ya kweli katika dokezo lake kwenye mambo madogo madogo ya pembezoni, itawezaje kuaminika na kutegemewa kuwa ya kweli na sahihi katika mambo ya msingi? Je Mungu mwenye uwezo wote, hawezi kuhifadhi waandishi-binadamu dhidi ya kufanya kauli za uongo katika kurekodi maneno yake? Haitafanya kuonekana kwamba Biblia ilikusudiwa iwe kama kitabu cha Sayansi au Historia. Kama katika taratibu za kuingiza ajenda yake ya kiroho, Mungu alidokeza kwenye jiografia, mambo ya dunia, au udaktari, Mungu hakudanganya, wala hawezi kuruhusu mtu aliyevuviwa kusema uongo.

Swali lazima litaulizwa; kama Mungu hawezi kushikilia mambo yasiyo ya muhimu, kama vile (uelekeo wa kijografia, au majina ya watu), kwa nini mtu afikiri kwamba wanaweza kumwamini kwa mambo mengine ya muhimu sana, kama usalama wa nafsi zao za milele, na kumtegemea kuyashikilia kwa njia iliyo bora? Au tukiliangalia jambo hili tokea upande mwingine. Zingatia swali  ambalo Yesu alimuuliza Nikodemu, “Kama nimekwambia mambo ya kimwili na huamini, utaaminije nikikwambia mambo ya mbinguni? (Yohana 3: 12). Kinachomaanishwa katika kauli hii ni ukweli kwamba, Yesu angemwambia Nikodemo mambo ya duniani, yangekuwa kweli. Fikra hizo hizo zinafuatana na Biblia. Kwa sababu ni neno la Mungu, ingekuwa sahihi katika jambo lolote inaloongelea. Na zaidi kama Biblia sio ya kweli kwa mambo ya kimwili, basi haiwezi kuaminika, inapoongelea mambo ya kiroho. Kweli wazo la uvuvio kwa sehemu, inatilia shaka kuaminika na asili ya Mungu, misuguano na ushahidi wa uvuvio, na unapaswa kukataliwa kama ni upotofu.

Watu wanaamini juu juu kwamba tofauti katika Biblia zinachangia kupunguza uhalisia wa maandiko, kwa sababu nyepesi  kwamba, watu wameumbwa na Mungu kufanya kazi kimantiki. Wanatambua kwamba, kwa tafasiri, ukweli unapaswa kujiendeleza wenyewe. Asili ile ile ya ukweli ni kwamba hauna kujipinga wala makosa. Kama Mungu ana uwezo wa kuwasilisha ukweli wake kwa binadamu, basi ni vyote havifikiriki, na kiakili haina maana  kwamba hawezi kufanya kwa muendelezo kamili na uhakika. Kutokuwa na makosa bila usahihi haviwezi kuvumiliwa bila kupingana.

Ni vibaya kiasi gani kwamba jaribio la kupatanisha kuaminika kwa maandiko matakatifu pamoja, sio la lazima, kwa mtazamo wa ukweli kwamba, hakuna lawama za kutofautiana dhidi ya Biblia ambazo zimeshatolewa. Maelezo yenye makosa yapo kama mtu atasoma na kutumia mwenyewe kwa uaminifu, uchambuzi wa kina wa ushahidi uliopo. Mungu ametoa ushahidi wa kutosha kumruhusu mtu mwaminifu kuufikia ukweli na kujua mapenzi yake (Yohana 6: 45; 7:17; 8: 32;). Wale wenye nia ya kukubaliana, na wale wanaoondoka na kuacha kujitoa na kukubali uvuvio wa maneno na usahihi wa maandiko wanaonyesha ukosefu wa imani katika Mungu na katika neno lake. 

Rejea

Cukrowsky, Kenneth L, Mark W. Hamilton, and James W. Thompson (2002), God’s Holy Fire

Gallup, George Jr. and Michael Lindsay (1999), Surveying the Religious Landscape: Trends in U.S. Beliefs

Geisler, Norman and Thomas Howe (1992), When Critics Ask

Kaiser, Walter C. Jr, Peter H. Davids, F. F. Bruce, and Manfred T. Brauch (1996), Hard Saying of The Bible

Marsden, George (1987), Reforming Fundamentalism: Fuller Seminary and the New Evangelism 

Morris, Leon (1995), The Gospel Acording to John

Packer, J. I. (1958), “Fundamentalism” and the Word of God.

Preus, Robert (1984), “Notes On the Inerrancy of Scripture”

Shelly, Rubel (1990), Prepare to Answer

Warfield, Benjamin (1970 reprint), The inspiration and Authority of the Bible

Imechapishwa, June 01; 2004


Published

A copied sheet of paper

REPRODUCTION & DISCLAIMERS: We are happy to grant permission for this article to be reproduced in part or in its entirety, as long as our stipulations are observed.

Reproduction Stipulations→