Menu

Upagani: Unajipinga Sana na Unaficha Ukweli

Wapagani wengi, wale wanaosema hakuna Mungu, mara nyingi wanaelezea baadhi ya vitu kama; “vinaweza kufanyiwa utafiti”, vibaya sana, au visivyofaa.” Mpagani maarufu duniani , mwaka 1976, ambaye pia ni mwanafalsafa wa upagani, Antony Flew, alikiri kwamba, utawala wa ki-Nazi ulifanya uharibifu halisi wa kimaadili miaka ya 1930 na 1940, walipochinja Wayahudi milioni sita (Waren & Flew 1976 Uk 248). Wapagani wengi wanakiri kwamba ingekuwa kosa kimaadili, kumbaka mwanamke au kumdhalilisha ki-ngono, na kutesa mtoto wa miaka 4. Richard Dawkin, Mpagani anayeheshimika sana duniani, leo amejidai kwamba, mtu asiyeamini “Evolution” huyo ni “mwovu” (1989). Utambuzi huo wa Wapagani kwamba kitu Fulani si sahihi ki-maadili, kinaleta swali; Inawezekanaje Mpagani akakiita kitu kuuwa kibaya sana, cha kutisha, kisichofaa  kisicho na maadili? Kwa mujibu wao, sisi si chochote ila maada inayotembea, inadhaniwa kuwa tulitokana na miamba na “slim” kwa mabilioni ya miaka. Tunadhaniwa tulitokana na wanyama- vitu vyenye uhai, visivyo na hisia yoyote juu ya maadili. Wanyama wanakula watoto wao, wanaua wenza wao, na wanamuibia chakula, mnyama mwingine yoyote wanaye muweza; akiwa ni rafiki, ndugu, adui au mwanafamilia. Wapagani hao wanadai sisi ni Wanyama. Tunapenda kufikiri  kwamba tumeinuliwa juu ya viumbe wengine. Lakini mwili wa binadamu, umetokana na Wanyama (Merchant 2008, 200(2678) 44 pamoja na fafanuzi).Hivyo, ukweli ni kwamba, kama Dr Thomas B. Warren, alivyohitimisha katika mdahalo wake na Antony Flew. “Msingi wa mfumo wa wapagani hauruhusu jambo kuwa sahihi kimaadili, au kutokuwa sahihi kimaadili (1976, Uk 49).

Mwanafalsafa wa kipagni,Jean Pul Sartre, alifupisha vyema juu ya kutokuwa na Mungu pale aliposema “ Kila kitu kinaruhusiwa kabisa, kama Mungu hayupo” (1961, Uk 485 pamoja na fafanuzi). Kama wapagani wanakataa kukiri kwamba “maadili halisi yapo”, basi wanalazimika kukubali kwamba, Wayahudi walipoteswa, kuchomwa kwa gesi, na kufanyiwa majaribio “kama wanyama”, basi walikuwa ni wanyama kweli (Marchant 2008) na kwamba wale wa-Nazi hawakufanya kosa lolote. Kama maisha ya binadamu hayana maana yoyote, ni kama bakteria (kama Mpagani Eric Pianka alisema asili ndivyo inavyotaka), basi kusingekuwa na shida kiukweli kuenea virusi vya Ebola ili kuondoa 90% ya watu duniani, kitu  ambacho Dr Pianka alishauri kwamba kinahitajika kitokee, ili kuiokoa dunia (Angalia Mims, 2006). Wapagani wanaochukua kinadharia, “atheistic evolution” kwenye hitimisho lake hasa, wanalazimika kukiri kile Dan Barker alichosema katika mdahalo na Kyle Butt, mwezi Februari 2009, kwamba kama ni lazima  anaweza kubaka mamilioni ya wasichana, ili kuokoa watu wengine (Butt & Barker 2009, Uk 33-36). Hata hivyo, kama sisi si chochote, ila Sokwe-Mtu aliyestaarabika, na “babu zetu, wamekuwa wazazi kwa kiasi tu, sababu walitumia kubaka” basi kama mwana mageuzi Randy Thornhill alikiri kwamba “kubaka ni jambo la ki-mageuzi, la kibaolojia na la asili” (2001, akinukuu Thornhill & Palmer, 2000) – Wazo linalokasirisha na kuudhi.

Mpagani anaweza kusema, “hatupendi kile” au “hatutathubutu kufanya kile”, lakini hawawezi kusema kwa dhati kwamba, jambo hili halifai au linafaa, au kwamba ni kosa au si kosa. Na kama watasema wanatoa kauli inayojipinga. Watakuwa wanapinga ile “asili.” Kama watakiri kwamba kwa wapagni, hakuna kipimio cha “wema” na “Uovu” kinachoweza kuwepo, basi kubaka pia kunaweza kuwa sahihi, na jambo jema kama hekima likawa baya. Vyovyote vile Upagani unapotea. Ama unapingana na kujipinga wenyewe, au ni mbaya na wakutisha, kwa kiwango cha kupuuzwa au kudharauliwa.

“Mpumbavu amesema moyoni, hakuna Mungu; Wameharibu matendo yao na kuyafanya chukizo, Hakuna atendaye mema” (Zaburi 14: 1).

Rejea

Butt, Kyle and Dan Baker (2009), The Butt/Baker Debate: Does God of The Bible Exist?

Dawkins, Richard (1989), “Book Review”

Marchant, Jo (2008), “We should Act Like the Animals We Are”

Mims, Forrest (2006), “Dealing With Doctor Doom”

Sartre, Jean Paul, (1961), “Exisistantialism and Humanism”

Thornhill, Randy (2001), “A Natural History of Rape”

Thornhill, Randy  and Craig T. Palmer (2000), A Natural History of Rape

Warren, Thomas B. and Antony Flew (1976), The Warren – Flew Debate


Published

A copied sheet of paper

REPRODUCTION & DISCLAIMERS: We are happy to grant permission for this article to be reproduced in part or in its entirety, as long as our stipulations are observed.

Reproduction Stipulations→