Umri Unaoonekana
Dunia ina umri gani? Hakuna anayejua idadi kamili ya mara ngapi dunia hii imeizunguka jua. Lakini kwa kutumia kronolojia ya kibiblia mtu anaweza kuhesabu umri wa dunia kuwa katika ujirani wa miaka 6,000.
“Lakini Dunia inaonekana kuwa na mamilioni ya miaka,” watu wengine watapinga. Kuna angalau majibu mawili kwa taarifa kama hiyo. Kwanza mtu anaweza kuuliza: Ikilinganishwa na nini; Dunia changa inaonekanaje?” Hatuna dunia nyingine ambayo tunajua ni changa kuliko hii, kwahiyo tungejuaje jinsi dunia changa inavyofanania. Pili, haipasi kutushangaza ikiwa sayansi huhesabu tarehe za zamani za dunia mara kwa mara, kwasababu ya dhana inayojulikana kama “fundisho la umri dhahiri.”
Wazo hili linapendekeza kwamba vitu ambavyo Mungu alivifanya wakati wa juma la Uumbaji viliundwa kikamilifu na kufanya kazi kikamilifu. Kwa mfano Adamu na Hawa alikuwa na umri gani sekunde mbili baada ya Mungu kuwaumba? Walikuwa na sekunde mbili! Hata hivyo walitembea, walizungumza na walionekana kama wanadamu wazima, na hata walikuwa na uwezo wa kuzaa (ambayo ilikuwa ni mojawapo ya amri ambazo Mungu aliwapa- Mwanzo 1:28). Ikiwa mti ungekatwa katika Bustani ya Edeni siku moja baada ya Juma la Uumbaji ungekuwa na pete ngapi? Inawezekana mamia, lakini ingekuwa na umri wa siku tano tu (miti na mimea mingine, kumbuka iliundwa siku ya tatu ya Juma la Uumbaji). Kwa hiyo umri halisi wa mti huo na umri unaoonekana wa mti ungekuwa tofauti kabisa. Kwa sababu tu dunia hii inavyo weza kuonekana ikiwa ya zaidi ya miaka 6000, hiyo haimaanishi ni zamani kuzidi hiyo.
Baadhi ya watu wamependekeza kwamba ikiwa Mungu aliifanya Dunia ionekane kuwa ya zamani zaidi kuliko ilivyo kweli, basi ametudanganya kwa sababu mambo si ya kale jinsi yanavyo onekana. Ukosoaji huu hauwezi kuwa wa kweli kwa kuwa Mungu alituambia Alicho fanya! Hakutuacha gizani au kujaribu “kutudanganya” au “kujaribu Imani yetu” kwa kutuficha habari muhimu ambazo tungehitaji. Badala yake, Alikuwa mnyoofu sana na mwaminifu kwetu. Kwa kuzingatia nyenzo zinazo patikana katika sura kumi na moja za kwanza za Mwanzo (na mahali pengine kupitia biblia), hakuna mtu anayeweza kumshtaki Mungu kwa sababu ya udanganyifu. Tukipuuza neno lake kuhusu yale aliyosema alifanya, je ni kosa la Mungu? Vigumu!
Ilichapishwa 31-Desemba-2000
UZALISHAJI NA KANUSHO: Tuna furaha kutoa ruhusa ili Makala haya yanakilishwe kwa sehemu au kwa ukamilifu, mradi tu masharti yetu yatazingatiwa. Masharti ya uzalishaji.
REPRODUCTION & DISCLAIMERS: We are happy to grant permission for this article to be reproduced in part or in its entirety, as long as our stipulations are observed.