Ubatizo na Kuzaliwa Upya
Mgawanyiko mkubwa ndani ya jumuia ya wakristo unahusu mahali ambapo “kuzaliwa upya” hutokea. Wengi wa jumuia ya wakristo hushikilia kwamba mtu huzaliwa mara ya pili, na hivyo dhambi imeoshwa na damu ya Kristo, mtu huyo anampokubali Yesu Kristo kuwa mwokozi wake. Kwa usemi huu ina maana kwamba mtu lazima kiakili au aamue kwa kinywa kumkubali Kristo kama Bwana wa maisha yake. Kwa hiyo kuzaliwa upya huonekana kuwa uamuzi wa mapenzi wakati Fulani ambapo mtu anamkubali kristo Akilini mwake na kuunganisha uamuzi huo kwa kuungama kwa mdomo. Kifungu katika agano Jipya ambacho kinarejelea haswa kuzaliwa mara ya pili kinahusu mazungumzo ambayo Yesu alikuwa nayo na ofisa wa cheo cha juu wa Kiyahudi.
“Basi palikuwa na mtu mmoja wa Mafarisayo, jina lake Nikodemo, mkuu wa Wayahudi. Huyo alimjia usiku, akamwambia, Rabi, twajua ya kuwa u mwalimu, umetoka kwa Mungu; kwa maana hakuna mtu awezaye kuzifanya ishara hizi uzifanyazo wewe, isipokuwa Mungu yu pamoja naye. Yesu akamjibu akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu. Nikodemu akamwambia, awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mammaye mara ya pili akazaliwa? Yesu akkajibu, Amin, amin, nakuambia, mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuingia ufalme wa Mungu. Kilicho zaliwa kwa mwili ni mwili; na kilicho zaliwa kwa Roho ni roho. Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, Hamna budi kuzaliwa mara ya pili (Yohana 3:1-7).
Katika jitihada za kuepuka kutambua maji (mstari wa 5) kuwa ubatizo wa maji, wengi katika jumuiya ya wakristo katika nusu karne iliyopita wamependekeza fasiri mbalimbali mpya. Kwa mfano, wengi wamependekeza kwamba “maji” ni kumbukumbu ya Roho mtakatifu. Ingawa ni kweli kwamba Yohana anatumia neno “maji” kwa njia ya mfano kuwakilisha Roho baadaye katika kitabu chake (7:38-39), ukweli huo ulipaswa kufafanuliwa na mwandishi aliye vuviwa. Hata hivyo katika sura ya tatu, maana ya kawaida, halisi inaonekana wazi, sit u kwasababu ubatizo wa maji katika Agano Jipya lote unahusishwa na tukio la wokovu kama (Matendo ya Mitume 2:38; 8:12-13, 36-38; 9:18; Wagalatia 10:27; 1 Petro 3:21), lakini hata katika muktadha huu, aya kumi na nane baadaye, neno hilo kwa uwazi lina maana halisi: “Yohana naye (Yohana 3:23). Zaidi ya hayo ikiwa “maji” katika (Yohana 3:5) ni dokezo kwa Roho Mtakatifu, matokeo yatakuwa yasiyo na maana: “mtu asipozaliwa kwa maji na Roho.”
Hoja nyingine inayotolewa ili kuepuka maana iliyo wazi ya Yohana 3;5 ni kwamba “maji” ni mfano wa damu ya Yesu. Kwa kweli, hakuna mantiki ya kufanya muunganisho kama huo. Maana pengine Yohana anarejelea waziwazi maji na damu, lakini anazozitofautisha kwa uwazi katika umuhimu wake (1 Yohana 5:6).
Labda dhana maarufu zaidi, iliyoendelea tu katika miaka ya hivi karibuni, ni kwamba “maji” ni kumbukumbu ya maji ya mwanamke mjamzito yaani maji ya amniotic ambayo yanaambatana na kuzaliwa kwa motto kimwili. Hata hivyo, pendekezo hili pia halipatani na muktadha wa maneno ya Yesu. Kwa kweli Nikodemo mwenyewe alifikiri kwamba Yesu alikuwa akimaanisha kuzaliwa kimwili (tumbo la uzazi la mama). Lakini Yesu alirekebisha maoni yake yasiyofaa, na akatofautisha mawazo hayo na maana iliyo kusudiwa ya “maji na Roho.” Kwakweli Yesu hangemwambia Nikodemo kwamba alihitaji kuzaliwa kimwili. Asinge jumuisha tendo la kuzaliwa kimwili katika orodha Yake ya masharti ya kuingia katika ufalme. Hilo lingemfanya Yesu aseme kwamba kabla mtu hajaingia katika ufalme lazima awe mtu kwanza! Kungekuwa na maana gani ya kusema kitu kama hicho? (Je, pengine ingekuwa kuhakikisha kwamba kila mtu anaelewa kwamba wasio wanadamu (Yaani, wanyama) hawawezi kuingia katika ufalme?). Baadaye katika sura hiyo hiyo, je, Yohana alibatiza karibu na Salimu “kwa sababu palikuwa na maji mengi ya pale”?
Ikiwa mtu anajali kuchunguza sehemu nyingine ya Agano Jipya ili kuruhusu Biblia kuwa mfasiri wake bora zaidi, na ili kuruhusu biblia kupatana nayo yenyewe, vifungu vya ziada vinatoa mwanga juu ya maana ya (Yohana 3:5). Kulingana na sehemu nyingine ya Agano Jipya dhana ya kiroho inatokea wakati injili (yaani mbegu ya Roho Mtakatifu-Luka 8:11) inapandikizwa katika moyo na akili ya mwanadamu (Yakobo 1:18; 1 Wakorintho 4:15; Waefeso 6:17; 1 Petro 1:23). Neno la Mungu, kwa upande wake, huzalisha Imani yenye toba ndani ya moyo wa mwanadamu (Warumi 10:17) ambayo inaongoza mtu kutii Injili kwa kubatizwa kwenye maji (Marko 16:16; Matendo 2:38; Waebrania 10:22). Hali ya matokeo ya mtu binafsi ni kwamba yeye sasa ni mtoto wa Mungu, raia wa ufalme, na mshiriki wa Kanisa la Kristo (Mathayo 28:19-20; Wagalatia 3:26-27; Warumi 6:4).
Mistari ya ziada katika agano Jipya inafafanua na kusisitiza maana hii ya Yohana 3:5, ikionyesha “kuzaliwa upya,” huku ikituruhusu kuelewa utendaji wa Roho Mtakatifu katika tendo la kuongoka.
Fikiria chati ifuatayo (Jackson, 1988).
| Yohana 3:5 | Roho | Maji | Ufalme |
| 1 Wakorintho 12:13 | Roho | Kubatizwa | Mwili |
| Waefeso 5:26 | Neno | Kuoshwa/maji | Kanisa lililotakaswa |
| Tito 3:5 | Upya wa roho | Kuoshwa kwa kuzaliwa upya | Kuokolewa kwa neema |
Mistari hii inaonyesha kwamba Mungu anafanikisha uongofu kupitia ujumbe wa Injili ulio andikwa na Roho Mtakatifu. Wakati mtu anapofikia ufahamu (Matendo 8:30) wa ujumbe huo uliovuviwa, Imani yake yeye kutubu inampelekea kuzamishwa kwenye maji kwa ajili ya ondoleo la dhambi (Matendo 8:36,38; 10;47). Matokeo ya jibu lake la utii kwa injili ni kwamba ameokolewa na kusafishwa kutoka kwa dhambi ya zamani na kuwekwa mara moja katika ufalme wa Kristo.
Tambua kwamba kunyenyekea kwa mpango mtakatifu wa wokovu haimaanishi kwamba wanadamu wanajiokoa wenyewe kwa kutekeleza wokovu wao wenyewe. Utiifu wao haupati wala haustahili msamaha wao. Badala yake masharti ya wokovu yamebainishwa na Mungu-si wanadamu-na ni onyesho la rehema zake! Wakati watu wanajisalimisha kwa masharti ya kuingia katika ufalme wa Kristo, wanaokolewa kwa damu ya yesu na neema ya Mungu-siyo juhudi zao wenyewe! Kuzamishwa kwenye maji hakupaswi kuzingatiwa kama “kazi ya haki ambayo tumeifanya” (Tito 3:5). Tunapojisalimisha kwa ubatizo, tunaokolewa kwa “fadhili na upendo wa Mungu mwokozi wetu” (Tito 3:5). Tunaokolewa kulingana na rehema zake” (Tito 3:5).
MAREJEO
Jackson Wayne (1988), “The New Birth: What is it?” Christian Courier, 24:14, Agosti.
UZALISHAJI NA KANUSHO: Tunafuraha kutoa ruhusa ili Makala haya yanakilishwe kwa sehemu au kwa ukamilifu, mradi tu masharti yetu yatazingatiwa.
Masharti ya uzalishaji.
REPRODUCTION & DISCLAIMERS: We are happy to grant permission for this article to be reproduced in part or in its entirety, as long as our stipulations are observed.