Menu

Tunaweza Kuthibitisha Kama Yesu Alikuwa Mtu Halisi?

Unaweza ukaona hili ni la kushangaza, lakini kuna watu wengi duniani leo, ambao hudhani kwamba Yesu sio kitu chochote zaidi ya kitu cha maigizo, ambacho makundi ya siri yalikitengeneza miaka 2,000 iliyopita. Inahisiwa, Jina lake linatoka katika maandiko hayo hayo ya kutunga ambayo yanajumuisha simulizi za kutunga, za kutisha, (Magic stries) zikijumuisha wahusika kama Peter Pan, Hercules, na Snow White na Seven dwarfs. Gerald Massey, katika kitabu chake, Gnostic and Historic Christianity, ametutaarifu kwamba “Ikiwa tutamchukulia kama  mtu aliyetengenezwa na Mungu, au kama Mungu aliyefanywa mtu, huyu mhusika, yaani Yesu, hakuwahi kuwepo kama binadamu”  (1985 uk 22). Wenye mashaka (skeptis) kama Massey, Acharya (1999), na wengine wanaamini kwamba Wakristo wamedanganywa kwa kufikiri kwamba aliwahi kuishi mtu kwa jina la Yesu, wakati kiukweli hakuwahi kuishi.

Ni vipi hao, miongoni mwetu wanaoamini katika uhistoria wa Yesu Kristo watakavyoyachukulia madai hayo? Tunaweza kufahamu kweli kwamba kulikuwa na  mtu asiye na dhambi, mtenda miujiza, mpinga-kifo, mwenye jina la  Yesu, aliyeishi hapa duniani, takriban miaka 2,000 iliyopita, au tumekubali uwepo wake ki-upofu upofu tu?

Ingawa Agano Jipya linahakikisha pasipo shaka kwamba Yesu kimsingi aliishi, huo ndio ushahidi pekee wa kihistoria uliopo. Kwenye miaka ya 94 BK, mwanahistoria wa Kiyahudi kwa jina la Yosefu, alitaja jina la Yesu mara mbili katika kitabu chake “Antiquities of the Jews”, katika kipengele cha 18 cha kazi hiyo, huyu Josefu aliandika “Na alitokea wakati kama huu, Yesu, mtu mwenye hekima, kama kweli tunaweza kumwita mtu; kwa maana alikuwa ni mfanya miujiza, mwalimu wa watu, aliyepokea ukweli kwa furaha” (pamoja na fafanuzi). Na katika kipengele cha 20, Josefu huyu aliandika jinsi mtu aitwaye Ananus alivyomleta barazani (Sanhedrin) mtu aitwaye Yakobo, ndugu wa Yesu aliyeitwa Kristo, na baadhi ya wengine (pamoja na fafanuzi).

Kama miaka 20 baadaye, Tacitus, mwanahistoria wa kirumi, aliandika kitabu kikiangazia historia ya utawala wa Rumi. Katika kitabu hicho alielezea jinsi Nero, (Mtawala wa Rumi) “alivyowaadhibu kwa lengo la kuimarisha utawala, wale wakristo watukutu (kama walivyoitwa wakati huo), aliendelea kuandika “mwanzilishi wao, Kristo, alikuwa ameshasulubiwa katika utawala wa Tiberius na gavana wa Yudea, Pontius Pilato” (Annals 15: 44, pamoja na fafanuzi). Ingawa Tactus, Josefu, na wanahistoria wengine wa karne ya kwanza na ya pili BK, hawakuwa wafuasi wa Kristo, lakini walikuwa na chochote cha kusema kuhusu Kristo, na hata walithibitisha kwamba Kristo alikuwa ni mtu halisi, tena aliyekuwa maarufu, na kwamba aliweza kuvuta hisia za mtawala wa Kirumi mwenyewe!

Sababu nyingine ya wazi ya kuamini kwamba Yesu alikuwa ni mtu halisi ni kwa sababu njia yetu ya tarehe, imeegemea kwenye uwepo wake. Herufi  KK (BC) ni kifupi cha Kabla ya Kristo, na BK (AD) ni Baada ya Kristo (Anno Domini,- in the year of the Lord). Kwa hiyo mwalimu wa historia, anapomuongelea Aleksanda mkuu, akitawala sehemu kubwa ya dunia miaka ya 330 KK, anakuwa anakiri au kukubali kwamba, huyo Aleksanda aliishi kama miaka 330 kabla ya Yesu hajazaliwa.

Ingawa hii ni baadhi tu ya mifano ya ushahidi unaomhusu mtu huyu aliyejulikana kama Yesu, inatosheleza kuthibitisha kwamba alikuwa ni mtu halisi na sio mtu wa kuhisia, au wa kufikirika. Hatukubali kuwepo kwake ki-upofu upofu tu, ni ukweli wa ki-historia.

Rejea

Josephus, Flavius (1957 reprint), The Life and Woks of Flavius Josephus.

Massey, Gerald (1985) Gnostic and Historic Christianity.

Acharya, S (1999), The Christ Conspiracy: the Greatest Story Ever Sold.

Tacitus, Cornelius P. (1952 reprint), The Annals and the Histories,


Published

A copied sheet of paper

REPRODUCTION & DISCLAIMERS: We are happy to grant permission for this article to be reproduced in part or in its entirety, as long as our stipulations are observed.

Reproduction Stipulations→