Tuhuma Zisizo na Uwiano
Miaka kadhaa iliyopita, gazeti la kila siku la Kerrville, Texas Daily Times online lilichapisha habari mbili kwenye ukurasa wao wa mbele kuhusu tukio la msingi-mkutano wa wahariri wasimamizi wa vyombo vya habari vya Texas Associated huko Galveston, Texas, Kichwa cha habari cha kwanza kilikuwa “Times Wins 17 Awards in Statewide contest” (Imeongezwa). Hadithi ya pili ilikuwa na kichwa “Times wins 16 Awards in first day. Habari moja ilionyesha wazi kwamba gazeti hili lilikuwa limeshinda tuzo 16, huku lingine likitumia nambari 17. Hata hivyo inaonekana hakuna mfanyakazi yeyote wa Kerriville Daily Times aliye amini kwamba hadithi zao zilipingana. (Hadithi zilisalia kwenye ukurasa wa mbele wa Daily Times kwa siku chache.) Zaidi ya hayo, hakukuwa na dalili kwamba wengine walikuwa wakilishutumu gazeti hilo kwa kukosa ulinganifu au kutokuwa mwaminifu katika ripoti zao. Kwa nini? Kwa sababu wengi waliosoma majina hayo mawili walielewa upesi kwamba gazeti hilo lilishinda tuzo 17 kwa ujumla-16 kati ya hizo walikusanya katika siku ya kwanza ya mkutano.
Kama mtu yeyote anaweza kuelewa na kukubali kwa urahisi tofauti kama zilivyopatikana kwenye tovuti ya Kerrville Daily Times, mtu hushangaa kwa nini tofauti sawa za kimantiki haziwezi kutambuliwa kwa urahisi katika maandiko. Kwa mfano, Musa alipoandika kuhusu uasherati na ibada ya sanamu ambayo Waisraeli walifanya huko Moabu, alisema kwamba “waliokufa kwa tauni walikuwa ishirini na nne elfu” (Hesabu 25:9). Mtume Paulo alipo rejelea hesabu ya Waisraeli waliofanya uasherati (yaonekana akirejelea matukio katika Hesabu 25:1-9), aliandika hivi “katika siku moja watu ishirini na tatu elfu wakaanguka” (1 Wakorintho 10:8). Wakosoaji na wengine Fulani (kama Davis, et al, 1996, uk 598-599) wangetufanya tuamini kwamba Paulo alikosea katika kuandika 23,000, badala 24,000. Lakini tambua kwamba Paulo alijumuisha kishazi “katika siku moja watu elfu ishirini na tatu walianguka.” Ingawa Musa angeandika baadaye kuhusu kile kilichotokea “siku ya tauni” (Hesabu 25:18; Mwanzo 2:17; 1 Wafalme 2:37, 42; Lyons, 2002), hakutumia kivumishi cha nambari kufafanua kwa uwazi kipindi kilichowekwa kwa siku moja kama Paulo alivyofanya. Hivyo tofauti katika zile namba mbili zaweza kutatuliwa kwa urahisi (na kwa njia ya umantiki) kwa kuzingatia kwamba hesabu ya Paulo ilitia ndani kile kilichotukia ndani ya muda halisi wa saa 24, huku hesabu ya Musa ilitia ndani kila mtu aliyekufa “ilipokuja tauni” (Hesabu 25:18), ingawa ilidumu kwa muda mrefu.
Bila shaka, kama vile tofauti nyingi za biblia zinazodaiwa, mara nyingi zaidi ya ufafanuzi mmoja unaowezekana upo kwa njia ya tofauti kati ya vifungu viwili au zaidi vya biblia. Kuhusu 1 Wakorintho 10:8, wengine wanaamini kwamba Paulo alikuwa anarejelea wakati tofauti katika historia ya Waisraeli (cf. Archer, 1982, uk, 458-459). Wengine wanaamini kwamba Hesabu 25:9, kwa hakika, ndiyo fungu halisi sambamba na 1 Wakorintho 10:8, lakini kwamba wale 1,000 wa ziada katika kitabu cha Hesabu pia walijumuisha wale ambao waamuzi waliwaua (Hesabu 25:4-5; tazama Jamieson, na wenzake, 1997). Bado huenda hesabu ya Paulo ilijumuisha tu sehemu ya wale ambao kwa hakika walikuwa na hatia ya “uasherati,” huku Musa akiwajumuisha makahaba na waabudu sanamu (Hesabu 25:1-3).
Ukweli ni kwamba, kuna maelezo kadhaa yenye kusadikika kuhusu tofauti kati ya Hesabu 25:9 na 1 Wakorintho 10:8. Ni nini hasa maelezo ya tofauti hiyo, labda hatujui kamwe. Lakini tunaweza kujua kwamba mwenye shaka hajathibitisha vifungu hivi kuwa ni tofauti. Zaidi ya hayo, ni mtu mwenye kutilia shaka ndiye anayepaswa kuulizwa ni kwa nini anakubali kwa urahisi tofauti zinazoeleweka, zisizo tofauti katika maandishi mengi ya kisasa (kama, Kerryville Daily Times), lakini anapinga kwa sauti kubwa tofauti sawa za kimantiki, zinazoweza kuelezeka katika Maandiko. Bila shaka, aina hii ya madai isiyo sawa inapaswa kuchunguzwa.
REJEA
Archer, Gleason L. (1982), An Encyclopedia of Bible Difficulties (Grand Rapids: Zondervan).
Davids, Peter H., Walter C. Kaiser, Jr., F.F. Bruce, and Manfred T. Brauch (1996), Hard Sayings of the Bible (Downers Grove, IL: InterVarsity Press).
Geisler, Norman L. and Thomas A. Howe (1992), When Critics Ask (Wheaton, IL: Victor Books).
Jamieson, Robert, et al. (1997), Jamieson, Fausset, Brown Bible Commentary (Electronic Database: Biblesoft).
Lyons, Eric (2002), “Why Didn’t Adam Die Immediately?” Apologetics Press, https://www.apologeticspress.org/AllegedDiscrepancies.aspx?article=797.
REPRODUCTION & DISCLAIMERS: We are happy to grant permission for this article to be reproduced in part or in its entirety, as long as our stipulations are observed.