Menu

SHERIA YA MSINGI YA MAISHA: MAGEUZI YANASHUKA

Kanuni ya sheria msingi ya maisha inatueleza kwamba ulimwengu unakwisha. Ulimwengu unazeeka na unachakaa kama jinsi kipande cha nguo kinavyochakaa, na hakuna jambo tunaloweza kufanya juu ya hilo. Inatoka katika hali ya utaratibu mzuri na kuingia katika machafuko. Biblia inathibitisha ukweli huu katika (Isaya 52:6). Hata hivyo, wazo hili ni athari za nadharia za asili, kama yalivyo mageuzi, kwa sababu mageuzi yanahitaji uhai kupinga sheria msingi ya maisha na mara kwa mara kubadilika Kwenda katika hali tata zaidi. Inasemekana kwamba uhai ulianza kama kiumbe kilicho na seli moja, na kutokana na mabadiliko kutokea, mwisho akapatikana binadamu. Mabadiliko ama mageuzi yanahitaji “Kwenda juu” lakini Ushahidi unaonesha “chini”.

Je kadri muda unavyosogea chumba chako kinakuwa kisafi ama kichafu? Kwa bahati mbaya kitakuwa kibaya zaidi kama usipokisafisha. Inabidi utumie nguvu katika chumba chako ili kupambana na machafuko yanayoongezeka ama sheria msingi ya maisha. Wanamageuzi wanasema kuwa hata jua lina athari kama hizo katika dunia. Eti kwamba jua linaongeza nishati kwenye sayari ambayo inapigana na sheria msingi ya maisha na inaruhusu mageuzi kutokea. Kwa kweli jua huongeza nishati muhimu kabisa katika dunia lakini vilevile inaweza kuweka uharibifu wake. Kwa mfano, lina yeyusha vitu, linachoma na kupunguza maji kwa watu, na pia huleta hali ya ujangwa katika maeneo. Ili kujua kama nishati ya jua ni muhimu vya kutosha kupambana na sheria msingi ya maisha ili kuruhusu mageuzi kutokea , tunahitaji kuangalia jeni ya binadamu yaani vinasaba vyetu.

Uthibitisho halisi wa chembe za urithi yaani jeni, unaonesha kuwa mabadiliko ya chembe hizi yanaweza kuchukuliwa kama yanamanufaa kwa viumbe yanakadiriwa kutokea mara moja tu katika mabadliko milioni moja. Hii inamaanisha kwamba  mabadiliko 999,999 kati ya milioni moja aidha hayafanyi kitu kwa kiumbe au yanamadhara kwa kiumbe yaani hayasaidii kabisa. Kwahiyo kwa mwenendo tunaouona ni kuelekea kuoza kwa hizi chembe za urithi na hata kutoweka kwetu wala si maendeleo ya chembe hizi za urithi kama  zinavyohitajika katika mageuzi. Badiliko moja kati ya milioni moja haliwezi kuitwa mwelekeo wa juu! Jua, bila kujali nishati yake kuwa yenye madhara au yenye faida, haipigani na sheria msingi ya maisha ya maumbile tunayoyaona pande zote. Kwa mara nyingine tena Biblia inakubaliana na Ushahidi wa kisayansi (zaburi 102:26; Ebrania 1:11). Mabadiliko hayafanyi hivyo.


Published

A copied sheet of paper

REPRODUCTION & DISCLAIMERS: We are happy to grant permission for this article to be reproduced in part or in its entirety, as long as our stipulations are observed.

Reproduction Stipulations→