Neno la Mungu ni Sahihi Kuhusu Ngono
Katika Mithali 29:18, Sulemani alibainisha kwamba jamii inapomtofautisha Mungu na Neno Lake, watu hufanya wanavyotaka bila msukumo mkubwa kutoka katika dhamiri zao au kutoka kwa wengine waliowazunguka. Kinyume chake, “heri yeye ashikaye sheria [ya Mungu].” Kama vile sheria za wazazi kwa watoto wao zinavyowalinda na kuwepo kwa manufaa yao (kwamfano, “Usigusejiko la moto”), Neno la Mungu ni kwa manufaa yetu daima (Kumbukumbu la Torati 6:24; 10:12-13; Zaburi 19:7-8; 119; Warumi 7:12). Ukweli huu unahusu pia jinsi gani watu katika jamii wanapaswa kujiendesha kimaadili katika masuala ya ngono. Utafiti mdogo usiojulikana sana, uliofanywa mapema miaka ya 1900 nakuchapishwa mwaka 1934, unathibitisha ukweli huu.
J.D. Unwin alikuwa mtaalamu wa kutafiti tabia za watu,uhusiano wao na utofauti wao na mtaalamu wa jamii kutoka Chuo Kikuu cha Oxford na Cambridge. Hakuwa mtetezi wa Ukristo wala dini yoyote. Katika kitabu chake, Sex and Culture, Unwin anajadili matokeo ya utafiti wake wajamii 86 kwa zaidi ya miaka 5,000ya historia. Jamii hizi zilichaguliwa kwasababu kulikuwepo ushahidiwakutosha kuthibitisha kanuni zao na matarajio yao kuhusu shughuli za ngono. Utafiti huo ulijumuisha jamii mbalimbali za Melanesia, Afrika, Polynesia, Assam, Paleo-Siberia, Wahindiwa Amerika Kaskazini, Wababiloni, Wagiriki wa Athene, Warumi, Waanglo-Saksoni na Waingereza.
Kila utamaduni ulipangwa kulingana na ukali wa sheria na matarajio yake kuhusu maadili ya ngono, hasa kuhusu mwenendo wa wanawake katika jamii hizo. Jamii hizo ziligawanywa katika madaraja saba ya udhibiti wa ngono.—matatu kabla ya ndoa na manne baada ya ndoa.
Kuhusu mila za kabla ya ndoa, baadhi ya jamii ziliruhusu:
- Uhuru kamili wangono kabla ya ndoa;
- Uhuru mdogo wangono kabla ya ndoa, kuruhusu mahusiano yasiyo ya mara kwa mara;
- Hakuna shughuli za ngono kabla ya ndoa—wanawake waliopatikana wakifanya ngono kabla ya ndoa wali huhukumiwa adhabu kali au hata kifo.
Kuhusu mila za baada ya ndoa, baadhiyajamii zilihusiana na:
- Poligamia(mke zaidi ya mmoja) ilikubalika, na hakukuwa na sheria za uaminifu wa ndoa. Hakuna mume wala mke aliyelazimika kuzuia mahitaji yake yakimapenzi kwa mwenzake kwa maisha yote;
- Monogamia ilikubalika, lakini bado hakukuwa na sheria za kudumu kwa uaminifu wa ndoa;
- Wake walilazimika kuwa waaminifu kwa waume zao, lakini waume waliruhusiwa kuwa na wake wengine (yaani, mitala);
- Monogamia kali ilihitajika—mume na mke walilazimika kuwa waaminifu kwa mwenzake pekee katika maisha yote (kurasa 341-343).Matokeo ya Unwin kuhusu makundi haya ni ya kuvutia na yanatia mwangaza mkubwa.
Kulingana na Unwin, “sheria ya msingi ya kwanza inayofanya kazi katika jamii zote za binadamu” ni kwamba “hali yakitamaduni ya jamii yoyote katika mazingira yoyote yakijiografia inategemea mbinu zake za zamani na za sasa za kudhibiti mahusiano kati ya jinsia mbili [kimaadili ya ngono—JM]” (uk. 340).
Katika kila hali, wakati kanuni za ngono katika jamii zinakuwa kali zaidi (yaani, kujizuia kabisa kabla ya ndoa na monogamia kali), jamii husika huendelea kwa kasi. Kadiri shughuli za ngono zinavyodhibitiwa zaidi katika jamii, ndivyo jamii hiyo inavyoendelea. Wakati vizuizi vinapopunguzwa, jamii husika huacha kuendelea na huanza kudhoofika, na hatimaye hutoweka ikiwa vizuizi hivyo havita rejeshwa kuwa imara tena.
“[K]ikomo cha fursa za ngono [yaani, kujizuia zaidi katika jamii—JM] kila mara kimeambatana na kuongezeka kwa maendeleo ya kitamaduni, na kwa kadiri ninavyojua, imekuwa hivyo daima” (uk. 2). Ukuaji huu hutokea tu baada ya kanuni hizo kuendelea kuwepo kwa angalau vizazi vitatu (uk. 321). “Upanuzi wowote wa fursa za ngono [yaani, udhibiti mdogo wa shughuli za ngono katika jamii—JM] kila mara utakuwa sababu ya moja kwa moja ya kushuka kwa maendeleo ya kitamaduni” (uk. 326).
Unwin anasisitiza kuwa jamii inapokuwa na uhuru mkubwa wa ngono, ni sharti kubwa la watu hutumika kutosheleza tamaa za ngono, badala ya kutumika katika maendeleo ya jamii hiyo. Kadiri jamii inavyokuwa na nidhamu kali ya maadili ya ngono, ndivyo nishati hiyo ya ziada inavyotumika kupanua nakuendeleza jamii husika.
“[U]tafiti wa kisaikolojia unaonesha kuwa kuwekwa kwa kizuizi cha lazima kwenye msukumo wa ngono, yaani, kupunguzwa kwa fursa za ngono, huleta fikira, tafakari, na nguvu. Sasa, ushahidi unaonesha kuwa maendeleo ya kitamaduni yamesababishwa na jambo linalochochea fikira, tafakari, na nishati ya kijamii… na kwamba hujitokeza tu pale ambapo fursa za ngono zinapopunguzwa. kwahivyo Ninapendekeza,kwamba kupunguzwa kwa fursa za ngono kunapaswa kuonekana kama chanzo cha maendeleo yakitamaduni…. Ikiwa wanaume na wanawake wako huru kimapenzi, tama zao za ngono zitatimizwa moja kwa moja; lakini ikiwa fursa za ngono zitapunguzwa, msukumo huo utazuiliwa. Hapo ndipo tama hizo zilizokandamizwa zitaoneshwa katika njia nyingine…. [M]ara nyingi mvutano unaosababishwa na mgongano wakihisia hujitokeza katika mfumo wa nguvu ya akili na jamii, ambapo kiwango cha nguvu hiyo hutegemea kiwango cha udhibiti wa lazima wa mahusiano ya kimapenzi [yaani, kiwango cha vikwazo vilivyowekwa kwenye shughuli za ngono—JM].”
Wakati fursa za ngono katika jamii zinapopunguzwa karibu hadi kiwango cha chini kabisa, nishati inayozalishwa kijamii husababisha “mafanikio makubwa katika jitihada za binadamu” na “ustaarabu.” Kadiri kiwango cha udhibiti kinavyopungua, ndivyo nguvu inayozalishwa inavyopungua” (uk. 317).
Miongoni mwa mafanikio ya jamii zilizo na nguvu kubwa ni upanuzi wa maeneo, ushindi wa kijeshi, ukoloni, na uanzishaji wa biashara kubwa ya kimataifa.
“Jamii inayoonesha nguvu ya kijamii yenye tija huendeleza rasilimali za mazingira yake na kwa kuongeza maarifa yake kuhusu ulimwengu wa asili, huweza kuidhibiti nakuibadilisha kwa manufaa yake. Mafanikio yote haya na mengine kama haya yanahitaji juhudi za awali za fikira na tafakari, kwa kuwahi zini hatua za lazima kabla ya mafanikio yoyote ya binadamu kutokea.” (uk. 315, maandishi ya msisitizo katika asili).
Unwin alibainisha kuwa, ingawa anaona kiwango cha juu cha kujizuia katika tabia za ngono kuwa sababu ya moja kwa moja ya nguvu ya kijamii, anatosheka kuhitimisha kuwa nisababu ya nguvu ya kijamii tu kwa maana ya kuwa kipengele cha lazima kisichoweza kuepukika; yaani, hata kama kuna vipengele vingine vya lazima vinavyofanya kazi, hakuna nguvu ya kijamii inayoweza kuonekana isipokuwa fursa za ngono zitakapodhibitiwa.
Hata hivyo, mambo mengine ya kiwa sawa, nguvu ya kijamii itaoneshwa najamii yoyote ambayo inaweka kikomo cha lazima juu ya fursa za ngono kwa wanachama wake. Kinyume chake, katika kila hali, upanuzi wowote wa fursa za ngonolazima usababishe kupungua kwa nguvu ya kijamii. Huo ndio ushahidi kutoka kwenye utafiti wakisaikolojia (uk. 320).
Nguvu yaasili ya fikira na nguvu inayoweza kuzalishwa na mwili wa binadamu inaweza tu kudhihirika pale ambapo misukumo ya ngono inadhibitiwa na sheria za kijamii; na kiwango cha nguvu na kina cha fikra hutegemea kiwango cha vizuizi ambavyo sheria hizi zinaweka.
Ikiwa kiwango cha udhibiti wa lazima wa mahusiano ya kimapenzi kitakuwa kikubwa, jamii itaonesha nguvu kubwa; ikiwa kitakuwa kidogo, kutakuwa na nguvu kidogo. Ikiwa hakuta kuwa na udhibiti wa lazima wa mahusiano ya kimapenzi, basi hakutakuwa na nguvu yoyote; itasalia tu kama nguvu inayoweza kuwepo lakini isiyoweza kudhihirika (uk. 339).
Tunapotazama jamii ya Marekani leo, ugunduzi wa Unwin, ikiwa ni wa kweli, ni maonyo yanayostahili kuzingatiwa, kwani kwa mujibu wa Unwin, “mara tu fursa za ngono za jamii, au za kikundi ndani ya jamii, zilipoongezwa, nguvu ya jamii hiyo, au ya kikundi ndani yake, ilipungua na hatimaye kutoweka” (uk. 382).
Kwa kutumia istilahi za kisasa zisizo za kitaalamu: Tamaa zisizo dhibitiwa za aina yoyote huwa na mwelekeo wakuteka fikra na muda wetu. Ikiwa jamii kwa ujumla inaruhusu tamaa zisizodhibitiwa kuenea, basijamii kwa ujumla itakuwa na sehemu kubwa ya uwezo wake wa kufikiri, na nguvu yake ikielekezwa katika kutimiza matamanio hayo badala ya kufanya mema kwa wengine na kuboreshajamii. Takwimu zinaonesha kuwa hali ya machafuko ya kingono inatawala Marekani. Ponografia, uzinzi, talaka na ndoa za mara kwa mara, kuishi pamoja bila kufunga ndoa (iwe na mtu mmoja au zaidi), ushoga, ndoa za wake wengi, na ulawiti wa watoto vimeenea katika jamii ya Marekani na hata vinahimizwa katika baadhi ya hali kupitia sheria, muziki, filamu, na vitabu.
Kinachovutia ni kwamba, kwa mujibu wa matarajio ya Mkristo anayezingatia Neno la Mungu, Unwin aligundua kuwa ndoa ya mke mmoja na mume mmoja kwa maisha yote ilipelekea kuwepo kwa jamii zilizoendelea zaidi. “Katika kumbukumbu za historia, kwa hakika hakuna mfano wa jamii iliyoonesha nguvu kubwa kwa muda wowote wa maana isipokuwa ile iliyokuwa na ndoa za mke mmoja na mume mmoja kabisa. Zaidi ya hayo, sijui kisa chochote ambacho jamii yenye ndoa ya aina hii ilishindwa kuonesha nguvu kubwa” (uk. 369).
“Jamii ambazo zimeendeleza desturi [ya ndoa za mke mmoja na mume mmoja kabisa—JM] kwa muda mrefu zaidi ndizo zimefikia kiwango cha juu zaidi cha maendeleo ya kitamaduni ambacho binadamu amewahi kufikia” (uk. 25). “Kwa ujumla, katika historia, pale walipoanza kuonesha nguvu kubwa…, jamii za binadamu zilikuwa na ndoa za mke mmoja na mume mmoja kabisa…. Nguvu ya jamii zilizoendelea zaidi kistaarabu, au ya kikundi chochote ndani yake, iliendelea kudhihirika kwa muda mrefu ilimradi kama walidumisha masharti yao madhubuti. Nguvu yao ilianza kufifia mara tu” masharti haya yalipoanza kulegezwa (uk. 343).
Unwin anasema kuwa ndoa ya mke mmoja na mume mmoja kwa uaminifu mkali huleta mazingira ambayo maendeleo yanaweza kupatikana kwa urahisi zaidi katika jamii. Anaeleza kuwa hatua inayofuata chini kwenye ngaziya udhibiti wa masuala ya kingono (ndoa za wake wengi kwa nidhamu kali) haipelekei maendeleo ya kijamii. “Jamii iliyo na ndoa za wake wengi kabisa huwepo lakini mila yake haiendelei. Haina nguvu ya kupokea mawazo mapya; inabaki kuridhika na misingi yake ya zamani” (uk. 368).
Ingawa anakubali kuwa hakufanya utafiti rasmijuu ya mada hii, ni jambo la kuvutia kutambua yale ambayo Jenerali maarufu George S. Patton aligundua wakati wa Vita ya Pili ya Dunia kuhusu nchi za Kiislamu za Afrika Kaskazini (ambazo zilifuata ndoa za wake wengi):
“Mtu hawezi kujizuia kufikiria swali hili: Je, nini kingetokea kama Waarabu wangekuwa Wakristo? Kwangu mimi, inaonekana dhahiri kuwa mafundisho ya hatima ya Mohammed na unyanyasaji wa wanawake ndiyo sababu kuu ya maendeleo ya Waarabu kusimama. Wako vile walivyokuwa mnamo mwaka 700, ili hali sisi tumezidi kuendelea. Hapa, nadhani, kuna somo la maana kwa ajili ya mahubiri yenye nguvu juu ya fadhila za Ukristo” (1947, uk. 43).
Katika Mathayo 19, Yesu aliwakumbusha wasikilizaji wake kuhusu mwanzo—wakati Mungu alipotoa tafsiri ya ndoa kwa wanadamu:
“Je, hamjasoma ya kuwa yeye aliyewaumba mwanzo aliwaumba mume na mke [Mwanzo 1:27], akasema, ‘Kwa sababu hiyo mtu atamwacha baba yake na mama yake, ataambatana na mke wake, nao wawili watakuwa mwili mmoja’ [Mwanzo 2:24]? Hivyo basi, wao si wawili tena bali ni mwili mmoja. Kwa hiyo, alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe” (Mathayo 19:4-6).
Ndoa ya Kimaandiko, kama ilivyokusudiwa na Mungu, inapaswa kuwa kati ya mwanamume mmoja anayefaa na mwanamke mmoja anayefaa, na hao wawili kuwa mwili mmoja kwa maisha yao yote. Ndoa ya uaminifu wa mke mmoja na mume mmoja ndio tafsiri ya ndoa kulingana na Biblia. Kwa mujibu wa Maandiko, tendo la ndoa ni jema na linapaswa kuhamasishwa katika muktadha huo (1 Wakorintho 7:3-5; Waebrania 13:4; Mithali 5; Wimbowa Sulemani). Utafiti wa Unwin unatusaidia kuelewa angalau sababu moja kwa nini ndoa ilifafanuliwa kwa namna hiyo.
[KUMBUKA: Utafiti wa Unwin bila shaka ulizingatia jamii zilizokuwepo mapema kabla ya miaka ya 1900 wakati ambapo utafiti huo ulifanyika—jamii ambazo nyingi kati yao huenda zilikuwa zimetengwa na ushawishi mkubwa wa tamaduni nyingine kutokana na hali ya teknolojia kabla ya miaka ya 1900 (mfano, kukosekana kwa simu, televisheni, intaneti, n.k.), pamoja na vizuizi vya kijiografia vya asili (yaani, kutoweza kusafiri kwa urahisi kati ya mataifa). Utafiti wa aina hii huenda ukawa mgumu zaidi leo, kwasababu jamii kwa kiasi kikubwa hazipo tena katika hali ya kujitenga, bali zinaathiriana kwa kiwango kikubwa. Jamii moja inaweza kuonekana kama inakua kinyume na madai ya Unwin, wakati kwa uhalisia, maendeleo yake yalitokana tu, kwa mfano, na kupokea teknolojia kutoka kwa jamii nyingine, kupokea misaada kutoka katika mataifa mengine, n.k.—mambo yanayofanyika mara kwa mara katika nyakati za sasa. Hata hivyo, kwa kuondoa ushawishi mwingi kama huo kwenye hesabu, kama ambavyo utafiti wa Unwin ulilazimika kufanya, kunauwezekano mkubwa wa kupata tathmini sahihi zaidi ya athari za mwenendo wa kingono katika jamii.]
MAREJELEO
Miller, Dave (2006), Sexual Anarchy (Montgomery, AL: Apologetics Press).
Patton, George S. (1947), War As I Knew It (New York: The Great Commanders, 1994 edition).
Unwin, J.D. (1934), Sex and Culture (London: Oxford University Press).
REPRODUCTION & DISCLAIMERS: We are happy to grant permission for this article to be reproduced in part or in its entirety, as long as our stipulations are observed.