Menu

Mungu, Mageuzi, na Thamani ya Uhai wa Mwanadamu

Mungu aliweka wazi katika sura ya kwanza kabisa ya Biblia kwamba aliumba maisha ya mwanadamu tofauti na viumbe vingine vyote duniani. Baada ya kuumba maisha ya mimea siku ya tatu na maisha ya wanyama siku ya tano na sita Mungu alisema:

“Natumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba. Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, zaeni mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi” (Mwanzo 1: 26-28).

Mungu alimuumba mtu kwa mfano Wake. Alimpa mwanadamu nafsi isiyoweza kufa (Mwanzo 35:18; Mathayo 10:28). Alimfanya mwanadamu awe wa thamani zaidi kuliko viumbe vingine vyote duniani (Mathayo 6:26-28). Alimfanya mwanadamu awe wa thamani zaidi kuliko viumbe vingine vyote duniani (Mathayo 6:26-30). Tangu mwanzo kabisa, Mungu alitarajia mwanadamu kula mimea (Mwanzo 1;29), na tangu angalau wakati wa Nuhu, Mungu amempa mwanadamu mamlaka ya kula wanyama (Mwanzo 9:2-3). Kwa kweli, mwanadamu amekua akiua wanyama (kwa ajili ya dhabihu, nguo, n.k) kwa kibali cha Mungu tangu dhambi ilipoingia ulimwenguni (Mwanzo 4:4; Waebrania  11:4; Mwanzo 8:20; linganisha Mwanzo 3:21). Hata hivyo, kumwaga damu ya mwanadamu ni tofauti kabisa. Kwa nini? Kwa sababu “Kwa mfano wa Mungu alimfanya mwanadamu” (Mwanzo 9:6).

Ingawa mtazamo wa ulimwengu wa kikristo umejikita katika thamani iliyotolewa na Mungu ya maisha ya mwanadamu na ukuu wa mwanadamu juu ya Uumbaji mwingine wa kidunia wa Mungu (Zaburi 8:5-8), mageuzi ya wasioamini Mungu yanashusha thamani maisha ya mwanadamu hadi kufikia hatua ambapo mwanadamu hana thamani, maisha ya mwanadamu hadi kufikia hatua ambapo mwanadamu hana thamani zaidi ya panya, mende na vimelea. Kwa miongo kadhaa, wanafunzi katika shule za umma za Amerika wamesoma kutoka kwa vitabu vya kiada ambavyo vinashusha thamani ya maisha ya mwanadamu. Katika utangulizi wa kitengo cha ufalme wa wanyama katika  kitabu cha biolojia cha darasa la 10 cha Holt, wanafunzi walifundishwa: “wewe ni myama, na unashiriki urithi wa pamoja na funza…..(Johnson, 1994, uk 453). Kitabu cha masomo cha sayansi ya Dunia cha mwaka wa 1989 kilichochapishwa na Harcourt, Brace, na Jovanovich kilidai kwamba “huenda wanadamu walitokana  na bakteria walioishi zaidi ya miaka bilioni 4 iliyopita” (uk. 356). Mnamo 2006, mwanaikolojia wa mageuzi DK. Eric Pianka alitajwa kuwa mwanasayansi maarufu wa mwaka wa Texas. Katika hafla yake ya tuzo, Pianka alilaani “wazo kwamba wanadamu wanashikilia nafasi ya upendeleo katika ulimwengu” na “kuboresha maoni yake kwa kusema, sisi sio bora kuliko bakteria!’’’ (Mims, 2006). Katika Makala ya New Scientist ya 2008 yenye kichwa, “Tunapaswa kutenda kama Wanyama Tulivyo,” mwanamazingira David Suzuki alisema katika mahojiano na Jo Merchant: “[Lazima] tukubali kwamba sisi ni wanyama… tunapenda kujiona kuwa tumeinuliwa juu ya viumbe vingine. Lakini mwili wa mwanadamu ulibadilika” (Marchant, 200[2678]:44).

Kwa hakika, kuna tofauti kubwa kati ya theism na mageuzi ya kutomwamini Mungu. Mmoja anasema kwamba Mungu alimuumba mwanadamu kwa njia maalum; mwingine anasema, “tunashiriki urithi wa pamoja na minyoo” Mmoja ansema kwamba mwanadamu kwa asili ana thamani zaidi kuliko wanyama; mwingine anasema “sisi ni wanyama.” Mmoja anasema kwamba mwanadamu ni bora kuliko bakteria; mwingine anasema, “sisi si bora kuliko bakteria!” Lakini ikiwa sisi si bora kuliko viumbe vidogo au dunia tunamoishi, ni nini kitakacho zuia ubinadamu kuamua kupunguza idadi ya watu hadi 10% ya idadi ya sasa ili “kuokoa dunia mama” kutoka kwa “wingi wa watu”? DK. Pianka alipendekeza wazo kama hilo wakati wa sherehe yake ya tuzo ya 2006. Nini kitawazuia wabunge kupiga marufuku kuua na kuliwa kwa wanyama (watu wanaodaiwa kuwa sawa)? Wako hai, pia. Tunawezaje kuhalalisha kula mimea na wanyama ikiwa sisi siyo bora kuliko bakteria? Tunawezaje kuhalalisha kutembea? Baada ya yote, tunaweza kukanyaga, na kuua, mdudu au bakteria. Tukilala, tunaweza kuharibu kunguni. Hata shida zaidi, ikiwa tutaendelea kupumua, tunaweza kuvuta na kuharibu microbe.

Kwa kweli, watu wanapokubali fikira isiyomcha Mungu kwamba uhai wa mwanadamu na aina nyingine zote za uhai ni sawa, kunakuwa na kichaa. Machafuko yatawala siku. Mtazamo wa ulimwengu wa kibiblia, hata hivyo, unaunda mpangilio mzuri unaofaa kwa uwepo wa mwanadamu.

REJEA

Earth Science (1989), (New York: Harcourt, Brace, & Jovanovich).

Johnson, George B. (1994), Biology: Visualizing Life (New York: Holt, Rinehart, & Winston).

Marchant, Jo (2008), “We Should Act Like the Animals We Are,” New Scientist, 200[2678]:44-45, October 18-24.

Mims, Forrest (2006), “Dealing with Doctor Doom,” The Citizen Scientist, http://www.sas.org/tcs/weeklyIssues_2006/2006-04-07/feature1p/ index.html.


Published

A copied sheet of paper

REPRODUCTION & DISCLAIMERS: We are happy to grant permission for this article to be reproduced in part or in its entirety, as long as our stipulations are observed.

Reproduction Stipulations→