Menu

Mlipuko Mkuu Ni Uongo: Mbingu na Nchi ni ya Milele Kweli?

Kama hutaki kukubali kwamba Mungu yupo, inabidi uwe tayari kuelezea uwepo wa Mbingu na nchi bila yeye kuviumba. Kama hayupo katika mpango huo, basi mbingu na nchi vilijiumba vyenyewe, au vimekuwepo tangu milele – hakuna namna nyingine (Spancer, 1882). Nadharia ambayo imezoeleka leo, ni ile ya Mlipuko Mkuu (Big Bang) ambayo inasema kwamba, Mbingu na nchi vilijiumba vyenyewe. Kumbuka mwaka 2014, Jarida la Sayansi, Machapisho na hata vyombo vya habari, vilipongeza uvumbuzi wa mionzi ya uvutano, ambayo wanasema ilithibitisha kupungua kwa huo Mlipuko mkuu (Miller, 2014). Suala la kupungua ni la msingi na lazima kwenye nadharia hiyo ya mlipuko mkuu, ikitakiwa kuweka sawa tatizo la ubapa na anga katika mbingu, kama hakuna Mungu wa kuviumba, lakini ambavyo bado hakuna ushahidi wa moja kwa moja. Kumbuka pia hapisho la “Nature” la mwaka 2015, lenye kichwa “Uvumbuzi wa miale ya uvutano sasa umekufa kiofisi” (Cowen, 2015). Kwamba iliyodhaniwa mwanzo kuwa ni miale ya uvutano, ushahidi wa Mlipuko Mkuu, ikawa ni vumbi vumbi la angani (galax dust) (Miller, 2015). Hivyo wale wasomi wa mlipuko mkuu, wako katika maneno ya msomi mwingine, Allan Guth wa MIT, aliyesema, “Vyema kabisa tunarudi tulipokuwa huko nyuma (kama ilivyonukuliwa katika McKee, 2015). Kwani tulikuwa wapi huko nyuma? Tulikuwa mahali ambapo hapakuwa na ushahidi wa kupungua. Kwa maneno mengine ya mwanafizikia na profesa wa Princeton, Paulo Steinhardt, Suala la kupungua linabadilika kiasi kwamba linakataa majaribio na uchunguzi. Na kwamba suala la kupungua kimsingi halijaribiki, na hivyo kisayansi halina maana (2014 pamoja na fafanuzi).

Kwa tangazo kwamba kwa mara nyingine tena, hakuna ushahidi wa kupungua, mtu anaweza akategemea kwamba nadharia mpya itatoka inayotatua tatizo la wanaoamini asili, kwamba labda Mbingu na nchi ni vya milele badala yake. Kwa kweli kabisa, wiki moja na siku mbili baadaye, Phys. Org, ilitangaza matokeo ya kimahesabu, yaliyofanywa na Ahmed Farag Ali, wa chuo kikuu cha Benha, huko Misri pamoja na Saurya Das, wa chuo kikuu cha Lethbridge huko Kanada. Hawa wawili walikiri na kuonyesha tatizo la msingi katika nadharia ya mlipuko mkuu, ambalo watafiti wameshalisemea kuwa; kama ni kweli huo mlipuko mkuu ulianzaje? Ule umoja, kile cha mwanzo, kilichokuja kulipuka, kilitoka wapi? Haiwezekani kwamba vilijiumba vyenyewe, kwa mujibu wa sheria za kisayansi. Na kama mtu anabisha kwamba hata hiyo sheria ya sayansi haikuwepo, ilijiandikaje na ikawepo pamoja na mada na nguvu? Na kama sheria hizo zilikuwepo, nani aliyezifanya? Maana kila sheria ina mtu aliyeifanya (Angalia Miller, 2013 kwa mjadala mpana juu ya hili). Ali na Das, wanadai wamemaliza tatizo hili kwa njia ya mahesabu na kuonyesha kwamba hapakuwahi kuwepo Mlipuko mkuu,- hakuna umoja, yaani hicho kilicholipuka (Zyga , 2015). Kwa mjibu wa wawili hao, mbingu na nchi ni vya milele. Jambo hili lina maana gani kwa watafiti wa uumbaji?

Kwanza; tunapenda kuonyesha kwamba, Ali na Das, wanakubaliana nasi kwamba kuna tatizo kubwa la kisayansi juu ya mlipuko mkuu kuhusu chanzo au asili ya ylem iliyolipuka. Hiyo pia isingejiumba yenyewe. Wazo kama hili sio la kisayansi wala sio la asili. Hakuna ushahidi wa kisayannsi kwamba jambo kama hilo linaweza kutokea. Na kama likitokea basi litakuwa sio la kawaida, au maajabu, au uchawi bila mchawi.

Pili; Tungeonyesha kwamba, kazi ya Ali na Das haijawa wazi kama halali na jumuia ya wanasayansi kwa ujumla. Mfano Jarida la Live Science, lilisema juu ya mahesabu haya kwamba, “kama nadharia hii itakuwa ni ya kweli, mbingu na nchi hazikuanza kwa mlipuko mkuu” (hose, 2015 pamoja na fafanuzi). Mpaka tunapoandika makala haya, miezi mitano imepita tangu tangazo la kazi ya Ali na Das. Na si Jarida la Science, wala Nature, wala Scientific American, wala New Scientist wala American Scientist ambayo yamewekea uzito mjadala huu.

Tatu; Tunaona kwamba umilele wa mbingu na nchi, sio wazo jipya. Kabla ya mlipuko mkuu kulikuwa na utupu, yaani vogue, Mifano ya umilele ilikuwepo na ilikuwa maarufu, kama ule wa bwana Fred Hoyle, lakini kadiri muda ulivyopita walikuja kuikataa kutokana na ushahidi unaoonekana. Kwa mfano, Robert Jastrow, mwana anga anayeamini mabadiliko ya viumbe (evolution), na mkurugenzi wa zamani wa taasisi ya anga katika NASA, aliandika;

Na hivi karibuni kumekuwepo na mjadala mkubwa juu ya ukweli kwamba, sheria nyingine ya kisayansi juu ya dunia, inaonyesha kwamba dunia inapungua kama saa. Kama inaungua, kuna wakati ilikuwa kamili … sasa mistari mitatu ya ushahidi – mwendo wa vitu vya angani, sheria za kisayansi, simulizi za maisha ya nyota – vyote vilielekeza kwenye hitimisho moja; vyote vinaonyesha kwamba, mbingu na nchi zilikuwa na mwanzo (1978 uk 48, 49, 111).

Kiufupi ni kwamba mbingu na nchi haviwezi kuwa vya milele, kwa mujibu wa sheria ya pili ya sayansi. Ushahidi wote uliopo wa kisayansi unaonyesha kwamba mada zote pamoja na nguvu vinamomonyoka au kuharibika. Kila kitu kinaelekea kwenye kukosa mpangilio na machafuko na tunapuguza ile nguvu inayotumika. Hali hii kuelekea kukosekana mpangilio na kuharibika haigeuziki, na inaitwa entropy. Ukweli usioepukika wa hii entropy ndiyo sababu ya mashine za mwendo usiokoma inaeleweka kwamba haziwezekani hapa duniani. Kama mbingu na nchi ni vya milele, basi hizo ni machine za mwendo usiokoma, ambazo sasa zinapingana na sheria ya pili ya sayansi, ambayo inajumuisha vyote.

Kama tutaweka hitimisho letu kwenye ushahidi halisi wa kisayansi, tunalazimika kuhitimisha kwamba, mbingu na nchi havikuweo tangu milele, au la zingekuwa zimeshaishiwa hizo nguvu zinazopungua na kuharibika. Yaani zingekuwa zimeshaharibika kabisa (Angalia Miller 2013 kwa mjadala zaidi wa sheria za kisayansi na asili ya mbingu na nchi). Kwa hiyo namna pekee ya mbingu na nchi kuwa vya milele, ni kama kuna mtu nje yake, ambaye anahesabu hiyo entropy, na kuongeza hizo nguvu zinazopungua na kuharibika kwa kipimo maalum. Na kama ni hivyo mjadala huu usingekuwa juu ya asili, bali ungekuwa wa ajabu (super nature), ambao watafiti wa asili waliufuatilia sana, lakini wanasayansi walikataa hata kuufikiria.

Hatimaye hakuna ushahidi kwamba nguvu au mada vinakuja angani – hivyo kuwepo kwa sheria ya kwanza ya sayansi. Kwa hiyo mbingu na nchi haviwezi kuwa vya milele. Na kama mmoja anaamini hivyo, anafanya hivyo kinyume na ushahidi wa kisayansi. Kwa sababu analeta hitimisho, lisiloruhusiwa na ushahidi, atakuwa sio wa kawaida (Ruby, 1960, uk 130, 131). Kiufupi, atakuwa “kipofu wa imani”.

Rejea

Cowen, Ron (2015), “Gravitational Waves Discovery Now Officially Dead”

Ghose, Tia (2015), “Big Bang Deflated? Universe May Have Had No Beginning”

Jastrow, Robert (1978) God and The Astronomers

McKee, Maggie (2015), “Big Bang Discovery Crumbles to Dust”

Miller, Jeff (2014) “Was the Big Bang Just Proven by Astronomers?”

Miller Jeff (2013), Science vs. Evolution

Miller, Jeff (2015), “Big Bang Inflation Officially Bites the Dust”

Ruby, Rionel (1960), Logic: An Introduction

Spencer, Herbert (1882), First Principles: A System of Synthetic Philosophy.

Steinhardt, Paul (2014), “Big Bang Blunder Bursts the Multiverse Bubble”

Zyga, Lisa (2015), “No Big Bang? Quantum Equation Predicts Universe Has No Beginning”


Published

A copied sheet of paper

REPRODUCTION & DISCLAIMERS: We are happy to grant permission for this article to be reproduced in part or in its entirety, as long as our stipulations are observed.

Reproduction Stipulations→