Menu

Mamlaka, Kutegemeka na Ukweli

Je, maswali kuhusu kutegemewa kwa Biblia ni muhimu sana? Je wao wana uzito sana kiasi kwamba wanaruhusu mazungumzo kwenye Tovuti yetu mara kwa mara? Je, muda wetu haungeweza kutumiwa vyema kwenye somo lingine?

Ni kweli kwamba wakristo wana jukumu la kufikiria mambo mengi mazito. Masomo kuhusu ibada inayokubalika, uwakili, uinjilisti, ushirika wa kanisa, n.k., zote ni mada ambazo wakristo wanapaswa kuzitafakari mara kwa mara. Hata hivyo, kwa kukiri kwamba ufahamu sahihi wa mada hizi (na nyingi zaidi) hutegemea mamlaka ya Maandiko, basi mashambulizi dhidi ya uaminifu wa maandiko si jambo dogo. Wenye mashaka wanafahamu vyema ukweli kwamba ikiwa wanaweza kudhoofisha kutegemewa kwa biblia, basi wanaweza kudhoofisha msingi wenyewe wa Ukirsto. Kwa bahati mbaya, kwa kuwa na vyeo mashuhuri katika shule za umma, vyuo vikuu, na vyombo vya habari, wachambuzi wa Biblia wamekuwa na nguvu na ushawishi mkubwa zaidi katika siku za hivi karibuni, na wanaweza kusikika ulimwenguni pote kwenye redio, Runinga na mitandaoni.

Katika toleo la Mei/Juni 2006 la “Biblical Archaelogy Review”, iliyoandikwa na Michael D. Coogan aliandika Makala yenye kichwa “Mamlaka ya maswali!” ambamo alihusisha suala la mamlaka (au ukosefu wake) na Biblia (katika) uthabiti.

“Biblia inasema” mara nyingi huonekana kuwa yenye maamuzi katika mijadala ya kisasa kuhusu masuala kama vile kutoa mimba, kusaidiwa kujiua, hali ya wanawake, mahusiano ya jinsia moja, adhabu ya kifo na vita na Amani. Tatizo ni kwamba Biblia mara nyingi hailingani. Biblia haisemi kwa sauti moja. Kwasababu tu kitu kimeandikwa katika biblia haimaanishi kwamba ni mtazamo pekee unao wezekana au hata kuwa ni kweli (2006, 32(3):24).

Profesa Cooogan alitoa mfano gani ili “kuthibitisha” maoni yake kuhusu kutopatana na kutotegemewa kwa Biblia? Eti kwa kuwa Biblia inafundisha kwamba Mungu huadhibu watoto kwa ajili ya dhambi za wazazi wao hadi kizazi cha tatu na cha nne (Kutoka 20:5; Kumbukumbu la Torati 5:9), lakini pia inasema “mwana hatauchukua uovu wa Baba yake, wala baba hatauchukua uovu wa mwanawe,”(Ezekiel 18:20; Yeremia 31:30), basi “Biblia haisemi kwa sauti moja” bali “hailingani” Je yuko sahihi?

Kwa kweli, fundisho la Biblia juu ya dhambi, kuteseka kwa matokeo ya dhambi, na kubeba hatia ya dhambi ya mtu mwenyewe ni thabiti sana. Tangu Adamu na hawa walipokula matunda wa mti wa ujuzi wa mema na mabaya mwanadamu amepatwa na matokeo ya dhambi. Mtu huteseka mara kwa mara kwasababu ya dhambi zake mwenyewe (1 Petro 4:15). Mara nyingi, hata hivyo, mwanadamu huteseka kwasababu ya dhambi za mababu zake (pamoja na wazazi,babu na mababu). Leo watoto wanaweza kuteseka kwasababu baba anatupwa gerezani kwasababu ya kuendesha gari akiwa amelewa, na hivyo hawezi kuandalia familia yake riziki. Ustaarabu wenye njaa unaweza kuteseka kwa kiasi kwasababu mababu zao waliweka mfumo wa Imani ambapo kula wanyama kama ng’ombe ni mwiko (kwa kuwa mnyama huyo anaweza kuwa babu aliyezaliwa upya.

Mungu aliwajulisha Waisraeli kwamba dhambi ya kuabudu sanamu (na tunda la dhambi hiyo) ni mbaya na chungu sana hivi kwamba watoto (hata kizazi cha tatu na cha nne) wangeteseka kutokana na hilo. Watoto wa wazazi walio abudu sanamu wakati Fulani waliteseka kifo kwasababu wazazi wao waliwatoa dhabihu kwa Baali (Yeremia 19:5). Wengine kama vile wale walioishi wakati wa waamuzi, waliteswa mara kwa mara na umasikini, magonjwa, na utumwa, kwasababu wao, kama wazazi wao, walimwacha BWANA wakamtumikia Baali na Maashtorethi” (Waamuzi 2:13). Watu wengine kama vile walioishi wakati wa waamuzi, waliteswa mara kwa mara na umasikini, magonjwa, na utumwa, kama wazazi wao. Huenda ikawa kwamba hata huko Marekani, waadilifu walio baki watateseka kwasababu ya uamuzi wa Mungu wa kuadhibu Taifa hilo mcha Mungu ambalo kwa sasa linamfukuza na kukumbatia dhambi kila kona.

Lakini ingawa uzao wa wasio na hatia wanaweza kuteseka kwa matokeo ya dhambi za mababu zao, wao hawabebi hatia ya matendo ya dhambi ya mababu zao (Ezekieli 18:20). Yaani hawarithi dhambi za wazazi wao. Biblia haidokezi kamwe kwamba watoto wana hatia ya kuabudu sanamu kwasababu tu wazazi wao walikuwa waabudu sanamu. Watoto hawana hatia; kiasi kwamba Yesu alisema “Ufalme wa Mungu ni wao” (Luka 18:16). Hatimaye kuwajibika kwa dhambi na kubeba hatia ya dhambi ni tofauti kabisa na kuteseka kwa matokeo ya kimwili ya matendo ya wengine.

Katika hitimisho la Makala yake katika “Archaelogy Review, Coogan aliandika: “kwasababu tu kitu kimeandikwa haimaanishi kuwa huo ndio mtazamo pekee unaowezekana au hata kuwa ni kweli” (2006, 32(3):24). Kwa kweli, ni Makala ya Coogan ambayo hayana ukweli, na ni mamlaka ya Makala yake (sio Biblia!) ambayo yanapaswa kutiliwa shaka.

MAREJEO

Coogan, Michael D. (2006), “Question Authority!” Biblical archeology Review, 32(3):24, Mei/Juni.

Imechapishwa 14-Mei-2006.

UZALISHAJI NA MAKANUSHO: Tuna furaha kutoa ruhusa ili Makala haya yanakilishwe kwa sehemu au kwa ukamilifu, mradi tu masharti yetu yatazingatiwa. Masharti ya uzalishaji.


Published

A copied sheet of paper

REPRODUCTION & DISCLAIMERS: We are happy to grant permission for this article to be reproduced in part or in its entirety, as long as our stipulations are observed.

Reproduction Stipulations→