Menu

Makosa katika Calvinism

John Calvin (1509- 1564) alikuwa mwanatheolojia Mfaransa wakati wa harakati za kiprotestanti ambaye mfumo wake wa theolojia ya kikristo ulioonyeshwa hasa katika taasisi ya dini ya kikristo, umekuwa na ushawishi mkubwa katika ulimwengu wa kikristo kwa karibu karne tano. Msingi mkuu wa mawazo yake umefupishwa chini ya TULIP ya akrosti.

Upotofu kamili= Wanadamu wote wamerithi dhambi ya Adamu kupitia kwa wazazi wao na hawawezi  kiadili kuchagua kumfuata Mungu na kuokolewa kwasababu ya asili yao potofu, ya dhambi ambayo inaenea kwenye kila sehemu ya utu wao.

Majibu ya Biblia

Ezekieli 18:19-23 – “Lakini ninyi mwasema, kwani yule mwana asiuchukue uovu wa baba yake? Yule mwana atakapofanya yaliyo halali na haki, na kuzishika amri zangu na kuzitenda, hakika ataishi. Roho itendayo dhambi, ndiyo itakayo kufa; mwana hatauchukua uovu wa baba yake,wala baba hatauchukua uovu wa mwanawe, haki yake mwenye haki itakuwa juu yake, na uovu wake mwenye uovu utakuwa juu yake. Lakini mtu mbaya akighairi, na kuacha dhambi zake zote alizozitenda, na kuzishika amri zangu zote, na kutenda yaliyo halali na haki, hakika ataishi, hatakufa. Dhambi zake zote alizo zitenda hazitakumbukwa juu yake hata moja wapo; katika haki yake aliyoitenda ataishi. Je, mimi ninafurahia kufa kwake mtu mwovu? Asema Bwana MUNGU; si afadhali kwamba aghairi, na kuiacha njia yake, akaishi?”

Ezekieli 28:15 – “Ulikuwa mkamilifu katika njia zako tangu siku ile ulipoumbwa, hata uovu ulipoonekana ndani yako.”

Zaburi 106:37-38 “Naam, waliotoa wana wao na binti zao kuwa dhabihu kwa mashetani. Wakamwaga damu isiyo na hatia, damu ya wana wao na binti zao, walio watoa dhabihu kwa sanamu za Kaanani; nchi ikatiwa unajisi kwa damu.”

Zekaria 12:1 “Ufunuo wa Neno la BWANA juu ya Israeli. Haya ndiyo asemayo BWANA, azitandaye mbingu, auwekaye msingi wa dunia, aiumbaye roho ya mwanadamu ndani yake.”

Mathayo 18:2-3 “Ni nani basi aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni? Akaita motto mmoja, akamweka katikati yao, akasema, Amin , nawaambia, msipoongoka na kuwa kama vitoto, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.”

Mathayo 19:14 “Lakini Yesu akasema, waacheni watoto wadogo waje kwangu; wala msiwazuie; kwamaana walio mfano wa hao, ufalme wa mbinguni ni wao.”

Warumi 7:9 “Nami nalikuwa hai hapo kwanza bila sharia; ila ilipokuja ile amri, dhambi ilihuika, name nikafa.”

Uchaguzi usio na masharti=Mungu alichagua tangu milele kuwaokoa watu Fulani bila kutegemea wema wowote ulio tarajiwa, Imani, au kukubalika kwa Injili. Mungu alichagua kuwapa rehema wale ambao amewachagua hasa na kuwanyima rehema wale ambao hawakuchaguliwa. Wale walio chaguliwa wanapokea wokovu kupitia Kristo pekee. Wale ambao hawajachaguliwa hupokea ghadhabu na laana.

Majibu ya Biblia

Luka 13:3- “Nawaambia, sivyo; lakini msipotubu, ninyi nyote mtaangamia vivyo hivyo.”

Yohana 3:16- “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.”

Yohana 8:24- “Kwa hiyo naliwaambieni ya kwambaya kwamba mtakufa katika dhambi zenu; kwasababu msipo sadiki ya kuwa mimi ndiye, mtakufa katika dhambi zenu.”

Matendo 10:34-35- “Petro akafumbua kinywa chake, akasema, hakika natambua ya kuwa Mungu hana upendeleo; bali katika kila taifa mtu amchaye na kutenda haki hukubaliwa nay eye.”

Warumi 2:5-11- “Bali kwa kadiri ya ugumu wako, na kwa moyo wako usio na toba, wajiwekea akiba ya hasira kwa siku ile ya hasira na ufunuo wa hukumu ya haki ya Mungu, atakaye mlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake; wale ambao kwa saburi katika kutenda mema wanatafuta utukufu na heshima na kutokuharibika watapewa uzima wa milele; na wale wenye fitina wasio itii kweli, bali wakubalio dhuluma, watapata hasira na ghadhabu; dhiki na shida juu ya kila nafsi ya mwanadamu atendaye uovu, Myahudi kwanza na Myunani pia; bali utukufu na heshima na Amani kwa kila mtu atendaye mema, Myahudi kwanza na Myunani pia; kwa maana hakuna upendeleo kwa Mungu.”

1 Petro 1:17- “Na ikiwa mnamwita Baba, yeye ahukumuye kila mtu pasipo upendeleo, kwa kadiri ya kazi yake, enendeni kwa hofu katika wakati wenu wa kukaa hapa kama wageni.”

Ufunuo 22:17- “Na Roho na Bibi-arusi wasema, Njoo! Naye asikiaye na aseme, Njoo! Naye mwenye kiu na aje; nay eye atakaye, na ayatwae maji ya uzima bure.”

Upatanisho wenye kikomo= Kristo alikufa tu kwaajili ya wale ambao Mungu aliamua mapema kuwaokoa (wateule) na si kwaajili yaw engine wowote.

1 Timtheo 2:3-4 “Hii ni nzuri, nalo lakubalika mbele za Mungu Mwokozi wetu; ambaye hutaka watu wote waokolewe, na kupata kujua yaliyo kweli.”

1 Timotheo 2:5-6 “Kwasababau Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu; ambaye alijitoa mwenyewe kuwa ukombozi kwa ajili ya wote, utakaoshuhudiwa kwa majira yake.”

Tito 2:11-12 “Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa; nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa;”

1 Yohana 2:2 “naye ndiye kipatanisho kwa dhambi zetu; wala si kwa dhambi zetu tu, bali na kwa dhambi za ulimwengu wote.”

Yohana 3:17 “Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili ahukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye.”

2 Petro 3:9 “Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyo kudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu yeyote apotee, bali wote wafikie toba.”

Matendo 10:34 “Petro akafumbua kinywa chake akasema, Hakika natambua ya kuwa Mungu hana upendeleo.”

Warumi 2:11 “Kwa maana hakuna upendeleo kwa Mungu.”

Neema isiyo zuilika= Neema ya Mungu itumikayo inatumika kwa wale ambao ameamua kuwaokoa (wateule), kushinda upinzani wao kwa wito wa Injili, kuwaleta kwenye Imani inayookoa. Hilo lamaanisha kwamba Mungu anapokusudia kwa enzi kuu kumwokoa mtu, mtu huyo hakika ataokolewa (hata dhidi ya mapenzi yake ikibidi). Ushawishi huu wa makusudi wa Roho mtakatifu wa Mungu, ambaye hujenga Imani ndani ya mtu binafsi, hauwezi kupingwa.

Majibu ya Biblia

Kumbukumbu la Torati 30:19 “Nazishuhudiza mbingu nan chi juuyenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, Baraka na laana; basi chagua uzima ili uwe hai wewe na uzao wako.”

Joshua 24:15 “Nanyi kama mkiona ni vibaya kumtumikia BWANA, chagueni hivi leo mtakaye mtumikia; kwamba ni miungu ile ambayo baba zenu waliitumikia ng’ambo yam to, au kwamba ni miungu ya wale Waamori ambao mnakaa katika nchi yao; lakini mimi na nyumba yangu tutamtumikia BWANA.”

Luka 7:30 “Lakini Mafarisayo na wana-sheria walilipinga shauri la Mungu juu yao, kwa kuwa hawakubatizwa naye.”

Yohana 12:42-43 “Walakini hata katika wakuu waliokuwamo wengi waliomwamini; lakini kwasababu ya mafarisayo hawakumkiri, wasije wakatengwa na sinagogi. Kwa maana walipenda utukufu wa mwanadamu kuliko utukufu wa Mungu.”

Matendo 7:51 “enyi wenye shingo gumu, msio tahiriwa mioyo wala masikio, siku zote mnampinga roho Mtakatifu; kama baba zenu walivyofanya, na ninyi ni vivyo hivyo.”

Matendo 13:46 “Paulo na Barnaba wakanena kwa ushujaa wakasema, Ilikuwa lazima neno la Mungu linenwe kwenu kwanza; lakini kwakuwa mnalisukumia mbali, na kujiona nafsi zenu kuwa hamkustahili uzima wa milele, angalieni, twawageukia Mataifa.”

Ustahimilivu wa watakatifu=Kwa kuwa Mungu ni Mkuu na mapenzi yake hayawezi kukatishwa tamaa na wanadamu au kitu kingine chochote, wale ambao Mungu amewaita katika ushirika pamoja Naye wataendelea katika Imani hadi mwisho. Hawawezi kupotea milele.

Majibu ya Biblia

Wagalatia 5:4 “Mmetengwa na Kristo, ninyi mtakao kuhesabiwa haki kwa sharia; mmeanguka na kutoka katika hali ya neema.”

2 Petro 2:20-22 “Kwa maana wale waliokwisha kuyakimbia machafu ya dunia kwa kumjua Bwana na Mwokozi Yesu Kristo, kama wakinaswa tena na kushindwa, hali yao ya mwisho imekuwa mbaya kuliko ile ya kwanza. Maana ingekuwa heri kwao kama wasingaliijua njia ya haki, kuliko kuijua, kasha kuiacha ile amri takatifu waliyopewa. Lakini imetukia kwao sawasawa na ile mithali ya kweli, mbwa ameyarudia matapiko yake mwenyewe, na nguruwe aliye oshwa amerudi kugaagaa matopeni.”

Waebrania 4:11 “Basin a tufanye bidii kuingia katika raha ile, ili kwamba mtu yeyote asije akaanguka kwa mfano uo huo wa kuasi.”

Waebrania 6:4-6 “Kwa maana haowalio kwisha kupewa nuru na kukionja kipawa cha mbinguni , na kufanywa washirika wa Roho Mtakatifu, na kulionja neno zuri la Mungu, na nguvu za zamani zijazo, wakaanguka baada ya hayo, haiwezekani kufanywa upya tena hata wakatubu; kwa kuwa wamsulubisha Mwana wa Mungu mara ya pili kwa nafsi zao, na kumfedhehi kwa dhahiri.”

Waebrania 10:38-39 “Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa Imani; naye akisitasita, roho yangu haina furaha naye. Lakini sisi hatumo miongoni mwao wasitao na kupotea, bali tumo miongoni mwa hao walio na Imani ya kutuokoa roho zetu.”

Yakobo 5:19-20 “Ndugu zangu, ikiwa mtu wa kwenu amepotelea mbali na kweli, na mtu mwingine akamrejeza; jueni ya kuwa yeye amrejezaye mwenye dhambi hata atoke katika njia ya upotevu ataokoa roho na mauti, na kufunika wingi wa dhambi.”

Ufunuo 2:5 “Basi kumbuka ni wapi uliko anguka; ukatubu, ukayafanye matendo ya kwanza. Lakini usipo fanya hivyo, naja kwako, name nitakiondoa kinara chako katika mahali pake usipo tubu.”

Ufunuo 3:5 “Yeye ashindaye atavikwa hivyo mavazi meupe wala sitalifuta kamwe jina lake katika kitabu cha uzima, name nitalikiri jina lake mbele za Baba yangu, na mbele ya malaika zake.”

Ufunuo 22:19 “Na mtu yeyote akiondoa lolote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima, na katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki.”


Published

A copied sheet of paper

REPRODUCTION & DISCLAIMERS: We are happy to grant permission for this article to be reproduced in part or in its entirety, as long as our stipulations are observed.

Reproduction Stipulations→