Maisha Yalitoka Wapi?
Kutokana na mtazamo wa mwanafikra asiyeamini, swali la asili ya maisha ni “mfumuko mkubwa” kwa hali bora. Kwa kuwa maumbile yameonesha kwa muda mrefu kwa maelfu ya miaka kwamba maisha yote ya kimwili hutokana na maisha yaliyokuwepo awali (sheria inayotambuliwa ya kisayansi ijulikanayo kama biogenesis), maelezo ya kiasili ya jinsi maisha yalivyodaiwa kuibuka kutokana na kutokuwepo kwa maisha ni tatizo kubwa sana. Stuart Clark hivi karibuni alirejelea kizungumkuti hiki katika mfululizo wa makala ya New Scientist kuhusu “fumbo kubwa zaidi la Dunia.” Clark aliiita moja ya makala yake kwa jina rahisi, “Maisha yalitoka wapi?” (2008, 199[2675]:30-31). Tafakari baadhi ya kukiri kwake.
“Kwa kuacha uwezekano wa mbali kwamba, maisha yalifika Duniani kwenye Kimondo kutoka mahali pengine,” Clark alikiri kwanza kuwa, “tunapaswa kudhani kwamba yalitokea kutokana na hali za kimwili na kiasili zilizokuwepo wakati wa kupevuka kwa sayari” (uk. 30, msisitizo umeongezwa).Katika mstari wa mwanzo wa makala yake, Clark alikiri kwamba,maelezo ya maendeleo ya maisha lazima yadhaniwe Kukiri kama hiki kinakumbusha kile alichokiri mmoja wa wataalamu wa juu zaidi wa asili ya maisha duniani katika mfululizo wa mihadhara iitwayo Asili ya Maisha. Dkt. Robert Hazen, mwanachama wa International Society for the Study of the Origin of Life, alikiri kutoka mwanzo: “Kozi hii inazingatia tu mbinu za kisayansi za swali la asili ya maisha. Katika mfululizo huu wa mihadhara, ninaweka dhana kwamba maisha yalitokea kutokana na vifaa vya kimsingi” (2005, 1:6, msisitizo umeongezwa). Ukweli ni kwamba, kilicho bora zaidi ambacho sayansi ya maendeleo inaweza kufanya kuhusu swali la asili ya maisha ni kudhani kwamba ilikuwa kiasili kabisa.
Pili, Clark alikiri kwamba:“Hakuna matukio yaliyoandikishwa ya ‘tukio la asili ya maisha’ kwenye Dunia ya kisasa” (uk. 30). Ingawa wafuasi wa nadharia ya maendeleo hawana tatizo kufundisha wanafunzi wanaoathirika katika madarasa ya sayansi duniani kote kwamba,maisha yalitokea kutokana na kemikali,mamilioni ya miaka iliyopita, wanapaswa kukiri, kama alivyofanya Bwana Clark, kwamba sayansi haina ushahidi (yaani, “hakuna matukio yaliyoandikishwa”) kwamba maisha ya kimwili yalitokea kutokana na kutokuwepo kwa maisha (ambayo ingekiuka sheria ya viumbe kutokana na viumbe vya awali). Kilicho bora zaidi alichoweza kufanya Clark ni kuhoji kama “hali sahihi” bado inakuwepo, au kudhani kama “inaweza kuwa inatokea katika vipande vidogo sana kiasi kwamba hatujaona” (uk.30, msisitizo umeongezwa).
Alipoendelea kupitia majibu yake kuhusu moja ya “mambo makubwa ya fumbo” ya Dunia, Clark alikiri “ugumu mwingine” (uk. 31). “[T]unakutana na hali ya swali la kuku na yai: ili vinasaba ifanye kazi yake inahitaji protini, lakini michoro ya protini hizo hutolewa na vinasaba. Kwa hivyo, kipi kilikuja kwanza? Jibu linaloaminika zaidi sasa linadhaniwa kuwa viliendelea kwa wakati mmoja kupitia mtandao wa miitikio kati ya kemikali rahisi zaidi” (uk. 31, emp. imeongezwa). Haiaminiki! Si tu kwamba wanasayansi wa mabadiliko hawajawahi kushuhudia maisha yakitokea kutoka kwa yasiyo ya uhai, bali wanakiri kwamba pendekezo hilo linamaanisha kuwa vinasaba na protini lazima viliendelea na kuungana kwa wakati mmoja kabisa. Inavyoonekana, upangaji huo sahihi wa vizuizi vya ujenzi wa maisha vyote vilitokea tu kwa bahati, bila aina yoyote ya akili. Kama mwanastronomia wa Uingereza Sir Frederick Hoyle alivyoandika miaka 27 kabla ya Stuart Clark katika jarida hilo hilo la sayansi, hesabu kama hizo ni “upuuzi wa hali ya juu” (1981, 92:527).
Basi maisha yalitoka wapi? Kulingana na mtaalamu wa maendeleo na mshindi wa Tuzo ya Nobel George Wald, “Chaguo pekee” kwa kizazi cha moja kwa moja ni “kuamini katika tendo moja la msingi la uumbaji wa kimungu. Hakuna nafasi ya tatu” (Wald, 1954, 191[2]:46). Maisha yaliumbwa, au yaliendelea kutokana na kutokuwepo kwa maisha. Kwa kuwa kila uchunguzi wa kisayansi unaojulikana kwa mwanadamu umeonesha kwamba maisha ya kimwili, kamwe hayajatokea kutokana na kutokuwepo kwa maisha, na hayawezi kutokea.Hitimisho la kiakili pekee ni kwamba, maisha yaliumbwa na mungu.
Kwa kweli, asili ya maisha ni ya kufadhaisha tu ikiwa mtu hataki kutambua matokeo ya sheria ya kisayansi ya viumbe kutoka kwa viumbe wa awali. Sayansi, Maandiko, na mantiki ya kawaida yanahitaji maelezo ya kimungu.
MAREJELEO
Clark, Stuart (2008), “Where Did Life Come From?,” New Scientist, 199[2675]:30-31, September 27.
Hazen, Robert (2005), Origins of Life (Chantilly, VA: The Teaching Company).
Hoyle, Fred (1981), “The Big Bang in Astronomy,” New Scientist, 92:521-527, November 19.
Wald, George (1954), “The Origin of Life,” Scientific American, 191[2]:44-53, August.
REPRODUCTION & DISCLAIMERS: We are happy to grant permission for this article to be reproduced in part or in its entirety, as long as our stipulations are observed.