Mageuzi Yanajipinga Yenyewe
Kuamini asili, ni imani kwamba kuwepo kwa ulimwengu kunaweza kuelezewa tu, kupitia aina fulani ya njia za kimageuzi za asili, kuliko muujiza wa asili. Kuamini asili, na kwa maana hiyo upagani, kiulazima wanajipinga wenyewe. Mtu hawezi kuwa Muumini wa asili (Mpagani) na asijipinge mwenyewe. Ki-vipi?
- Kama mtu ni muumini wa asili (Naturalist), lazima aamini kwamba ulimwengu ni matokeo bila kisababishi. Ushahidi kutoka kwenye asili hata hivyo ni kwamba vitu vyote vilivyotokea lazima viwe na kisababishi.
- Kama mtu ni muumini wa asili (Mpagani), lazima aamini kwamba, mada na nguvu, vinaweza kujiumba vyenyewe au kuishi milele. Ushahidi kutoka kwnye asili, hata hivyo ni kwamba mada na nguvu haviwezi kujiumba vyenyewe (sheria ya kwanza ya nguvu-mwendo), wala haviwezi kuishi milele (sheria ya pili ya nguvu-mwendo)
- Kama mtu ni muumini wa asili (Mpagani), lazima aamini kwamba, aina moja ya kiumbe kinaweza kubadilika (morph) kuwa, au kuzaa kiumbe kingine tofauti kabisa baada ya muda; mageuzi madogomadogo (micro-evolution) yakitokea. Ushahidi toka kwenye asili hata hivyo ni kwamba maisha yanazalishana kwa aina zake, na sio kwa aina nyingine.
Muumini wa asili (Mpagani) anajipinga mwenyewe kwa sababu lazima aamini katika hali isiyo ya kawaida ambayo haitokei kwa asili. Matokeo yasiyo na kisababishi, Sheria bila mtunga Sheria, uzalishaji wa ghafla wa mada/nguvu na maisha, na mageuzi kupitia mipaka ya phylogenic, haitokei kwa asili. Kama mtu atachagua kuamini kwamba kitu kama hicho kinaweza kutokea kwa asili, huyo si muumini wa asili tena. Anaamini katika vitu visivyo vya asili – vya ajabu – visivyo vya kawaida (phenomena). Muumini wa asili hasa ni muumini wa “ajabu” japo anajiita wa asili. Tunaweza angalau kukubalina na muumini wa asili kwa kitu kimoja, hata kama asingetaka kukikiri au kukikubali; mwanzo wa ulimwengu unahitaji shughuli za “ajabu”. “Mbingu zauhubiri utukufu wa Mungu” (Zaburi 19: 1). Kuchagua kutomwamini ni “hata wasiwe na udhuru” (Warumi 1: 20).
REPRODUCTION & DISCLAIMERS: We are happy to grant permission for this article to be reproduced in part or in its entirety, as long as our stipulations are observed.