Menu

Maadili Yalitoka Wapi?

“Wanasaikolojia wa mabadiliko wanaamini kwamba wanakaribia kuelewa mojawapo ya mafumbo yaliyo salia ya maisha, sharia ya maadili ya ulimwenguni pote ambayo hutegemeza mawazo yetu angavu ya mema na mabaya.” Hayo yalikuwa maneno ya mhariri mkuu wa Newsweek Jerry Adler katika Makala yake, yenye kichwa cha habari “The New Naysayer” (2006).

Imefahamika kwa muda mrefu kuwa maadili yapo (tazama Taylor, 1945, uk. 83):  kuna wema na kuna uovu; kuna haki na kuna makosa. Watu tofauti huchora mstari wa maadili katika sehemu tofauti, lakini “wote wanakubali kwamba kuna mstari kama huo kuchorwa” (Taylor, 1945, p. 83). Kwa nini?

Ni kwanini wanadamu tu wenye maadili, ikiwa kama wanavyo fundisha wanamageuzi kwamba, tulitokana na chanzo kisicho na uhai, kisicho na akili, na lisilo na fahamu kwa mabilioni ya miaka? Kwanini wanadamu wanahisi hisia ya “lazima” kuwasaidia maskini, wanyonge, na wanaokandamizwa ikiwa tu tulibadilika kwa sharia ya asili ya “uwezo wa kufanya haki” (yaani, mwenye nguvu zaidi ndiye atakaye ishi)? Alder alimwelezea Richard Dawkins kwenye jarida lake la “New Naysayers” kama mmoja wa wanazuoni watatu wanao bisha kwamba atheism ni bora” (2006, uk.47). Inavyoonekana, mfano mmoja wa ubora wa atheism unatokana na maelezo mapya ya wanamageuzi kuhusu maadili, ambayo wanayaelezea kama mojawapo ya mafumbo yaliyosalia ya maisha (uk. 48). Kulingana na alder,

“Dawkins anajaribu kuonyesha jinsi misukumo ya juu zaidi ya mwanadamu, kama vile uelewa, hisani na huruma, ingeweza kuibuka kwa utaratibu uleule wa uteuzi asilia ulio unda kidole gumba. Wanabailojia wanaelewa kwamba nguvu inayoongoza katika mageuzi ni kuishi na kuenezwa kwa chembe zetu za urithi.Huenda zikatusukuma kufanya matendo ya wema hata inapoonekana kutofaa kwa maslahi yetu-tuseme, kwa kuhatarisha maisha yetu ili kuokoa mtu mwingine. Saikolojia ya mageuzi inaweza kueleza jinsi tabia ya kutojitolea inavyo weza kuwa imeibuka (uk. 48-49).

Na ni nini hasa maelezo haya? (1) “Mpokeaji wa matendo yetu ya wema anaweza kuwa ni jamaa wa damu ambaye amebeba baadhi ya chembe zetu za urithi.” (2) “Au matendo yetu yanaweza kutuletea shukrani ya wakati ujao, au sifa ya ushujaa ambayo hutufanya tutamanike zaidi kama wenzi wa ndoa.” (3) “msukumo wa ukarimu lazima uwe uliibuka wakati wanadamu waliishi katika vikundi vidogo ambavyo karibu kila mtu alikuwa na uhusiano, hivyo kwamba wema ukawa matarajio ya kibinadamu ya msingi” (UK. 49).

Hapo unayo maelezo ya “kutokuamini (Atheism)” ya ubora kwa maadili. Ingawa “nguvu ya kuendesha” ya mageuzi-uteuzi wa asili-inaenda kinyume na maadili kama vile misukumo ya kibinadamu kama uelewa, hisani na huruma, sasa tunaambiwa “inaweza kutusukuma kwa vitendo vya asili vya wema…hata wakati inaonekana kuwa isiyofaa maslahi binafsi (UK. 48). Kwa muhtasari, hisia zetu za “ustahili” wa kimaadili inadaiwa hutokana na (1) kupitisha nasaba (gene) zetu, (2)kutokana na tamaa ya kuwa shujaa na kupata umaarufu, au (3)kwa chaguo la msingi (default).

Kiuhalisia, “wasio amini kuwa kuna Mungu wenye akili zaidi” ni upumbavu uliokithiri (Zaburi 14:1; 1 Wakorintho 1:25). Tamaa ya kupitisha nasaba (gene) au kuwa shujaa inashindwa kueleza chimbuko la maadili ya mwanadamu. Mtu anapomwona mtoto asiyemfahamu akining’inia kwenye gorofa ya sita na kuhisi kwamba analazimika kumwokoa mtoto huyo kutokana na kifo (ingawa hakuna anayemtazama), hisia hiyo ya jukumu la kimaadili lazima lifafanuliwe kwa njia nyingine isipokuwa mageuzi. Mtu anapolazimika kutumia wakati, pesa, na nguvu zenye thamani ili kumsaidia mgeni maskini aendelee kuishi, ingawa hatua hiyo inaweza kumaanisha kuhatarisha majeraha au kifo, maelezo ya kiasili hayatafanya kazi. Kusema “wema ukawa matarajio ya kawaida ya mwanadamu” ni kielelezo tu cha kukosa maelezo ya kutosha ya asili.

Maadili yapo na yana maana ikiwa tu kuna Mungu, kwasababu ni Mungu pekee ndiye angeweza kuyaumba. Ikiwa maelezo yote ya asili ya kuwepo kwa maadili yameonyeshwa kuwa hayatoshi, kimsingi maelezo  pekee yenye mantiki lazima yawe ya Kiungu (yaani Mungu).

MAREJEO

Adler, Jerry (2006) “The New Naysayers,” New’s week, 11-Septemba, UK 47-49.

Simpson, George Gaylord (1967), The meaning of evolution (New Haven, CT: Yale University Press), revised edition

Taylor, A.E. (1945), Does God exist? (London: Macmillan).


Published

A copied sheet of paper

REPRODUCTION & DISCLAIMERS: We are happy to grant permission for this article to be reproduced in part or in its entirety, as long as our stipulations are observed.

Reproduction Stipulations→