Kwa nini Mungu Aliahirisha Kuandikwa kwa Agano Jipya?
Swali:
Kwa nini Mungu alisubiri kwa miaka 20 baada ya kanisa kuanzishwa ili kuanza kuandika agano Jipya? Kwa nini muda mrefu hivyo?
Jibu:
Kwa kawaida tunapozungumzia uandishi wa Agano Jipya, tunafanya hivyo kwa kuzingatia ukweli kwamba Mungu aliongoza wanaume kuandika kuhusu Yesu na mapenzi yake kwa kanisa miaka 20-65 baada ya kifo na ufufuo wa Mwokozi. Labda cha kustaajabisha zaidi ni wingi wa ushahidi wa asili ya Agano Jipya katika karne ya kwanza. Kwa sababu ya wingi wa hati za kale, matoleo, manukuu ya hati za Agano Jipya, hata wasomi wengi huria wamekubali kwamba Agano Jipya lazima liwe limekamilika mwishoni mwa karne ya kwanza. Ingawa nakala zilizopo za Plato, Thucydides, Herodotus, Tacitus, na wengine wengi zimetenganishwa na wakati. Watu hao waliandika kwa miaka 1,000, uthibitisho wa maandishi ya Agano Jipya unafikia mbali sana kama karne ya pili ya mapema, ambayo imesababisha wasomi wengi kuhitimisha kwa usahihi kwamba Agano Jipya, kwa hakika, ni toleo la karne ya kwanza (Lyons, 2007; Bruce, 1953, p.16 Geisler na Nix, 1986, uk 408, 475; kama vile Irwin H. Linton alivyosema kuhusu masimulizi ya injili: “Uhakika unaojulikana kwa wote ambao wametoa uchunguzi wowote kwa somo hili ni kwamba vitabu hivi vilinukuliwa, kuorodheshwa, kuunganishwa, kutajwa kuwa mamlaka na waandishi mbalimbali wakristo na wapagani, kipindi cha nyuma kabisa wakati wa mitume” (1943, uk. 39).
Bado wengine wanashangaa kwa nini Mungu alichagua kusubiri takriban miaka 20 ili kuanza kuandika Agano Jipya. Kwa nini mitume na manabii wa karne ya kwanza hawakuanza kuandika Agano Jipya mara tu kanisa lilipoanzishwa?
Jibu rahisi na la moja kwa moja ni kwamba hatuwezi kusema kwa uhakika kwa nini Mungu alisubiri miongo miwili kuanza kuandika Agano Jipya. [KUMBUKA: Wasomi wa kihafidhina kwa ujumla wanakubali kwamba hati za Agano Jipya za mapema zaidi kuandikwa, zilikuwa kama Wagalatia na 1&2 Watheselonike, yaelekea ziliandikwa kati ya A.D. 48-52.] Tunaweza kuuliza idadi yoyote ya maswali kuhusu kwa nini Mungu alifanya au hakufanya jambo Fulani: kwa nini Mungu alisubiri miaka 2,500 hivi baada ya Uumbaji na miaka 1,000 hivi baada ya gharika kuandika simulizi kamilifu, lililopuliziwa kuhusu matukio hayo? Kwa nini Mungu alitumia sura 11 pekee katika Biblia kutueleza kuhusu miaka 2,000 ya kwanza ya historia ya mwanadamu na sura 1,178 zinazotueleza kuhusu miaka 2,000 zinazofuata? Kwa nini Mungu alikomesha ufunuo maalum, ulioandikwa kwa zaidi ya miaka 400 (kati ya Malaki na Agano Jipya)? Kuna maswali mengi, hata yale mahususi kuhusu muundo wa ufunuo ulioandikwa wa Mungu, ambayo hayajajibiwa, lakini Mungu hajatufunulia habari hii.
Baada ya kutoa kanusho hilo, tunaweza kupendekeza sababu chache za kimantiki kwa nini Mungu alisubiri kuwavuvia mitume na manabii wa karne ya kwanza kuandika Agano Jipya. Kwanza, kanisa la kwanza lilikuwa na hazina ya Injili “katika vyombo vya udongo” (2 Wakorintho 4:7), ikimaanisha kwamba mitume waliongozwa kimuujiza na roho katika yale waliyofundishwa (Wagalatia 1:12; 1 Wakorintho 2:10-16) Roho wa Mungu aliwaongoza “katika kweli yote” (Yohana 16:13). Pia wale ambao mitume waliwachagua kuwawekea mikono katika makanisa ya kwanza walipokea miujiza, karama za kiroho za unabii, maarifa, hekima, n.k (Matendo 8:14-17; 1 Wakorintho 12:1-11). Ingawa kanisa lilikosa maandishi yaliyoongozwa na roho ya Paulo, Petro, na Yohana kwa miaka michache, Mungu hakuwaacha Wakristo Wake wapya bila mwongozo. Kwa njia Fulani, walikuwa na Agano Jipya linalotembea, linaloishi. Wakati enzi ya miujiza ilipoisha (1 Wakorintho 13:8-10; tazama Miller, 2003), hata hivyo, kanisa lingehitaji aina Fulani ya mwongozo wa kuendelea. Kwa hiyo, wakati wa enzi ya miujiza, Mungu aliwavuvia mitume na manabii kuweka katika hali ya kudumu ufunuo wake mkamilifu na kamili ili kuliongoza kanisa hadi kurudi kwa Yesu (tazama 2 Timotheo 3:16-17).
Pili, ilikuwa muhimu kwa Mungu kuchelewesha kuandikwa kwa Agano Jipya, badala ya kuandika mara tu baada ya kuanzishwa kwa kanisa, kwa sababu vitabu na barua zinazounda Agano Jipya awali ziliandikwa kwa ajili ya hadhira mahususi na madhumuni mahususi (ingawa inatumika kwa Wakristo wote).
Kwa mfano, nyaraka ambazo Paulo aliandikia kanisa la Korintho hazingeweza kuandikwa hadi kuwe na kanisa huko Korintho. Ikiwa kanisa la Korintho halikuanzishwa hadi safari ya pili ya umishonari ya mtume Paulo (Yapata B.K 49-520, basi ni wazi Paulo aliwaandikia Wakristo wa Korintho baada ya wakati huu. Zaidi ya hayo, kwa kuwa katika 1 Wakorintho Paulo alishughulika na matatizo mahususi ambayo yalikuwa yametokea katika kanisa la Korintho (kama mgawanyiko, uasherati, n.k.), hangeweza kuzungumzia mambo haya kwa undani hadi baada ya kutimia. Hivyo, kulikuwa na haja ya muda kupita kabla ya hati za agano Jipya kuandikwa.
Ingawa wengine wanaweza kusumbuliwa na ukweli kwamba Mungu alingoja takriban miaka 20 ili kuanza kuandika agano jipya kupitia waandishi wake waliovuviwa, tunaweza kuwa na uhakika kwamba alikuwa na sababu nzuri za kuahirishwa huku kwa muda mfupi. Ni kweli kwamba Mungu hakuonyesha waziwazi kwa nini alikawia kuweka wosia na agano lake la mwisho katika maandishi. Bado sababu za kimantiki zipo-hasa zaidi, ukweli kwamba hati zinazounda Agano Jipya ziliandikwa kwa watu maalium na kwa makusudi maalum.
REJEA
Bruce, F.F. (1953), The New Testament Documents—Are They Reliable? (Grand Rapids, MI: Eerdmans), fourth edition.
Comfort, Philip W. and David P. Barrett (2001), The Text of the Earliest New Testament Greek Manuscripts (Wheaton, IL: Tyndale House).
Geisler, Norman L. and William E. Nix (1986), A General Introduction to the Bible (Chicago, IL: Moody), revised edition.
Linton, Irwin H. (1943), A Lawyer Examines the Bible (Grand Rapids, MI: Baker), sixth edition.
Lyons, Eric (2007), “Inspired Writers and Competent Copyists,” Reason & Revelation, 27[3]:17-23, https://apologeticspress.org/apPubPage.aspx?pub=1&issue=587#.
Miller, Dave (2003), “Modern-Day Miracles, Tongue-Speaking, and Holy Spirit Baptism: A Refutation—Extended Version,” Apologetics Press, https://apologeticspress.org/apcontent.aspx?category=11&article=1399.
REPRODUCTION & DISCLAIMERS: We are happy to grant permission for this article to be reproduced in part or in its entirety, as long as our stipulations are observed.