Menu

Kuua, Mauaji na Biblia

Dakika nane na sekunde kumi na nane katika hotuba yake ya ufunguzi ya dakika 15 wakati wa mjadala wetu wa siku ya Darwin wa 12-Februari-2009, Dan Barker alidai kwamba Mungu wa Biblia hawezi kuwepo kwa sababu mafundisho ya Biblia kuhusu mauaji yanapingana. Alisema:

Katika Kutoka 20:13, katika Amri Kumi: “usiue.” Katika      Mambo ya Walawi 24:17 maneno yake tofauti yenye neno tofauti     la Kiebrania: “Yeyote atakaye muua mtu yeyote lazima    atauwawa.” Hata hivyo tunapata katika Kutoka 32: “Bwana Mungu asema hivi, kila mtu na aweke upanga wake ubavuni mwake, kila mtu amwue ndugu yake, na mwenzake, na jirani yake.” 1   Samweli: “Watu wakaomboleza kwa sababu Bwana alikuwa    amewapiga watu wengi kwa mauaji makubwa.” Biblia imejaa      mifano ya Mungu wa kibiblia akitenda, kuamuru, na kuachilia   mauaji. Mungu wa Biblia anasema “usiue.” Tena Mungu wa B  iblia anasema “ua” Hayupo (Butt na Barker, 2009).

Je, ni kweli kwamba msimamo wa kibiblia kuhusu kuua unapingana kabisa na unaweza kutumiwa kuwa uthibitisho wa kwamba Mungu wa Biblia hawezi kuwepo? Hakika sivyo. Maagizo ya kibiblia kuhusu kuua yanapatikana kikamilifu na yenyewe, na kanuni za haki, na hayawezi kutumika kama ushahidi dhidi ya Mungu wa Biblia.

Kwanza, kulingana na Dan, amri ya kuepuka kuua katika Amri kumi ni taarifa ya blanketi ambayo inajumuisha kuepuka kila aina ya mauaji. Hata hivyo, ni lazima tuzingatie kwamba sura moja tu baadaye, katika Kutoka 21:12-17, tunasoma maagizo kadhaa yanayohusu adhabu ya kifo ambapo hukumu ya kifo inaruhusiwa kwa wale wanaomuua mtu mwingine kimakusudi kwa sababu ya uovu, wanaoteka nyara mtu kumuuza, au amlaaniye baba yake au mama yake. Wasomaji wa awali walielewa kwamba amri katika Kutoka 20:13 haikumaanisha kwamba mauaji yote yalikuwa mabaya, ikiwa ni pamoja na adhabu ya kifo. Walielewa kwamba sifa Fulani, kama zinavyofafanuliwa kwa kina katika sharia nyinginezo, ziliweka mipaka, vizuizi, na posho kwa neno “kuua.” Barker angetutaka tuamini kwamba yeyote aliyeandika kitabu cha kutoka alikuwa mjinga kiasi kwamba hakupata kauli zinazopingana ambazo zimetenganishwa na chini ya sura moja. Walakini, wazo kama hilo ni la kipuuzi kwa kuzingatia usahihi wa ajabu na ufahamu wa maagizo ya Agano la Kale (Tazama Butt, 2008) ambayo yalitumiwa na jamii ya Wayahudi kwa karibu miaka 1,500, ambayo mingi ilikuwa msingi wa kanuni za kisheria za mataifa ya kisasa. Kiburi cha jumuiya ya sasa ya wasioamini Mungu kudhani kwamba wasomaji wa awali wa agano la Kale walikuwa na akili finyu kiasi cha kukubali kauli zinazopingana chini ya sura moja pekee ni ya kushangaza. Iwapo tamko kuhusu kuua litatolewa, na ndani ya aya chache, kauli hiyo itastahiki na kufafanuliwa, madai kwamba mauaji yote yanajumuishwa katika maagizo ya awali hayawezi kudumishwa.

Pili, Barker mara kwa mara anatumia madai haya ya kupingana katika maandishi yake pamoja na mijadala yake. Katika kitabu chake, “Bila kumcha Mungu” alidai kwamba amri iliyopo katika Kutoka 20:13 haiwezi kutafsiriwa “Usiue,” kwa sababu neno la Kiebrania “ratsach” nyakati Fulani haimaanishi kitu kingine isipokuwa kuua. Ili kuthibitisha hoja yake, aliorodhesha maneno matano yafuatayo ya Kiebrania yanayotafsiiriwa kwa kawaida kuwa “kuua.”

Muth: (825) kufa, kuchinja, mauaji, kuua

Nakah: (502) piga, kuua, chinja, piga, umiza, mauaji, haribu

Zabach (140) dhabihu, kuua

Ratsach (47) chinja [23], mauaji [17], kuua [6], kuuawa [1] (Barker, 2008, uk 204).

Kuthibitisha zaidi hoja yake, aliorodhesha sehemu kadhaa katika Agano la Kale ambapo neno ratsach, halimaanishi kitu kingine isipokuwa mauaji. Alitaja andiko la Kumbukumbu la Torati 4:42, mstari unaotumia neno hilo kurejelea kuua bila kukusudia. Pia alitaja Hesabu 35:30-31, ambamo neno hilo linatumiwa kwa ajili ya adhabu ya kifo inayokubalika ambayo muuaji anapewa. Mabishano ya Barker, basi, ni kwamba ikiwa neno hilo linaweza kutumika kumaanisha kitu kando na mauaji, basi lazima litumike kwa njia hiyo katika Kutoka 20:13.

Dosari mbaya katika madai ya Barker ni ile ya usawa. “usawazishaji unaainishwa kama udanganyifu rasmi na usio rasmi. Ni matumizi ya kupotosha ya neno lenye maana au maana zaidi ya moja (kwa kuangazia maana inayokusudiwa kwa wakati Fulani”) (2equivocation,” 2009,) {KUMBUKA: Ingawa Wikipedia kwa kawaida haizingatiwi kuwa chanzo cha kitaaluma, usawaziko ni dhana inayotumiwa sana na maneno ya Wikipedia yalikuwa mafupi na ya wazi zaidi kati ya vyanzo mbalimbali visivyoshauriwa.] Tazama jinsi Barker anavyosawazisha katika tukio hili. Anasema kwa usahihi kwamba neno ratsach linaweza kutumika kwa mauaji yanayohalalishwa kama vile adhabu ya kifo, lakini anasisitiza kwamba ufafanuzi huu lazima utumike katika Kutoka 20:13.

Hata hivyo tunapoona tafsiri zingine, kama vile kuua na tunatambua kwamba ufafanuzi wa mauaji unalingana na muktadha wa Kutoka 20:13, wala si dhana ya mauaji yanayowezekana kama vile adhabu ya kifo. Kwa kulazimisha neno ratsach kuwa na ufafanuzi sawa kila mahali, Dan anadai kuwa amepata ukinzani. Dan alisema: “ni lazima mhubiri wa kisasa awe na akili kuliko watafsiri wa Kiebrania ikiwa wanadai kwamba ratsach inamaanisha “mauaji” pekee (1992, ukurasa wa 207-208). Lakini dai si kwamba neno hilo linamaanisha kuua pekee, bali ni kwamba katika muktadha wa kutoka 20;13 muktadha unaonyesha kwamba neno hilo linamaanisha kuua. Kwa kweli, Barker lazima awe na akili kuliko taifa zima la Waebrania na wanaisimu wote tangu wakati wa kuandikwa kwa Biblia ili aweze kuthibitisha kwamba ratsach haiwezi kumaanisha mauaji katika Kutoka 20:13, wakati muktadha na maana za kawaida za neno huruhusu kuwa hivyo. Upotovu wake wa kimantiki wa kusawazisha, hata hivyo, uko wazi na hauna udhuru kwa mtu ambaye amekuwa akijifunza Biblia yake na kujadili kwa miaka mingi.

Njia pekee sahihi ya kuamua maana ya neno lenye maana nyingi ni kuangalia muktadha. Katika muktadha wa Kutoka 20:13 na maagizo mengine ya kuepusha “kuua,” maana iliyo wazi ni kwamba baadhi ya aina za mauaji, kama vile mauaji ya kukusudia kwa sababu ya nia mbaya, yamekatazwa, huku aina nyingine za mauaji, kama vile yale yanayofanywa na serikali kama adhabu kwa makosa Fulani, inaruhusiwa.

Matumizi ya neno letu la Kiingereza “Kill” yanatoa mfano mzuri wa jinsi maneno yanavyoweza kutumiwa. Tuseme: “Ni kosa kumuua jirani yako” lakini kisha tunasema, “Si kosa siku zote polisi kumuua jirani yake” Je, kauli hizi mbili zinapingana? Hapana. Si kama katika tukio la kwanza tunatumia neno “kuua” kumaanisha kuua kwa makusudi, kwa nia mbaya, n.k., lakini pili tunamaanisha kwamba polisi anaweza kumpiga risasi jirani yake ikiwa jirani yake alikuwa akimpiga risasi, au alikuwa akimshikilia mateka kwa mtutu wa bunduki, n.k. Kauli za Biblia kuhusu mauaji, na adhabu ya kifo hazipingani.

Kando na utata huu unaodaiwa, Dan na wasioamini kuwa kuna Mungu pia wanapinga kwamba si haki kwa Mungu kuwa katika nafasi ya kuamua wakati kuua kunakubalika au la. Wanadai kwamba wanadamu wanapaswa kuwa na haki sawa ya kuamua ni nani anayeishi na kufa jinsi Mungu anavyo paswa kuwa. Hivyo, wasema, Mungu hawezi kuwa na uwezo wa kuamua ni wakati gani kuua kunahalalishwa  ikiwa wanadamu hawako katika hali hiyo hiyo. Sheria zile zile lazima zitumike kwa Mungu kama wanadamu wote. Barker alitoa maoni haya: “kwa nini Mungu ni wa pekee?” (2008, ukurasa 204). Wasio amini Mungu huwa wanapuuza, hata hivyo, dhana ya idhini. Sio kila mtu ana mamlaka sawa ya kutoa adhabu. Ingawa ni kweli kwamba mwizi anaweza kustahili kifungo cha miaka 10 gerezani, mtu mmoja hawezi kukamata mwizi, kumfungia katika chumba chake cha chini kwa miaka kumi na kuzingatiwa kuwa  na maadili. Ni serikali pekee iliyo na haki ya kumshtaki mwizi, kumpata na hatia na kumhukumu kifungo Mlinzi hawezi kuingia katika gereza la shirikisho na kuwaua wafungwa wote walio hukumiwa kifo, ingawa wamehukumiwa kifo. Kwa nini? Kwa sababu mtu huyo hana idhini ya kuua watu hao. Mungu ana mamlaka juu ya uhai na kifo kwa sababu Yeye huwapa, na anajua mawazo yote ya wale wanaotenda uhalifu na matokeo yote ya adhabu anayotoa (Tazama Butt,2004). Mabishano ya wasioamini kwamba Mungu na wanadamu wana haki sawa juu ya mambo ya uhai na kifo yana kasoro za kimantiki.

Kwa kuhitimisha maagizo ya kibiblia kuhusu kuua, yanapotazamwa katika muktadha na sio sawa, yanapatana wazi wazi na bila kupingana. Aina Fulani za mauaji, kama vile mauaji ya kukusudia yanayofanywa kwa nia mbaya, yanatambuliwa kwa urahisi kutokana na muktadha kama mauaji yaliyo katazwa. Ingawa adhabu ya kifo inayotolewa na mamlaka inayofaa haijadiliwi katika taarifa za Biblia dhidi ya “kuua.” Madai ya kupingana kwa Biblia yanayoonyesha usomi na ukosefu huo wa unyoofu yapasa kuonwa na mtazamaji mwenye akili timamu kuwa uthibitisho dhidi ya kutokuamini kuwako kwa Mungu na usahihi na umoja wa Biblia. Barker, Dan (2008), godless (Berkeley, CA: Ulysses Press).

Rejea

Butt, Kyle and Dan Barker (2009), The Butt/Barker Debate: Does the God of the Bible Exist? (Montgomery, AL: Apologetics Press).

Butt, Kyle (2004), “The Skeptic’s Faulty Assumption,” [On-line], URL: https://apologeticspress.org/articles/2230.

Butt, Kyle (2007), Behold! The Word of God, (Montgomery, AL: Apologetics Press).

“Equivocation” (2009), Wikipedia, [On-line], URL: http://en.wikipedia.org/wiki/Equivocation


Published

A copied sheet of paper

REPRODUCTION & DISCLAIMERS: We are happy to grant permission for this article to be reproduced in part or in its entirety, as long as our stipulations are observed.

Reproduction Stipulations→