KURUKA NDANI YA GIZA?
Mojawapo ya mistari iliyotumiwa vibaya sana katika maandiko yoteni2Wakorintho 5:7: “Maana twaenenda kwa Imani, si kwa kuona.”Mara nyingi,walewanaofafanua maneno ya mtume Paulo wanaeleza kwamba Imani haimaanishikitukidogo kuliko ujuzi, yaani, wanafundisha kwamba ni lazima tukubaliuthibitisho kwa upotofu na kuwa na imani kubwa. Wengi wanaoitwa waalimunawahubiri, wanapotoa maoni kuhusu 2 Wakorintho 5:7, wana bishana kwa ajiliyakutenganisha Imani na ukweli. Mwana theolojia wa Kijerumani HansKungalishikilia wazo hili la Imani ya kibiblia alipoandika: “Basi, hata katikaImani hakuna uhakika usio na shaka. Kwa Imani, ni lazima tujitoe kwajambolisilo hakika (1980, uk, 61). Sawa na wazo la Kung kuhusu Imani na kauliyamwinjilisti Robert Chuller, ambaye alipendekeza: “Imani ni kujitoleakwadhana isiyoweza kuthibitishwa” (1984). Ikiwa watu hawa wako sahihi, Imaniniama kitu kisicho na uthibitisho wowote au kitu kinachojumuisha kiasi kidogocha ujuzi na dozi kubwa ya kutokuwa na uhakika ambayo inaruhusu wanaumekutenda kama wanajua kila kitu wakati, kwakweli, hawajui. Je, hii ndiyoainaya imani ambayo Paulo alikuwa akiizungumzia alipoandika waraka wake wapilikwa Wakorintho?
Wakorintho wa pili 5:7 imekuzwa na kufafanuliwa na mstari wa 16 wasurahiyohiyo “Hata imekuwa sisi tangu sasa hatumjui mtu awaye yote kwa jinsiyamwili, Ingawa sisi tumemtambua Kristo kwa jinsi ya mwili, lakinisasahatumtambui hivi tena.” Kwa maneno mengine hapo awali Yesu alikuwepo katikamwili, na alikuwa akionekana kwa macho. Lakini wakati Paulo alipokuwaakiandika nyaraka zake kwa Wakorintho, hali ilikuwa imebadilika kwani Kristohakuwepo duniani. Hivyo, Mtume Paulo anafafanua usemi wake kuhusu “kwajinsiya mwili ” na kimaandiko “ lakini sasa hatumtambui hivi tena. ”Nikwelikwamba Kristo anaweza kufahamika sasa, lakini si katika mwili. KamaPauloalipoandika waraka wapili kwa Wakorintho wakati Yesu alipo kuwa katikamwiliduniani, hivi vifungu (5:7, 16) kamwe visingejumuishwa katika maoniyake.Lakini kwa kuwa viliandikwa muda kidogo baada ya kupaa kwa Kristo, basiPauloalilazimika kufanya ulinganisho alioufanya katika 2 Wakorintho 5:7.
Hoja yake, kwa urahisi kabisa, ili kuwa hii. Kulikuwa na wakati ambapoimanina kuona vilienda sambamba. Hivyo ni kusema, wakati fulani katika historia,wanadamu walitembea kwa imani kwa sababu ya kuona. (Yohana 4:41; 20:25-29).Hata hivyo, hatimaye wafuasi wa Yesu walikuwa na imani ndani yake ambayohaikujengwa juu ya kuona, bali juu ya mambo kama vile, ushuhuda wa kuaminika,kupunguzwa na ufunuo. Yesu alionesha kibali chake kwa wale ambao imaniyaoinategemea ujuzi ulio patikana kwa njia nyingine isipokuwa kwa kuonaalipomwambia Tomaso mwenye shaka. “Yesu akamwambia, wewe kwa kuwa umeniona,umesadiki; wa heri wale wasioona wakasadiki.” (Yohana 20:29).
Leo wakristo wanaweza kuwa na imani ya kweli bila kuona, kwasababu yamambokama vile ushuhuda wenye kutegemeka kutoka kwa mashahidi wenye kutegemekawaliojionea (kama vile Petro, Yakobo, Yohana na Paulo) na njia nyinginezozaujuzi ambazo siyo lazima zitegemee kuona jambo fulani kwanza (1 Petro 1:8-9).Sote tuna aminika katika watu, mahali na matukio ambayo hatujawahikuonakibinafsi, lakini hiyo haipunguzi ukweli wao. Wala kukosekana kwakuonahakudhoofishi imani inayotolewa mara kwa mara kupitia ushuhuda wa kuaminikakutoka kwa watu wa zamani ambao walishuhudia mambo kama hayo. Ni dhahiri,mtuanaweza kutembea kwa imani si kwa kuona na bado akawa na imani yenye ujuzi.
MAREJEO
Kung, Hans (1980), Does God Exist? (New York: Doubleday).
Schuller, Robert (1984), “The Hour of Prayer,”February 5.
UCHAPISHAJI NA VIELELEZO: Tunafurahi kutoa ruhusa kwa makalahiikunukuliwa kwa sehemu au kwa ukamilifu, mradi masharti yetu yatazingatiwa.
REPRODUCTION & DISCLAIMERS: We are happy to grant permission for this article to be reproduced in part or in its entirety, as long as our stipulations are observed.