Kuliitia Jina la Bwana
Kwakufikiria jinsi watu wengi katika jumuia ya wakristo hufundisha kwamba mtu anaweza kuokolewa kwa kudai tu kwamba anamwamini Kristo, haishangazi kwamba watu wenye kulitilia shaka hudai kwamba Biblia inajipinga yenyewe katika jambo hilo. Ingawa Petro na Paulo walitangaza kwamba “kila mtu atakaye liitia jina la Bwana ataokolewa” (Matendo ya Mitume 2:21; Warumi 10:13; Yoeli 2:32), wenye shaka wanawakumbusha upesi wasomaji wao kwamba Yesu alisema wakati mmoja: “Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni” (Mathayo 7:21; Luka 6:46). Inadaiwa Mathayo 7:21 inakinzana na vifungu kama vile Matendo ya Mitume 2:21 na Warumi 10:13 (Tazama Morgan, 2003; Wells, 2001). Kwa kuwa wengi wanao dai kuwa wakristo wanaonekana kusawazisha “kuliitia jina la Bwana” na wazo la kumwambia Yesu, “Bwana niokoe” Wachambuzi wa Biblia wanahisi kuwa wana haki hata zaidi katika tamko lao la “ushuhuda wenye kupingana.” Je, ni jinsi gani watu Fulani wanao daiwa kuwa wafuasi wa Kristo wanaweza kudai kwamba waliokolewa kwa “kumwita Kristo,” wakati Kristo mwenyewe alitangaza kwamba kumwita tu hakungemwokoa mtu?
Ufunguo wa kuelewa kwa usahihi kifungu cha maneno “kuliitia jina la Bwana” ni kutambua kwamba mengi yanahusika katika tendo hili kuliko ombi la maneno tu linalo elekezwa kwa Mungu. “wito” unaotajwa katika Matendo 2:21, Warumi 10:13, na Matendo 22:16 (ambapo Paulo alikuwa akiliitia jina la Bwana”), haulinganishwi na wito (“Bwana, Bwana”) ambayo Yesu aliyazungumza katika mahubiri ya mlimani (Mathayo 7:21).
Kwanza, inafaa kutaja kwamba hata katika nyakati za kisasa “kumwita” mtu mara nyingi humaanisha mengi zaidi ya kuomba tu jambo Fulani. Daktari anapo enda hospitalini ili kuwaita baadhi ya wagonjwa wake, yeye haendi tu chumbani nakusema “nilitaka tu kupita na kusema ‘Halo’ nakutakia kila lakheri, sasa nilipe.” Badala yake, anajihusisha katika huduma. Anamchunguza mgonjwa, anasikiliza mahangaiko ya mgonjwa, anatoa maagizo zaidi kuhusu kupona kwa matumaini kwa mgonjwa, na kisha mara nyingi kuagiza dawa. Vipengele hivi vyote vinaweza kuhusishwa na daktari kumwita mgonjwa katikati ya karne ya ishirini. Ilikuwa kawaida kwa vijana “kuwaita” wasichana, tena wito huu ulimaanisha kitu tofauti kuliko tu “kufanya ombi” (Brown, 1976, ukurasa 5).
Pili, mtu anapochukua wakati kujifunza kuhusu usemi “kumwita Mungu” unavyo tumiwa katika maandiko, njia pekee ya kuja na hitimisho lililo sahihi, kama vile vifungu vinavyo fanana vinakuwa na maana ya ndani kwa Amerika ya kisasa. Usemi “kumwita Mungu” mara nyingi ilikuwa na maana kubwa zaidi nyakati za Biblia. Kwa mfano fikiria maneno ya Paulo katika Matendo 25:11: “nataka rufani kwa Kaisari.” Neno rufaa (epikaloumai) ni neno lile lile lililo tafsiriwa “wito” (au “kuita”) katika Matendo 2:21, 22:16, na Warumi 10:13. Lakini, Paulo hakuwa akisema tu, “Ninamwita Kaisari aniokoe.” Kama James Bales alivyosema:
“Paulo, alipokata rufaa kwa Kaisari, alikuwa akidai haki ya uraia wa Rumi ya kuhukumiwa na Kaisari. Alikuwa akiomba kwamba kesi yake ihamishwe kwenye mahakama ya kaisari na kwamba kaisari asikilize na kutoa hukumu juu ya kesi yake. Kwa kufanya hivyo, alionyesha kwamba Kaisari asikilize na kutoa hukumu juu ya kesi yake. Kwa kufanya hivyo, alionyesha kwamba alikuwa akiegemeza kesi yake kwenye hukumu ya kaisari. Ili jambo hili lifanyike ilimbidi Paulo ajitiishe kwa lolote lililokuwa la lazima ili kesi yake iletwe mbele ya Kaisari. Ilimbidi kujisalimisha kwa askari wa Kirumi waliompeleka Rumi. Ilimbidi kutii taratibu au utaratibu wowote ambao kaisari alidai kwa wale waliokuja mbele yake. Haya yote yalihusika katika rufaa yake kwa Kaisari (1960, ukurasa 81-82).
“Wito” wa Paulo kwa Kaisari ulihusisha kujitiisha kwake. T. Pierce Brown, aliandika kwa ufupi kuwa kumwita Bwana huhusisha utiifu (1976, uk.5). Siyo kumtambua Mungu kwa maneno tu, au ombi la mdomo kwake. Wale ambao Paulo (kabla ya kugeuzwa kwake kwa Kristo) alitaka kuwafunga huko Dameski wakristo waliofafanuliwa kuwa “waliitialo jina Lake (Yehova)” hawakuwa watu walio Sali tu kwa Mungu, bali wale waliokuwa wakimtumikia Bwana; na ambao, kwa utii wao walikuwa wakijitiisha kwa mamlaka yake (Mathayo 28:18). Kwa kuvutia, Sefania 3:9 inaunganisha “mwito” wa mtu na utumishi wake: “Maana ndipo nitakapo warudishia mataifa lugha iliyo safi, wapate wote waliitie jina la Bwana, wamtumikie kwa nia moja.” Mtu anapo jitiisha kwa mapenzi ya Mungu anaweza kuelezwa kwa usahihi kuwa “kumwita Bwana” Matendo 2:21 na Warumi 10:13 (miongoni mwa vifungu vingine) havipingani na Mathayo 7:21. Kwa sababu kumwita Bwana kunahusisha zaidi ya kusihi tu wokovu; inahusisha kujitiisha kwa mapenzi ya Mungu. Kulingana na Wakolosai 3:17, kila tendo moja ambalo mkristo anafanya (kwa neno au tendo) linapaswa kutekelezwa na mamlaka ya Kristo. Kwa asiye mkristo anayepokea wokovu, hii siyo tofauti. Ili kupata wokovu, mtu lazima anyenyekee kwa mamlaka ya Bwana. Hivi ndivyo vifungu katika Matendo 2:21 na Warumi 10:13 vinafundisha kuwa ni juu yetu kwenda kwingine katika Agano Jipya ili kujifunza jinsi ya kuliitia jina la Bwana.
Baada ya Petro kunukuu unabii wa Yoeli na kuwaambia wale waliokuwa Yerusalemu siku ya Pentekoste kwamba “kila mtu atakaye liitia jina la Bwana ataokolewa” (Matendo 2:21), aliwaambia jinsi ya kwenda “kuliitia jina la Bwana.” Watu katika hadhira katika Matendo 2 hawakuelewa nukuu ya Petro ya Yoeli kumaanisha kwamba mwenye dhambi mgeni lazima aombe kwa Mungu kwaajili ya wokovu. Swali lao katika Matendo 2:37 (ndugu zetu tufanye nini?) linaonyesha hivyo. Zaidi ya hayo, Petro alipojibu swali lao na kuwaambia la kufanya ili waokolewe, yeye hakusema, “mimi tayari nimekuambia la kufanya. Unaweza kuokolewa kwa kumwomba Mungu akupe wokovu kupitia maombi. Liitieni tu jina Lake.” Badala yake, Petro alilazimika kuwaeleza maana ya “kuliitia jina la Bwana. Badala ya kurudia usemi huu wakati umati ulipotafuta mwongozo zaidi kutoka kwa mitume, Petro aliwaamuru akisema, “Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu” (Matendo 2:38). Zingatia usambamba kati ya Matendo 2:21 na 2:38.
| Matendo 2:21 | Kila atakaye | liitia | jina la Bwana | ataokolewa |
| Matendo 2:38 | Kila mmoja | Tubuni mkabatizwe | Kwa jina lake yesu Kristo | kwa ondoleo la Dhambi. |
Wasikilizaji wa Petro wasio wakristo walijifunza kwamba “kuliitia jina la Bwana kwa wokovu” ilikuwa sawa na kutii Injili, ambayo takriban watu 3,000 walifanya siku hiyohiyo kwa kutubu dhambi zao na kubatizwa katika Kristo (2:38, 41). Lakini vipi kuhusu Warumi 10:13? Je ni wito gani uliotajwa kwenye aya hii? Angalia Warumi 10:11-15:
“Kwa maana andiko lanena, kila amwaminiye hata tahayarika. Kwamaana hakuna tofauti ya myahudi na myunani; maana yeye yule ni Bwana wa wote, mwenye utajiri kwa wote wamwitao. Kwakuwa kila atakayeliitia jina la Bwana ataokoka. Basi wamwiteje yeye wasiyemwamini? Tena wamwaminije yeye wasiye msikia? Tena wamsikieje pasipo mhubiri? Tena wahubirije, wasipopelekwa? Kama ilivyo andikwa, ni mizuri kama nini miguu yao wahubirio habari ya mema!
Ingawa kifungu hiki hakifafanui kwa usahihi kile kinacho maanishwa na mtu “kuliiitia jina la Bwana” Kinaonyesha kwamba mtenda dhambi mgeni hawezi “kuita” hadi baada ya kusikia Neno la Mungu na kuliamini. Hilo linamaanishwa na maswali ya Paulo ya kiajabu: Basi watamwombaje yeye ambaye hawakumwamini? Na watamwaminije yeye ambaye hawakusikia habari zake? Matamshi ya Paulo katika kifungu hiki yanapatana na matamshi ya Petro katika Matendo 2. Ilikuwa tu baada ya umati wa watu siku ya Pentekoste kumwamini Kristo aliyefufuka ambaye Petro alimhubiri (kama inavyoonekana kwa “kuchomwa mioyoni” na swali lao lililofuata, “tutendeje ndugu zetu?”) kwamba Petro aliwaambia jinsi ya kuliitia jina la Bwana na kuokolewa (2:38).
Labda maelezo ya wazi zaidi ya maana ya mtenda dhambi mgeni “kuliitia jina la Bwana” yanapatikana katika Matendo 22. Mtume Paulo alipokuwa akihutubia umati wa watu huko Yerusalemu, alizungumza kuhusu kukutana kwake na Bwana, ambaye alimwomba “Nifanye nini?” (Matendo 22:10; 9:6). Jibu ambalo Yesu alimpa wakati huo halikuwa “kuliitia jina la Bwana.” Badala yake, Yesu alimwagiza “simama ,uingie Dameski, na huko utaambiwa habari za mambo yote yaliyoamriwa uyafanye” (Matendo 22:10). Paulo (au Sauli Matendo 13:9) alionyesha Imani yake katika Yesu alipoingia jijini na kusubiri maagizo zaidi. Katika Matendo 9, tunajifunza kwamba katika siku tatu zilizo fuata, alipokuwa akisubiri kukutana na Anania, Paulo alifunga na kuomba (mstari 9,11). Ingawa wengine leo wanaweza kufikiria kile ambacho Paulo alikuwa akifanya wakati huu kuwa “kuliitia jina la Bwana.”
Anania mjumbe mteule wa Mungu kwa Paulo, hakufikiri hivyo. Hakumwambia Paulo, “naona tayari umemwita Mungu. Umesamehewa dhambi zako.” Baada ya siku tatu za kufunga na kuomba, Paulo bado alikuwa amepotea katika dhambi zake. Ingawa kwa hakika aliamini katika hatua hii, na alikuwa amesali kwa mungu, bado alipaswa “kuliitia jina la Bwana” kwa wokovu. Wakati Anania hatimaye alikuja kwa Paulo, alimwambia: simama ubatizwe, ukaoshe dhambi zako, ukiliitia jina lake” (Matendo 22:16). Anania alijua kwamba Paulo alikuwa bado ‘hajaliitia jina la Bwana kama Petro alivyo jua kwamba wale waliokuwa kwenye Pentekoste hawakufanya hivyo kabla ya amri yake ya kutubu na kubatizwa. Hivyo, Anania alimwagiza Paulo abatizwe na kuoshwa dhambi zake. Kishazi kishirikishi “kuliitia jina la Bwana” kinaeleza kile ambacho Paulo alikuwa akifanya alipo batizwa kwaajili ya ondoleo la dhambi zake. Kila asiye mkristo anayetamani “kuliitia jina la Bwana ili kuokolewa,hufanya hivyo, si kwa kusema tu, “Bwana, Bwana” (Mathayo 7:21) au kwa kusema tu sala kwa Mungu kama Paulo (Matendo 9:22; Warumi 10:13-14), lakini kwa kutii maagizo ya mungu ya “tubu na kubatizwa…..katika jina la Yesu Kristo mpate ondoleo la dhambi zenu” (Matendo 2:38).
Hii haimaanishi kwamba toba na ubatizo vimekuwa (au kwa kawaida leo) vimekuwa ni sawa na “kuliitia jina la Bwana.” Ibrahimu hakubatizwa wakati “alipoliitia jina la Bwana” (Mwanzo 12:8; 4:26), kwa sababu ubatizo haukutakiwa na Mungu kabla ya nyakati za Agano Jipya. Na kama nilivyo eleza hapo awali, wakati Agano Jipya linapoeleza watu ambao tayari ni wakristo kama “wanaoliitia jina la Bwana” (Matendo 9:14, 21; 1 Wakorintho 1:2), kwa hakika haimaanishi kwamba wakristo daima walikuwa wakibatizwa kwa ondoleo la dhambi zao baada ya kubatizwa na kuwa mkristo. (1 Yohana 1;5-10). Kutegemea wakati na mahali ambapo kishazi “kuliitia jina la Bwana” kinatumika kunajumuisha (1) utiifu kwa mpango wa injili ya wokovu; (2) kumwabudu Mungu; na (3) utumishi mwaminifu kwa Bwana (Bates, 1979, uk. 5). Hata hivyo, haitumiki kamwe katika maana ya kwamba mwenye dhambi mgeni ili aokolewe ni lazima alie na kusema “Bwana, Bwana niokoe.”
Kwa hiyo, madai ya wasioamini kwamba Mathayo 7:21 inapingana na Matendo 2:21 na Warumi 10:13 hayana uthibitisho. Na, yule anayedai kuwa mkristo anayefundisha kwamba yote ambayo mtu lazima afanye ili kuokolewa ni kusema tu maombi ya mwenye dhambi, yuko katika makosa.
REJEA
Bales, James (1960), The Hub of the Bible—Or—Acts Two Analyzed (Shreveport, LA: Lambert Book House).
Bates, Bobby (1979), “Whosoever Shall Call Upon the Name of the Lord Shall be Saved,” Firm Foundation, 96:5, March 20.
Brown, T. Pierce (1976), “Calling on His Name,” Firm Foundation, 93:5, July 20.
Morgan, Donald (2003), “Biblical Inconsistencies,” [On-line], URL: http://www.infidels.org/library/modern/donald_morgan/inconsistencies.shtml.
Wells, Steve (2001), Skeptic’s Annotated Bible, [On-line], URL: http://www.Skepticsannotatedbible.com.
_______________________________________________________________
Imechapishwa 26-Mei 2004
UZALISHAJI NA KANUSHO: Tuna furaha kutoa ruhusa ili Makala haya yanakiliwe kwa sehemu au kwa ukamilifu, mradi tu masharti yetu yazingatiwe.
Masharti ya uzalishaji
REPRODUCTION & DISCLAIMERS: We are happy to grant permission for this article to be reproduced in part or in its entirety, as long as our stipulations are observed.