Menu

Kufuru dhidi ya Roho Mtakatifu “Dhambi Isiyo Sameheka”

Kwa miaka mingi, waandishi wengi wamechukua jukumu la kueleza maoni yaliyosemwa na yesu kuhusu “dhambi isiyoweza kusamehewa”-kufuru dhidi ya Roho mtakatifu. Kutokana na maandishi haya kumekuja mafundisho mengi ya uwongo, uzushi, na maelezo yaliyo pendekezwa. Ni kusudi la mamlaka haya kueleza “kufuru dhidi ya Roho mtakatifu” kuwa si nini na ni nini hasa, na kutoa maoni kuhusu kama bado kunaweza kufanywa leo.

Masimulizi matatu kati ya manne ya  injili yana marejeleo ya kauli aliyo sema Yesu kuhusu kumkufuru Roho Mtakatifu. Vifungu hivi vitatu vinasomeka hivi.

“Kwa sababu hiyo nawaambia, kila dhambi na kila neno la kufuru watasamehewa wanadamu, ila kwa kumkufuru Roho hawatasamehewa. Na mtu yeyote atakaye nena neno juu ya mwana wa Adamu atasamehewa, bali  yeye atakayenena neno juu ya Roho Mtakatifu hatasamehewa, katika ulimwengu wa sasa, wala katika ule ujao.”(Mathayo 12:31-32).

“Amin, nawaambia, Dhambi zote watasamehewa wanadamu, na kufuru zao watakazo kufuru zote; bali mtu atakaye mkufuru Roho Mtakatifu hana msamaha hata milele; ila atakuwa ana dhambi ya milele, kwa vile walivyosema, Ana pepo mchafu.”(Marko 3:28-30).

“Na kila mtu atakaye nena neno juu ya mwana wa Adamu atasamehewa, bali aliye mkufuru Roho Mtakatifu hatasamehewa.”(Luka 12:10).

Kila moja ya vifungu hivi kwenye maneno yaliyo semwa na Yesu yanathibitisha kwamba Yesu alisema waziwazi kwamba kuna dhambi ambayo haitasamehewa. Biblia ya American Standard Version inaeleza dhambi kama “dhambi ya milele” (Marko 3:29). Yesu alifafanua dhambi hiyo kuwa “kufuru dhidi ya Roho.” Kumkufuru Roho ni nini basi?

Ili kuelezea dhambi hii kikamilifu, ni muhimu kuangalia muktadha wa jumla wa taarifa. Mathayo anatoa habari nyingi zaidi kuhusu mazingira ambayo maneno ya Yesu yalitolewa. Katika (Mathayo 12:22), andiko hilo linaonyesha kwamba mtu Fulani aliyekuwa na roho waovu aliletwa kwa Yesu ili aponywe. Kama ilivyo kuwa desturi yake ya kawaida, Yesu alimtoa pepo mchafu, na kumponya mtu huyo upofu wake na ububu. Baada ya kuona muujiza huo wa nguvu umati ulimfuata yesu na Kuuliza, “Je, huyu anaweza kuwa mwana wa Daudi?” (12:23). Walipo sikia maneno hayo, mafarisayo, wakitaka kudharau chanzo ambacho Yesu alipokea mamlaka yake walitangaza kwamba Yesu alikuwa akitoa pepo kwa “Belzebuli, mkuu wa pepo.” Yesu aliendelea kueleza kwamba Ufalme uliogawanyika wenyewe haungeweza kusimama, na kama alikuwa akitoa pepo kwa nguvu za mapepo, basi angekuwa anajishinda mwenyewe. Ilikuwa baada ya shtaka hili la mafarisayo, na utetezi wa Yesu wa matendo yake, kwamba Kristo alitoa maoni kuhusu kumkufuru Roho. Kwa kweli, andiko la Marko linasema waziwazi kwamba Yesu alitoa maelezo kuhusu kufuru dhidi ya Roho “Kwasababu walisema, ‘ana roho mchafu.’”

Kipande kingine muhimu cha habari kinacho hitajika kufafanua kauli ya Yesu ni ufafanuzi wa kufuru. Wayne Jackson aliandika: “kufuru imetokana na neno la Kigiriki “blasphemia,” ambalo wanazuoni wanaamini kwamba huenda linatokana na mizizi miwili, “blapto” kuumiza, na “pheme”kusema. Neno hilo lingependekeza taarifa mbaya.” (2000). Bernard Franklin, katika Makala yake kuhusu kufuru dhidi ya Roho Mtakatifu, alipendekeza:

Neno “kufuru” katika namna zake mbali mbali (kama kitenzi, nomino, kivumishi, n.k) lilionekana kama mara hamsini na tisa katika agano Jipya. Ina tafsiri mbali mbali kama vile kufuru, kutukanwa, kusemwa vibaya, n.k. Mifano ya tafsiri hizi mbalimabali ni: “Walio pita walitukanwa naye.” (Mathayo 27:39). “Yeye atakaye kufuru” (Marko 3:29). “Wale waliokuwa wakipita njiani walimtukana” (Marko 15:29). “Njia ya kweli itasemwa vibaya” (2 Petro 2:2). “Hawa huyanena mambo haya mabaya” (Yuda 10). Ni ushahidi kutokana na hili kwamba kufuru ni dhambi ya kunena, dhambi ya ulimi. Waandishi wote wa Agano Jipya isipokuwa mwandishi wa Waebrania anatumia hilo neno (1936, uk.224-225).

Zaidi ya hayo, Yesu alifafanua neno hili wakati, baada ya kurejelea kukufuru, alitumia maneno “anasema neno dhidi” kwenye (Mathayo 12:32).

IPI SIYO DHAMBI ISIYO SAMEHEKA

Kwa kuufanyia kazi ufafanuzi wa maana ya kukufuru ni “kusema dhidi” au “kusema vibaya,” ni rahisi kukataa dhambi kadhaa ambazo hazistahili kuwa dhambi isiyo weza kusamehewa. Mara kwa mara mauaji yanapendekezwa kama dhambi isiyosameheka. Hivyo haiwezi kuwa hivyo. Kwanza, kwa kuwa kufuru ni dhambi ya ulimi, mauaji hayange angukia katika kundi hili. Pili, vifungu kadhaa vya Biblia vinaonyesha dhambi ya kuua inaweza kusamehewa. Mfalme Daudi alipofanya uzinzi na kuamuru Uria Mhiti auawe, nabii Nathan alimjia, na kumwarifu kwamba Mungu ameona kwamba Daudi “alimuua Uria Mhiti kwa upanga” (2 Samweli 12:9). Daudi alipoungama kwa Nathani na kutubu, nabii alimwambia Daudi “BWANA naye ameiondoa dhambi yako;  hamtakufa” (2 Samweli 12:13). Na ingawa Daudi aliadhibiwa kwa ajili ya uovu wake, alisamehewa. Biblia inaonyesha wazi kwamba kuua siyo dhambi isiyo weza kusamehewa.

Uzinzi hujitokeza kama dhambi nyingine inayowekwa mbele kama isiyoweza kusamehewa. Bado mawazo yale yale yanayo tumika kupunguza mauaji kama dhambi isiyosameheka inaweza kutumika kuondosha uzinzi. Kwanza, hailingani na kategoria ya kufuru. Pili Daudi alisamehewa uzinzi, kama vile tu alivyosamehewa mauaji. Mtume Paulo alitoa orodha ya dhambi zisizo pungua kumi (pamoja na uzinzi) ambazo ndugu wa Korintho walikuwa wamesamehewa           (1 Wakorintho 6:9-11). Uzinzi haiwezi kuwa dhambi isiyo sameheka.

Dhambi nyingine iliyowekwa wazi kama dhambi isiyoweza kusamehewa ni kufuru ya aina yoyote, si hasa dhidi ya Roho mtakatifu. Tunajua, hata hivyo, kwamba kufuru kwa ujumla haiwezi kusamehewa kwa sababu mbili. Kwanza, katika muktadha wa dhambi isiyoweza kusamehewa, Yesu alisema wazi kwamba “kufuru zozote” ambazo wanadamu wanaweza kusema (mbali na Roho Mtakatifu) zinaweza kusamehewa. Pili Paulo alikiri kwamba kabla ya kuongoka kwake, hapo awali alikuwa “mtukanaji, mtesaji, na mtu mwenye jeuri; lakini nilipata rehema kwa sababu nilifanya hivyo bila kujua” (1 Timothy 1:13). Hivi vifungu viwili vya Biblia uwezo wa kufuru kwa ujumla kuwa dhambi isiyo sameheka.

Basi, tunaanza kuona kwamba hatuwezi kuamua kiholela ni dhambi zipi tunazodhania kuwa ni mbaya, alafu tu kuzihusisha nazo kuwa hazina msamaha, hasa tukizingatia ukweli kwamba hata wale waliokuwa na hatia ya kumsulubisha mwana wa Mungu walipata fursa hiyo ya kusamehewa. (Matendo ya Mitume 2:36-38). Kwa hiyo, kwa vile dhambi isiyo sameheka inaangukia katika kundi lake lenyewe, na haiwezi kuwa mauaji, uzinzi, kufuru ya jumla n.k., baadhi ya wanachuoni wameweka dhana kwamba dhambi isiyo samehewa si dhambi hata moja, lakini badala yake ni hali ya ukaidi wa mtu ambaye anadumu katika kutokuamini. Uelewa huu, hata hivyo, unashindwa kutilia maanani muktadha wa sasa wa “dhambi isiyo sameheka” Gus Nichols, akitoa maelezo juu ya wazo hili la “kudumu katika kutokuamini” alisema: “Ni kweli umati mkubwa wa watu wanaingia katika uasi dhidi ya Mungu ili wapotee hatimaye na milele; bali ni kwaajili ya kukataa na kupuuza msamaha unao tolewa kwa neema katika injili wakati wanaishi, si kwa sababu wametenda dhambi isiyo weza kusamehewa.” (1967, ukurasa  236). Wendell Winkler, chini ya sehemu yenye kichwa cha habari “kukufuru dhidi ya Roho mtakatifu siyo,” aliandika kwamba, sivyo kuahirishwa kwa utii hadi kufa. Andiko hilo linadokeza kwamba wale wanaotenda dhambi ya milele wanaendelea kuishi huku wakiwa wamepoteza nafasi yote ya wokovu; ambapo wale wanao ahirisha utii kwa Kristo (isipokuwa wale wanao fanya dhambi ya milele) wangeweza kutii wakati wowote kabla ya kifo chao (1980, ukurasa  20).

KATIKA WAKATI HUU AU WAKATI UJAO

Yesu alisema kwamba kufuru dhidi ya Roho haitasamehewa “katika ulimwengu huu au ujao” (Mathayo12:32). Mashirika Fulani ya kidini yameshikilia kauli hii ili kupendekeza kwamba Yesu anafikiria hali ambayo dhambi Fulani zitaondolewa baada ya kifo-lakini si dhambi hii. Wazo hili ya hali inayo fanana na toharani, ambapo roho za wafu zimepewa “nafasi ya pili” ya kufanya toba kwa ajili ya dhambi walizofanya katika maisha yao ya kidunia, halipati uhalali wowote katika kauli hii iliyotolewa na Kristo (wala katika kifungu kingine chochote katika Biblia kuhusu jambo hilo). R.C.H. Lenski alisema kwamba matumizi ya Yesu ya maneno yaliyo jadiliwa yalimaanisha “kabisa kamwe” (1961, ukurasa  484). Hendriksen alikubaliana na Lenski alipoandika:

Kwa kupita , ifahamike kwamba maneno haya bila hata chembe ya mawazo yanamaanisha kwamba kutakuwa na msamaha wa dhambi Fulani huko akhera. Kwa maana yoyote hawaungi mkono fundisho la toharani. Usemi huo unamaanisha tu kwamba dhambi iliyoonyeshwa haitasamehewa kamwe (1973, ukurasa  528).

Kama vile mwandishi wa Waebrania alivyo andika kwa ufupi, “Na kama vile watu wanavyo wekewa  kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu.” (Waebrania 9:27).

Pia imependekezwa na waandishi kadhaa kwamba “zama ijayo” iliyo jadiliwa na Yesu inarejelea enzi ya Ukristo. Kulingana na wazo hili, Yesu alitoa tamko hilo katika enzi ya Kiyahudi, wakati sharia ya Musa ilipo fanya kazi, na “zama itakayo kuja” iliashiria enzi ya kikristo iliyo fuata mara moja, wakati sharia ya Kristo ingetawala. Kuweka maana hii kwenye maneno mara nyingi huwaongoza watetezi wa nadharia hii kuhitimisha kwamba dhambi isiyo weza kusamehewa inaweza kufanywa katika enzi ya kikristo, baada ya ufufuo wa Kristo. Kama Winkler alivyo sikia “Kwahiyo, kwa kuwa Bwana wetu alikuwa akizungumza wakati enzi ya kiyahudi ilikuwapo, alikuwa akithibitisha kwamba kufuru dhidi ya Roho mtakatifu haita samehewa katika (a) enzi ya Kiyahudi, wala katika (b) enzi ya ukristo. , umri uliofuata” (1980, ukurasa  21).

Nichols, baada ya kuthibitisha pendekezo hilo hilo, alihitimisha:

Inafuata kwamba dhambi hii, kwa hiyo, inaweza kutendeka wakati wa huduma ya kibinafsi ya Kristo, na kisha ikafanywa kama tulivyoona, na inaweza pia kufanywa chini ya enzi ya injili au kipindi cha injili. Wangeweza kuhusisha kazi za Roho kwa shetani baada ya Pentekoste, sawa na hapo awali (1967, ukurasa  234).

Sehemu mbili za msingi za ushahidi, hata hivyo, zinapinga wazo la Yesu la kurejea “zama zijazo” kulimaananisha enzi ya ukristo. Kwanza katika (Marko 10:30), mwandishi wa injili ame mnukuu Yesu akitumia huo usemi (“katika wakati ujao”) kurejelea wakati ambapo wafuasi wa Kristo wangerithi uzima wa milele (tazama Luka 18:30). Hii ni kumbukumbu ya wazi ya maisha baada ya kifo, kwa kuwa Paulo alisema “mwili na damu haziwezi kurithi ufalme wa Mungu” (1 Wakorintho 15:50). Pili masimulizi ya Marko kuhusu dhambi isiyo weza kusamehewa yanafafanua dhambi kuwa “dhambi ya milele.” Wafasiri wa New King James Version waliandika kwamba mtu anayetenda dhambi “hana msamaha kamwe, bali yuko chini ya hukumu ya milele” (Marko  3:29). Akaunti ya Marko, pamoja na msisitizo wake juu ya umilele, inaonyesha kwamba maneno hayo yana maana ya kusisitiza ukweli kwamba dhambi hii haitasamehewa kamwe” (Lenski, ukurasa  484). Basi, si sahihi kutumia maneno “katika wakati ujao” kurejelea toharani. Pia ni ngumu kutumia kifungu hicho kurejelea Enzi ya ukristo. Ufafanuzi bora zaidi, ni kumnukuu Hendrickson tena, ni kwamba “usemi huo unamaanisha tu kwamba dhambi inayoonyeshwa haitasamehewa kamwe” (ukurasa  528).

DHAMBI ISIYO SAMEHEKA NI IPI

Kama ilivyo elezwa hapo awali, kumkufuru Roho Mtakatifu ndiyo dhambi pekee katika Biblia inayopewa hadhi ya kutosamehewa au ya milele. Kwa hakika, Yesu alitanguliza mjadala wake wa dhambi hiii kwa kusema kwamba, “kila dhambi na kufuru watasamehewa mwanadamu” isipokuwa kukufuru dhidi ya roho. Kwa kutumia maana inayo fanya kazi ya kufuru kama “kusema mabaya,” inakuwa wazi kwamba dhambi iliyo elezwa na Yesu ilikuwa “dhambi ya ulimi” ambayo mafarisayo walikuwa wameifanya, au angalau walikuwa karibu na hatari ya kuifanya.

Mafarisayo walikuwa wamefanya nini ambacho kingewaweka katika hatari ya kutenda dhambi isiyosameheka? Kulingana na ushuhuda wake mwenyewe, wakati wa Yesu hapa duniani alitoa pepo kwa “Roho wa Mungu” (Mathayo 12:28). Mafarisayo walipoona kwamba Yesu alikuwa amefanya muujiza wa kuthibitishwa, hawakuweza kubishana na ukweli kwamba Kristo alikuwa na nguvu Fulani ambazo wengine (pamoja na wao wenyewe) hawakuwa nazo. Kwa hiyo ili kutia mashaka juu ya huduma ya Yesu, walidai kwamba alikuwa akitoa pepo kwa Belzebuli, mtawala wa pepo. Jina Belzebuli ni jina lingine la shetani (Franklin, 1936, ukurasa 227), kama inavyo weza kuonekana kutokana na marejeo ya Yesu kwa Shetani katika (Mathayo 12:26). Hata walipokabiliwa na utendaji wa kimiujiza wa Roho Mtakatifu kupitia kwa Yesu, mafarisayo walikuwa, kimsingi, wakihusisha nguvu za Yesu kwa shetani, na kudai kwamba Yesu alikuwa “shetani mwenye mwili badala ya Mungu mwenye mwili.” Ni hivi, na si kingine chochote, ambacho Bwana wetu anaita kufuru dhidi ya Roho Mtakatifu. (Franklin, ukurasa  227). Maxie Boren aliandika: “Muktadha wa Mathayo 12:22 na kuendelea inaonyesha wazi kwamba hii ilikuwa kweli dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu kuhusisha muujiza uliofanywa na Yesu kwa nguvu za shetani. Yesu alisema imenywa na “Roho wa Mungu” (mtari wa 28) lakini wao (mafarisayo) walisema imefanywa na Belzebuli. Ni wazi kwamba kufuru dhidi ya Roho mtakatifu ni ya uhakika, dhambi moja, ambayo ingeweza kufanywa na mafarisayo wakati wa maisha ya Yesu.

JE,DHAMBI ISIYOSAMEHEWA NI SAWA NA ILE DHAMBI YA MAUTI?

Yohana katika waraka wake ule wa kwanza, alitaja ukweli kwamba “kuna dhambi iletayo mauti” na kuna “dhambi isiyo ya mauti.” (Yohana 5:16-17). Kauli yake katika mistari hii imeunganishwa na zaidi ya watu wachache na maelezo ya Yesu kuhusu “dhambi ya milele.” Hata hivyo, ni wazi kwamba uhusiano huo unategemea zaidi maoni kuliko kujifunza Biblia kimaandishi.

Kwanza, hakuna ushahidi wa kibiblia unao unganisha kifungu katika 1 Yohana na mashtaka ya mafarisayo. Zaidi ya hayo, muktadha wote wa 1 Yohana huwapa wasomaji wakristo tumaini la kusamehewa dhambi zote ambazo huenda walitenda. Yohana aliandika hivi: “Tukiziungama dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu na kutusafisha na udhalimu wote.” (1 Yohana 1:9). Katika upeo wa waraka wa Yohana, ukosefu wowote wa uadilifu uliofanywa na wasomaji wake ungeweza kusamehewa ikiwa mkosaji angechukua hatua zinazofaa zinazodaiwa na Mungu ili kupokea msamaha unaopatikana. Kwa upande mwingine, kufuru dhidi ya Roho ilikuwa dhambi mahususi, ya milele ambayo kamwe isingesamehewa.

JE, DHAMBI ISIYO SAMEHEKA INAWEZA KUTENDWA LEO?

Swali linalofuata linalo ulizwa kwa kawaida kuhusu dhambi hii ni kama bado inawezekana kufanywa leo au la. Maoni juu ya swali hili hakika yanatofautiana, na wasomi wanaonekana kugawanyika katika nafasi zao. Ushahidi, hata hivyo, unaonekana kuelekezwa kwenye wazo kwamba dhambi hii haiwezi kufanywa leo. Kwanza mazingira ambayo dhambi inaelezwa hayawezi kushinda leo, kutokana na ukweli kwamba enzi ya miujiza imekoma (tazama miller, 2003). Hakuna mtu leo ambaye atakuwa na fursa ya kushuhudia Yesu akitenda miujiza ana kwa ana (2 Wakorintho 5:16).

Pili. Hakuna mtajo mwingine wa dhambi katika kifungu chochote cha Biblia kilicho andikwa baada ya ufufuo wa Kristo. Hakuna hata mmoja wa waandishi wa Agano Jipya walio vuviwa anaye rejelea dhambi katika waraka wowote au katika kitabu cha matendo, na hakuna anayetoa maonyo kwa waongofu wapya kuhusu kuepuka dhambi hiyo baada ya Pentekoste. Franklin aliona:

Ikiwa ingewezekana kufanywa, je, kusingekuwa na onyo Fulani dhidi yake? Je kungekuwa na hatari yoyote kuhusu jambo hilo, je mtume Paulo, aliyeandika nusu ya vitabu vya Agano Jipya, angekosa kuonya dhidi ya utume wake? Paulo hata hataji kukufuru dhidi ya Roho Mtakatifu. Dhambi inayozungumziwa kwa hakika ilitendwa katika siku za huduma ya Bwana wetu duniani, lakini haifuati kwamba ingetendwa akiwa hayupo (ukurasa  233).

Katika kujadili suala hili, Gus Nichols aliandika: “Inaonekana kwamba dhambi zote zilizofanywa leo zinaweza kusamehewa, na kwamba wote wanaweza kuokolewa, “ikiwa watafanya” (1967, ukurasa  239). V.E. Howard, alitoa maoni sawa na hayo aliposema kwamba “hakuna dhambi isiyo sameheka leo” (1975, ukurasa  156).

Kwa kuhitimisha, kumkufuru roho mtakatifu ndiyo dhambi pekee isiyoweza kusamehewa inayotajwa katika Biblia, na inatajwa katika muktadha wa mafarisayo wakimshtaki Yesu kuwa amepagawa na Ibilisi. Muktadha unaonyesha kwamba ilikuwa ni dhambi mahususi, na si msururu wa dhambi zinazoweza kusamehewa, au mtazamo wa kuendelea kutokuamini. Baada ya ufufuo, hakuna mwandishi aliye vuviwa anaye taja dhambi hiyo na hakuna maonyo yoyote dhidi yake yaliyo andikwa. Hakuna ushahidi thabiti kwamba inaweza kufanywa leo. Ukweli kwamba haukutajwa baada ya ufufuo, unajitokeza kwenye wazo kwamba bado hauwezi kufanywa. Kwa kweli, dalili kutoka kwenye vifungu kama vile (1 Yohana 1:7, 9) ni kwamba “ukosefu wote” ambao mtu anaweza kufanya leo unaweza kusamehewa kwa damu ya Yesu. Kama vile Howard alivyo sema alipomalizia maelezo yake kuhusu dhambi ya milele: “katika andiko hilo hilo  Bwana wetu alitoa uhakikisho kamili kwamba kila dhambi na kufuru dhidi ya ‘Mwana wa Adamu’ atasamehewa. Leo injili ya Kristo inapaswa kuhubiriwa kwa kila mtu duniani na kila mtu atakaye tii injili ataokolewa (Marko 16:15-16) (ukurasa  157)

REJEA

Boren, Maxie B. (no date), “The Blasphemy Against the Holy Spirit,” Class Handout, Brown Trail church of Christ, Bedford, Texas, Lesson 4.

Franklin, Barnard (1936), “The Blasphemy Against the Holy Ghost: An Inquiry into the Scriptural Teaching Regarding the Unpardonable Sin,” Bibliotheca Sacra, 93:220-233, April.

Hendriksen, William (1973), The Gospel According to Matthew (Grand Rapids, MI: Baker).

Howard, V.E. (1975), The Holy Spirit (West Monroe, LA: Central Publishers).

Jackson, Wayne (2000), Blasphemy—What Is This Great Sin?, [On-line], URL: https://www.christiancourier.com/articles/168-blasphemy-what-is-this-great-sin.

Lenski, R.C.H. (1961 reprint), The Interpretation of St. Matthew’s Gospel (Minneapolis, MN: Augsburg).

Miller, Dave (2003), “Modern-day Miracles, Tongue-speaking, and Holy Spirit Baptism: A Refutation,” Reason and Revelation, 23(3):17-23, March.

Nichols, Gus (1967), Lectures on the Holy Spirit (Plainview, TX: Nichols Brothers).

Winkler, Wendell, ed. (1980), What Do You Know About the Holy Spirit? (Fort Worth, TX: Winkler Publications).

UZALISHAJI NA KANUSHO:Tuna furaha kutoa ruhusa ili Makala haya yanakiliwe kwa sehemu au kwa ukamilifu, mradi tu masharti yetu yatazingatiwa.

Masharti ya uzalishaji.


Published

A copied sheet of paper

REPRODUCTION & DISCLAIMERS: We are happy to grant permission for this article to be reproduced in part or in its entirety, as long as our stipulations are observed.

Reproduction Stipulations→