Menu

Kanisa la Mungu na Uungu wa Kristo

Kanisa ambalo Wakristo wote wanapaswa kuwa sehemu yake ni kanisa la Mungu. Ingawa wengi wanaojiita Wakristo hudai kuwa washiriki wa kanisa ambalo Mungu alilianzisha karibu miaka 2000 iliyopita,mara nyingi wao huvaa majina yanayoonyesha umiliki wa, au utii kwa, wanaume (au ofisi za wanadamu). Wengine hujiita “kanisa la kilutheri” (baada ya Martin Luther). Wengine hujiita baada ya viongozi wa mahali walioteuliwa  wa kanisa, kama Episcopalians (kutoka neno la Kigiriki kwa mzee). Maandiko, hata hivyo yanaweka wazi kwamba kanisa ambalo watoto wote wa Mungu wanapaswa kuwa wamoja si kanisa lililoanzishwa na mwanadamu (1 Wakorintho 1:10-17). Wakristo lazima wakubali ukweli kwamba kanisa la Agano Jipya ni kanisa la Mungu, si la mwanadamu.

Mara kadhaa katika agano Jipya, neno “kanisa” (kigiriki ekklesia) linaunganishwa pamoja na neno la Kigiriki “Theos” (Mungu), na hivyo mtu anaweza kuthibitisha kwa urahisi ukweli kwamba kanisa ambalo waumini watiifu wanashiriki ndilo kanisa lililoanzishwa na kumilikiwa na Mungu. Paulo aliandika “kanisa la Mungu lililoko Korintho” (1 Wakorintho 1:2; 2 Wakorintho 1:1), na baadaye akawaamuru Wakorintho “[msiwe] kosa kwa kanisa la Mungu.” (1 Wakorintho 10:32-33). Alikiri kwa makanisa ya Galatia kwamba alikuwa “amelitesa kanisa la Mungu” kabla ya kuwa Mkristo (Wagalatia 1:13). Paulo pia aliwaandikia Wakristo wa Thesalonike, akiwakumbusha jinsi walivyokuwa “waigaji wa makanisa ya Mungu yaliyoko Yudea” (1 Wathesalonike 2:14), na hata kujisifu kuwahusu “kati ya makanisa ya Mungu yaliyoko Yudea” (1 Watheselonike 2:14), na hata kujisifu kuwahusu “kati ya makanisa ya Mungu” kwa saburi yao kwa mateso (2 Watheselonike 1:3-4). Mtu lazima asikose uhakika kwamba kanisa la Agano jipya ni kanisa la Mungu. Ni asili ya Kiungu na imara kulingana na “kusudi la milele” la Uungu (Waefeso 3:11).

Jambo la kupendeza ni kwamba mara nyingi waandishi wa Biblia hurejelea “kanisa la Mungu” kuwa mwili au kanisa la Kristo. Karibu na mwisho wa barua yake kwa Wakristo huko Roma, Paulo aliandika: “makanisa yote ya Kristo yawasalimu” (Warumi 16:16). Aliwafundisha Wakristo wa Korintho jinsi walivyokuwa “viungo kibinafsi” vya “mwili wa Kristo” (1 Wakorintho 12:27). Kwa kuwa Paulo alijulisha makanisa ya Efeso na Kolosai kwamba kanisa ni mwili wa Kristo (Waefeso 1:22-23; Wakolosai 1:18, 24), mwili wa Kristo ni sawa na kanisa la Kristo (4:11-12). Kwa ufupi, ni kanisa la Yesu. Aliahidi kulijenga akisema “nitalijenga kanisa Langu” (Mathayo 16:18), na baadaye akalinunua “kwa damu yake mwenyewe” (Maatendo 20:28; Waefeso 1:7, 14; Waebrania 9:14).

Mistari hii haiwafahamishi Wakristo tu juu ya majina ambayo wanapaswa kujitambulisha kwayo,  pia yanaonyesha jambo muhimu kuhusu asili ya Kristo. Ingawa baadhi ya wanaodaiwa kuwa waamini wa Biblia (kama vile mashahidi wa Yehova), wanadai kwamba Yesu si Mungu, uhakika wa kwamba waandishi wa Biblia walisawazisha “kanisa la Mungu na mwili/kanisa la Kristo” ni mojawapo ya uthibitisho mwingi kwamba Yesu ni Mungu. Paulo mara kwa mara alitumia misemo hii kwa kubadilishana katika nyaraka zake zote. Hivyo, kusema kanisa ni la Kristo ni kusema kanisa ni la Mungu, kwa sababu Kristo ni Mungu (Yohana 1:1-3; 20:28). Yeye ndiye kichwa, Mwokozi, Mkombozi, na mmiliki wa kanisa (Waefeso 5:23; Wakolosai 1:18). Na tujiweke chini ya utii wa Kristo kama Mungu (Waefeso 5:24), na tuvae majina ya kimaandiko tu kama vile “kanisa la Mungu” au “kanisa la Kristo.” Katika maneno ya mtume Paulo kwa  wazee wa Efeso: “Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa dammu  yake mwenyewe”(Matendo 20:28).


Published

A copied sheet of paper

REPRODUCTION & DISCLAIMERS: We are happy to grant permission for this article to be reproduced in part or in its entirety, as long as our stipulations are observed.

Reproduction Stipulations→