Jehanamu na Uwepo wa Mungu Kila Mahali
Swali
Kwakuwa Mungu yuko kila mahali, je, hilo lamaanisha kuwa atakuwepo Jehanamu?
A.
Bila shaka Biblia inaonyesha kwamba Mungu anajua yote na yuko daima. “Wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake, lakini vitu vyote vi utupu na kufunuliwa machoni pake Yeye aliye na mambo yetu” (Waebrania 4:13).
Kupitia Nabii Yeremia Mungu aliuliza hivi “Mimi ni Mungu aliye karibu, asema Bwana, Mimi si Mungu aliye mbali. Je mtu yeyote anaweza kujificha mahali pa siri, nisimwone? Asema BWANA. Je, mbingu na nchi hazikujawa…? Asema BWANA” (Yeremia 23:23-24). Kwakweli Mungu hujaza mbingu na dunia. Sulemani alisema “Lakini Mungu je? Atakaa kweli kweli juu ya nchi? Tazama mbingu hazikutoshi, wala mbingu za mbingu; sembuse nyumba hii niliyo ijenga!” (1 Wafalme 8:27). Hakuna awezaye kuukimbia uso wa Mungu (Zaburi 139:7). Yeye ni mjuzi wa vyote na yuko kila mahali.
Hata hivyo, Biblia husema juu ya uwepo wa Mungu katika maana tofauti. Mungu yupo kwenye kiti cha enzi mbinguni (Waebrania 8:1; 12:2; Ufunuo 21:5). Sulemani alitaja Mbingu kama makao ya Mungu ambako Yeye husikia maombi ya watu wake (1 Wafalme 8:30). Mungu yuko ndani na kati ya kanisa lake (1 Wakorintho 3:16). Ingawa Mungu ameuficha uso wake kutoka kwa wenye dhambi ambao wamejitenga kiroho na Mungu (Isaya 59:1-2), Mungu bado anaijaza dunia uwepo wake, akijua na kuona kila kitu (Waebrania 4:13; Yeremia 23:23-24). Zaidi ya hayo, ingawa Mungu yuko pamoja na wakristo (Waebrania 13:5), na yuko duniani kila wakati. Mungu pia amefanya matukio ya moja kwa moja, ya mara kwa mara katika sura za roho au za kimwili (Mwanzo 18:1; Matendo 23:11).
Biblia inafunua kwamba Mungu yuko hata katika sheoli (makao ya wafu kwa Kiebrania na Kigiriki Hades ambapo wenye haki na wasio haki huenda wanapo kufa “sheol” 1986). Mwandishi wa Zaburi aliuliza “Niende wapi nijiepushe na Roho yako? Niende wapi niukimbie uso wako? Kama ningepanda mbinguni, wewe uko; Ningefanya kuzimu kitanda chake, wewe uko.” (Zaburi 139:7-8). Ayubu alitangaza kwamba “Kuzimu na uharibifu wa wazi mbele za BWANA; si zaidi basi, mioyo ya wanadamu?” (Ayubu 26:6; tazama Mithali 15:11). Ikiwa mtu anaingia kwenye maisha baada ya kifo paradise (Luka 23:43; 16:22) au mateso Luka 16:23), Mungu yuko huko kwa namna Fulani. Anajua yote na anaona yote.
Akielezea nia yake yake kuacha maisha haya ya sasa na kuwa pamoja na Yesu Paulo aliandika “Basi siku zote tuna moyo mkuu; tena twajua yakuwa, wakati tuwapo hapa katika mwili, tunakaa mbali na Bwana. Maana twaenenda kwa Imani, si kwa kuona.” (2 akorintho 5: 6-7; tazama Wafilipi 1:23). Kwa maana moja, Kristo alikuwa “pamoja na Paulo” kama mkristo na mtume (Mathayo 28:20; Matendo 18: 10), kwa maana nyingine alipokuwa hapa duniani Paulo “hakuwapo kwa Bwana” (2 Wakorintho 5:6) kwa mara nyingine tena, maandiko yanarejelea uwepo wa Mungu katika maana tofauti.
Mwishowe, waliookolewa “watakutana na Bwana hewani” na “watakuwa na Bwana daima” (1 Watheselonike 4:17). Tunaenda mahali ambapo ametutayarishia na kuwa pale anaposema “Mimi (Mungu) nipo” (Yohana 14:2-3). Lakini vipi kuhusu wakaaji wa kuzimu na uwepo wa Mungu kila mahali? Inaweza kuonekana kwamba, kwakuwa Mungu aliumba kuzimu kwaajili ya ibilisi, malaika zake na waovu wote (Mathayo 25:41), na kwakuwa Biblia huweka wazi kwamba kabla ya hukumu Mungu ana aina Fulani ya uwepo katika kuzimu na paradise ijapokuwa kuna shimo kubwa linalotenganisha paradise na kuzimu (Luka 16:26), uwepo wa Mungu uko kuzimu kwa namna Fulani. Ingawa kwa upande mmoja waovu watatengwa na Mungu milele (Mathayo 7:23; 25:41), na hawataepuka kamwe hukumu Yake ya milele na milele.
REJEA
“Sheol” (1996), Nelson’s Illustrated Bible Dictionary (Electronic Database: Biblesoft).
REPRODUCTION & DISCLAIMERS: We are happy to grant permission for this article to be reproduced in part or in its entirety, as long as our stipulations are observed.