Menu

Je, Yesu Kristo Alikuwepo katika umbo la Mungu Akiwa Duniani?

KUMBUKA: Mwandishi wa Makala yafuatayo alikuwa mwanzilishi mwenza wa AP. Hivi majuzi alipita kutoka kwa maisha haya hadi mahali pazuri zaidi. Hata hivyo, “yeye akiwa amefariki angali anazungumza” (Waebrania 11:4).

Baadhi ya waandishi wahafidhina wamejaribu kutetea wazo la kwamba Nafsi ya pili ya Uungu wakati wa kufanyika mwili (yaani, “Neno alifanyika mwili” (Yohana 1:14), “aliweka kando namna ya Mungu.” Wanadai kwamba dhana ya Mungu asiye na mwisho kuvikwa ndani ya mwili wa mwanadamu haina mantiki. Ingawa waandishi hawa bila shaka wanamaanisha vyema msimamo wao ni potofu kabisa kuhusu asili ya Kristo mwenye mwili.

Hoja kadhaa zimetumika katika kujaribu kusisitiza msimamo huu. Kwa mfano, imejadiliwa: (a) Mungu hawezi kujaribiwa (Yakobo 1:13); lakini (b) Yesu alijaribiwa (Waebrania 2:18). Kwa hivyo, hitimisho linafaa kuwa: Yesu hakuwepo katika umbo la Mungu.

Matokeo ya kimantiki ya msimamo huu ni kwamba Yesu Kristo hakuwa Mungu katika mwili. Watetezi wa maoni haya kwa kawaida hawamaanishi kuthibitisha kwa uwazi hitimisho hilo, lakini hapo ndipo mawazo kama hayo yanapoongoza. Jambo ambalo waandishi hawa wameshindwa kutambua, kuhusiana na Yakobo 1:13, ni kwamba Mungu Baba si Kristo Mwana anaonekana katika muktadha huo. Yakobo hakuwa anajadili asili na/au jukumu la Kristo. Kwa hiyo, haifai kujumlisha juu ya asili ya Bwanakutoka kwa kumbukumbu hii fupi.

Andiko ambalo kwa kawaida lilivutia kama uthibitisho kwamba Yesu hakuwepo duniani katika “umbo la Mungu” ni Wafilipi 2:6. Hapa kuna Muktadha kamili wa kile Paulo aliandika:

Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani        ya Kristo Yesu; ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya   Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha      kushikamana nacho; bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa      namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa mwanadamu; tena alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa   mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba (Wafilipi 2:5-8).

Lakini msimamo unaotetewa sio sahihi kwasababu zifuatazo:

Katika Wafilipi 2:6, Paulo alisema juu ya Kristo kuwa “yuko katika namna ya Mungu.” Neno “iliyopo” haipo katika wakati uliopita. Inatafsiri neno la Kigiriki “huparchon,” neno la wakati uliopo. Wakati wa sasa unaonyesha kuwepo kwa Mwokozi, katika “umbo la Mungu,” ni hali iliyo dumishwa ya kuwa, si ile iliyokatizwa na kupata mwili. A.T. Robertson aliangazia tofauti kati ya wakati uliopo, “huparchon” (inayomaanisha kuwapo milele katika “morphe” yaani (umbo) la Mungu), na Bwana kuwa kwa mfano wa mwanadamu (1931, 4:445). Kulikuwa na wakati ambapo Nafsi ya pili ya Uungu haikuwepo kama mwanadamu; hakujawa na wakati ambapo hakuwa katika “umbo la Mungu.”

W.E. Vine alitoa maoni kwamba umbo hili la kisarufi linaashiria “kuwepo au hali zote mbili zilizopita kwa mazingira yaliyotajwa na kuendelea baada yake” (1991, p, 279). Msomi mwingine alibainisha kuwa neno hilo linaonyesha “kuendelea kwa hali au hali iliyo tangulia” (Abbott-Smith, 1923, p. 457). Hendriksen alikuwa sahihi kabisa alipouliza: “Kristo alijivua nini mwenyewe? Hakika si kuwepo kwake katika umbo la Mungu.” (1962, p. 106). Wuest alikuza umbo la wakati uliopo wa kiima kwa kupendekeza kwamba Yesu “siku zote amekuwa na hata sasa anaendelea kuishi” katika umbo la Mungu (1961, ukurasa 462). Sio lazima kuzidisha mifano ya ziada.

Kinyume na uthibitisho, hata hivyo, imedaiwa kwamba ingawa Kristo alikuwepo katika umbo la Mungu Kabla ya kupata mwili alijitenga na hadhi hiyo alipokuwa duniani. Hatimaye, kulingana na nadharia iliyochunguzwa, Yesu alianza tena umbo la asili ya Mungu aliporudi mbinguni. Hakuna msaada wa kibiblia kwa dhana hii, ambayo inakiuka ushuhuda wa wazi wa maandiko.

Neno la Kigiriki la “umbo” ni morphe. Neno hili linamaanisha kile ambacho ni “ashirio la asili ya ndani” ya kitu (Green, 1907, ukurasa 384), au kama Kennedy alivyoona, morphe “daima humaanisha aina ambayo kwa kweli na kikamilifu hounyesha kiumbe kinachokisimamia” (1956, 3:436). Trench alitoa maoni kwamba “hakuna anayeweza kuwa “en morphe theou” (katika umbo la Mungu) ambaye hakuwa Mungu” (1890,ukurasa 263). Haya yote yanamaanisha kwa urahisi kwamba ikiwa Yesu alitoa “umbo la Mungu” Alipopata mwili, basi alikoma kuwa Mungu wakati huo. Hilo ni sawa na fundisho linalotetewa na mashahidi wa Yehova, yaani, kwamba Kristo hakuwa “kitu zaidi ya mtu mkamilifu.” Lazima niseme, kwa njia ya upole iwezekanavyo, kwamba nafasi inayochunguzwa haiwakilishi mafundisho ya Agano Jipya.

Lakini inadaiwa kwamba Yesu hangeweza kuwepo katika “umbo la Mungu” kwa sababu Agano Jipya husema kuhusu Bwana akiongozwa na Roho, akilindwa na malaika, n.k. Kwa hiyo, ni wazi kwamba kristo hakuwa “Mungu asiye na mwisho.”

Jambo ambalo linaonekana kuwa mzizi wa kutokuelewana huku ni kushindwa kutambua kwamba mapungufu ya Bwana duniani hayakuwa matokeo ya asili ya chini ya Mungu; badala yake, yalikuwa ni matokeo ya utii uliojiwekea unaoakisi utekelezaji wa mapenzi yake makuu. Kristo “alijiweka tupu” mwenyewe alipo fanyika mwili.

A.H Strong alieleza vyema alipobainisha kwamba, kwa njia ya kupata mwili, Yesu, “hakuacha kumiliki, wala hata kutumia kabisa, bali zoezi la kujitegemea, la sifa za Kimungu” (1907, ukurasa 703). Kusema jambo lilelile kwa njia nyingine, hadhi ya Bwana kupata mwili ilihusisha, si kutenganisha umbo/kiini au sifa za kimungu, bali utiishaji wa sifa hizo kwa Baba kulingana na majukumu. Yesu alipothibitisha “Yeye Baba ni mkuu kuliko mimi” (Yohana 14:28), hakuwa anakataa asili ya Kimungu; bali, Alikuwa akidai kwamba Alikuwa amejitiisha kwa hiari kwa mapenzi ya Baba.

Fikiria kuhusu hili kwa muda: Je, Kristo angeweza kutokuwa na sifa za Kimungu, nab ado awe mtakatifu? Kitu ni jumla ya sifa zake. Huu ni ugumu usioweza kushindwa kwa wale wanaobisha kwamba Kristo mwenye mwilihakuwa katika “umbo la Mungu.”

Ikiwa Kristo hakuwa Mungu kamili, yaani, kuwepo katika “umbo la Mungu” Yeye alikuwa ni nani hasa? Robo Mungu? Mungu nusu? Je, inaonekana tu kuwa Mungu (kama wanostiki Fulani walivyoshikilia)? Mwanaume kamili tu? Je! Zaidi ya hayo, ikiwa Yesu hakuwepo katika “umbo la Mungu” alipokuwa akiishi duniani, angewezaje kudai kuwa “mmoja” (jinsia isiyo ya asili, inayodokeza umoja wa asili) na Baba (Yohana 10:30)? Kwanini Bwana alimruhusu Tomaso kumwita “Mungu” (Yohana 20:30)? Kwanini Yesu alikubali kuabudiwa (Mathayo 8;2), wakati alifundisha waziwazi kwamba ni Mungu pekee ndiye anayestahili kuabudiwa (Mathayo 4:10)?

Hatimaye, ikiwa itajadiliwa kwamba Kristo aliweka kando hadhi yake ya kuwa katika “umbo la Mungu” kwa sababu ya ubinadamu wake na utii wake kwa Baba, basi lazima mtu akubali, kuwa thabiti kwamba Yesu hana “umbo la Mungu” sasa, kwa sababu kama mpatanishi wetu Yeye ni “mwanadamu, Kristo Yesu” (1 Timotheo 2:5), nabado yuko chini ya Baba (1 Wakorintho 15:27).

Wengine wanaweza kuhisi kuwa hili ni suala la (inconsequential semantics). Hata hivyo wakati mwingine (semantics) ni muhimu sana. Kweli ya Injili ni ujumbe wa maneno, na mwalimu Mkristo anahitaji kuwa sahihi katika lugha anayotumia. Bwana na atusaidie kuwa sahihi katika usemi wa ukweli wa Biblia.

MAREJEO

Abbott-Smith, G. (1923), A Manual Greek Lexicon of the New Testament (Edinburgh: T. & T. Clark).

Green, Samuel (1907), Handbook to the Grammar of the Greek Testament (London: Religious Tract Society).

Hendriksen, William (1962), Philippians, Colossians, Philemon (Grand Rapids, MI: Baker).

Kennedy, H.A.A. (1956), “Philippians,” The Expositor’s Greek Testament, ed. W.R. Nicoll (Grand Rapids, MI: Eerdmans).

Robertson, A.T. (1931), Word Pictures in the New Testament (Nashville, TN: Broadman).

Strong, A.H. (1907), Systematic Theology (Old Tappan, NJ: Fleming H. Revell).

Trench, R.C. (1890), Synonyms of the New Testament (London: Kegan, Paul, Trench, Trubner, & Co.).

Vine, W.E. (1991), Amplified Expository Dictionary of New Testament Words (Iowa Falls, IA: World Bible Publishers).

Wuest, Kenneth (1961), The New Testament—An Expanded Translation (Grand Rapids, MI: Eerdmans).

Imechapishwa 1-Machi 1995

UZALISHAJI NA KANUSHO: Tunafuraha kutoa ruhusa ili Makala haya yanakilishwe kwa sehemu au kwa ukamilifu, mradi tu masharti yetu yazingatiwe.

Masharti ya Uzalishaji


Published

A copied sheet of paper

REPRODUCTION & DISCLAIMERS: We are happy to grant permission for this article to be reproduced in part or in its entirety, as long as our stipulations are observed.

Reproduction Stipulations→