Je Yesu Alifanya Miujiza Au La?
Bwana mmoja, aliyekuwa anahangaika na imani yake katika usahihi wa Biblia, hivi karibuni aliwasiliana na ofisi zetu, akiuliza, kwa nini Yesu aliwaambia Waandishi na Mafarisayo kwamba “hakuna ishara itakayotolewa kwa kizazi hiki” (Marko 8: 12; Mathayo 12: 39; 16: 4; Luka 11: 29). Kwa kuwa maandiko mengine yanafundisha wazi wazi kwamba Yesu alifanya “Ishara nyingi” (Yohana 12: 37; 20: 30, 31; 3: 2 na Matendo 2: 22), inakuwaje Yesu kwa kweli na bila kujipinga, aseme, “hakuna ishara itakayotolewa kwa kizazi hiki”? Kwa mujibu wa wale wanaohoji Biblia (Bible Critics), Yesu alikuwa nabii wa uongo kwa sababu, tangu “alipobashiri kwamba hakuna ishara itakayotolewa kwa hicho kizazi ni uongo wa wazi” (McKinsey, 1995 uk 114, & Wells 2010). Je Mkristo anaweza kujibuje ki-Biblia na kwa hoja madai kama hayo?
Bahati mbaya, hao wanaohoji Biblia (na baadhi ya Wakristo) wanapenda kutoheshimu muktadha, ambao kwao kauli za Biblia zinapatikana. Na bado hakuna kauli inayoweza kueleweka vizuri, bila aina fulani ya muktadha au habari za utangulizi. Maneno yanamaanisha vitu kutegemea na jinsi , lini, na wapi yametamkwa. Muundo wa hotuba zinafunga katika mila duniani kote. (Lyons 2010). Watu wa kweli. Kwa mfano, wamekuwa wakitania, wakiongeza maneno, na kutumia maneno ya kejeli kwa miaka mingi sana (Ayubu 12: 2; Zaburi 58: 3), na muda huo wakitegemea wasikilizaji wao kutafasiri lugha yao kwa usahihi na bila madai yoyote ya kudanganya. Bahati mbaya, wale wenye mashaka na uvuvio wa Biblia (skeptics), mara nyingi wanapuuza habari za lazima zinazotakiwa ili kuelewa vizuri maandiko matakatifu.
Yesu alipotoa kauli hii kwa mara ya kwanza, “hakuna ishara itakayotolewa” kwa kizazi hiki (Mathayo 12: 39; Luka 11: 29), alikuwa ametoka tu, kumponya mtu aliyekuwa kipofu, bubu na kupagawa na mapepo (Mathayo 12: 22; Luka 11: 14). Angalia kwamba, kuliko kukiri kwamba, miujiza mikuu, Yesu aliyofanya ilikuwa ni kwa kuthibitisha Uungu wake (Yohana 20: 30, 31), Mafarisyo wenye moyo mgumu walidai kwamba nguvu zake zinatokana na Shetani (Mathayo 12: 24). Hawakugeukia mbali toka wa Yesu; waligeuka nyuzi 180 mbali na ulekeo ambao miujiza kama ile iliwaongoza wale waaminifu na wenye moyo safi wanaotafuta ukweli. Na maadui wa Yesu hawakuwa wameona muujiza hata mmoja. Mapema katika Mathayo 12, Yesu alikuwa amemponya mtu mwenye mkono uliolemaa (mstari 9-13). Mafarisayo walifanya nini? Badala ya kukiri nguvu ya Kristo, “walipanga jinsi ya kumwangamiza” (Mstari 14). Ukweli ni kwamba mpaka wakati huu katika huduma ya Yesu, ameshafanya miujiza kadhaa (Mathayo 11: 4, 5), na wengi wa Waandishi na Mafarisayo walikataa kabisa kumwamini (Mathayo 9: 32-34). Bila kujali kile alichofanya Yesu wala alichosema, baadhi ya maadui wake, wasingeweza kushawishiwa (Mathayo 12: 31, 32; Angalia pia Butt 2003).
Hivyo ni nini Yesu alimaanisha aliposema kwenye matukio mawili tofauti kwamba “hakuna ishara” ambayo ingetolewa kwa “kizazi hiki” isipokuwa “Ishara ya nabii Yona” (Mathayo 12: 39; 16: 4; Marko 8: 12; Luka 11: 29)? Yesu alikuwa akiwajibu Mafarisayo waliotamani kuona ishara. Lakini walikuwa wamesha shuhudia na kusikia juu ya miujiza mingi ya Yesu. Walitaka kitu cha “zaidi”. Walitaka “ishara toka mbinguni” (Luka 11: 16; Mathayo16: 1; Marko 8: 11, pamoja na fafanuzi). Kitu ambacho maadui wa Yesu walimaanisha hasa kwa hili hatuwezi kujua. Tujuacho ni kwamba, akiwa bado duniani, Yesu alithibitisha uwezo wake juu ya nguvu za asili, magonjwa, mapepo, na kifo (Angalia Lyons & Butt, 2007), bado Mafarisayo walisema walitaka zaidi. Inaonekana, kama Burton Coffman alivyoandika, “walimaanisha maajabu yasiyo na heshima, lakini ambayo yanasisimua kwa udadisi wa binadamu (Coffman, 1984, uk 179). Yesu hata hivyo, mara kwa mara alikataa kufanya miujiza ya namna hiyo. Alikataa kugeuza mawe kuwa mikate au kujirusha kutoka kilele cha mlima wa Hekalu, kwa sababu tu Shetani alimtaka afanye hivyo (Mathayo 4: 1-7). Yesu angeweza kufanya muujiza wowote aliotaka – ikiwa ni pale alipojaribiwa na Shetani, alipochochewa na Herode (Luka 23: 8 – 12), au alipojaribiwa na Mafarisayo. Angeweza kuvuta Sungura kutoka kwenye kofia kwa lengo zima la kuwafurahisha watu, angeweza kubadilisha maadui zake wayahudi kuwa mawe, au akawapa macho matatu, angeweza kuamuru mvua ya kawaida inyeshe paka na mbwa. Angeweza kuchoma nguo za mafarisayo kwa moto kwa kufyatua vidole vyake na kuwaambia kwamba Jehanamu kutakuwa na moto huo mara kumi. Angeweza kufanya idadi yoyote ya miujiza. Lakini Mafarisayo wasio waaminifu hawakuona chochote kati ya hayo (“hakuna ishara kama hizi zitakazotolewa”).
Ni ishara gani ambayo ingetolewa? Zaidi ya aina ya miujiza ambayo maadui wa Kristo wameshaikataa, ishara pekee nyingine ambayo Yesu alitabiri ilikuwa ni “ishara ya nabii Yona” (Mathayo 12: 39; 16: 4; Luka 11: 29) – kufa, kuzikwa na kufufuka kwa Yesu.
Kwa uhakika kabisa Yesu alifanya miujiza, na ingawa Yesu, “alijinyenyekeza, … akatwaa namna ya mtumwa” (Wafilipi 2: 7, 8), alikataa kuingia kwenye ngazi ya kiroho ya daima ya maadui zake. Hakufanya miujiza ya aina ya miujiza Mafarisayo waliyotaka kuona. Lakini hakufanya makosa, alifanya aina nyingi za miujiza ambayo alizitoa kwa watu wanye moyo wa uaminifu ushahidi wa kutosha kufikia hitimisho kwamba Kristo ni Mwana wa Mungu hasa (Yohana 20: 30, 31)
Rejea
Butt, Kyle (2003), “Blasphemy Against The Holy Spirit – The Unpardonable Sin”
Coffman, Burton (1984), “Matthew”
Lyons, Eric (2010), “The Twelve”
Lyon, Eric & Kyle Butt (2007), “The very Works that I Do Bear Witness Of Me
McKinsey, Dennis (1995), “The Encyclopedia Of Biblical Errancy
Wells, Steve (2010), “Did Jesus Perfom Many Signs And Wonders”?
REPRODUCTION & DISCLAIMERS: We are happy to grant permission for this article to be reproduced in part or in its entirety, as long as our stipulations are observed.