Menu

JE WATOTO HUZALIWA NA DHAMBI?

Je, umewahi kuona uso wa mtoto mchanga, kugusa ngozi laininamashavu yake ya rangi ya ua la rozi na kuhisi kutokuwa nahatiawakati unayatazama macho yake mazuri? Ni kinyume kabisanamafundisho ya Katoliki yanayodai kwamba “watoto wadogo niwenyedhambi!” Katekisimu ya kanisa katoliki inatangaza hivyo: 

Wakiwa wamezaliwa na asili ya ubinadamu iliyoanguka na kuchafuliwana dhambi ya asili, watoto pia wanahitaji kuzaliwa upyakatikaubatizo ili kuwa huru kutokana na nguvu za giza nakuletwa katika ulimwengu wa uhuru wa watoto wa Mungu ambao wanadamuwotewameitiwa. 

Biblia inafundisha kwamba watoto hawabebi dhambi za wazaziwao(Kutoka 32:32-33; Kumbukumbu la torati 24:16; 2 Wafalme 14:6;2Nyakati 25:4; Yeremia 31:30; Ezekieli 18:20). Hatahivyo,wakatoliki kwa haraka wanabainisha kwamba Daudi alitangazakwakusema: “ Tazama mimi naliumbwa katika hali ya uovu; mamayangualinichukua mimba hatiani” (Zaburi 51:5). Ili kuelewa funguhili,ni lazima kukumbuka kwamba somo la Zaburi 51 linahusu dhambiyaDaudi, na sio dhambi ya asili. Zingatia nomino na viasiliambavyoDaudi alitumia kuashiria kwamba dhambi aliyokuwa akiizungumziani dhambi aliyoifanya. “ uyafute makosa yangu ”(vs.1); “unioshekabisa na uovu wangu, unitakase dhambi zangu ”(vs.2); “Maananimejua mimi makosa yangu na dhambi yangu i mbele yangudaima”(vs.3); “Nimekutenda dhambi wewe peke yako”(vs.4); n.k.Hakunakidokezo hata kidogo cha aina fulani ya dhambi ya asili katikaduaya mtunga Zaburi. Alikuwa anazungumza kuhusu dhambi aliyoifanyana kutaka kuwekwa huru. 

Lakini, kwa nini alirejelea wakati ambapo aliumbwa katika tumbolauzazi la mama yake? Mtunga Zaburi angeweza kutumia tamathalimubaalagha (Zaburi 58:3; Colley, 2004), au kusisitiza haliambayomama yake alimzaa kwayo. Katika kisa cha mwisho, ingawa alizaliwabila dhambi, alizaliwa katika ulimwengu ambao ulikuwa umefunikwawenye taabu na kusukumwa na dhambi. 

Fikiria pia kwamba mtunga Zaburi aliomba msamaha akiwa mtumzima.Alitumia vitenzi vya wakati uliopo kuomba msamaha. “EeMunguunirehemu…uyafute makosa yangu.”(vs.1); “Unioshe kabisanauovuwangu, unitakase dhambi zangu ” (vs.2); “Maana nimejuamimimakosa yangu ” (vs.3); “ Unisafishe kwa hisopo naminitakuwasafi”; “Unifanye kusikia furaha na shangwe”; “Usitiriusowako usitazame dhambi zangu; Uzifute hatia zangu zote ”(vs.9); “Uniumbie moyo safi, uifanye upya roho iliyo tulia ndaniyangu”(vs.10). 

Maombi ya Daudi ya kuomba kusamehewa yalitokana nadhambializozifanya muda mrefu baada ya kuzaliwa kwake. MtungaZaburimwenyewe aliweka ukweli huu wazi katika kifungu sambamba,ambapoaliomba: “Usiyakumbuke makosa ya ujana wangu wala maasiyangu”(Zaburi 25:7).  Ikiwa Zaburi ya 51 ni ombi la kuhitaji kuwa huru kutokananadhambi ya asili, wakatoliki hueleza je kwamba Mungu alimtiamafuta,akambariki, na kumtumia Daudi alipo kuwa amebeba dhambiyamwanadamu wa kwanza?

Zaidi ya hayo, mtunga zaburi alitangaza ya kwamba “ameumbwa”na“alichukuliwa mimba” katika uovu (zaburi 51:5). Hili sirejeleola kuzaliwa (kama ukatoliki unavyodai), bali mimba.Ilikukubaliana na wazo la Kikatoliki kwamba zaburi ya 51inaungamkono fundisho la dhambi ya asili, ni lazima tufikiemuafakakwamba dhambi ya asili hupitishwa wakati wa kuchukua mimba.Ikiwani hivyo, kanisa Katoliki litalazimika kufanyia kaziupyatheolojia yake kuhusu ubatizo ili kujumuisha njia ya “kubatiza”watoto kabla ya kuzaliwa ili kuwaokoa kutoka kwenye “nguvuzagiza” (Katekisimu…1994, 1250). 

Ili kufikia tafsiri sahihi ya Zaburi 51, lazima pia tuzingatievifungu vingine vya Biblia ambapo maneno yanayofanana yanatumiwa.Kwa mfano Isaya alisema: “ Bwana ameniita tangu tumboni;tokatumbo la mama yangu amenitaja jina langu”(Isaya 49:1).KwenyeYeremia 1:5, Mungu anamwambia nabii wake: “Kabla sijakuumbakatika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni nalikutakasa.”Ikiwa kwa usemi “ Tazama mimi naliumbwa katika hali yauovu”(Zaburi 51:5), Daudi alidokeza juu ya dhambi ya asili aliyobeba,wakatoliki wanaelezaje matamko ya Isaya na Yeremia ya utakatifutangu tumbo la uzazi? Je hawa Manabii wawili walizaliwabilakuchafuliwa na dhambi ya asili? Kulingana na ukatoliki, niYesunaMaria pekee waliozaliwa katika hali takatifu kabisa. Vifunguhivihaviwezi kupatanishwa na Imani ya kikatoliki ya dhambi yaasili(tazama Colley, 2004). 

Lakini, vipi kuhusu Warumi 5:12, ambapo mtume Paulo aliandika:“Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni,nakwadhambi hiyo mauti na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwasababuwote wamefanya dhambi?. ” Je, kifungu hiki kinafundishakwambatumerithi dhambi ya Adamu? La hasha!. Tukitazama Makalazingine(Pinedo, 2009), kifungu hiki kinafundisha kwamba kifoyaanimatokeo ya dhambi ilisambaa kwa watu wote, sio kwasababuAdamualitenda dhambi, bali “kwasababu wote wametenda dhambi”(5:12; Warumi 3:23). Bila shaka haya yote hayawezi kumrejelea Adamupekee.Hakuna chochote katika biblia kinachofundisha, kinachoonesha,aukudokeza kwamba watoto huzaliwa na dhambi. 

Paulo alionesha kwamba pasipo na sheria, hakuna dhambi(Warumi3:20; Yohana 15:22). Na mtume Yohana alitangaza kwamba “dhambiniuasi” (1 Yohana 3:4). Ikiwa mtoto mchanga hawezi kujua sheriayaMungu au kuelewa, hawezi kufanya uasi. 

Yesu mwenyewe alisema: “ Waacheni watoto wadogo waje kwangu,msiwazuie; kwa maana watoto kama hawa ufalme wa Mungu niwao”(Marko 10:14). Paulo alisema hakuna aliye mchafu atakayeingiakatika ufalme wa mbinguni (Waefeso 5:5). Yesu aliongezea:“Basiyeyote ajinyenyekezaye mwenyewe kama mtoto huyu, huyo ndiyealiyemkuu katika ufalme wa mbinguni” (Mathayo 18:3). Kama watotohujaduniani na asili ya mwanadamu iliyo anguka na kuchafuliwanadhambi ya asili (kwa kutumia maneno ya katekisimu), kwaniniwatuwanapaswa kuwa kama watoto wadogo ambao wamechafuliwa nadhambi?Biblia iko wazi: Dhambi hairithiwi. Hakuna mtoto kamwe aliyezaliwaambaye amebeba hatia ya dhambi ya Adamu. Hakuna anayebebajukumula dhambi ya Adamu bali Adamu mwenyewe. 

MAREJEO 

Katekisimu ya Kanisa Katoliki (1994), (Mahwah, NY: PaulistPress).

Colley, Caleb (2004), “Did David Authorize Infant Baptism?,”[On-line], URL: https://apologeticspress.org/articles/2626.

Pinedo, Moisés (2009), “Was Mary Sinless?,”[On-line], URL: https://apologeticspress.org/articles/240062.

UCHAPISHAJI NA VIELELEZO: Tunafurahi kutoa ruhusa kwa makalahiikunukuliwa kwa sehemu au kwa ukamilifu, mradi masharti yetuyatazingatiwa. 


Published

A copied sheet of paper

REPRODUCTION & DISCLAIMERS: We are happy to grant permission for this article to be reproduced in part or in its entirety, as long as our stipulations are observed.

Reproduction Stipulations→