Je Sayansi na Maandiko Matakatifu Vinakubaliana? Ndiyo (Ni Dhahiri)
Imewahi kusemwa kwamba Biblia na sayansi havikubaliani – haviwezi vyote kuwa kweli. Wale wanaoamini Biblia na wanaokubali madai hayo, wanajifariji wenyewe kwa kukiri kwamba Biblia sio “kitabu cha Sayansi” na kwa hiyo hakitegemewi kusema kwa usahihi juu ya masuala ya kisayansi. Ki ukweli, bila kujali kwamba Biblia ni kitabu cha sayansi, jiografia, historia au somo jingine lolote, kama Biblia imevuviwa na Muumba mwenye ujuzi wote, aliyeumba mbingu na nchi, itakuwa sahihi katika kila inachosema. Inapogusa mambo ya sayansi, inapaswa kuwa sahihi katika maelezo – na ndivyo ilivyo.
Ki ukweli, kwa mujibu wa Biblia, Mungu mwenyewe alianzisha fani ya sayansi. Pale alipowaumba watu siku ya sita na akawaambia “waitawale” nchi na “kuitiisha” (Mwanzo 1: 28). Alikuwa anamwamuru mwanadamu kufanya kitu kingine ambacho kingehitaji uchunguzi mpana wa kisayansi na majaribio. Kama Mungu alianzisha sayansi, kwa nini iwe kitu cha ajabu kwenye neno lake? Mungu aliposema, kupitia mtumishi wake Paulo, katika Warumi 1: 20 kwamba uwepo wake na baadhi ya sifa zake, vinaweza kueleweka kwa kusoma uumbaji wake, alikuwa anaweka muhuri wake kuruhusu uchunguzi wa kisayansi kwenye uumbaji wake – “vitu vilivyoumbwa” . Aliposema katika 1 Wathesalonike 5: 21, “jaribuni mambo yote, lishikeni liilo jema” alikuwa kimsingi akifupisha njia za kisayansi. Kwa kuhamasisha watu kusoma “kazi za Bwana” (mfano, uumbaji na gharika), alikuwa anaidhinisha sayansi (Zaburi 111: 2). Mungu alipomtaka Adamu awape majina wanyama, alianzisha fani ya Baiolojia yaani, elimu ya viumbe (Mwanzo 2: 19). Alipomuonyesha Ayubu, sheria za asili zinazoongoza ulimwengu, alikuwa akihamasisha kusoma Fizikia (Ayubu 38: 33). Ayubu 12: 8 – 10, panafafanua elimu ya miamba, wakati Zaburi 19: 1 na Mwanzo 15: 5, panahamasisha, elimu ya anga (Astronomy). Hesabu 19, tena panafafanua wazi vichocheo vya msingi kwa ajili ya sabuni za kuua wadudu (bacteria) – hii ni kemia ikifanya kazi. Sulemani, katika hekima yake iliyovuviwa, aliidhinisha kusoma sayansi ya baiolojia, akihamasisha kuwasoma; Tai, na nyoka (Mithali 30: 18, 19), pamoja na siafu, Wibari, Nzige, na Mijusi (Mithali 30: 25 – 28). Yesu alihamasisha elimu ya mimea alipovuta hisia za wasikilizaji wake juu maua ya kondeni (Mathayo 6: 28), mbegu (Mathayo 13: 1 – 9, 24 – 30), Miti na Mizabibu (Mathayo 7: 16 – 20), na Nyasi (Mathayo 6: 30); Onitholojia (Elimu ya ndege) kwa kuonyesha ndege wa angani kama ufafanuzi (Mathayo 6: 26); Entomolojia (Elimu ya wadudu) alipokuwa akitaja nondo (Mathayo 6: 19, 20); na Zoolojia (Elimu ya Wanyama) alipoongelea kondoo, mbwa na nguruwe (Luka 15: 3-7; Mathayo 7: 6). Katika hotuba ya Mungu kwa Ayubu, katika sura za 38 -41, Mungu alichagua kumshusha Ayubu na kumuelekeza kwa kumpa somo la sayansi likijumuisha; jolojia, kosmolojia, elimu ya anga, fizikia, elimu ya bahari, elimu ya uono, hali ya hewa, na biolojia; ikijumuisha elimu ya wanyama, wadudu, ndege, mimea na viumbe wa majini. Mwisho kabisa: Mungu alianzisha, aliidhinisha na hata kuamuru sayansi. Sayansi haiko kinyume na maandiko matakatifu.
Sasa kwa nini kuna mchanganyiko? Mchanganyiko mwingine unatoka katika asili ya sayansi ya uchunguzi; hatuwezi kuonja, kugusa, kunusa, kusikia au kumuona Mungu, uumbaji au gharika. Hivyo suluhisho ambalo wengi wanalichukua ni kwamba Uumbaji wa kibiblia haukubaliki Kisayansi. Wakati ni kweli kwamba aina kadhaa ya mifano ya Biblia haiwezi kuthibitishwa kwa vitendo kwani hatuwezi kuvichunguza leo. Tunaweza kusema hivyo pia kwa baadhi ya hatua muhimu katika nadharia za asili (mfano, Mlipuko mkuu, yaani Big Bang, mwanzo wa maisha, aina za viumbe, nk). Hiyo ndiyo asili ya “sayansi ya historia”; kuchunguza kutoka ushahidi usio wa wazi lazima itumike kuthibitisha nadharia inayohusu matukio ya kihistoria yasiyochunguzika, katika hali hiyo hiyo, wataalamu wa alama wanatumia sayansi kuchunguza matukio ambayo wao binafsi hawakuyashuhudia. Mifano ya Biblia, sawasawa na mifano ya kihistoria lazima ithibitishwe kwa ushahidi usio wa moja kwa moja, kuliko ule wa moja kwa moja. Kama tulivyoonyesha sehemu nyingine, (Angalia www.apologeticspress.org), mifano ya asili inapingana na ushahidi, na mifano ya Biblia inathibitishwa na ushahidi.
Mchanganyiko zaidi unatokana na kulinganisha maandiko na mtazamo wa asili, na sayansi ya asili. Ni kweli kwamba nadharia nyingi maarufu, zimeibuka siku hizi zinazopingana na Biblia, lakini ni kweli pia kwamba, ukikagua sana mifano hiyo inaonekana kupingana na sayansi ya kweli katika mambo ya msingi. Kwa mfano, mtu hawezi kuwa mfuasi wa asili (naturalistic) na bado akaamini katika vitu ambavyo havitokei kwa asili (mfano, vinasababisha madhara kidogo, uanzishwaji wa sheria za kisayansi, maisha, mada/nguvu, taarifa za kijenetiki, ubunifu, nk). Nadharia haiwezi kujipinga yenyewe na bado ikawa ya kweli. Sayansi ya kweli haitakuwa na kujipinga kwa ndani, kama hivyo vya nadharia ya asili.
Mifano ya ki-Biblia, hata hivi, haiungi mkono huko kutoendana kwa ndani kwa nadharia za sayansi za uongo. Badala yake inaeleza kwa uwazi kwamba, ulimwengu uliumbwa, ex nihilo, na Yehova, Mbunifu mkuu katika siku sita – wazo ambalo halipingani na ushahidi, na ambalo linaungwa mkono na ushahidi usio wa moja kwa moja. Miaka mamia kadhaa baada ya wiki ya uumbaji, gharika ya dunia ilitokea, ambayo iliathiri sana dunia. Ushahidi wa kisayansi unaunga mkono pia maelezo ya Biblia juu ya tukio hilo,ikijumuisha ushahidi toka katika jolojia, paleontolojia, elimu ya anga, biolojia na hali ya hewa.
Mfano wa ki-Biblia ni wa kisayansi kwa sababu unaweza kuelezea chanzo cha sheria za kisayansi. Ni wa kisayansi kwa sababu unaweza kulezea ulimwengu na sifa zake bila kujipinga. Mfano wa ki-Biblia ni wa kisayansi kwa kwa sababu unaelezea kwa ufasaha kabisa baadhi ya sheria za kisayansi kabla hazijagunduliwa (mfano, sheria ya mauaji, sheria ya nguvu-mwendo nk). Mfano wa ki-Biblia ni wa kisayansi kwa kuwa umethibitisha makadirio mengi ya kisayansi. Mwisho wa yote; Mungu alianzisha sayansi. Pale utafiti halali wa kisayansi unatafasiriwa sawasawa na kwa haki, sayansi inaunga mkono Biblia na Ukristo. Haipingani kwa hakika na maandiko – kwani vinachangia mwanzilishi yuleyule!
Rejea
Jeff Miller (2011), “God and the Law of Science; The Law of Causality”
Jeff Miller (2012), “The Laws of Science – by God”
Jeff Miller (2013), “Evolution and the Laws of Science: The Laws of Thermodynamics”
Jeff Miller (2012), “The Laws of Biogenesis (Part 1)”
Jeff Miller (2014), “God and the Laws of Science; Genetics vs. Evolution (Part 1)”
Jeff Miller (2017), “Atheists’ Design Admissions”
Paul Garner (2011), The New Creationism
Jeff Miller (2017), Science vs. Evolution
Jeff Miller (2014), “Bill Nye/Ken Ham Debate Review; Tying up Really Loose Ends”
REPRODUCTION & DISCLAIMERS: We are happy to grant permission for this article to be reproduced in part or in its entirety, as long as our stipulations are observed.