Je, Ni Ubaguzi Kupinga Ushoga?
Mbinu moja inayopendwa na wale wanaotaka kuendeleza ajenda ya ushoga nchini Marekani ni kulinganisha upinzani dhidi ya ushoga na ubaguzi wa Waamerika wenye asili ya Afrika ambao umeonyesha baadhi ya sehemu za watu wa Marekani. Ikiwa unapinga kuhalalishwa kwa ushoga na kupendelea kupigwa marufuku kwa ndoa za watu wa jinsia moja, wewe ni “sawa na wabaguzi wa rangi ambao waliwakandamiza weusi kusini.”
Kwa hakika Biblia inafundisha kwa uwazi sana kwamba kutendwa vibaya kwa wanadamu wenzako ni dhambi, na kwamba Mungu hatofautishi wanadamu kwa msingi wa rangi ya ngozi, kabila, au utaifa (1 Samweli 16:7; Matendo 17:26; Warumi 2:11, 28-29; Yakobo 2:1 na kuendelea; Walakini, tabia ni jambo tofauti. Ushoga, kwa ufafanuzi, unajumuisha vitendo ambavyo mtu hutekeleza kutokana na utekelezaji wa chaguo la binadamu.
Tambua kwamba kabila la mtu halihusiani na tabia au chaguo. Ikiwa ngozi ya mtu ni nyepesi au nyeusi, maamuzi ambayo anafanya siyo matokeo ya kuepukika ya sababu hiyo ya maumbile. Tabia huamuliwa na mambo yasiyo ya kinasaba (gene) ikiwa ni pamoja na uzoefu wa zamani., ushawishi wa wazazi na rika, elimu na utamaduni. Mhispania hana uwezekano mkubwa wa kuishi kwa njia Fulani kwa sababu tu ya muundo wake wa maumbile. Mtu ambaye kundi lake la vinasaba (genes) ni la Kihispania si zaidi au chini ya uwezekano wa kupendelea, tuseme, tamale, kuliko yule ambaye maumbile yake ni ya Caucasian. Watu kama hao watakuwa na mapendeleo ambayo yametokana na vyanzo na hali zingine isipokuwa asili yao ya maumbile.
Kinyume kabisa, hata hivyo, hamu/mapendeleo ya ngono hayana uhusiano wowote na muundo wa vinasaba (genes). Ni matokeo ya mazingiraa, uzoefu, tamaduni, na mambo mengine ambayo yanaweza kufinyanga na kuunda watu binafsi katika michakato yao ya kufanya maamuzi ya kibinafsi.
Mielekeo ya kingono ambayo shoga anasisitiza kwamba kwa asili “anahisi” si tofauti na hisia na mielekeo ambayo mlawiti anayo katika mvuto wake wa kingono kwa watoto, au ambayo muuaji anahisi kuhusiana na mielekeo yake ya jeuri. “Hisia” kwa wote watatu ni dhahiri kabisa; lakini ni kosa kuzipata hisia hizo kwa sababu yoyote ya msingi ya vinasaba (genes). Na haikubaliki kibiblia na kimaadili kwa mtu huyo kutenda kulingana na hisia hizo. Hapa kuna tofauti muhimu kati ya kabila na ushoga. Wamarekani Waafrika na washiriki wa Caucasions hawawezi kubadilisha rangi yao ya ngozi. Lakini wanaweza kubadilisha tabia yao. Na mashoga pia wanaweza.
REPRODUCTION & DISCLAIMERS: We are happy to grant permission for this article to be reproduced in part or in its entirety, as long as our stipulations are observed.