Je, Mungu Huumba Uovu?
KUMBUKA: Mnamo tarehe 12- Februari- 2009, mdahalo kati ya Darwin Day na Kyle Butt, Dan Barker aliorodhesha tofauti 14 zinazo daiwa kuwa za Biblia kama ushahidi dhidi ya kuwepo kwa Mungu. Alisisitiza (dakika saba na sekunde 25 katika hutuba yake ya ufunguzi) kwamba Biblia inatoa maelezo yanayo pingana kuhusu kuwa Mungu ni mwema, lakini anaumba uovu. Madai yake yamekanushwa katika Makala ifuatayo iliyoandikwa na Wayne Jackson mwaka wa 1982.
Q.
Andiko la Isaya 45:7 laonekana kuonyesha kwamba Mungu “Huumba uovu” Je, hii ni sahihi?
A.
Katika Isaya 45:7, nabii aliandika hivi juu ya Mungu: “Mimi naiumba nuru, na kulihuluku giza; mimi nafanya suluhu, na kuhuluku ubaya; Mimi ni BWANA, niyatendayo haya yote.” Katika matukio fulani wasioamini hutumia sana mstari huu ili kujaribu kuhusisha Biblia katika matatizo ya kiadili, kwakuwa andiko hilo yaonekana kupendekeza kwamba Mungu aliumba uovu. Mkristo anapaswa kujibuje shtaka kama hilo?
Kwanza kabisa, mstari huo hauwezi kuwa na marejeleo ya uovu wa kimaadili kwakuwa unapingana na utakatifu usio na kikomo wa Mungu (Isaya 6:3). Yehova ni “Mungu wa uaminifu na asiye na uovu” (Kumbukumbu la Torati 32:4). Yeye si “Mungu apendezwaye na uovu” (Zaburi 5:4). Wala haliwezi kudhaniwa kwamba mstari huu unahusiana na uumbaji wa awali wa Yehova, kwakuwa mwishoni mwa juma la uumbaji; Mungu akaona kila kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana” (Mwanzo 1:31).
Muktadha wa Isaya 45:7, pamoja na vifungu kadhaa vyenye maana sawa, hufunua ukweli wa jambo hilo. Yehova kupitia nabii Isaya alitangaza kiunabii kwa mfalme Koreshi wa Uajemi (karne moja na nusu kabla ya kuzaliwa kwa mfalme huyo!) kusudi lake la kumtumia mfalme huyo mpagani kuwa chombo cha mapenzi yake matakatifu.
Ndani ya Isaya 45:1-7 kuna uthibitisho mkuu wa enzi kuu ya Mwenyenzi Mungu; hakika hakuna kama yeye (mstari wa 5). Hivyo anathibitisha “Mimi naumba nuru, na kuumba giza (yaani, kuthibitisha asili); Mimi nafanya Amani na kuumba uovu (yaani natawala mataifa); Mimi ndimi Yehova nifanyaye mambo haya yote.”
REJEA
Haris, R. L…G. L Archer, and b.k Waltke, (1980), Theological Wordbook of the Old Testament (Chicago, IL: Moody).
Imechapishwa 15- Februari – 2009
UZALISHAJI NA KANUSHO: Tuna furaha kutoa ruhusa ili Makala haya yanakilishwe kwa sehemu au kwa ukamilifu mradi tu masharti yetu yatazingatiwa.
Masharti ya uzalishaji.
REPRODUCTION & DISCLAIMERS: We are happy to grant permission for this article to be reproduced in part or in its entirety, as long as our stipulations are observed.