Je Mungu Anaweza Kufanya Kila Kitu?
Swali;
Je Mungu Anaweza Kufanya Kila Kitu?
Jibu;
Wakristo na hata Wapagani kwa ujumla wamedhani ya kwamba kama Mungu anayezungumzwa katika Biblia yupo, basi anaweza kufanya kitu chochote – kwa maana amewakilishwa kama mwenye nguvu zote. Hata hivi hisia hizi sio sahihi. Biblia haidai kwamba huyu ambaye ana nguvu/uwezo wote, anaweza kufanya kila kitu, na kitu chochote. Kiukweli, kufanya kila kitu kwa tafasiri haiwezi na haitaweza kuhusiana na uwezo au mamlaka. Wababaishaji na Wapagani wameonyesha mashaka kwamba wanahisi kuliondoa suala la kuwa na uwezo wote, na mahali pake kuweka kwamba Mungu hayupo. Kwa mfano ni Je Mungu anaweza kuunda jiwe kubwa au mwamba mkubwa kabisa ambao hata yeye hawezi kuunyanyua?
Tofauti na tena mbali na ukweli kwamba Mungu hana mwili, na kwamba ndiye aliyeumba vitu vyote vinavyoonekana, ingawa yeye sio sehemu ya Ulimwengu, wala sio sehemu ya vitu hivyo, swali hilo ni la kijinga. Ni sawa na kuuliza, Je, Mungu anaweza kuunda mraba wa duara au pembe tatu yenye pembe nne? Hapana hawezi, – lakini sio kwa sababu iliyozingatiwa na Wapagani; kwamba hayupo au hana uwezo. Badala yake ni kwa sababu swali lenyewe linajipinga na halikupangiliwa vizuri. Ni msamiati usioingia akilini. Kuliko kusema Mungu hawezi kufanya kitu hiki, ingekubaliana na ukweli kusema vitu kama hivyo haviwezi kufanyika kabisa. Mungu ana uwezo usio na mwisho, lakini uwezo huo maana yake ni kwa vitu vinavyoweza kufanyika, kwa vile vinavyo wezekana, na sio kwa visivyo wezekana. Ni ujinga kusema “uwezo wowote” (uwezo usio na kikomo) kuweza kufanya vile ambavyo haviwezi kufanyika. Akili ya kijinga haiwezi kuvifanya viwezekane, na hivyo swala sio uwezo, hata kama ni uwezo usio na kikomo (Angalia Warren, 1972 uk 27…).
Zaidi, ukisema Mungu ana mapungufu, au ana kikomo cha uwezo, kwa sababu hawezi kuunda mwamba au jiwe kubwa, ambalo yeye hawezi kulinyanyua, ni kumaanisha kwamba angeweza kufanya hivyo kama kiurahisi angekuwa na uwezo zaidi. Lakini huo ni uongo. Kuunda mwamba, ambao yeye mwenyewe hawezi kuubeba, au kuunda pembetatu yenye pembe nne, au kutengeneza mpira ambao ni mweusi pote na wakati huohuo ni mweupe pote, au kumuumba kijana wa miaka 90, au kutengeneza gari ambayo ni kubwa kwa ndani kuliko kwa nje – kuwaza hivyo ni kuthibitisha kupingana na kuthibitisha ujinga. Mawazo kama hayo hayasemi jambo lolote kabisa. Japo mtu anaweza kudhani mawazo ya kijinga, ambayo hayawezi kufanyika, hayaleti kitu dhidi ya mtazamo kwamba uwezo wa Mungu hauna kikomo.
Kwa hiyo hapana, wazo la kuwa na uwezo wote halimaanishi kwamba, hakuna kikomo kwa mwenye uwezo huo kufanya vitu. Wakati Mungu anaweza kufanya chochote kinachoweza kufanyika, kiukweli ni kwamba atafanya vile tu ambavyo vinakubaliana na asili yake. Ukweli Biblia inaonyesha vitu maalum ambavyo Mungu hawezi kuvifanya. Mfano Biblia inasema Mungu hawezi kusema uongo (Hesabu 23: 19; I Samweli 15: 29; II Timotheo 2: 13; Tito 1: 2). Ni Nafsi ambayo uwepo wake unaendana na ukweli. Uongo kwake hauendani na hali yake ya ki-ungu.
Kingine kisichowezekana kwa upande wa uwezo wa Mungu ni ukweli kwamba hana upendeleo (Kumbukumbu 10: 17; Warumi 2: 11; Wakolosai 3: 25; I Petro 1: 17). Yuko wazi na akishikilia vitu vyote sawia. Anaweza kuonekana kushirikiana na binadamu, kama alivyosema kwamba atafanya. Anavyotuchukulia inategemeana na tabia tulizochagua na sio asili yetu wala ngozi (Matendo 10: 34-35; I Samweli 16: 7).
Namna nyingine ya tatu, inayofaa kwa maana ya kuwa na uwezo wote, inaonekana katika Mungu kutomsamehe mtu ambaye hatatubu na kuacha dhambi (Yoshua 24: 19; Mithali 28: 13; Mathayo 6: 15; 18: 35; Luka 13: 3, 5). Jinsi zilivyo kuu, rehema na misamaha ya Mungu haiwezekani kuonyesha msamaha kwa mtu ambaye hataki kutafuta huo msamaha kwa kutimiza masharti ya kuondolewa. Mungu anaonekana kama hana nguvu za kutoa msamaha kwa njia nyingine zaidi ya damu ya Yesu na kutii injili ya Kristo (Warumi 1: 16; 2: 8; II Wathesalonike 1: 8; I Petro 4: 17; Yohana 3: 5).
Kadiri mtu anavyosoma Biblia, akichunguza sifa na tabia za Mungu, zilizoonyeshwa hapa, ndivyo anavyozidi kukumbana na; (1) Uvuvio wa Biblia – kwa kuwa ujuzi wake wa kuyachukua mambo hayo, unaiweka Biblia juu ya madai ya kujipinga (2) Hofu inayotokana na ukuu wa Mungu. Hakuna hata moja ya mambo yaliyojadiliwa katika makala haya inayoonyesha uhalisia wa uweza wa Mungu. Lakini ni wazi kabisa kwamba mtu anaweza kuishi kwa kumpa Mungu wa mbinguni udhaifu wa kumsaidia mtu huyo. Ni muhimu kwamba kila binadamu atambue haja ya kuelewa mapenzi yake na kufanya tabia zetu ziendane na mapenzi yake. Ni muhimu kila mmoja kuepuka kujiweka kwenye nafasi ya hatari ya kuhitaji kitu ambacho Mungu hawezi kukifanya.
Rejea
Warren, Thomas B. (1972), Have Atheist Proved There is No God.
REPRODUCTION & DISCLAIMERS: We are happy to grant permission for this article to be reproduced in part or in its entirety, as long as our stipulations are observed.