Menu

Je Mungu Anajua kila Kitu Kweli?

Aya kadhaa za maandiko zinafundisha waziwazi kwamba Mungu anajua kila kitu. Biblia inaweka wazi kwamba Mungu “anajua siri za moyo” (Zaburi 44: 21) na kwamba macho yake “yako kila mahali” (Mithali 15: 3), na kwamba “uelewa wake hauna mwisho” (147: 5). Kuhusu Yehova, mtunga Zaburi aliandika

Ee Mungu umenichunguza na kunijua, wewe wajua kuketi kwangu na kuondoka kwangu. Umelifahamu wazo langu tokea mbali. Umepepeta kwenda kwangu na kulala kwangu. Ningefanya kuzimu kitanda changu wewe uko, Umeelewa na njia zangu zote. Maana hamna neno ulimini mwangu, usilolijua kabisa Bwana. … Maarifa hayo ni ya ajabu, yanishinda mimi, hayadirikiki, siwezi kuyafikia. Niende wapi nijiepushe na Roho yako? Niende wapi niukimbie uso wako? Kama ningepanda mbinguni wewe uko (Zaburi 139: 1 – 4; 6-8).

Agano jipya linasisitiza tena na tena ukweli huu; “Mungu ni mkubwa kuliko roho zetu, na anajua vitu vyote” (1 Yohana 3: 20). Sio tu kwamba anajua yaliyopita na yaliyopo, bali yajayo pia (Matendo 15: 18; Rejea Isaya 46: 10). Kwa mujibu wa Biblia, hakuna kilicho nje ya ufahamu wa Mungu.

Mpagani Dan Barker, hata hivyo, alidai katika mdahalo wake wa Februari 12; 2009 wakijadili na Kyle Butt, kwamba, Biblia inaonyesha picha inayojipinga ya Mungu na ufahamu wake. Wakati ambapo baadhi ya maandiko yanaonyesha kwamba Mungu anajua mambo yajayo, yanadai, Mungu wa Biblia, hawezi kuwepo, kwa sababu aya nyingine zimeonekana kufundisha kwamba Mungu hajui mambo yajayo. Dakika 12 na sekunde 54, katika hotuba yake ya kwanza, Barker alipaza sauti;

      Angalia alichosema Mungu baada ya kukisimamisha (Kafara ya Ibrahimu alipomtoa Isaka – ELI). Alisema; “Usimnyooshee kijana  mkono wako, wala usimtende neno; kwa maana, sasa najua ya kuwa unamcha Mungu, iwapo hukunizuilia mwanao”. Najua sasa? Nilifikiri Mungu anajua kila kitu. Biblia inasema Mungu anajua yajayo, lakini hapa anasema “hata sikujua”. Biblia hata inasema kwamba Mungu anatafiti na kujua fikira zote za moyo. Mungu wa Biblia anajua yajayo. Mungu wa Biblia hajui yajayo (2009).

Je Bwana Barker yuko sahihi? Je Biblia inaonyesha picha inayojipinga ya ujuzi wa Mungu? Je baadhi ya aya zinadhihirisha ujuzi wa yote alio nao Mungu, wakati nyingine zikionyesha kwamba ana ukomo katika kuelewa kwake?

Aina ya lugha inayopatikana katika Mwanzo 22: 12 hasa ni ya wakati wa sasa pote katika maandiko. Mwanzoni kabisa (Mwanzo 3) Mungu alimuliza, Adamu “uko wapi? (Mwanzo 3: 9). Katika Mwanzo 4, alimuuliza Kaini “ndugu yako yuko wapi? (4: 9). Kitabu cha Ayubu kinadhihirisha kwamba mwanzo wa hotuba ya kwanza ya Mungu kwa Ayubu, Mungu alimuuliza Ayubu, “ulikuwa wapi, nilipoilaza misingi ya dunia? (38: 4). Je tudhanie maswali kama haya, au kauli kama hizo zinazopatikana katika  Mwanzo 22:12 na 18: 21 (“Nitajua”) inamaanisha kukosa ufahamu kwa upande wa Mungu?

Kwanza, mtu lazima akiri kwamba maswali wakati mwingine yanaulizwa, na kauli hutolewa mara kwa mara kwa sababu tofauti. Tunadhani hasa kwamba Muumba wa mbingu na nchi, hakujua Adamu alipo, alipomuuliza, “uko wapi”? (Mwanzo 3: 9) Je tuamini kwamba Mungu hakujua Ayubu alipokuwa, alipoufanya ulimwengu (Ayubu 38: 4)? Kwa hakika hapana! Ni baba gani, akishamuona mwanaye ameharibu mlango wa gari, ingemaanisha kutojua kwa kuuliza “nani kafanya hivi”? Ni hakika, yule baba hakuuliza swali kupata habari, bali kuona kama mtoto atakiri kile baba anachofahamu tangu mwanzo. Kwenye tukio fulani Yesu alitumia maswali au alitoa kauli kwa lengo kama hilo. Alipowauliza Wanafunzi wa Mafarisayo na Maherode kuhusu, anwani iliyokuwa kwenye pesa. Ki uwazi haikuwa kwa sababu hakujua (Mathayo 22: 15-22). Vile vile Yesu alipowauliza umati uliomfuata “Ni nani aliyenigusa”? (Luka 8: 45), haikuwa sababu mwanamke aliyemgusa alikuwa amejificha asimuone (Luka 8: 47). Yesu alimjua mwanamke aliyeponywa kwa kugusa mavazi yake, hata kabla hajakiri kumgusa (Marko 5: 32). Swali lake lilikusudia kuvuta hisia kwenye imani yake kubwa na nguvu yake(Yesu) kubwa (Marko 5: 34). Maswali anayouliza Mungu, au kauli anazotoa sio ishara ya yeye kutojua yote. 

Pili, neno “kujua” (kiebrania yada, kigiriki ginosko) au neno lingine lolote linaloendana nalo (mfano, alijua, kujulikana nk) yametumika katika maandiko, katika njia tofauti tofauti. Mara kadhaa yametumika  kurejea mwanamume na mwanamke wakilala pamoja (Angalia Mwanzo 4: 1, 17, 25; Waamuzi 11: 39; 19: 25). Yesu alitumia neno hili akirejea anavyojua kondoo wake (yaani watu – Yohana 10: 27). Kinyume na njia ya mwovu ambaye ataangamia, mtunga Zaburi aliandika kwamba Mungu “anajua” (yaani anaruhusu, anafurahishwa nk) na njia za  wenye haki (Zaburi 1: 6). Paulo alitumia neno “kujua” katika Waefeso 3: 19 kwa maana ya kujua “kwa majaribio ni nini ki-akili kilicho  nje ya uwezo wa kufahamu” – upendo wa Kristo (Jamieson, 1977). Ukweli ni kwamba, kama maneno mengine katika maandiko (na kwa siku hizi) neno “kujua” lina maana mbalimbali. Kilicho cha zaidi, sio Dan Barker wala mtoa hoja wa Biblia anaweza kuthibitisha kwamba neno “kujua” katika mwanzo 22: 12 moja kwa moja linapingana na ujuzi wa Mungu kujua yote.

Tatu, matumizi ya Biblia ya neno kama “sasa najua” (Mwanzo 22: 12) au “nitajua” (Mwanzo 18: 21), yakimrejea Mungu hasa, yako kwa faida ya binadamu. Katika Biblia yote matendo ya binadamu (kama “kujifunza”) mara nyingi yanahusishwa na Mungu kwa kusudi la kutusaidia kuelewa vyema umilele wake. Yehova aliposhuka chini kuona mji na mnara” uliojengwa Babeli (Mwanzo 11: 5), haikuwa kwa lengo la kupata ufahamu. Kauli kama hizi hazimaanishi kuwaza kwamba Mungu mda wote hayuko macho, au hajui kinachoendelea. Badala yake, kama kwa suala la Babeli, maneno kama yale yalitumika kuonyesha kwamba alikuwa akilichunguza rasmi na kihakimu, suala lile, na kulizingatia. (Morris, 1976 uk 272). Mwenyezi Mungu alitembelea Sodoma na Gomora huenda, “kwa suala la kutokea kwamba watu wajue moja kwa moja kwamba Mungu ameona hasa hali halisi kabla hajatenda katika hukumu” (Uk 342). “Miji hii ilitakiwa kufanywa sampuli ya ukali wa Mungu, kwa vizazi vingine vijavyo, na kwa hiyo uthibitisho uliotolewa kwamba hukumu haikuwa nyepesi wala iliyozidi (Ezekieli 18: 23; Yeremia 18: 7) [Jamieson, 1997]. Vile vile kwa suala la Mungu kumjaribu Ibrahimu juu ya Isaka, ingawa Mungu tayari alishajua nini Ibrahimu atachagua kufanya, bado kulikuwa na sababu kumpa Ibrahimu nafasi kuonyesha imani yake kubwa na kujua kwamba Mungu ameshuhudia hasa (katika muda halisi na sio tu katika ufahamu wake wa kabla), matendo ya Ibrahimu. Mungu alikuja “kujua” imani ya Ibrahimu kwa majaribio halisi. Maana ya neno “kujua” imani halisi ya Ibrahimu kwa majaribio halisi. Maana ya kauli “sasa najua” (Mwanzo 22:12), kwa hiyo, “sio kwamba Mungu, kwa matukio ya uchunguzi huu, alipata taarifa juu ya tabia za Ibrahimu ambazo hakuwa nazo mwanzo; bali kwamba sifa hizi zimekuwa dhahiri, zimeendelezwa kwa tendo la nje” (Jamieson, 1997).

Sawasawa na jinsi Mungu anavyomwagiza wanadamu kuomba na kufanya shida zetu“zijulikane” kwa Mungu, kwa faida yetu (Wafilipi 4: 6), ingawaje anajua tayari maombi yetu na mahitaji kabla hayajatolewa sauti, au hayajaombwa (Mathayo 6: 8), kwa faida yetu Mungu anayejua yote wakati mwingine amesemwa katika lugha ya kuchukuliana kama anayehitaji kufahamu.

Rejea

Butt, Kyle & Dan Barker (2009), “Does The God of the Bibl Exist?

Jamieson,Robert, et al. (1997), Jamieson, Fausset, Brown Bible Commentary

Morris, Henry M. (1976), The Genesis Record


Published

A copied sheet of paper

REPRODUCTION & DISCLAIMERS: We are happy to grant permission for this article to be reproduced in part or in its entirety, as long as our stipulations are observed.

Reproduction Stipulations→