Je Mungu Alituumba Tukiwa na Hamu ya Kufanya Dhambi?
Hakuna shaka kwamba binadamu anataka kufanya dhambi. Kwa nini Mungu mwenye upendo, ambaye hataki tufanye dhambi, atuumbe na hamu hiyo? Ni kitu kibaya namna gani kukifanya! Ni dhahiri anataka tufanye dhambi! Hii ni halali ki-vipi? Angetutegemea vipi kutofanya dhambi na akatujaribu kwa kutupa hamu ya kuifanya? Huku ni kuugua. Anawezaje kuwa Mungu mwenye upendo? Miezi kadhaa iliyopita, binti mmoja, alinikaribia na kutoa tuhuma hizi dhidi ya Mungu. Huu ni mtanziko kwa Mungu wa Biblia?
Kwa ajili ya hoja, tutafikiria kwa muda kuwa ni kweli kwamba, Mungu alituumba na hamu ya kufanya dhambi. Kwanza kama tutaruhusu kwamba alituumba na hamu ya kufanya dhambi, itakuwa si kweli pia kwamba alituumba na uwezo wa kuchagua kutofanya dhambi? Kwa maneno mengine, hakutuumba ili kwamba tufanye dhambi. Alitupa kabisa uhuru wa kuamua – uhuru wa kufanya uamuzi wetu wenyewe. Kila mtu mwenye uwezo anathibitisha kila siku kwamba, anao uhuru wa kufanya au kutofanya shughuli mbalimbali. Sisi sio roboti zisizo na akili, zinazofanya tu kwa silika. Unaweza kuchagua kusoma sentensi hii au la. Haijalishi jaribu hilo ni kali kiasi gani, imethibitishwa kwamba inaweza kuzuiliwa na binadamu. Sasa kama Mungu alitutaka tufanye dhambi, na alikuwa na uwezo wa kutusababisha tufanye dhambi, Kwa nini alituumba na uwezo wa kuchagua kutofanya hivyo? Hii haingii akilini. Cha kushangaza, mwanzoni kabisa mwa muda, Mungu alisema waziwazi kwamba sio yeye anataka dhambi itutawale. Dhambi ina hamu ya kufanya hivyo, lakini alituumba tukiwa na uwezo wa “kuitawala” (Mwanzo 4: 7).
Na zaidi sana, hata kama Mungu alituumba tukiwa na “hamu ya kufanya dhambi”, je sio ajabu pia kwamba angetupa na njia ya kusafishwa au kusamehewa kutoka katika ubaya huo tunaotaka kuufanya? Kama alitaka tushindwe, kwa nini alifanya kitu hicho? Zawadi ya kusamehewa katika mfano wa Biblia inatofautiana waziwazi na wazo kama hilo, na kutumika kama kithibitisho rasmi kwamba Mungu hataki tufanye dhambi. Na kwa udadisi zaidi, kama angetutaka tufanye dhambi, kwa nini utaratibu wa msamaha alioanzisha unahusisha kifo chake mwenyewe? Tendo kama hilo la kutojijali, sio kitu ambacho Mungu angekifanya, kama angetutaka tufanye dhambi na kwenda kuzimu. Tabia kama hizo ni pengine kitu ambacho Mungu wa rehema, angefanya – Mungu ambaye alitaka kutupa kujitegemea na uhuru wa kuchagua, na bado akatupa njia ya kusamehewa pale tunapofanya maamuzi mabaya.
Kifupi sio sahihi kusema kwamba, Mungu alimuumba binadamu akiwa na hamu kwa ndani ya kufanya uovu. Kama chochote, kwani alitupa nia na hisia za ndani za kujua haki. Alituumba na mvuto au msukumo wa kutofanya baadhi ya vitu. Kila binadamu hapa duniani, anaelewa kwamba, kuna baadhi ya vitu, ambavyo ni halali, na vingine ambavyo sio halali na nia zetu zisizochoma zinatusukuma kufanya mambo mema kwa wengine.
Zaidi sana, wakati muda mwingine tunaweza kutamani kufanya mabaya, sio kweli pia kwamba, kwa wakati mwingine tuna hamu ya kufanya mema? Mtu mmoja anaweza kwa urahisi kabisa na kwa usawa akauliza swali, “Je Mungu alituumba na hamu ya kufanya mema? Hata yule mpagani mgumu, na asiyeamini, (mfano Bart ehrman), anakiri kwamba anataka (yaani anajaribiwa) kufanya mema, na anafanya hivyo (yaani anaanguka katika majaribu hayo) kupitia vitendo mbalimbali vya kisamaria. Kama Mungu alituumba na hamu ya kufanya dhambi. Lazima pia ikubaliane kwamba alituumba na hamu ya kufanya mema pia.
Je kupingana huku kwa dhahiri kunaweza kuelezewa vipi? Sio kwamba inawezekana Mungu hakutuumba na hamu ya kufanya dhambi? Tunatamani matendo yote wakati mwingine kwa sababu tumegundua kwamba yote yanaweza kutufanya tujisikie vizuri katika namna tofauti. Ambayo ilisema ni haki na inakubalika kuhitimisha kwamba Mungu alituumba na hamu hiyo – yaani hamu ya kujisikia vizuri (kuwa na furaha, kufurahia raha, kutamani starehe, na kuridhika), sio hasa hamu ya kufanya maovu. Kwa mfano, tuliumbwa kutamani kula – kujisikia vizuri kwa kufanya hivyo – lakini sio kwa hamu ya kuwa “wala watu”. Labda ingekuwa vyema kuvielezea hivi; Mungu alituumba na uwezo wa kukutana na kufurahia “kujisikia vizuri”. Tunapojisikia vizuri, kwa asili tunataka kuendelea kuwa na hisia hizo. Vitu hivyo ambavyo kwavyo tunachagua kujaza tanki la “kujisikia vizuri” ndio maamuzi yetu sisi binafsi kwa hiari kabisa. Maamuzi hayo bila shaka yamehamasishwa na vitu vingi (Mfano; uzoefu, kiburi, wazazi wetu, na waalimu – Mithali 22: 6; 19: 27), rafiki zetu (1 Wakorinto 15: 33; Mithali 13: 20), Shetani (2 Wakorinto 2: 11) nk. Lakini ushawishi mbaya au tamaa mbaya, havitoki kwa Mungu. Yakobo 1: 13,14 panasema “Mtu ajaribiwapo asiseme najaribiwa na Mungu, maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu wala yeye mwenywe hamjaribu mtu, Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa”. Tunatamani kufanya vitu vibaya, kwa sababu ya furaha za muda mfupi, au hisia nzuri vinazoweza kutupa, na sio kwa sababu Mungu anataka tufanye maovu. Mtu mwenye hekima atagundua kwamba sio furaha zote lazima zifanywe kwa nia. Atachagua kuvumilia mateso ya muda, kama ni lazima kufanya mema, badala ya kufurahia “furaha inayopita ya dhambi” (Waebrania 11: 25).
Lakini kwa nini asingetuumbia mazingira ambamo hatuna maingiliano na wengine tusipate kushawishiwa vibaya nao? Katika mazingira kama hayo, tungeweza kupoteza baraka tunazopokea kwa kujumuika na wengine pia (kama vile; maongezi; ushirikiano, kusaidiana, kufarijiana, kutibiana, kupeana zawadi nk). Kuna sababu, kwanini kujitenga, au kufungiwa sehemu ya upweke ni adhabu, kwenye mifumo ya gereza. Kutengwa na upweke havina afya. “Si vyema mtu huyu awe peke yake” (Mwanzo 2:18). Kuchangamana na wengine, na baraka tunazoweza kupata kutokana na mchangamano huo, ni zawadi kutoka kwa Mungu. Tunaishi kwenye sayari ambayo ina zaidi ya watu wengine bilioni saba. Kwa kuwa sote tunaishi pamoja, hisia zetu bila shaka zinawaathiri hao wanaotuzunguka, iwe kwa wema au kwa ubaya. Kama tusingewaathiri wengine kwa maamuzi yetu, basi tungekoma pia kuwa na hisia kuwaathiri watu hao, kwa wema au kwa ubaya. Kwa kuweka tu mazingira ambamo watu wote wangelazimika kumtii Mungu, wangeondolewa. Lakini katika mazingira kama hayo, Mungu angekoma kuwa Mungu wa upendo, ambaye ametupa uhuru. Angekuwa dikiteta, akimlazimisha kila mtu kumtii kama mashine zisizo na akili (roboti)
Lakini kwa nini Mungu atupe uwezo wa kujisikia vizuri kabisa? Kama inatufanya tutende mabaya, hiyo inakuwaje kitu kizuri? Hapana shaka kwamba, chaguo la Mungu kuturuhusu kuwa na furaha ni baraka kwetu, kuliko hatari. Ni nani anaweza kubisha kiungwana kabisa kuwa na maisha yasiyo na hisia za furaha au kujisikia vizuri ingekuwa kitu kizuri? (cha kufurahisha). Wazo hilo hilo linajipinga. Kwa sababu ileile, tunatafuta kuwapa watoto wetu furaha na kuwapa raha katika maisha. Mungu alituumba ili tuwe na uwezo wa kuzoea hayo hayo. Mtu hawezi kutegemea Mungu asiye na upendo, aliyetaka wanadamu wafanye dhambi, na kutufanya tuwe na uwezo wa kuzoea furaha na raha. Wazo kama hilo hata hivyo linaweza kukubaliana vizuri kabisa na Mungu wa upendo, wa rehema, na ambaye anatujali na anayependa kutubariki kwa furaha, licha ya maamuzi mabaya ambayo sisi na wanaotuzunguka mara kwa mara tunayafanya. Angalia kwamba hamu ya kujisikia vizuri na kuzoea raha kimsingi ni baraka, sio laana, maadamu alitupatia, pamoja na uwezo wa kuifurahia raha., uwezo wa kutofautisha aina nzuri ya raha kutoka katika zile mbaya, ama kupitia maelekezo au kutengeneza mazingira ambamo tutajifunza kutokana na uzoefu.
Sio kweli kwamba mzazi anayempenda mtoto wake anaweza kuongeza furaha au raha kwa mtoto wake? Hii inajumuisha kumpa yule mtoto mazingira, ambayo anaweza akawa na uhuru kiasi fulani na kujitegemea. Hajafungiwa kwenye kitanda chake maisha yake yote, lakini amepewa maelekezo au ushauri, maonyo juu ya nini kitatokea kama mtoto atachagua furaha (starehe) mbaya, na ule uhuru wa kuamua kama atii au asitii zile amri na maelekezo aliyopewa. Anaweza kuchagua kuwaamini wazazi wake, kwamba wanajua nini kitamfanya awe na furaha, au kuamini kwamba, njia zake zitakuwa na matokeo mazuri. Mtoto anaweza kufikiria kwamba, atakuwa na furaha zaidi kama atapuuza maonyo ya wazazi wake, na akagusa jiko la moto. Mtoto atapata raha kwa muda, ile tunayopata kwa kujichagulia wenyewe la kufanya, na kadiri anavyojisikia vizuri kwa uhuru anaoamini kwa kiburi kwamba amewathibitishia wazazi wake kwamba wao hawajui, mda mchache tu baadaye, anapokuwa ameungua, ndipo anapogundua kwa nini wazazi waliweka sheria kule mwanzo, na hivyo hujifunza kuwaamini. Lakini vipi pale alipogusa lile jiko kama hakuna ambalo lingetokea kwa sababu jiko lile halina moto? Katika hali kama hiyo maonyo ya yule mzazi anayempenda mwanaye yametolewa ili kuhakikisha mtoto yule asiguse lile jiko siku nyingine- linapokuwa na moto. Ingawa mtoto bado hajaelewa kwa nini sheria zimewekwa wakati wa mwanzo (kwa sababu hakuna kilichotokea aliposhika jiko mara ya kwanza), atajifunza kuwatii wazazi wake hata hivyo, na kadiri muda unavyo kwenda atajifunza pia kuamini hekima yao kupitia kuhakikisha hekima ile kwa maonyo mengine na sheria. Lakini kwa nini wazazi wanapitia njia hii? Ni wazi kuongeza furaha ya mtoto kwa siku zijazo.
Mungu amefanya kitu kama hicho hicho kwetu. Kwanza, Mungu alitengeneza mazingira yanayofaa kujifunzia mema na mabaya. Angalia “utaratibu” ulioumbwa una mfumo wa adhabu ukifanyiwa kazi ndani yake ili kutusaidia kutofautisha baadhi ya vitu sisi wenyewe. Kwa mfano, furaha inaweza kwa kawaida, kutokana na kujamiiana kwa aina yoyote, lakini hiyo haimaanishi kwamba aina zote hizo zitatuzidishia furaha yetu. Kwa hiyo Mungu alitupa baadhi ya njia ambazo zitatumika kwa jambo hilo ili kutuongezea furaha. Pia alipangilia mfumo wa asili, ambapo tukikiuka sheria zake kuhusu kujamiiana, maumivu na huzuni kwa njia moja au nyingine, (hata kama hatutambui kwamba tabia zetu ndiyo sababu hasa). Wakati bado tuna uhuru wa kukataa mapenzi ya Mungu, yeye bado anatusihi kufanya mema, kupitia mfumo wa adhabu, ukifanya kazi ndani ya utaratibu aliouumba (mfano; magonjwa ya zinaa, hatari za kimwili kwa kutojali, tabia mbaya, hatari ya kutumia madawa ya kulevya, kansa, dhambi, ugomvi wa familia, upweke/kutengwa nk). Pia katika utaratibu ulioumbwa, kuna kutiana moyo mara kwa mara vinavyotusaidia kuenenda vyema (Mfano; kutoka na msukumo wa nafsi kuenenda katika njia kadhaa, kupitia mafunzo tupatayo kwa uchunguzi wetu kwa wengine, pamoja na pongezi toka kwa wale waliofanya maamuzi mabaya). Je uumbwaji wa mazingira kama hayo yanaonekana kama ni kazi ya Mungu anayetaka tufanye dhambi au tusifanye? Je mfumo kama huo unathibitisha kuwa muumba anataka kutuhamasisha dhahiri kabisa kumtii, akitupa pia uhuru na hiari ya kutomtii, kama tutachagua hivyo?
Pili, kama mzazi anayempenda mwanaye angetegemewa kufanya, Mungu alikuwa na uhakika wa kutupa malekezo ya moja kwa moja ili kutuonya juu ya starehe nzuri na mbaya. Biblia pia iko wazi kutueleza wazi kwamba furaha yetu ni kihamasishi kikuu nyuma ya sheria ambazo Mungu ametupa (mfano, Zaburi 19: 7, 8). Sheria ndani ya Biblia hazikuchaguliwa bila mpangilio kwa ajili tu ya kumdhibiti binadamu, kwa njia kama hiyo sheria za mzazi apendaye mtoto, hazichaguliwi hivyo. Hotuba ya mlimani inaanza na “Amebarikiwa”, ambazo ni sheria za Mwana wa Mungu, akimaanisha “kuwa na furaha” (yaani ‘amebarikiwa’) katika maisha. Katika Kumbukumbu 10: 12, 13, Musa anawakumbusha Waisraeli kwamba sheria za Mungu zilikuwapo kwa ajili yao na kwa faida yao. Pia katika Kumbukumbu 6: 24, anasema sheria zipo ili “tuone mema siku zote, ili atuhifadhi hai kama hivi leo”. Amri za Mungu mara nyingi ni zaidi ya jinsi ya kwenda mbinguni. Zinaathiri maisha yetu hapa na tena sasa. Katika Mithali 29: 18, Sulemani anamuonya mwanaye, kwamba kuondoa sheria za Mungu (yaani ufunuo wake) toka katika jamii bila shaka utaruhusu uhuru mkubwa na usiozuilika kwa tabia za hiyo jamii, (yaani watu wataondoa vizuizi vyote), na hizo tabia zisizojali nafsi, zitaonekana ndizo njia za kuendea furaha. Uhuru huo mkubwa, hata hivi, kinyume na tunavyoweza kudhania, hautaleta watu kwenye furaha. Sulemani anaonya, “ana heri mtu yule azishikaye amri za Mungu.
Mtoto anaweza kufikiri kwamba kutokuwa na sheria kuhusu kutembea tu mitaani kutamfanya awe na furaha, lakini kiukweli, furaha ni matokeo ya muda mrefu ya; (1) Kuwa na hizo sheria na (2) Kutii sheria za wazazi wake. Tunaweza mara kwa mara kukataa kwa sasa kwamba kile anachosema kitatupa raha, kama ambavyo mtoto hakubaliani mara zote na wazazi wake, lakini, kama kwa mtoto mara kwa mara hatuko katika nafasi ya kujua kwa mbali nini kitakuwa chema kwetu na wale wanaotuzunguka. Mtoto angependa kufanya hayo maamuzi mwenyewe, na kufanya mfumo wake mwenyewe wa mema na mabaya. Anafikiri kwamba anaweza kufanya hivyo kwa mafanikio – kama ambavyo hata watu wazima wanavyodhani tunajua zaidi ya Mungu kile kitakachotupa furaha. Lakini mwisho wa mambo ni kwamba wazazi wanajua zaidi sana juu ya kitakacholeta furaha ya kudumu, na hivyo wazazi wanafundisha, wanaweka sheria na kuzisimamia – kama afanyavyo Mungu. Tofauti ni kwamba binadamu sio wakamilifu kimaumbile na kusimamia sheria, kama mtoto, hatujui pia kila kitu tunachopaswa kujua kukifanya barabara. Wazazi waliturudi kama walivyoona vema wenyewe” (Waebrania 12: 10), lakini sheria za Biblia zilifanywa na akili inayojua vyote (Mungu), aliyeumba akili ya binadamu. Ambaye kwa vyovyote anajua zaidi, nini kitaleta furaha kwenye akili ya binadamu, kuliko yeye aliyeiumba?
Je Mungu alituumbia kwa ndani hamu ya kufanya maovu? Hapana. Mungu alituumba na uwezo wa kuzoea starehe na furaha na hamu ya kuvifuatilia au kuvitafuta. Alituumba na uwezo wa kufurahia starehe na kujisikia vizuri, kupitia macho yetu, masikio, ulimi, pua na neva, ikiwa ni pamoja na katika nafsi zetu. Aliumba mazingira ambapo tunaweza kuchagua kuzijaza tanki zetu za starehe kwa namna tofauti – njia njema na mabaya – kama afanyavyo mzazi na mtoto wake, na baadaye Mungu alitupa maagizo yenye thamani, ambayo kwayo kuna machaguo mema. Kwa kuumba mazingira au uhuru kama yale, maumivu, magonjwa na ubaya haviepukiki, kwa sababu binadamu kwa wakati mwingine watakataa amri za Mungu na maonyo. Lakini kwa uamuzi mbaya usiokwepeka kama huo, alihakikisha anatoa namna ambayo kwayo tunaweza kusamehewa, na hatimaye kuishi naye katika mazingira mbali na uovu wote.
Rejea
Kyle Butt, (2004), “Do children Inherit The Sin of Their Parents?
Caleb Colley (2004), “Did David Authorize Infant Baptism?
And Moises Pinedo (2009), “Arechildren born with Sin”?
Kyle Butt & Bart Ehrman (2014), “…Pain, suffering and God’s existence
REPRODUCTION & DISCLAIMERS: We are happy to grant permission for this article to be reproduced in part or in its entirety, as long as our stipulations are observed.