Je, Mariamu Anawaombea Wakristo?
Imetolewa hoja kwamba “Mariamu ndiye kiumbe aliye karibu zaidi na Mungu. Aidha, wakati Kristo ni mpatanishi wa neema yote kati ya Mungu na viumbe, maria ni mpatanishi wa neema yote kati ya Kristo na wanadamu. Kwa hiyo Mariamu ni mwombezi mwenye nguvu kwa wote wanao mgeukia” (tazama Zoltan, 1994). Biblia inafundisha waziwazi kwamba Mariamu si Mungu na hapaswi kuabudiwa (Pinedo, 2009). Ikiwa Yeye si Mungu, je, ana daraka la utendaji mbinguni, akiwaombea Wakristo mmoja-mmoja? Je, anatuombea kwa maombi au ana athari katika wokovu wetu?
Mariamu hayupo karibu na Mungu kuliko mtu mwingine yeyote wa zamani au sasa.
Inaporejelea Uungu, Biblia inmtaja tu Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu (Mathayo 28:19; Mathayo 3:16-17; Yohana 10: 30; 17:21; Matendo 5:3-4) Maria hatajwi kamwe katika muktadha huo. Zaidi ya hayo, mbingu ambamo Mungu na malaika zake wanakaa (Kumbukumbu la Torati 10:14; 26:15; 1 Wafalme 8:27, 30) bado haijakaliwa na wanadamu. Yesu alisema: “Hakuna mtu aliye paa mbinguni, ila Yeye aliyeshuka kutoka mbinguni, yaani mwana wa Adamu (Yohana 3:13). Maneno haya yanawakilisha ukweli kuhusu watu wote ambao wameuacha ulimwengu huu (ikiwa ni pamoja na Maria) Hakuna aliye mbinguni kwa sababu mbingu imehifadhiwa kwaajili ya watumishi wote waaminifu wa Mungu tangu zamani (rejea Yohana14:1-3). Sio mpaka baada ya ujio wa pili wa Kristo ndipo itakuwa nyumbani kwa waaminifu, walio hai na walio kufa (Mathayo 25:31-46; 1 Watheselonike 4:13-18).
Wazo la kwamba mariamu anachukua nafasi ya pekee mbinguni, karibu na Mwana, ni desturi. Inaonyesha ukosefu wa ufahamu kuhusu mafundisho ya Biblia juu ya maisha baada ya kifo. Katika Luka 16: 19-31, Yesu alieleza kwamba wafu (waliookolewa na walio potea) wanakwenda mahali paitwapo kuzimu (Luka 16:23 sheol kwa Kiebrania) mahali pa kiroho pa kusubiria ambayo imetengwa na sehemu ya faraja ya wenye haki (inayojulikana kama paradiso), kama vile Luka 23:43. Kutoka kwa mateso ya waovu katika kuzimu, wenye haki wanaanza kuonja sehemu ya furaha inayo wangoja katika umilele, huku waovu wakianza kungoja sehemu ya mateso yanayo wasubiri. Kuzimu si makao ya Mungu; Mungu anakaa mbinguni. Mariamu pamoja na Ibrahimu na watumishi wengine waaminifu wa zamani, wanangoja kuzimu hadi wafu wake watakapo tolewa, wakati Bwana atakaporudi kuhukumu kila mwanaume na mwanamke kulingana na kazi zake (Ufunuo 20:13). Katika ulimwengu huu wa kiroho unao tangulia mbinguni, hakuna kitu ambacho wale walioko wanaweza kuwafanyia wale walio hapa (Luka 16:27-31).
Kipawa cha Maombezi Haikutolewa kwa Mariamu
Wakatoliki wamempa Maria cheo cha “mwombezi wa watakatifu,” ingawa hakuna mahali popote katika Biblia kinatumiwa kumhusu. “Maombezi” maana yake ni “kutafuta uwepo na kusikilizwa kwa Mungu kwa niaba ya wengine” (Vine, 1966, 2:267). Kuna maneno mawili tu ambayo Wakristo wanahitaji uwakilishi: wokovu na maombi. Ikiwa Mariamu sasa, au amewahi kuhusika, kama “Mwombezi wa Watakatifu,” kunapaswa kuwa na ushahidi wa kutosha katika maandiko.
Kuhusu wokovu mtume Petro alisema wazi wazi kwamba “hakuna wokovu katika mwingine awaye yote; kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo” (Matendo 4:12). Bila shaka alikuwa akimaanisha Yesu Kristo. Paulo aliandika: “Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na mwanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu.” (1 Timotheo 2:5). Mwandishi wa Waebrania aliongeza hivi: “Naye, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa Yeye;maana yu hai sikuzote ili awaombee.” (7:25). Yesu ndiye mpatanishi mmoja pekee (mwombezi) kati ya Mungu na mwanadamu, na Anaishi ili kuendelea kuwaombea wale wanaokuja kwa Mungu.
Lakini vipi kuhusu sala? Je, Mariamu anaombea katika maombi ya wakristo? Hapana, yeye hana. Maombezi haya pia ni ya Yesu. Alipokuwa akiwafundisha wanafunzi wake kusali kwa Baba (Mathayo 6:9), Yesu hakuwafundisha kusali kwa (au kupitia) Mariamu. Na bado ukatoliki ulitengeneza sala ya “salamu Maria” ili kutia ndani maneno “Maria mtakatifu, mama wa Mungu utuombee sisi wenye dhambi sasa, na saa ya kufa.” Katika Yohana 14:13-14, Yesu alisema: “Nanyi mkiomba lolote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana. Mkiniomba neno lolote kwa jina langu nitalifanya.” (Tazama Yohana 16:24). Yesu ndiye Yeye pekee Anayeweza kupatanisha au kufanya maombezi katika maombi yetu, kwa kuwa “vitu vyote alivyo navyo Baba ni vyake” (Yohana 16:15). Ikiwa vitu vyote alivyo navyo Baba ni vya Mwana, basi ni nini kinachosalia kwa Mariamu?
Haki ya maombezi inayo daiwa kutolewa kwa Mariamu pia inabishaniwa kutokana na ukweli kwamba “aliomba” mbele ya Yesu kwa niaba ya familia katika arusi huko Kana kwa sababu divai ilikuwa ikiisha wakati wa sherehe (Yohana 2:2-3). Huu uzi mdogo, mrahisi wa pekee wa mabishano, ulio potea katika mtafaruku wa kuchanganyikiwa, umetumiwa vibaya sana na wafuasi wa Imani ya Mariamu. Kwa kumwendea Yesu na ombi la msaada, Mariamu hakuwa akiingilia kati kwa niaba ya mahitaji ya kiroho ya mtu yeyote; aliripoti hali hiyo kwa Yesu pekee. Zaidi ya hayo, fikiria jibu la Yesu: “Mama una nini na mimi?” (Yohana 2:4). Kwa maneno haya, alisisitiza kwamba wasiwasi wa mariamu haukuamuru matendo yake. Chochote alicho fanya huko Kana siku hiyo kingekkuwa kulingana na mapenzi ya Mungu, si kwa sababu ya uvutano au matamanio ya kibinadamu au ya mama.
Ikiwa hali iliyo nukuliwa katika Yohana sura ya pili yathibitisha Mariamu kuwa “mwombezi wa watakatifu,” tunapaswa kukata kauli gani kutokana na mathayo 8:5-13 na vifungu vingine vinavyosimulia hali kama hizo? Katika Mathayo 8:5-13 na vifungu vingine vinavyo simulia hali kama hizo? Katika Mathayo sura ya nane akida “aliyemwombea” mbele ya Yesu kwaajili ya mtumishi wake aliyekuwa kitandani, aliyepooza, na kuteswa sana. Alipoona Imani ya akida, Yesu alifanya muujiza na kumponya mtumishi huyo mgonjwa. Je, tumchukulie jemedari huyu kama “mwombezi wa waliopooza, wagonjwa na wanaoteswa?” Je, mtu yeyote aliyepooza, au yeyote anayeugua ugonjwa wa kimwili au wa kiakili, anapaswa kumwomba mtu huyu mwenye Imani kuu, akimwomba awaombee kwa Mungu kwa niaba yao? [Biblia inashutumu zaidi kitendo cha kuwaita wafu (Kumbukumbu la Torati 18:10-13; 1 Mambo ya nyakati 10:13-14; Isaya 8:19)]. Wala Jemedari huyu, wala Ibrahimu, wala Mariamu, wala mtu mwingine yeyote-walio hai au waliokufa-anaweza kufanya maombezi mbele ya kiti cha enzi cha Mungu kwa niaba ya Mkristo mwaminifu, isipokuwa Yesu Kristo mwenyewe.
Mariamu, kama Wanaume na Wanawake wote, Alihitaji Maombezi
Katika Luka 1:47, Mariamu alipaza sauti yake na kusema:Na roho yangu imemfurahia Mungu, Mwokozi wangu.” Ikiwa alikuwa na mwokozi, basi alihitaji wokovu, basi pia alihitaji Mwombezi pekee wa wokovu- Yesu Kristo (Waebrania 7:25). Kwa hiyo hali ya Mariamu haikuwa tofauti na kila mwanadamu kabla au baada yake. Alifanya dhambi (Warumi 3:23), na alihitaji mwombezi pekee ambaye angeweza kufanya amani kati yake na Mungu (2 Wakorintho 5:18-19; Wakolosai 1:20). Kama vile Yesu “alivyoombea” kwa niaba ya Mariamu kabla hajafa ili kuhakikisha mahitaji yake ya kimwili yalitimizwa (Yohana 19:26-27). Alifanya maombezi kwa niaba yake ili kuhakikisha mahitaji yake ya kiroho yametimizwa. Mariamu hawezi kumwombea Mkristo yeyote kwa kuwa yeye mwenyewe alihitaji maombezi. Hatimaye, ingawa Wakristo wanaagizwa kuombeana (1 Watheselonike 5:25; Waebrania 13:18; Yakobo 5:16), Yesu ndiye mpatanishi wetu pekee katika maombi. Kupitia yeye maombi yetu yanajibiwa.
MAREJEO
Pinedo, Moises (2009), “Is Mary the mother of God?” [on-line],
URL:https://apologeticspress.org/articles/240077.
Vine, W.E. (1966), An Expository Dictionary of New Testament Words (Old Tappan, N.J:Fleming H. Revell).
Zoltan, Abraham (19940, “A Detailed Guide to our Lady’s Rosary,” [on-line], URL:http://www.blessedtrinityorlando.org/rosary.html.
REPRODUCTION & DISCLAIMERS: We are happy to grant permission for this article to be reproduced in part or in its entirety, as long as our stipulations are observed.