Menu

Je, Mafundisho ya Yesu yanakinzana na Mafundisho ya Musa?

Katika “Mahubiri yake ya Mlimani” yenye ustadi, je, Yesu alitofautisha mafundisho yake na yale ya Musa? Je, alionesha kwamba mafundisho yake yangerekebisha makosa katika sheria ya Musa? Je, alipendekeza kwamba sheria yake ingeshughulikia moyo wa mwanadamu, wakati Sheria ya Musa ilizungumzia matendo ya nje tu? Kwa ufupi, je, Yesu na Musa kimsingi wanapingana?

Idadi ya wale ambao, kwa karne nyingi, wanashambulia uvuvio wa Biblia wameongezeka na kuwa jeshi kubwa. Hata hivyo, Biblia inajibu mapigo na kubaki katika hali yake ya kuwa imevuviwa bila kuathiriwa. Hakuna tofauti, mkanganyiko, au kosa moja ambalo limeweza kudumishwa kwa mafanikio.Katika Mathayo sura ya 5, usomaji wa juu juu wa matamshi ya Yesu katika “Mahubiri yake ya Mlimani” humfanya mtu kuhoji kama Yesu alikuwa akidharau mafundisho ya Musa katika Agano la Kale, na huku akithibitisha ubora wa mafundisho yake mwenyewe.

  Katika Mathayo5:17-48, haiwezekani kuwa Yesu anazungumza kwa kudharau Sheria ya Musa. Kwani baada ya hapo, alizungumza kuhusu mafundisho ya Kiyahudi juu ya Sabato (Mathayo 12:8). Kwa nini basi awapuuze au awadhihaki? Yesu alijua kwamba amri za Agano la Kale zilikuwa “takatifu, na za haki, na njema” (Warumi 7:12) na muhimu sana (Zaburi 19:7-11; 119). Yesu alijua kwamba Agano la Kale lingeendelea kufanya kazi kwa manufaa ya watu wa Mungu wakati wa enzi ya Ukristo (Warumi 15:4; 2 Timotheo 3:14-17). Mitazamo hasi kuhusu Sheria za kale inatokana na maoni potofu kuhusu utekelezaji wa Sheria.

  Badala ya kupinga mafundisho ya Musa, kwa kweli, Yesu alikuwa akitofautisha, kwa njia iliyo wazi na ya kuvutia, tofauti kati ya makusudio ya awali ya Mungu yaliyomo ndani ya sheria za Musa na upotoshaji wa kifarisayo na waandishi wa sheria za Mungu ilikuwa imekusanywa kwa karne nyingi. Katika mazungumzo yake yote kuhusu jambo hili, Yesu hasemi, “Imeandikwa” au “Musa alisema” kama alivyofanya nyakati nyingine. Badala yake, Anatumia vishazi vya utangulizi kama vile “Mmesikia kwamba ilisemwa zamani” (Mathayo 5:21) na “Mmesikia kwamba imenenwa”

  (Mathayo 5:38). Vidokezo hivi vyenye utata vinamtahadharisha msomaji juu ya kuwepo kwa makundi ya ufafanuzi na hasa ule ufafanuzi wa marabi ambao ulikuwa umejikusanya taratibu, na kuja kuficha na pengine kupingana kabisa na sheria asilia ya Musa. Yesu aliwashutumu mara kwa mara viongozi wa kidini kwa kugeuza nia ya kweli ya Sheria ya Musa iliyopelekea kutoelewa kwake na kuwasilishwa vibaya kabisa kinyume na Maandiko yalivyo (Mathayo 15:3,6; 12:7,12). Fikiria uchambuzi ufuatao wa ufafanuzi unaoonyesha kwamba Yesu hakupingana na mafundisho ya Musa.

  Mstari wa 17-20

  Mistari ya 17-20 zinatumika kama utangulizi wa mistari ya

  21-48. Mstari wa 20 unaweka msingi wa fundisho kuu la Yesu, yaani, uadilifu wa waandishi na Mafarisayo (hasa mafundisho yao na utendaji wao) kwamba haukuwa sawa na uadilifu wa kweli unaompendeza Mungu. Wayahudi walikuwa na bidii ya kidini na shauku za kidini (kama wengi wanaofuata mitindo ya ibada na dini za uwongo), lakini utendaji wao wa dini ulikuwa umejaa ujinga na imani potofu kuhusu kiini halisi cha maudhui ya shughuli sahihi za kidini (Warumi 10:1-3).

  Kwa sababu mafundisho ya Yesu yalikuwa tofauti sana na njia iliyoenea ya mafundisho ya kidini iliotokana na viongozi wa kidini wa Kiyahudi, na maoni ya watu wengi bila shaka walidhani kwamba fundisho la Yesu lilipinga mafundisho ya Musa ambayo yalishikiliwa na uongozi wa Kiyahudi. Lakini kwa hakika, Mafundisho ya Yesu, yalipingana na sehemu kubwa ya dini ya Kiyahudi ya siku zake, lakini mafundisho Yake hayakupingana na mafundisho ya Musa hata kidogo. Kazi ya Yesu Kristo ilikuwa ni mwendelezo wa kimantiki wa dini ya Agano la Kale.

  Ili kuepuka dhana potofu hii, kwa tamko moja la kusisimua na la wazi, alithibitisha tena uhusiano wake mzuri na Sheria za Kale: “Msidhani kwamba nimekuja kuondoa Torati au Manabii; sikuja kuondoa bali kutimiliza” (Mathayo 5:17). Uhusiano wake na Sheria haukuwa wa upinzani wa kuharibu bali wa utimilifu wa kujenga. Maisha na kazi ya Yesu yalikuwa, kwa kweli na lengo la mantiki la Sheria za Musa (Warumi 10:4). Alileta dini ya Agano la Kale kutimia na kuzaa matunda. Hii ilimaanisha wazi kwamba sheria za Musa zingekuwa “zikichakaa” hivi karibuni (Waebrania 8:13) na hivyo kuondolewa kama njia halali ya kumkaribia Mungu (Waebrania 10:9). Lakini Yesu hakutaka kuacha maoni kwamba alikuwa na mtazamo hasi kuhusu Sheria za Kale. Kinyume chake, Sheria za Kale zilikuwa chombo cha kimungu kilichoundwa kutimiza makusudi ya kimungu.

  Yatupasa kujifunza kwa makini maneno matatu ya Agano Jipya ambayo yametumika kuelezea hali ya Agano la Kale. Yesu alitangaza kwamba hakuja “kuondoa” Sheria (Mathayo 5:17). Neno “Katalusai” linamaanisha “kuondoa athari au uhalali wa kitu,””kutupilia mbali,””kuharibu, kubomoa, kuangusha chini.” Kwa maneno mengine, maisha na kazi ya Yesu hayakuwa yamekusudiwa “kuondoa” au “kukatisha tamaa” mpango na madhumuni ya Sheria. Badala yake, lengo lake lilikuwa

  “kuitimiliza” au kuikamilisha Sheria. Kwa upande mwingine, Sheria ya Kale kama chombo cha muda ambacho Wayahudi walitumia kuonesha imani kilifutwa (exaleipsas, Wakolosai 2:14) na hivyo kutofanya kazi tena na kupoteza nguvu zake (katargesas, Waefeso 2:15). Kwa maneno mengine, Sheria za Kale zilifanya kazi yake wakati wa kipindi kilichokusudiwa, lakini tangu Yesu alipokuja na kufanya kazi yake, Sheria za Kale kwa sasa hazina kazi—hazina ufanisi wa kisheria tena na hivyo kupoteza ushawishi na nguvu zake kama njia maalum

  ya kuonesha imani. Hatuhitaji tena “msimamizi” au “mlezi” (paidagogos—Wagalatia 3:24-25) sasa kwamba tunaweza kuwa “watoto wa Mungu kwa imani katika Kristo Yesu” (Wagalatia 3:26). Mstari wa 18 unasisitiza kwamba Sheria ingebaki kamili na kufanya kazi kikamilifu hadi Yesu alipotimiza madhumuni yake kwa kujitoa mwenyewe kama tiba ya mwisho kwa kutengwa kwa mwanadamu na Mungu. Hakuna herufi moja wala nukta moja ya herufi ingepita kabla ya utimilifu kutimia.

  Akiwa na tathmini hii ya kweli na sahihi ya Sheria za Kale, Yesu aliwaeleza watu wa wakati wake umuhimu wa kubaki wanyenyekevu na watiifu kwa sheria za Mungu zilizotolewa kupitia Musa (Mathayo 5:19). Viongozi wa Kiyahudi hasa walikuwa wasiojali, wasiofuata sheria kwa ukamilifu, wakifanya mzaha na kutotii kabisa katika maeneo mengi ya sheria za Mungu. Walikuwa wanadharau utii wa unyenyekevu na kamili na kuwafundisha wengine kufanya vivyo hivyo. Mtazamo huu mbaya kuhusu dini ya Mungu chini ya Agano la Kale ungebebwa kwa kawaida hadi kwenye Agano Jipya. Yesu alitangaza kwamba watu kama hao wangehesabiwa kuwa “wa mwisho,” yaani, kuchukuliwa kwa dharau na kutothaminiwa. Wale ambao ni “wakuu” katika ufalme ni wale wanaoshikilia amri zote za Mungu kwa heshima kuu—hata zile ambazo wanadamu wanaona kuwa si muhimu kulingana na makadirio ya kibinadamu. Tofauti na wale wanaokataa utii kamili kwa kisingizio cha “Neema,” wale ambao ni “wakuu” katika ufalme wa Kristo ni wale wanaoonesha umakini na kujali sana kufuata kila amri ya Mungu.

  Lakini ni nani katika siku za Yesu angeweza kuthubutu kukiuka sheria za Agano Jipya na kuwafundisha wengine kufanya vivyo hivyo? Ni wazi, waandishi na Mafarisayo— viongozi wa kidini wa siku hizo. Kwa namna gani hasa walikuwa wakifanya hivyo? Kwa kupotosha na kufasiri vibaya sheria za Agano la Kale kwa ajili ya maslahi yao binafsi (angalia Mathayo 15:1-9). Kwa hiyo, ili watu wa wakati wa Yesu waweze kukubalika kwa Mungu, “haki” yao, yaani, matendo yao ya kidini, ilihitaji kuzidi haki ya viongozi wao wa kidini (Mathayo 5:20). Hiyo ina maana kwamba wale waliotaka kumpendeza Mungu walihitaji kufasiri sheria za Musa kwa usahihi na kuishi kwa kuzifuata.

  Kuanzia mstariwa 21, Yesu anaendelea kueleza maana ya “kuzidi haki ya waandishi na Mafarisayo.” Anafanya hivyo kwa kuashiria baadhi ya “michongoma” iliyokua kuzunguka sheria asilia za Musa. Kisha anaeleza nia za kimungu zinazozingatia masuala kadhaa ya Agano la Kale, akielezea kusudi la awali la mapenzi ya Mungu kuhusu mambo kadhaa ya sheria za Musa.

  Yesu alielewa kikamilifu wema kamili wa sheria za Mungu

  (tazama Kumbukumbu la Torati 10:13; Zaburi 119). Kama Mungu Mwenyewe, alijua kwamba sheria za Mungu katika kila kipindi cha historia ya binadamu zimekusudiwa kukuza hali ya kiroho kwa wale ambao wangetii kwa unyenyekevu. Sheria za Mungu daima zimekuwepo kuzaa utakatifu na usafi wa moyo. Watu wa wakati wa Yesu walihisi kwamba msisitizo wao wa nje na wa kiraia kwenye Sheria za Kale ulikuwa wa kutosha, lakini Yesu alisisitiza kwamba utii dhaifu kama huo ulifanya Neno la Mungu kupitia Musa kuwa bure (yaani, kubatilisha na kuondoa kusudi la awali na nguvu ya sheria). Matokeo yake, Yesu aliendelea kukemea utii wa nje tu kwa sheria za kimungu (kwa mfano, Mathayo 23). Hakuupunguza kamwe utii kwa vipengele maalum vya sheria za Musa wakati wa maisha yake duniani. Mtazamo kama huo si “Utiifu.” Wakati wa Yesu, watu walipotosha dini ya kweli kwa kusisitiza utii wa nje huku wakipuuzia nia ya ndani.

  Mstari wa21-26

  Yesu alitoa kinyume kingine. Suala la mauaji lilishughulikiwa katika Amri Kumi (Kutoka 20:13; Kumbukumbu la Torati 5:17). Marejeo ya “hatari ya hukumu” hayapatikani katika Agano la Kale. Yesu anachanganya nukuu hizi mbili ili kusisitiza ukweli kwamba sheria dhidi ya mauaji hatimaye ilionekana kama katazo tu dhidi ya tendo la nje. Kwa hiyo, Wayahudi walijisikia wana haki wakati walipokuwa na kinyongo na hasira mioyoni mwao kwa mwingine mradi tu hawakutekeleza hasira hiyo kwa mauaji. Walihisi wangeweza kutii kwa matendo na kupuuza mtazamo. Lakini, waziwazi, sheria ya Mungu kupitia Musa haikukusudiwa tu kukataza mauaji huku ikiruhusu hasira ya mauaji kubaki moyoni. Ni hakika, Agano la Kale lilikemea mara kwa mara hisia za hasira na chuki (Mambo ya Walawi 19:17; Mithali 24:12, 1718, 29; 25:21-22). Kwa hiyo, aya za 22-26 zinajumuisha uchambuzi wa Yesu kuhusu maana ya sheria asilia ya Mungu kuhusu mauaji bila upotoshaji wa miaka ya maoni ya marabi.

  [KUMBUKA: Angalia kwamba dai la kawaida kwamba Sheria za Musa zilishughulikia tu tendo la nje, wakati sheria za Yesu zilikwenda mbali zaidi kwa kushughulikia moyo na nia nyuma ya tendo la nje, yumkini hili ni dai lisilo sahihi. Soma

  Mambo ya Walawi 19:17-18; Mithali 4:23; 25:21-22 (iliyotajwa na Paulo katika Warumi 12:20).]

  Yesu alieleza kwamba Mungu alitaka Wayahudi (na jambo hilo hilo linabaki kwa watu wanaoishi leo—Wakristo na wasio Wakristo) wawe na uhusiano wa upendo, amani, na umoja. Maneno ya matusi (kwa mfano, “raka” na “mpumbavu”) mara nyingi yanaonesha moyo uliojaa chuki. Yesu alitangaza kwamba mtazamo wa chuki ni sawa na mauaji (tazama 1 Yohana 3:15). “Raka” inamaanisha “kichwa tupu” na inakumbusha neno letu “mpumbavu.” Matusi kama hayo sio tu yanaonesha moyo usio na huruma wa mtumiaji bali pia yanamjeruhi kwa zaidi mtu ambaye yanaelekezwa kwake. Kwa hakika, kuna nyakati ambapo maneno kama hayo yanafaa (kwa mfano, Zaburi 14:1; Mathayo 23:17). Hata hivyo, hapa Yesu anakemea mtazamo mkali, wenye dhambi wa hasira ambao hujidhihirisha kwa maneno ya uhasama na dharau. Sisi wanadamu tuna tabia ya kupima hali ya kiroho kwa matendo ya nje tu. Lakini Mungu anaangalia moyo (1 Samweli 16:7). Anaona mahali ambapo lugha na matendo mabaya inatoka.

  Sisi wanadamu pia tuna tabia ya kuhisi kwamba tunaweza kuwa sawa na Mungu na kuwa ndani ya neema zake nzuri huku tukiwa tumetengana isivyo haki na binadamu wenzetu. Mstari wa 2324 inaendeleza mafundisho juu ya hasira kwa kusema kwamba ibada inayotolewa kwa Mungu haiwezi kuwa na maana wakati tunapokuwa na ugomvi na ndugu zetu. Ikiwa hatuwezi kumpenda binadamu mwenzetu ambaye tumemuona, hatuwezi kumpenda Mungu ambaye hatujamwona (1 Yohana 4:20). Hatupaswi kuacha hasira yetu idumu muda mrefu (Waefeso 4:26). Ikiwa tumemfanyia mtu mwingine jambo baya ambalo hatukupaswa kulifanya, Mungu anataka tusafishe jambo hilo. Atatuhesabu kuwa na hatia kwa hilo kwenye hukumu na tunaweza kuwajibika katika maisha haya ikiwa mtu aliyekosewa ataamua kwenda mahakamani na kutushtaki (Mathayo 5:25-26). Mkosaji atafanya vyema kusuluhisha jambo hilo na aliyekosewa njiani kuelekea mahakamani kabla ya jaji kutoa hukumu dhidi ya mkosaji na kutupwa gerezani! Tena, Yesu alitoa maelezo ya kitaalamu juu ya maana asilia ya sheria ya Musa.

  Mstari wa 27-32

  Yesu aligeukia suala jingine la kisheria linalohusiana na Sheria za Musa na tafsiri mbaya ya Kiyahudi (Mathayo 5:27). Kimsingi, Yesu alitangaza, “Mmelewa Sheria ya Kale kukataza tu tendo la nje la uzinzi. Lakini nawaambia kwamba sheria ya asili ilikusudiwa kuzuia tamaa na talaka—vitu ambavyo vinaenda sambamba na uzinzi.” Kisha alieleza (mstari wa 28) kwamba wakati wanaume wanamtamani kwa mioyo yao mwanamke, wanakuwa wanazini kisaikolojia, kitu ambacho sheria ililaani (tazama 2 Petro 2:14). Mtu angefanya vyema kukata kabisa kiungo cha mwili wake kinachowezesha uovu huo (mstari wa 29-30; tazama pia Mathayo 10:28). Bila shaka, Yesu hakuwa anahimiza kukata viungo vya mwili. Badala yake, alisisitiza uzito wa dhambi jinsi inavyotoka moyoni na kupokea msukumo kutoka kwa hisia zetu za kimwili. Tunapaswa kuua viungo vyetu vya mwili (Wakolosai 3:5) katika maisha hayala sivyo, tutakabiliwa na shida kubwa zaidi: jehanamu ya milele.

  Mstari wa 31-32

  Wayahudi walipoamua kupotosha Kumbukumbu la Torati 24 kwa maana kwamba wangeweza kuwapa talaka wake zao kwa sababu yoyote, walikuwa wanavunja amri dhidi ya uzinzi zaidi (Mathayo 5:31). Walikuwa na jukumu la kusababisha wake zao waende kwa wanaume wengine na hivyo kufanya uzinzi (Mathayo 5:32). Kwa kuwa mwanamke alikuwa ametupwa nje kwa sababu nyingine isipokuwa uasherati, yeyote atakayemwoa atakuwa na hatia ya kufanya uzinzi pia. Kumbuka kwamba mwongozo wa Kumbukumbu la Torati 24 haukuwa sehemu ya kanuni asilia za Sinai. Ilikuwa ni ruhusa iliyotolewa kutokana na ugumu wa mioyo yao (Mathayo 19:8) na ililenga—siyo juu ya uhalali wa talaka—bali juu ya haki za mke asiye na hatia.

  Kwa hiyo Yesu hakuwa akiiweka Sheria ya Musa (“usiwe mzinzi”) kinyume na mafundisho yake mwenyewe (“usiwe na tamaa na mwanamke”). Agano la Kale lenyewe lilipiga marufuku tamaa kwa wanawake (Kutoka 20:17; Mithali 5; 6:25; 7:25). Badala yake, Yesu alikuwa anaeleza kwamba sheria ya awali iliyokataza uzinzi, kwa maana yake, ilikataza chochote ambacho kingeweza kusababisha au kuchangia uzinzi.

  Mstari wa 33-37

  Yesu alihutubia upotoshaji wa wakati wake kuhusu sheria za kale zinayohusu viapo na kuapa. Vipengele vya Agano la Kale vinavyohusiana na viapo vilikuwa vinataka uaminifu na kujitolea kwa kweli. Kiapo kilikuwa ni tamko rasmi la nia ya mtu binafsi. Sheria za Kale hazina dalili yoyote ya viwango tofauti vya dhamira kwa upande wa mwenye kiapo. Viapo vyote vilitakiwa kuchukuliwa kwa msingi wa uwepo wa Mungu na kuwajibika mbele yake.

  Hata hivyo, kwa muda uliopita, Wayahudi walikuwa wameendeleza zaidi mfumo wa kuchukua viapo ambao uligawa kati ya viwango tofauti vya ukali kulingana na vitu mbalimbali (k.m., mbingu, dunia, Yerusalemu, nywele). Viongozi wa kidini wa wakati wa Yesu walikuwa wamefikia hatua ambapo uhalali wa kiapo haukutegemea—sio juu ya uaminifu wa mtu binafsi—bali juu ya utakatifu wa kitu ambacho mtu alikiapia. Yesu aliilaani siasa za aina hiyo zisizokuwa na maana na kuthibitisha tena nia asilia ya mapenzi ya kimungu: sema ukweli katika hali zote. Baada ya yote, Mungu yuko juu ya kila kitu ambacho mtu anaweza kukiapia ili kuthibitisha kiapo chake. Kwa hiyo viapo vyote vinapaswa kuwa tu uthibitisho wa ukweli kwa mwanga wa uwepo wa Mungu kila mahali. Yakobo aliendelea kutoa mafundisho kama hayo (Yakobo 5:12). Kwa hiyo, Yesu hakuwa anakataza viapo vya kisheria vinavyofanana na uthibitisho wa “ndio” au “hapana” wa ukweli. Alikuwa anakataza kuapa kwa vitu kwa lengo la kuepuka kutangaza ukweli kwa uwazi.

  Mstari wa 38-42

  Marejeo ya Bwana wetu yaliyofuata yalikuwa upotoshaji wa sheria za Musa ambazo zilipangilia adhabu kulingana na uhalifu (Mathayo 5:38). Vipengele vya Agano la Kale vilivyoshughulikia jambo hili vilikusudiwa awali kukuza malipo ya haki, kutoa adhabu inayofaa kwa uhalifu uliofanywa dhidi ya binadamu mwenzako. Maagizo haya yalikuwa, hatua za kizuizi zilizoundwa kuweka mipaka katika adhabu wakati ikionesha maoni ya Mungu kuhusu dhambi na makosa. Mtazamo huu uliakisi haki ya kibinadamu ya Mungu na kumsaidia mwanadamu kukuza mtazamo mzuri kuhusu nini kinachostahili kujibiwa kwa tabia isiyo sahihi na yenye madhara kwa binadamu. Aidha, msemo wa “jicho kwa jicho” ulifanya kama kizuizi ambacho kilizuia mtenda dhambi kutoka kwa kuhatarisha maisha yake mwenyewe kwa kumdhuru mwingine.

  Kuna nyakati, hisia za Kiyahudi zilielewa adhabu ya kifo kama njia ya “kulipiza kisasi” kwa mtu aliyeshambulia. Waliona sheria hii kama njia ya kujipatia kisasi badala ya kizuizi cha huruma na wema. Kwa njia hii, hasira na uadui vilichochewa zaidi badala ya kupingwa kama Mungu alivyokusudia. Kwa njia nyingi, jamii yetu inaonekana imezama katika hamu isiyoshibika ya kushtaki mtu yeyote kwa kila jambo. Roho ya kulipiza kisasi na tamaa imeenea katika utamaduni wa duniani. Matumizi mabaya na unyanyasaji wa mfumo wetu wa kisheria umefanya dhihaka ya sheria ambazo awali zilikusudiwa kurahisisha fidia sahihi. Sasa mfumo unapanuka kwa roho ya kisasi na kisasi kutoka kwa raia na tamaa ya mawakili wao—picha mbaya ya haki. Tunahitaji marekebisho ya maneno kama aliyoyatoa Yesu kwa Wayahudi.

  Yesu alitangaza kile kilichokuwa akilini mwa Mungu katika matamshi ya awali ya Musa. Ingawa sheria lazima iwepo ambayo inazuia na kuadhibu wakiukaji wa sheria mara kwa mara pamoja na kulinda wasio na hatia (1 Timotheo 1:8-9; Warumi 13:1-7), Mungu anataka watu kumpenda na kuishi kwa amani na wenzao, na kusameheana wanapofanya makosa. Kwa hiyo, muumini anapaswa “kutojiteteadhidiyamtumwovu” (Mathayo 5:39). Kwa njia ya kufafanua kauli hiyo ya kishujaa, Yesu ananukuu hali tatu maalum ambazo zinaonesha maana ya kutokujitetea: (1) kugeuza shavu lingine, (2) kutoa joho, na (3) kwenda maili ya pili (Mathayo 5:39-41).

  Tazama kwamba katika kila moja ya hali hizi, Yesu alikuwa akielekeza, siyo utaratibu maalum, bali tabia iliyopo nyuma ya hali hizo tatu. Hapa ndipo hasa fikra za waandishi wa kiyahudi zilikuwa na kasoro. Tunapaswa kukamata tabia ya moyo iliyojikita katika mifano hii ili kutumia kwa usahihi mafundisho ambayo Yesu anayahimiza hapa kwa wingi wa hali ambazo tunakabiliana nazo katika maisha. Tunapenda kupunguza na kutoa nguvu ya maneno ya Yesu katika mifano hii ili tuwe huru kulipiza kisasi tunapohisi inafaa. Ingawa hatungekataa kwamba kuna nyakati zinazofaa ambapo Mkristo anaweza kujitetea kwa haki (k.m., Matendo 16:36-38; 22:25; 25:10-11), tunapaswa kuwa makini sana kwamba hatujiingizi katika roho ileile ambayo Yesu aliikemea: roho ya kisasi na kulipiza kisasi. Ikifika wakati tunapomaliza kueleza maana ya Yesu ya “kugeuza shavu lingine,” tunaweza kuwa tumetenda kinyume kabisa na alichomaanisha Yesu.

  Yesu, Mwenyewe, ni mfano halisi wa maana ya “kutokujitetea dhidi ya mtu mwovu” (mstari wa 39). Aliuvumilia kwa upole unyanyasaji uliofanywa kwake binafsi—jambo ambalo Petro analifafanua kwa ukali na kwa kina (1 Petro 2:21-23). Tazama kwamba kauli hii dhidi ya kujitetea inaelezwa na misemo kadhaa inayofanana katika Agano Jipya: (1) Warumi 12:19—”toa nafasi kwa hasira” (yaani, jiepushe na kisasi na mruhusu Mungu kulipiza kisasi kwa njia yake mwenyewe kwa wakati wake mwafaka); (2) 1 Wakorintho 4:12—”tukidhulumiwa, twavumilia” (yaani, tunastahimili au kuvumilia ukandamizaji badala ya kujibu washambuliaji wetu); (3) 1 Petro 2:19-20— “kustahimili mateso, tukiteswa isivyo haki” na “uvumilie” (yaani, kuvumilia unyanyasaji usiostahili bila kulipiza kisasi); (4) 1 Petro 2:23—”hakutoa mashutumu….hakutishia bali aliweka mwenyewe mikononi mwa yeye atendaye kwa haki” (yaani, Yesu alipokea makonde bila kujibu kwa dharau au kulipiza kisasi); na (5) Warumi 12:17—”usimzawadie mtu yeyote uovu kwa uovu” (yaani, usianguke kwenye tamaa ya asili ya binadamu ya kujibu pale unapodhulumiwa).

  Kimsingi, Paulo alizungumzia jambo lilelile ambalo Yesu alizungumzia katika Mathayo 5. Kufanya hivyo, Paulo anakimbilia kwenye Agano la Kale—akiimarisha zaidi ukweli kwamba Yesu alikuwa akithibitisha na kutetea Sheria za Kale katika Mahubiri ya Mlimani. Paulo ananukuu Kumbukumbu la Torati 32:35 na Methali 25:21-22 ili kusisitiza kwa Mkristo yule yule ambaye Mungu na Kristo walitaka Myahudi wa Agano la Kale atambue, yaani, kwamba kulipiza kisasi hakupo katika mapenzi ya Mungu na kwamba kurudisha mema kwa mabaya ndiyo hatua inayofaa kuchukuliwa kwa wale wanaompenda Mungu.

  Kama mwana wa Mungu anakabiliwa na vurugu za kimwili, haki isiyofuata sheria, au dhuluma ya kiserikali, atajitahidi sana kuepuka mzozo. Atajali kwa dhati wale wanaomtendea vibaya (angalia Matendo 7:60). Atakuwa na wasiwasi mdogo kuhusu kujilinda na zaidi kuhusu ustawi wa binadamu mwenzake (angalia Luka 10:30-37). Badala ya kuwa mwenye tahadhari, wa kujilinda, mchoyo, na “mwenye kushikilia” vitu “vyetu,” tutakuwa wawazi, wenye ukarimu, wakarimu, na wenye upendo (Methali 21:26; Luka 6:38). Yesu alihitimisha katika mstari wa 38-41 kwa kutoa tangazo chanya katika mstari wa 42: “Mpe yule anayeomba kwako, wala usimuache yule anayetaka kukopa kwako.” Amri hii inakumbushia Kumbukumbu la Torati 15:7-11. Chunguza kwa makini sana kifungu hiki cha Agano la Kale, kwa kuwa kinathibitisha kwa hakika, siyo tu kile ambacho Yesu anahimiza kuhusu kulipiza mema kwa mabaya, lakini pia kwamba dini ya Agano la Kale pia ililenga moyo, tabia, na hamasa zinazojenga mienendo yetu ya nje.

  Mstari wa 43-48

  Kifungu cha mwisho cha sura ya 5 kinahusu mchanganyiko wa sheria za Musa na utamaduni kuhusu jinsi ya kuwatendea maadui. Kauli “penda jirani yako” inapatikana katika Mambo ya Walawi 19:18 lakini dhana ya “chukia adui yako” haipo katika Maandiko na ilikuwa dhahiri ni upotoshaji wa Sheria za Kale za Mungu ili kukidhi matakwa ya kibinadamu. Kwa kweli, Matendo mema kwa maadui yanapendekezwa katika Agano la Kale (Kutoka 23:4-5). Ni kweli kwamba Mungu alitaka taifa la Kiyahudi litoe kisasi cha haki kwa jamii za maadui waovu, wasio wa Mungu katika nyakati mbalimbali za historia (linganisha na Warumi 13:1-7). Lakini amri hizi za kiraia hazikuwa na nia ya kuunga mkono, kuthibitisha, au kukuza chuki kwa watu kwa msingi wa upendeleo binafsi.

  Angalau kwa nyakati mbili tofauti, Yesu Mwenyewe aliweka wazi kwamba amri ya asili ya Musa ya “penda jirani yako” ilimaanisha kwamba mtoto wa Mungu anapaswa kutafuta ustawi wa kila mtu—ikiwa ni pamoja na adui yake. Kwenye tukio moja, Aliitambulisha Mambo ya Walawi 19:18 kama amri ya “pili” kuu ya Sheria za Kale (Mathayo 22:39). Kwenye tukio jingine, Aliieleza amri hii kwa kusimlia hadithi ya “Msamaria mwema” na kuonesha kwamba “jirani” yetu ni yeyote, bila kujali kabila la anayehitaji msaada wetu (Luka 10:2527). Yesu kwa makusudi alimchagua Msamaria—adui wa kifo wa Myahudi—kuwa “shujaa” katika hadithi hii ili kusisitiza kwamba kupenda jirani yako kunajumuisha hata maadui. Stefano (Matendo 7:59-60) pia aliwakilisha maana ya Mathayo 5:44.

  Baba, ambao wana mwana au binti mwenye vipaji maalum ambaye anatimiza tendo fulani kubwa, wanakuwa na uwezekano wa kueleza fahari yao kwa mtoto wao kwa kumchekea rafiki kwa kifundo cha mkono, kumwelekeza mtoto wao anayefanya kazi, na kusema, “Huyo ni mwana wangu.” Kwa njia kama hiyo, watoto wa Mungu (5:45) ni wale ambao “wanamfurahisha” Mungu kwa kutendea mpinzani mwovu kwa njia ya upendo. Kwa kweli, kiungo hiki cha kiitikadi ni mwakilishi wa Mungu Mwenyewe. Kutoa baraka zake za kimwili (yaani, jua na mvua—mstari wa 45; linganisha na Matendo 14:17) kunapangwa hata kwa wale ambao hawastahili. Mungu ni mwenye fadhili hata kwa wasio na shukrani na waovu (Luka 6:35).

  Sio tu kwamba kutendeana mema kunatufanya tuwe kama Mungu, bali pia hutufanya tofauti na wasio wa Mungu. Hata wakusanyaji wa kodi na watu wa mataifa (teloni, ethnikoi) wasio na toba na wakaidi wanadhihirisha upendo, wema, na salamu za kirafiki kwa watu wa aina yao. Yaani, mkusanyaji wa kodi msaliti na mwenye tamaa na mtu asiye Myahudi—wote ambao wasikilizaji wa Yesu wangewaona kama wapotovu— walikuwa na kiasi cha “upendo” na mwenendo mwema. Lakini mfuasi wa Mungu anazidi tendo la kawaida, la kibinadamu kwa kuwapita na kufikia mahali pa juu zaidi ya maisha ya kiroho.

  Hatimaye, Yesu analeta kwa kifupi, kwa maneno ya haraka, kifungu kinachofaa cha kufunga mawazo haya kuhusu mapenzi ya Mungu na upendo kwa binadamu mwenzake. Anawaomba

  Wayahudi (na Wakristo leo) kuwa “kamili” kwa njia ile ile ambayo Mungu ni “kamili” (5:48). Neno teleioi halirejelei ukamilifu kwa maana ya kutokuwa na dhambi. Badala yake, “kamili” inamaanisha “kukomaa,””kuwa mkamilifu,””kuwa kamili katika maana ya maadili.” Katika muktadha, Yesu anapinga njia iliyovunjika ambayo Wayahudi walikuwa wakiitumia katika mahusiano yao. Upendo wao kwa jirani ulikuwa umegawanyika na haujakamilika. Walihitaji kupenda hata maadui zao pamoja na marafiki zao. Kwa msingi huu, wanakumbushwa kuwa kamili kwa njia ile ile ambayo Mungu ni kamili. Anawapenda ulimwengu wote wa binadamu—ikiwa ni pamoja na wabaya (Yohana 3:16). Vivyo hivyo, upendo ambao Wayahudi walipaswa kuwa nao kwa binadamu mwenzao ulipaswa kuwa kamili, na wa kina. Upendo wao ulipaswa kuwa wa jumla, wa ukamilifu, hata kwa maadui.

  HITIMISHO

  Uchambuzi wa kina, wa mstari kwa mstari wa Mathayo 5 unaonesha kuwa, mbali na kudharau Sheria za Musa, Yesu alitangaza kwa wenzake lengo la mantiki la Sheria hiyo, yaani, Yeye mwenyewe. Sio tu kwamba Hakuukosoa mfumo wa Musa, yeye mwenyewe alifuata mafundisho yake kikamilifu (linganisha na Waebrania 4:15). Alihimiza Wayahudi wengine wote kufanya vivyo hivyo. Badala ya kuzungumza kwa dharau kuhusu Sheria, au kukanusha sheria, Yesu alitoa mapendekezo mazuri kuhusu masuala mbalimbali ya kisheria ambayo uongozi wa Kiyahudi ulikuwa umeyavuruga na kuyapotosha katika majukumu yao ya uongozi. Aliwachochea wenzake (na sisi sote) kwenda zaidi ya utekelezaji wa kiasili wa sheria za Mungu. Tunahimizwa kuelewa uwezo kamili wa miongozo hai na inayotoa uhai ya Muumba katika maisha yetu. Tunaitwa kujiepusha na kupotosha mapenzi ya Mungu na kufuata nia ya kimungu. Tunatakiwa kuwa na haki ambayo inazidi dini iliyo duni, iliyopunguzwa, iliyochujwa ya wale ambao wamepoteza lengo la Mungu kwa ajili ya roho zetu. Anataka tufurahi kwa njia ambayo watu kamwe hawatafurahi—isipokuwa wakipamba mioyo yao, akili, na maisha yao kwa ukweli wa nguvu na wa milele wa Mungu.Yesu hakukanusha au kupunguza heshima ya sheria za Musa. Badala yake, alizithamini.

  MAREJEO

  1. Angalia mfululizo wa The Anvil Rings uliyopo kutoka Apologetics Press, pamoja na vitabu vingi kupitia karne ambavyo vinajibu kwa ufanisi madai ya wakosoaji.

  2. Linganisha na Warumi 3:19-20; 7:7,12,14; Wagalatia 3:21. Chambua mjadala wa Gordon Ferguson kuhusu uhusiano kati ya neema, sheria, na upendo katika Thomas B. Warren na Garland Elkins, wahariri. (1978), Mungu Anahitaji Mahubiri ya Kiimani (Jonesboro, AR: National Christian Press), uk.225-236. Bila shaka, Sheria ya Kale ilikuwa dhaifu (Waebrania 8:7) kutekeleza lengo kuu la Mungu duniani. Kama mwandishi wa Waebrania alivyosema mara nyingi, Agano Jipya na vipengele vyake vyote ni “bora” (Waebrania 1:4; 6:9; 7:7,19,22; 8:6; 9:23; 10:34; 11:16,35,40; 12:24) kuliko mfumo wa Musa uliokuwa kabla yake. Lakini hii ni hivyo kwa sababu Sheria ya Musa haikuwa imekusudiwa kufanya kile ambacho sheria ya Kristo ingeweza kufanya. Kile kinachoonekana kama kudharau kwa Sheria katika Agano Jipya kwa kweli ni kuelekezwa kwa maoni potofu na mitazamo isiyofaa ambayo wengi wa Wayahudi walikuwa nayo kuhusu Sheria. Ni jambo la kusikitisha kwamba mtu yeyote angeambatisha na maelezo hasi kisha akateka dhana sawa kwamba Wakristo hawako chini ya sheria au hawahitajiki kufanya utii wa kina.

  3. Tofauti hii inaendelea katika sura ya 6 ambapo yeye anaongeza maoni ya marekebisho yanayohusiana na kutoa kwa upendo (6:1-4), sala (6:5-15), kufunga (6:16-18), na materialismu (6:19-34).

  4. Marko 1:44; 7:10; 10:3; 12:26; Luka 24:27; Yohana 3:14; 5:45-46; 7:19 na kadhalika.

  5. Neno la Kigiriki katika Warumi 10:4 (telos) linahusu ukweli kwamba Kristo (mpango aliotekeleza) ni “mwisho,” yaani, lengo/mwongozo/mkazo/mahitaji, wa sheria. Katika Biblico-Theological Lexicon ya New Testament (Edinburgh: T.&T. Clark), uk. 541, Hermann Cremer alibainisha kwamba neno “halimaanishi, kama ilivyo kawaida, kwanza kabisa mwisho, kufikia kwa wakati, bali lengo lililofikiwa, ukamilifu au hitimisho ambalo lolote linawasilishwa, kama matokeo au kumalizika, na hivyo kujumuisha kumalizika kwa kilichotangulia,” inasisitiza asilia.

  6. Frederick Danker (2000), Kamusi ya Kigiriki-Kiingereza ya Agano Jipya na Fasihi Nyingine ya Kikristo (Chicago, IL:Chuo Kikuu cha Chicago), toleo la tatu, uk. 522; JamesMoulton na George Milligan (1930), Lugha ya Kigiriki ya Agano Jipya Iliyoonyeshwa kutoka katika Papyri na Vyanzo vingine Visivyo vya Fasihi (Grand Rapids, MI: Eerdmans, 1982 chapisha tena), uk. 329; Robert Mounce (2006), Mafanikio ya Kamusi ya Maneno ya Agano la Kale na Jipya ya Mounce (Grand Rapids, MI: Zondervan), uk. 1183.

  7. Danker, uk. 344, 525.

  8. Hii haimaanishi kuwa Agano la Kale halina thamani kwa Mkristo. Paulo alisema kwa kiasi kikubwa kwamba ni muhimu sana katika Enzi ya Kikristo—Warumi 15:4; 1 Wakorintho 10:6,11; 2 Timotheo 3:15-17; n.k. Badala yake, Agano la Kale lililenga kwa kipekee kwa Waisraeli—si Mataifa—na lilifika kilele cha kihistoria kwenye msalaba. Sasa, chini ya Ukristo, binadamu wote—Wayahudi na Mataifa—wanapaswa kufuata masharti ya Agano Jipya.

  9. Bila shaka, Yesu hakuwa anasema kwamba tamaa ni sawa na uzinzi na,  hivyo, sababu za talaka. Alikuwa tu anabainisha kwamba tamaa na uzinzi wote ni dhambi. Uzinzi ambao ni sababu halali ya talaka (Mathayo 19:9) unahusisha kitendo cha kimwili—kama vile mauaji yanahusisha kitendo cha kimwili cha kuchukua maisha ya mtu mwingine.

  10. Tazama Jack P. Lewis (1978), “From the Beginning It Was Not So…” katika Your Marriage Can Be Great, ed. Thomas B. Warren (Jonesboro, AR: National Christian Press), uk. 410-419. Tazama pia Dave Miller (2020), “Did Moses Command Divorce? (Deuteronomy 24:1- https://apologeticspress.org/did-moses-commanddivorce-deuteronomy-241-4-5880/.

  11. Kutoka 20:7; Mambo ya Walawi 19:12; Hesabu 30:2; Kumbukumbu la Torati 5:11; 23:21-23.

  12. Katika kiwango kirefu talion inaeleweka kama kauli ya kiafya ya haki ya kishairi, ambapo wazo kuu ni sahihi ya kukaa, ukamilifu wa kulingana. Acha adhabu ifanane na kosa”—William Miller (2006), Eye for an Eye (New York: Cambridge University Press), uk. 65.

  13. Kutoka 21:24; Mambo ya     Walawi 24:20; Kumbukumbu la Torati 19:21.

  14. “Ilifunga mlango wa kisasi usio na kikomo na kuweka adhabu isizidi kosa”—Bruce Metzger na Michael Coogan, eds. (2001), “V” katika The Oxford Guide to Ideas & Issues of the Bible (New York: Oxford University Press).

  15. Danker, uk. 995-996.

   KUNAKILI & MASHARTI: Tuna furaha kutoa ruhusa kwa nakala hii kunakiliwa sehemu au kwa jumla, ikiwa tu masharti yetu yanazingatiwa.


   Published

   A copied sheet of paper

   REPRODUCTION & DISCLAIMERS: We are happy to grant permission for this article to be reproduced in part or in its entirety, as long as our stipulations are observed.

   Reproduction Stipulations→