Je, Imani ni Zawadi Kutoka kwa Mungu?
“Kwa maana mmeokolewa kwa neema kupitia imani. Na hii si kazi yenu wenyewe; ni zawadi ya Mungu, si kwa matendo, ili mtu yeyote asije kujivuna” (Waefeso 2:8-9 ESV).
Kwa karne nyingi, waandishi wa Biblia wamekuwa na maoni tofauti juu ya rejeo halisi la kiwakilishi “hii” (“ile” katika KJV ASV) katika Waefeso 2:8. Je, “hii” (neno la kigiriki “touto”) linarejelea imani kama wengi walivyosema ? (Augustine, Chrysostom, Westcott, Lenski, n.k.) au “hii” inarejelea wokovu kutoka dhambini? Je, imani ni “zawadi ya Mungu” au zawadi hii ni wokovu kwa neema kupitia imani?
Kukubali, kutokana na kusoma kwa haraka Waefeso 2:8 inaweza kuonekana kuwa, kiwakilishi kinachooneshwa, “hii” kina maanisha imani kama kiwakilishi cha kisarufi. Wale wanaoamini kuwa imani ni zawadi (yaani, imani ya miujiza) kutoka kwa Mungu mara nyingi wanasema kuwa katika aya hii “imani” ni kiwakilishi cha karibu zaidi cha “hii” (“Kwa maana mmeokolewa kwa neema kupitia imani. Na hii si kazi yenu wenyewe; ni zawadi ya Mungu”). Hata hivyo, mtu anapochunguza Waefeso 2:8 katika lugha ambayo iliyoandikwa awali (Kigiriki), atagundua kuwa kiwakilishi “hii” (neno “touto”) ni jinsi isiyo na jinsia, yaani neuter kwa lugha ya kilatini) wakati neno imani yaani pistis kwa kwa kigiriki hutumika kwenye jinsia ya kike. Kwa kuwa kanuni ya jumla katika sarufi ya Kigiriki ni kwamba jinsia na idadi ya kiwakilishi inafanana na ile ya kiwakilishi chake (Mounce 1993, ukurasa 102-109), basi hali maalum ya lugha, matumizi maalum ya nahau au sababu nyingine itahitajika kuonesha uhalali wa kuunganisha “hii” na “imani.” Kama sababu ya kutosha haiwezi kuoneshwa, basi mtu analazimika kuendelea kujifunza kifungu hicho ili kujua uhakika wa zawadi hii ya Mungu ni nini.
Ikiwa hakuna kiwakilishi cha wazi kinachopatikana ndani ya maandiko, msomi wa Kigiriki William Mounce anapendekeza kwa busara kwamba mwanafunzi wa Biblia ajifunze muktadha wa kifungu husika ili kusaidia kuamua ni nini kiwakilishi hicho anachokirejelea (1993, ukurasa 111). Muktadha wa jumla wa sura tatu za kwanza za Waefeso ni wokovu wa mwanadamu unaopatikana ndani ya Kristo.
- “Ndani yake tuna ukombozi kupitia damu yake, msamaha wa dhambi, kulingana na utajiri wa neema yake”(1:7).
- Urithi wa mbinguni unapatikana ndani ya Kristo (1:11).
- Baada ya kuamini habari njema ya wokovu kupitia Kristo, Waefeso walitiwa muhuri kwa Roho Mtakatifu wa ahadi (1:13).
- Wenye dhambi wanafanywa “hai pamoja na Kristo” na kuokolewa “kwa neema” (2:5).
- Wenye dhambi wanaletwa karibu na Mungu “kwa damu ya Kristo” (2:13).
- Paulo alifanyika mtumishi wa Kristo “kwa kadiri ya kipawa cha neema ya Mungu…kwa utendaji wa nguvu zake” (Waefeso 3:7).
Siyo tu kwamba muktadha wa wokovu ni muktadha wa jumla wa sura tatu za kwanza za Waefeso, bali muktadha wa karibu wa Waefeso 2:8-9 ni wa wokovu si wa imani. Mistari hii miwili inatoa maelezo ya jinsi gani mtu anaokolewa, si jinsi gani mtu anaamini.
- Wokovu ni kwa neema.
- Wokovu ni kupitia imani.
- Wokovu si wa nafsi zenu wenyewe.
- Wokovu ni zawadi ya Mungu.
- Wokovu si wa matendo.
Paulo hakuwa akieleza juu ya imani katika barua yake kwa Waefeso. Wokovu ulikuwa ndilo lengo lake. Imani inatajwa kama njia ambayo wokovu unakubaliwa. Wokovu ni kupitia imani. Kama vile maji yanavyopokelewa ndani ya nyumba katika karne ya ishirini na moja hapa Amerika kupitia bomba, mwenye dhambi anapokea wokovu kupitia imani inayotii. Lengo kuu la ujumbe wa Paulo katika Waefeso 2:8-9 lilikuwa wokovu (“maji yaliyo hai yanayobubujika hadi uzima wa milele”—linganisha na Yohana 4:14), sio njia ya wokovu.
Imani si zawadi ya moja kwa moja kutoka kwa Mungu inayotolewa kwa wengine na si kwa wengine. Badala yake, kama Paulo alivyoandika kwa kanisa la Roma, “imani huja kwa kusikia, na kusikia kwa neno la Mungu” (Warumi 10:17). Imani kwa Kristo kama Mwana wa Mungu inapatikana tu kwa wale ambao kwanza wamesikia Neno la Mungu, na kisha wakaamini (linganisha na Yohana 20:31).
MAREJELEO
Mounce, William D. (1993), Basics of Biblical Greek (Grand Rapids, MI: Zondervan).
UZALISHAJI & MASHA RTI: Tunayo furaha kutoa ruhusa ya makala hii kuzalishwa kwa sehemu au kwa ukamilifu, ili mradi masharti yetu yazingatiwe.
REPRODUCTION & DISCLAIMERS: We are happy to grant permission for this article to be reproduced in part or in its entirety, as long as our stipulations are observed.