Je! Hatimaye Sayansi Itamuua Mungu?
Dhana isiyowezekana, na bado imeteka hisia za vyombo vya habari kwa miaka mingi (kama Wolchover, 2012). Je,sehemu kubwa ya jamii itaelekea kuendeleza harakati zake mbali na Mungu katika miaka ijayo? Pengine, kwa kuwa huo umekuwa mwelekeo wa kihistoria, ndani na nje ya biblia. Lakini Mungu hajawahi kuondolewa katika mawazo ya mwanadamu katika maelfu ya miaka ya kuwepo kwa mwanadamu, kwa sababu mkono wake wa uangalizi huleta adhabu kwa jamii katika nyakati hizo ambapo idadi ya watu kwa idadi ya kutosha inampa Mungu kisogo. Kisha bila kuepukika kurejea kwa wengi kwa mambo ya kiroho (Tazama Miller, 2008).
Bado, kulingana na NBC News, Sean Carroll, mwanacosmolojia kinadharia katika Taasisi ya Teknolojia ya California, anaamini kwamba hatimaye sayansi itaondoa hitaji la Mungu katika mlinganyo kueleza matukio Fulani ya ulimwengu. Anasema kwamba, “Upeo wa ushawishi wa Mungu umepungua sana katika nyakati za kisasa” (Wolchover). Hatuna uhakika ni wapi anapata taarifa zake, kwa sababu kitakwimu, dunia ina nadharia nyingi (84%) wasio mwamini Mungu “theists” ( mfano “Dini kuu za dunia” 2007), na asilimia ya watu katika nchi hii wanaoamini hivyo kuwa Mungu amekuwa na jukumu katika asili ya ulimwengu ni (78%) ni zaidi ya jumuia ya mageuzi ya kilimwengu ambayo ni (15%) (Tazama Miller, 2012). Ingawa kwa hakika kumekuwa na ongezeko la safu za jumuiaya zisizo za kidini katika miaka kadhaa iliyopita, Dunia bado, kwa mbali, ni ya kidini.
Carroll anadai zaidi kwamba matukio mengi ambayo yalionyeshwa mara moja kama uthibitisho wa kuwapo kwa Mungu, kwa kuwa sayansi haikuweza kuelezea matukio hayo, yanaondolewa hatua kwa hatua, kwa maoni yake. Anaamini kwamba hitaji la Mungu kusababisha mlipuko mkubwa “BIG BANG” linachangiwa na wazo la ulimwengu wa milele-ulimwengu kama ule unao nadharia na mtindo wa “Oscillating Universe Big Bang.” [KUMBUKA: Hii haimaanishi kwamba tunaamini Nadharia ya “Big Bang” kuwa ya kweli. Tumeelezea masuala kadhaa ambayo yanaonyesha “Big Bang” kuwa ya kweli. Tumeelezea masuala kadhaa ambayo yanaonyesha “Big Bang” kuwa ya uwongo kwingineko (kama., Thompson, Harrub, May, 2003). Tunashughulikia tu madai yake.] Anaamini kwamba tatizo la kuwa na sababu ya lazima kwa ulimwengu, hata kama ulimwengu sio wa milele, linaimarishwa na wazo kwamba wakati ulianza kwenye mlipuko mkuu, na kwa hiyo, hakuna haja ya sababu ya awali. Kulingana na Alex Filippenko, mtaalamu wa elimu ya nyota katika Chuo Kikuu cha California, Berkeley ambaye amenukuliwa katika Makala hiyo, “The big Bang” ingeweza kutokea kutokana na sheria za fizikia kuwa huko. Kwa sheria za fizikia, unaweza, unaweza kupata ulimwengu. Carroll anadai zaidi kwamba hoja ya “mipangilio mizuri” inayotumiwa na wanatheists kuhusiana na uthabiti mwingi wa kimaumbile ambao unaonekana kufaa kabisa kwa uwepo wetu, inaweza kubadilishwa kwa kutumia nadharia kuhusu ulimwengu sambamba zaidi ya yetu (Wolchover).
Maoni kadhaa yanafaa kutajwa katika kumjibu Carroll. Kwanza kabisa, ona kukiri kimyakimya kwamba Mungu bado anahitajika ili kueleza baadhi ya mambo katika ulimwengu, hata kama yanaweza kuondolewa katika akili ya Carroll. Masuala mengi yanayoelezeka kwa Mungu yameondolewa, kwa maoni ya Carroll: lakini hiyo inamaana kwamba baadhi yamesalia.
Pili, jaribio lake la kukabiliana na tatizo la kuhitaji “kichochezi” cha mlipuko mkubwa kwa kutoa uthibitisho kwa nadharia zinazodai umilele wa ulimwengu, halitoi wazo la kwamba sayansi imeondoa hitaji la Mungu katika eneo hilo. Kinyume chake, sayansi tayari imezungumza juu ya jambo hilo. Hakuna kinachodumu milele, kwa mujibu wa sheria ya 2 ya Thermodynamics (Tazama Miller, 2007 kwa mjadala wa kina wa sheria za Thermodynamics jinsi zinavyohusiana na ulimwengu kwa ujumla). Kwa hiyo nadharia kama hizo hazipatani na matokeo ya sayansi. Kwa kuwa hakuna kitu kinachodumu milele katika asili, ulimwengu haungeweza kudumu milele-Mungu anahitajika.
Jaribio lake zaidi la kuachilia mbali suala la kuhitaji sababu ya mwanamitindo asiyekuwa wa milele wa ulimwengu, mlio mkubwa,” kwa kubishana kuwa wakati ulianza kwenye “Big Bang”, ni kumkumbusha maoni ya hivi majuzi ya Stephen Hawking kuhusu suala hilo. Hata hivyo, kama tulivyojadili mahali pengine (Tazama Miller, 2011), wazo hilo pia haliambatani na ushahidi wa kisayansi. Ulimwengu haungeweza kujisababisha wenyewe kwani, kwa asili, hakuna kitu kinachotoka kwa chochote. Nishati haiwezi kuzalisha yenyewe, kulingana na ushahidi kutoka kwa sayansi-haswa sharia ya 1 ya Thermodynamics (Tazama Miller, 2007). Nadharia zinazotoa dhana hizo potofu hazipatani na sayansi. Kwa hiyo, kwa mara nyingine tena, sayansi haijaondoa uhitaji wa Mungu katika hali hiyo pia. Kuwepo kwa ulimwengu bado kunahitaji sababu ya kutosha, kulingana na ushahidi kutoka kwa sayansi.
Maoni ya Filippenko yanakazia tu suala jingine ambalo sayansi haiwezi kueleza bila Mungu-kuwapo kwa sheria za fizikia. Shairi linahitaji mshairi. Sheria inahitaji mwandishi wa sheria. Kama vile mwanafizikia mashuhuri wa nadharia ya kutokuwepo kwa Mungu, mwanacosmolojia, na mwanabiolojia wa Chuo Kikuu cha Arizona State, Paul Davies, alivyosema, “ Unahitaji kujua sheria hizo zinatoka wapi. Hapo ndipo siri ilipo-sheria (Swali la Uumbaji…,” 2011). Mtu asiyeamini kuwa kuna Mungu hana maelezo ya jinsi sheria za sayansi zingeweza kujiandikisha kuwapo, na hakuna maelezo ya kimantiki nje ya mwandishi wa sheria ya ulimwengu.
Majaribio ya Carroll ya kuachilia mbali suala la hoja ya ulimwengu iliyopangwa vizuri ya (theist) kwa kuwasilisha ulimwengu sambamba sio hoja nzuri. Sayansi haijathibitisha nadharia kama hiyo. Hakuna ulimwengu mbadala ambao umewahi kushuhudiwa, na kwa hiyo hauko nje ya upeo wa ufafanuzi wa jumuiya ya mageuzi ya sayansi ya majaribio. Hoja kama hiyo ni dhana tu na uvumi-sio ushahidi. Kwa hivyo tena, sayansi haijatupilia mbali hitaji la Mungu katika tukio hili pia.
Mara kwa mara, Carroll hujaribu kueleza hoja yake kwa sayansi kumuondoa Mungu, kwa kutegemea nadharia ambazo haziwezi kuthibitishwa na sayansi au zinazopingana na ushahidi wa sayansi imewahi au inaweza kumuondoa Mungu. Kitu pekee ambacho amethibitisha ni kwamba watu wasioamini Mungu hawakubaliani na maoni yao juu ya suala hili.
Je, ni kweli kwamba watu wengi leo wanakubali “ushahidi” huo na hivyo wanamwacha Mungu? Je, wako katika mchakato wa kumfanya Mungu aondolewe katika akili zao-yaani “kutomweka [Mungu] katika ujuzi wao” (Warumi 1:28)? Je, kuna uwezekano kwamba kutakuwa na watu zaidi na zaidi katika miaka ijayo ambao watajiunga na magendo katika kumkataa Mungu? Hakika. Hata hivyo tabia hiyo haitokani na uthibitisho kutoka kwa sayansi ya kweli, bali ni kutokana na tamaa zao wenyewe (rejea. Warumi 1:20-32). Jambo la kushangaza ni kwamba ingawa watu kama hao wasioamini Mungu huota ndoto kwamba siku moja sayansi itamuua Mungu, sayansi tayari imeondoa kutokuwepo kwa Mungu kama maelezo ya asili ya ulimwengu (tazama, www.apologeticspress.org ili upate ushahidi kuhusu suala hili).
REJEA
“The Creation Question: A Curiosity Conversation” (2011), Discovery Channel, August 7.
“Major Religions of the World Ranked by Number of Adherents” (2007), http://www.adherents.com/Religions_By_Adherents.html.
Miller, Jeff (2007), “God and the Laws of Thermodynamics: A Mechanical Engineer’s Perspective,” Reason & Revelation, 27[4]:25-31, April, https://www.apologeticspress.org/articles/3293.
Miller, Jeff (2008), “The Cycle of Unbelief,” Apologetics Press, https://www.apologeticspress.org/APContent.aspx?category=7&article=2495.
Miller, Jeff (2011), “A Review of Discovery Channel’s ‘Curiosity: Did God Create the Universe?’” Reason & Revelation, 31[10]:98-107, https://www.apologeticspress.org/apPubPage.aspx?pub=1&issue=1004&article=1687.
Miller, Jeff (2012), “Literal Creationists Holding Their Ground in the Polls,” Reason & Revelation, 32[9]:94-95, September, https://www.apologeticspress.org/APPubPage.aspx?pub=1&issue=1093&article=2040#.
Thompson, Bert, Brad Harrub, and Branyon May (2003), “The Big Bang Theory—A Scientific Critique [Part 1],” Reason & Revelation, 23[5]:33-47, May, https://www.apologeticspress.org/apPubPage.aspx?pub=1&issue=541&article=540.
Wolchover, Natalie (2012), “Will Science Someday Rule Out the Possibility of God?” NBC News: Science, September 18, http://www.msnbc.msn.com/id/49074598/ns/technology_and_science-science/#.UFnWIlEpCeZ.
REPRODUCTION & DISCLAIMERS: We are happy to grant permission for this article to be reproduced in part or in its entirety, as long as our stipulations are observed.