Menu

Isaya na Uungu wa Kristo

Imekuwa maarufu katika miaka ya hivi karibuni kuichukulia asili ya kiungu ya Kristo kama fundisho lililobuniwa tu na Wakristo mara baada ya kifo cha Yesu. Katika kitabu chake maarufu The Da Vinci Code, Dan Brown alidai kuwa Uungu wa Yesu ulikuwa umetungwa miaka 300 baada ya kusulubishwa Kwake (2003, uk. 233- 234). Mashahidi wa Yehova pia mara kwa mara husambaza fasihi inayosisitiza kwamba asili ya kiungu ya Kristo ni ya mafundisho ya wanadamu, na si mafundisho ya kweli ya Mungu (ona “What Does…,” 1989, uk. 12-16). Ingawa vifungu vingi katika Agano Jipya vinaweza kuchunguzwa ili kuelezea na kufafanua Uungu wa Yesu (k.m., Yohana 1:1-5,14; 20:28; Wafilipi 2:6; Waebrania 1:5-13; n.k.), cha kuvutia hasa ni ukweli kwamba muda mrefu kabla Yesu hajatokea duniani katika umbo la mwanadamu katika karne ya kwanza, katika Agano la Kale nabii Isaya alitabiri Uungu Wake.

Katika takriban 700 K.K., Isaya alitabiri kuhusu mambo mengi yanayomhusu Kristo. Msomi wa Kiebrania Risto Santala aliandika hivi: “Hali ya umasihi wa kitabu cha Isaya iko wazi kwamba vyanzo vya kale vya kiyahudi, Targumi, Midrash na Talmud, vinazungumza juu ya Masihi katika muunganiko wa mistari tofauti ipatayo 62” (1992, kur. 164-165), ikiwemo Isaya 9:6. “maana kwa kwa ajili yetu,” Isaya alitabiri, “maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa…; na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake. Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa Ajabu, Mungu Mwenye Nguvu, Baba wa Milele, Mfalme wa Amani” (9:6, miss.uliongezwa). Kuhusu Masihi, Isaya pia aliandika, asingekuwa tu “Mfalme wa Amani,” na “Mshauri wa Ajabu” (NASB), lakini pia “Mungu Mwenye Nguvu” na “Baba wa Milele.” [KUMBUKA: “The Targumi inafafanua aya hii, ikisema: ‘Jina lake limekuwako tangu nyakati za kale…” na, kuhusu kipengele cha ‘Baba wa Milele’ kwamba ‘Masihi amekuwako milele’” (Santala, 1992, 196), au kwamba Yeye ni “Baba wa milele” (ona Jamieson, et al., 1997)]. Zaidi sana, Isaya pia alitabiri juu ya kuzaliwa kwa Masihi na bikira, na kwamba jina lake litakuwa “Imanueli” (7:14), likiwa na maana ya “Mungu pamoja nasi” (Mathayo 1:23, miss. umeongezwa). Kwa nini Isaya angemwita Masihi kuwa ni “Mungu Mwenye Nguvu,” “Baba wa Milele,” na “Imanueli,” kama Yeye hakuwa Mungu?

Inavutia kwamba, zaidi ya miaka 100 kabla ya Yesu kudaiwa kuwa “Mungu aliyetengenezwa” kwenye Baraza la Nicea mwaka wa 325 B.K. (taz. Brown, uk. 233-234), Irenaeus alinukuu kutoka Isaya 9:6 na kutumia majina ya kiungu kwa Kristo, Ambaye “Yeye ni Mwenyewe katika haki Yake… Mungu.”

…huyu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.Kwa jinsi nilivyoonyesha kutoka katika Maandiko kwamba hakuna hata mmoja wa wana wa Adam aliye kwa kila kitu, na pasipo shaka, anayeitwa Mungu, au aitwaye Bwana. Lakini kwamba ni Yeye Mwenyewe katika haki Yake Mwenyewe, aliye zaidi ya wanadamu awaye yote aliyewahi ishi, Mungu, na Bwana, na Mfalme wa Milele, na Neno Lilofanyika mwililililotangazwa na manabii, mitume wote, na kwa Roho Mwenyewe,  wanaweza kuonekana kwa wote waliopata hata sehemu ndogo ya ukweli. Sasa basi, Maandiko yasingekuwa yameshuhudia mambo haya juu Yake, kama alikuwa ni mtu wa kawaida tu kama walivyo watu wengine. Lakini zaidi ya wengine wote, Yeye alikuwako ndani Yake Mwenyewe, kwamba kule kuzaliwa kulikotangulia kumetokana na Baba aliye Juu, na pia uzoefu huo wa awali, uzao wa mwili ambao unatoka kwa Bikira, Maandiko yanamshuhudia Mungu katika mambo yote mawili: …kwamba Yeye ndiye Bwana mtakatifu, wa Ajabu, Mshauri Mzuri wa sura, na Mungu Mwenye Nguvu, anayekuja kutoka mawinguni kama Hakimu wa watu wote; maandiko yalitabiri mambo haya yote juu Yake (Kitabu cha III, Sura ya 19, msisitizo umeongezwa).

Isaya hakurejelea tu kuwa Yesu ni “Mungu Mwenye Nguvu” waziwazi katika 9:6, alidokeza pia asili ya uungu wa Masihi katika unabii kuhusu Yohana Mbatizaji katika 40:3. “Sikiliza, ni sauti ya mtu aliaye, itengenezeni nyikani njia ya Bwana; Nyoosheni jangwani njia kuu kwa Mungu wetu.” (ASV, msisitizo umeongezwa; Malaki 3:1). Kulingana na Agano Jipya, huyu “mtayarishaji” (au mtangulizi) alikuwa Yohana Mbatizaji (Yohana 1:23). Alitayarisha njia kwa ajili ya Yesu, kama injili zote nne zinavyoshuhudia (Mathayo 3:1-17; Marko 1:1- 8; Luka 3:1-23; Yohana 1:15-34). Ona kwamba Isaya aliandika kwamba Yohana angetayarisha “njia ya Yehova; Mungu wetu” (40:3,). Hivyo, Isaya alidai kwamba Masihi ni Mungu

Kweli, muda mrefu kabla ya enzi ya Ukristo, hata kabla ya kuzaliwa kwa Kristo, nabii Isaya alitoa kwa ushuhuda uliovuviwa wa asili ya Kristo. Yeye ni Yehova, Mungu Mwenye Nguvu, Imanueli (“Mungu pamoja nasi”), Baba wa Milele, “Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho” (Ufunuo 1:8; cf. Isaya 44:6).

MAREJEO   

Brown, Dan (2003), The Da Vinci Code (New York: Doubleday).

Irenaeus (1973 reprint), “Irenaeus Against Heresies,” The Ante-Nicene Fathers (Grand Rapids, MI: Eerdmans).

Jamieson, Robert, et al. (1997), Jamieson, Fausset, Brown Bible Commentary (Electronic Database: Biblesoft).

Santala, Risto (1992), The Messiah in the Old Testament: In the Light of Rabbinical Writings, trans. William Kinnaird (Jerusalem, Israel: Keren Ahvah Meshihit).

“What Does the Bible Say About God and Jesus?” (1989), Should You Believe in the Trinity? (Brooklyn, NY: Watch Tower Bible and Tract Society).


Published

A copied sheet of paper

REPRODUCTION & DISCLAIMERS: We are happy to grant permission for this article to be reproduced in part or in its entirety, as long as our stipulations are observed.

Reproduction Stipulations→