Imani, Ushahidi, na Ushuhuda wa Kuaminika
Kwa kuwa Biblia hushuhudia kwamba Imani ya Wakristo ina msingi katika ukweli, kufikiri, ujuzi, na uthibitisho (Warumi 1:20; Zaburi 19:1-4; Yohana 5:31-47; Matendo 1:3; 26:25) wengine wanashangaa kwa nini Yesu aliwakemea mitume kwa kutilia shaka ufufuo wake kabla ya kumwona akiwa hai (Marko 16:14; Luka 24:38). Je, Yesu alitarajia mitume wake wawe na imani katika ufufuo wake bila uthibitisho? Na kwa nini Yesu alimwambia Tomaso, “Heri wale ambao hawajaona na bado wameamini” (Yohana 20:29). Je, Yesu alikuwa akipongeza Imani isiyoweza kuthibitishwa na yenye kubadilika-badilika?
Ukweli ni kwamba, si Tomaso wala mtume yeyote aliye kemewa kwa kutaka uthibitisho wa ufufuo wa Yesu. Walikemewa kwa kufaa, hata hivyo,
- Kwakutilia shaka uthibitisho wa kusadikika ambao tayari walikuwa wamepokea.
- Kwaajili ya kudai uthibitisho zaidi kuliko uliokuwa lazima kwao, kuwa na Imani thabiti katika Mwokozi aliyefufuka.
Unabii
Mtu yuleyule ambaye Petro alikiri alikuwa “Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai” (Mathayo 16:16) Mtu yuleyule ambaye mitume walikuwa wamemwona akimfufua Lazaro kutoka kwa wafu (Yohana 11:43-44); Mtu yuleyule waliyemwona akibadilika sura (Mathayo 17:5-9); Mtu yuleyule aliyefanya miujiza mingi ya ajabu mbele yao (Yohana 20:30); Mtu yuleyule aliyetabiri kwa usahihi kukanushwa kwa Petro mara tatu (Mathayo 26:34, 75); Mtu yuleyule aliye tabiri kwa usahihi usaliti Wake Mwenyewe, kupigwa mijeledi, na kusulubishwa (Mathayo 20:18-19): Mtu huyu alitabiri tene na tena kuhusu ufufuo wake, hata kutabiri siku ile ile ambayo ungetukia (Yohana 2:19; Mathayo 12: 40; 16:21; 17: 22-23; 20:18-19; 26:32). Unabii wa Yesu wa Kufufuka kwake kutoka kwa wafu siku ya tatu ulijulikana sana hivi kwamba hata adui zake walikuwa wanajua. Kwa kweli wakuu wa makuhani na mafarisayo wakakusanyika pamoja kwa Pilato, wakisema,Bwana, twakumbuka kwamba alipokuwa angali hai, jinsi yule mdanganyifu alisema, “Baada ya siku ya tatu, wasije wanafunzi wake wakaja usiku na kumwiba” (Mathayo 27:62-64).
Basi kwa nini Yesu aliwakemea mitume wake kwa kutoamini kwao baada ya kufufuka kwake? Je, alikuwa akimaanisha kwamba walipaswa kuishi kama watu wajinga na kuamini kila kitu ambacho wamewahi kusikia kutoka kwa mtu yeyote? “Mjinga huamini kila neno, bali mwenye busara huzifikiri sana hatua zake” (Mithali 14:15). Sivyo. Yesu alikuwa na kila haki ya kukemea kutokuamini kwa mitume Wake, kwanza kabisa kwasababu walikataa kuamini neno lake (Warumi 10:17). Walikuwa wamemwona akiwafufua wafu. Walikuwa wamesikia maneno Yake thabiti ya Ukweli, ikijumuisha unabii wake unao rudiwa na sahihi wa mambo mbalimbali, ikijumuisha usaliti wake, kukamatwa, kupigwa, na kusulubishwa. Walikuwa na kila sababu ya kimantiki ya kuamini yale ambayo Yesu alikuwa ametabiri kuhusu ufufuo wake. Kila kitu ambacho walikuwa wamewahi kuona na kusikia kutoka kwa Yesu kulikuwa safi, sahihi na kweli. Hata hivyo badala ya kutarajia mkombozi aliyefufuka Jumapili asubuhi, wazo kama hilo “lilionekana kwao kama upuuzi” (Luka 24:11). Badala ya kusafiri hadi Galilaya na kumtafuta Bwana aliye hai mara tu Jua lilipotokea siku ya tatu (Mathayo 26:32), walibaki Yerusalemu kwa milango iliyofungwa “kwa hofu ya Wayahudi” (Yohana 20:19).
Yesu alitaka wanafunzi wake waelewe kuhusu kifo na ufufuo wake. Aliwaambia: “Yashikeni maneno haya masikioni mwenu, kwa kuwa Mwana wa Adamu anakwenda kutiwa katika mikono ya watu” (Luka 9:44). Alitamani wawe na imani ya kweli, yenye nguvu, yenye uthibitisho. Cha kusikitisha ni kwamba, woga, mawazo ya awali kuhusu masihi na ufalme wake na upotofu wa kiroho (Luka 9:44; 2 Wakorintho 4:4) hapo awali viliingilia Imani ya mitume katika ufufuo wake.
Ushuhuda wa Kuaminika
Yesu alipomwambia Tomaso, “Heri wale ambao hawajaona na bado wameamini” (Yohana 20:29), je, alikuwa akiidhinisha Imani isiyojali? Je, alikuwa akiendeleza wazo la dini inayoongozwa na hisia, na kujisikia vizuri? Je, tunapaswa kutarajia Wakristo wanaoishi miaka 2,000 upande huu wa ufufuo wa Kristo wawe na Imani ya kuridhisha katika Mwokozi aliyefufuka? Ikiwa tofauti na Tomaso na mitume wengine, Yesu hajawahi kututokea, tunawezaje kutazamia kuwa na Imani yenye msingi?
Mungu yuleyule ambaye kwa haki anatazamia uumbaji wake wa kibinadamu kuchunguza uthibitisho na kupata ujuzi juu yake bila hata kumuona kihalisi, ndiye Mungu yule ambaye humtazamia mwanadamu kufuata mambo hakika yanayoongoza kwenye Mkombozi aliyefufuliwa bila hata kushuhudia kibinafsi ufufuo wake. Hakuna anaye mwamini Mungu kwasababu wanaweza kumweka chini ya darubini na kumwona. Hakuna anaye weza kuthibitisha kuwa yupo kwa kumgusa. Hatuwezi kutumia hisia tano kuona na kuthibitisha kiini halisi cha Mungu (Yohana 4:24; Luka 24:39). Hata hivyo, tulicho nacho mikononi mwetu ni ushahidi mwingi wa kutegemewa ambao unashuhudia kwa niaba ya Mungu. Uwepo wenyewe wa vitu venye ukomo hushuhudia kwamba kuna Muumba wa milele, asiye na kikomo. Mifano isiyo na kikomo katika ulimwengu inatoa ushahidi kwa mbunifu mkuu. Sheria za sayansi (kama sharia ya biogenesis) zinashuhudia kuwepo kwa Mungu. KUMBUKA: Kwa maelezo zaidi kuhusu kuwepo kwa Mungu, angalia https://apologeticspress.org/ APContent.aspx?category=12.
Imani thabiti katika ufufuo wa Yesu, vilevile, inategemea ushuhuda mwingi wa kutegemeka. Kama vile ushuhuda wa kuaminika (na siyo ujuzi wa moja kwa moja) umesababisha mabilioni ya watu kuamini. Kwa kuhalalisha hivyo, kwamba, Alexander the Great, Napoleon, na George Washington walikuwa watu halisi, mamilioni ya wakristo wamefikia hitimisho la kimantiki kwamba Yesu alifufuka kutoka kwa wafu. Masimulizi ya mashahidi waliojionea wenye umri wa miaka kumi na tisa juu ya ufufuo wa Yesu yapo katika kitabu cha kale kilicho sahihi zaidi duniani- Agano Jipya. Tukio hili lilionyeshwa na kutabiriwa katika Agano la kale (Zaburi 16:10; Yohana 1:17-2:10; Mathayo 12:40). Ingawa hatua kali sana za kuzuia zilichukuliwa ili kuuweka mwili wa Kristo haukupatikana kamwe (na, bila shaka, wenye kutilia shaka wa karne ya kwanza, hasa wayahudi wasiotubu waliomuua, hawangependa chochote zaidi ya kuutoa mwili uliokufa wa Yesu kwa Wakristo wa awali).
Wanafunziwaliokuwa na hofu na mashaka walibadilika haraka na kuwa kundi la Wakristo jasiri, na wenye kujiamini ambao waliteseka na hatimaye kufa kwaajili ya Imani na mafundisho yao yenye kuendelea kuhusu Bwana aliyefufuka. Mamia ya Wakristo wa awali waliweza kushuhudia kuwa walimwona Yesu baada ya kufufuka kwake (1 Wakorintho 15:5-8). Makumi ya maelfu ya wayahudi waliokuwa na mashaka wakati mmoja, ambaye si mdogo wao alikuwa Sauli wa Tarso, walichunguza uthibitisho huo, wakaiacha dini ya Kiyahudi, na kumkiri Yesu Kristo kuwa mwana wa Mungu (Matendo 2:41, 47; 4:4; 5:14; 6:7). Zaidi ya hayo Wayahudi hawa walibadilisha siku yao ya Ibada kutoka Jumamosi hadi Jumapili (Matendo 20:7; 1 Wakorintho16:1-2). Kamailivyo kwa ushahidi wa kuwepo kwa Mungu au uvuvio wa Biblia, kesi ya jumla ya ufufuo wa Kristo kutoka kwa ushuhuda wa kuaminika iko katika moyo wa Imani iliyoimarishwa.
HITIMISHO
Yesu aliwakemea mitume kwa halali kufuatia kufufuka kwake. Walipaswa kumsadiki Mariamu Magdalena kwa kuwa alikuwa shahidi wa uhakika ambaye hakusema kingine chochote zaidi ya kile alichokisema Mwana wa Mungu mara nyingi hapo awali kwamba kitatokea: Atafufuka siku ya tatu kufuatia kifo chake. Cha zaidi ni kwamba Baraka ambazo Yesu alimtamkia Tomaso (“walio barikiwa ni wale ambao hawajamwona na bado wakamwamini- Yohana 20:29) haukuwa uidhinishaji wa dini kipofu, inayoegemezwa na hisia, na kujisikia vizuri, lakini uungwaji mkono uliotumwa na mbingu kwa uthibitisho wa kweli, wa kusadikika ambao huongoza mwenye nia wazi, mtafuta ukweli kumkiri yeye kama “Bwana na Mungu.”
REPRODUCTION & DISCLAIMERS: We are happy to grant permission for this article to be reproduced in part or in its entirety, as long as our stipulations are observed.