Menu

Imani Katika Mungu Imesimikwa Kwa Nguvu Ndani ya Mwanadamu

C. Grayling aliandika kitabu chenye kichwa “Hoja ya Mungu”. Wale walio katika mduara wa Upagani, wamekisifu, kama ni kazi kubwa na kinaangazia kwa kina sana mambo ya upagani. Na kweli bwana Grayling anafanya kosa, ambalo ni la kawaida sana ndani ya maandiko ya wasioamini. Anatetea kwamba binadamu hana asili ya dini na kwamba imani yote katika Mungu, ni matokeo ya mafundisho yaliyorithishwa kwa watoto toka kwa wazazi, walimu, au mazingira. Aliandika;

Ingekuwa, japo, nzuri kwa mbali, kama mafundisho ya kidini na ya mfumo yasingefundishwa kwa watu, mpaka wanapokuwa wakubwa. Kama ingekuwa hivyo, ni wangapi wangejiunga na dini? Bila kupewa mafundisho, kupitia mafunzo ya utotoni kwamba kufikiri kuwa huenda kuna vitu, katika imani nyingi na zinazopingana za kidini, ambavyo hutolewa, na jibu linalowezekana kwa uhakika litakuwa; sio vingi sana.

Inaonekana kama vile Grayling anashindwa kutambua kiasi kikubwa cha utafiti,  ambacho kinathibitisha kuwa, imani katika Mungu inakuja yenyewe, ni ya asili na imeshindiliwa katika mishipa ya binadamu. Mpagani Richard Dawkins anapingana na Grayling na anakiri kwamba binadamu ana “Uhitaji wa miungu”. Aliona kwamba watu wana ile “hali ya kuzaliwa kwamba wao ni waumbaji au waundaji pia”, na akasema kwamba watoto ni wanatheolojia wazawa na wengi hawaondoki humo”. Mpagani mwingine mwenye kuheshimiwa, Sam Harris analazimika kukubaliana kwamba, majaribio kadhaa yanawaza kwamba watoto wapo kwa  ajili ya kudhania muundo na  makusudi nyuma ya kila matukio ya asili – tukiacha wanasaikolojia wengi na wana anthropolojia kuamini kwamba, watoto, wakiachwa wenyewe, watagundua fikra kadhaa kuhusu Mungu.

Kwa kuwa upagani hauwezi kuelezea kwa nini watu wamezaliwa ili wamuamini Mungu, wengi wao wanakataa kiurahisi, ukweli kwamba wako hivyo. Maelezo ya kina, juu ya hii imani ya kuzaliwa, ni hili wazo kwamba “Muumbaji  aliweka umilele” ndani ya mioyo yetu (Mhubiri 3: 11), ili kwamba watu “wamtafute Bwana, ingawa ni kwa kupapasa-papasa wakamwone, ijapokuwa hawi mbali na kila mmoja wetu (Matendo 17: 27).

Rejea

 A.C. Grayling (2013), The God Argument: The Case Against Religion and for Humanism  (New York: Bloomsbury), p. 39.

See Kyle Butt (2013), “Why is Belief in God Natural to Mankind?” https://www.apologeticspress.org/APContent.aspx?category=12&article=4655.

Richard Dawkins (2006), The God Delusion (New York: Houghton Mifflin), p. 169.

 Ibid., pp. 180-181.

 Sam Harris (2010), The Moral Landscape (New York: Free Press), p. 151, emp. added.


Published

A copied sheet of paper

REPRODUCTION & DISCLAIMERS: We are happy to grant permission for this article to be reproduced in part or in its entirety, as long as our stipulations are observed.

Reproduction Stipulations→