Menu

Hadithi za Gharika

Wataalamu wa elimu ya Visakale ambao wanasoma hadithi na ngano kutoka sehemu mbalimbali za kijiografia na tamaduni tofauti wamekuwa wakiripoti mara kwa mara kundi moja la hadithi ambalo ni la kawaida takribani kila ustaarabu. Hadithi zimejitokeza katika mamia ya tamaduni ulimwenguni kote kuzungumzia mafuriko makubwa, ya kikatili ambayo yaliharibu sehemu kubwa ya binadamu, na ambayo walionusurika ni watu wachache na wanyama. Ingawa wanahistoria wengi ambao wamesoma suala hili wanakadiria kuwa hadithi hizi ziko takribani 200, kulingana na mwanajiolojia wa mageuzi Robert Schoch, “Nuhu ni hadithi moja tu katika mkusanyiko wa hadithi za mafuriko zipatazo 500 duniani kote, ambazo ni za zamani zaidi kati ya hadithi zote za kale na kwa hivyo zinaweza kuzingatiwa kuwa kati ya za zamani zaidi” (2003, ukurasa 249). Schoch aliendelea kusema:

Hadhithi za mafuriko makubwa zinapatikana kote ulimwenguni…. Hadithi za mafuriko makubwa zinapatikana katika kila bara linalokaliwa na watu na kati ya vikundi vingi vya lugha na tamaduni (ukurasa 103, 249).

Zaidi ya karne moja iliyopita, mwanajiolojia maarufu wa Kanada, Sir William Dawson, aliandika kuhusu namna ambavyo kumbukumbu za Mafuriko

zinavyohifadhiwa katika baadhi ya hati za kihistoria za zamani zaidi, za jamii mbalimbali za wanadamu, na inavyothibitishwa moja kwa moja na historia ya awali ya jamii nyingi zilizostaarabika” (1895).

Hadithi hizo zimeripotiwa kutoka mataifa kama vile China, Babilonia, Meksiko, Misri, Sudan, Siria, Uajemi, India, Norway, Wales, Ireland, Indonesia, Romania, nk.—zikiwa na orodha inayoweza kuendelea kwenye kurasa nyingi (tazama Perloff, 1999, ukurasa 167). Ingawa idadi kubwa ya hadithi hizi inashangaza, pia inashangaza kufanana katika maudhui yake. James Perloff alibainisha:

Katika asilimia 95 zaidi ya hadithi za mafuriko 200, mafuriko yalikuwa ya ulimwengu mzima; katika asilimia 88, familia fulani ilipendelewa; katika asilimia 70, kunusurika kulifanyika kwa njia ya mashua; katika asilimia 67, wanyama pia waliokolewa; katika asilimia 66, mafuriko yalitokana na uovu wa binadamu; katika asilimia 66, walionusurika walikuwa wamepewa onyo kabla; katika asilimia 57, walimalizia kwenye mlima; katika asilimia 35, ndege walitumwa kutoka kwenye mashua; na katika asilimia 9, watu wanane tu walinusurika” (ukurasa 168).

HADITHI ZA WAHINDI WA AMERIKA

Wahindi wa Azteki wanaeleza hadithi ya mafuriko ya ulimwengu mzima katika hadithi yenye kufanana kwa kushangaza na mafuriko ya kibiblia. “Ni watu wawili tu, shujaa Coxcox na mke wake, waliopona mafuriko kwa kuelea kwenye mashua ambayo ilifika kwenye mlima” (Schoch, ukurasa 103). Kisha, muda mfupi baada ya mafuriko, majitu yaliunda piramidi kubwa kwa jitihada za kufikia mawingu. Madai haya yanasemekana kuwa yaliwakera miungu, ambao waliwatawanya majitu hayo kwa moto uliotumwa kutoka mbinguni (angalia Mwanzo 11:1-9).

Katika nchi ya kale tunayoiita sasa Meksiko, kabila moja la Wahindi linalojulikana kama Tolteki lilisimulia kuhusu mafuriko makubwa. Katika hadithi yao, mafuriko yaliharibu “ulimwengu wa kwanza” miaka 1,716 baada ya kuumbwa. Ni watu wachache tu walionusurika katika mafuriko hayo ya ulimwengu mzima, na walifanya hivyo ndani ya “toptlipetlocali” (neno linalomaanisha “sanduku lililofungwa”). Baada ya watu hawa wachache kutoka kwenye sanduku lililofungwa, walizunguka duniani na walipata mahali ambapo walijenga “zacuali” (mnara mrefu) iwapo mafuriko mengine yangetokea duniani. Wakati wa “zacuali,” lugha za Tolteki zilivurugwa na hivyo kukosa mapatano  baina yao,hadi kuamua kuhamia sehemu tofauti za dunia.

Kabila jingine la kale la Meksiko liliandika hadithi ya mtu aitwaye Tezpi ambaye alitoroka mafuriko kwenye mashua iliyokuwa na wanyama. Sawa na Nuhu, ambaye alituma kunguru (ndege mlozi) ambaye hakurudi, na njiwa ambaye alirudi na tawi la mzeituni, “Tezpi alitoa mwewe, ambaye alikaa mbali, akila mizoga. Kisha akamtoa ndege mdogo, na akarudi kwake akiwa na kijiti” (Schoch, ukurasa 104).

HADITHI ZA KALE ZA KIYUNANI


Kulingana na hadithi ya Kigiriki ya mafuriko, wanadamu walikuwa wabaya sana. Zeus, kiongozi wa miungu wengi katika hadithi za Kigiriki, alitaka kuwaangamiza wanadamu kwa mafuriko, kisha kuleta kundi jingine. Hata hivyo, kabla ya kufanya hivyo, mtu mmoja aitwaye Deucalion na mke wake Pyrrha walionywa kuhusu janga linalokuja. Wanandoa hawa wenye bahati waliwekwa kwenye sanduku kubwa la mbao na mmoja wa miungu asiyekufa aitwaye Prometheus. Kwa siku tisa na usiku, maji ya mafuriko yalifunika takribani dunia nzima.Ni vilele vya milima michache tu vilivyobaki. Sanduku la mbao lilikaa kwenye kilele cha Mlima Parnassus. Baadaye, baada ya kutoka kwenye sanduku la mbao, Deucalion alitoa sadaka kwa Zeus.

HADITHI ZA CHINA NA ASIA

Katika nchi ya China, kuna hadithi nyingi kuhusu mafuriko makubwa. Moja ya hizo inatoka katika kundi la watu wanaojulikana kama Nosu. Kulingana na hadithi yao, Mungu alituma mjumbe binafsi duniani kuwaonya wana wa kiume watatu kuwa mafuriko yanakuja. Ni mwana wa kiume mdogo tu, Dum,ndiye aliyemtii mjumbe huyo. Alijenga mashua ya mbao kujiandaa kwa mafuriko yanayokuja. Maji yalipowasili, Dum aliingia kwenye mashua yake, na akaokolewa. Baada ya maji kuanza kupungua, mashua ilifika kwenye milima ya Tibet, ambapo Dum alipata wana watatu ambao walirudia kuijaza dunia. Jambo la kuvutia ni kwamba, hata herufi moja ya Kichina ya “mashua” inaweza kuonesha hadithi ya Nuhu na watu wengine saba kwenye safina. Vipengele vitatu vinavyotumiwa kuashiria mashua ni:

Watu wa Iban wa Sarawak wanazungumzia shujaa aitwaye Trow,    ambaye alielea kwenye safina pamoja na mke wake na wanyama wengi wa kufugwa (Schoch, uk. 252). Wenyeji wa India     wanasimulia hadithi kuhusu mtu aitwaye Manu ambaye alijenga    safina baada ya kuonywa kuhusu mafuriko. Baadaye,maji   yalipungua, naye akatua juu ya mlima (Schoch,ukurasa 250).

HADITHI ZA KALE ZA BABILONI

Labda Machapisho maarufu zaidi ya mafuriko (mbali na rekodi ya kibiblia ya Nuhu na Mafuriko) inatoka kwenye himaya ya kale ya Babilonia. Makala ya The Gilgamesh Epic, iliyoandikwa kwenye vidonge vya udongo kumi na viwili vilivyodumu tangu karne ya saba K.K., inazungumzia shujaa aitwaye Gilgamesh. Katika kutafuta maisha ya milele, Gilgamesh alimtafuta Utnapishtim, mtu aliyepewa maisha ya milele kwa sababu aliokoa wanyama na wanadamu wengi wakati wa mafuriko makubwa. Katika ukurasa wa kumi na moja wa hadithi hii ya mafuriko iiliyoandikwa ambayo inafanana na chapisho la la Mwanzo katika maeneo mengi. Kulingana na hadithi, miungu walimwagiza Utnapishtim kujenga mashua kwa sababu mafuriko mabaya yalikuwa yanakuja. Utnapishtim alijenga mashua, akaifunika kwa lami, na kuweka wanyama wa aina zote juu yake, pamoja na baadhi ya vyakula. Baada ya Utnapishtim kuingia ndani ya mashua na familia yake, mvua ilinyesha kwa siku sita mchana na usiku. Mafuriko yalipoisha, mashua ilikaa juu ya Mlima Niser. Baada ya siku saba, Utnapishtim alituma njiwa ili kuona kama maji yalikuwa yamepungua. Njiwa alirudi, kwa hiyo alimtuma mbayuwayu, ambaye pia alirudi. Hatimaye, alimtuma kunguru—ambaye hakurudi. Utnapishtim na familia yake hatimaye walitoka nje ya mashua na kutoa dhabihu kwa miungu wao (angalia Roth, 1988,ukurasa 303-304).

Je, kuna umuhimu gani wa hadithi mbalimbali za mafuriko? Jibu linaonekana wazi: (a) tuna hadithi zaidi ya 200 za mafuriko zinazozungumzia mafuriko makubwa (na labda zaidi ya 500—Schoch, ukurasa 249); (b) hadithi nyingi zinatoka katika enzi na tamaduni tofauti ambazo haiwezekani kuwa walinakili hadithi yoyote kati ya zinazofanana; (c) hadithi zilirekodiwa muda mrefu kabla ya wamisionari wowote kufika kuwaambia hadithi ya Mwanzo ya Nuhu; na (d) takribani utamaduni zote zina aina fulani ya hadithi za mafuriko.

Hitimisho linalotokana na ukweli huo ni kwamba katika kipindi cha zamani sana, kulikuwa na mafuriko makubwa ambayo yaliathiri historia ya ustaarabu wote.

Wale waliokuwa wakiishi baada ya Mafuriko hawakuwa na kitabu cha Mwanzo cha kusoma kwa kizazi chao. (Mwanzo hakikuandikwa hadi mamia ya miaka baada ya Mafuriko.) taarifa ya Mafuriko ilipitishwa kutoka kizazi hadi kizazi. Wazazi na babu na bibi wengi waliwaambia watoto wao na wajukuu wao kuhusu safina kubwa, wanyama wa ajabu, na Mafuriko ya kutisha,muda mrefu kabla rekodi ya Mwanzo kuwepo. Kwa miaka mingi, maelezo ya hadithi yalibadilishwa, lakini maelezo mengi ya kweli yalibaki sawa. Alfred Rehwinkel aliandika:

Mapokeo yanayofanana na rekodi hii yanapatikana miongoni mwa mataifa na makabila yote ya jamii ya wanadamu. Na hii ndiyo jinsi mtu anavyotarajia iwe. Ikiwa maafa hayo ya ajabu ya dunia, kama ilivyoelezwa katika Biblia, yalitokea kweli, kuwepo kwa mapokeo ya Mafuriko kati ya watu waliojitenga sana na wa kizamani ni jambo linalotarajiwa. Ni kawaida kwamba kumbukumbu ya tukio hilo ilikuwa ikisimuliwa masikioni mwa watoto wa walionusurika tena na tena, na pengine ilifanywa kuwa msingi wa baadhi ya sherehe za kidini” (1951,ukurasa 127-128).

Harold W. Clark, katika kitabu chake cha “Fossils, Flood and Fire”, alitoa maoni:

Kuhifadhiwa katika hadithi na ngano za karibu kila watu kwenye uso wa dunia ni kumbukumbu ya maafa makubwa. Ingawa ngano haziwezi kuwa na thamani ya kisayansi, lakini ni muhimu kwa kuashiria ukweli kwamba hisia zilibaki katika akili za jamii ya wanadamu ambazo zisingeweza kufutwa” (1968, ukurasa 45).

Baada ya“vifaa” kuondolewa kutoka kwenye msingi wa ukweli katika hadithi mbalimbali, takribani kuna makubaliano kamili miongoni mwa akaunti zote za mafuriko ambayo ni: (a) uharibifu wa ulimwengu wa maji kwa jamii ya binadamu na viumbe wengine wote ulitokea; (b) safina, au mashua, ilitolewa kama njia ya kutoroka kwa baadhi yao; na (c) mbegu ya wanadamu ilitolewa ili kuendeleza binadamu. Kama Furman Kearley alivyobainisha mara moja: “Mapokeo haya yanaendana kwenye mambo mengi muhimu mno hadi huenda kuwa yalianzia kwenye tukio moja la ukweli” (1979, uk. 11). Katika juzuu ya tatu ya kitabu chake cha mfululizo, The Native Races of the Pacific Slope—Mythology, H.H. Bancroft aliandika: “Hakuna hadithi yoyote bila maana;… hakuna hadithi yoyote kati ya hizi, haijalishi jinsi inavyoonekana kuwa ya kijinga au isiyo na maana, ambayo haikuanzishwa na ukweli” (1883).

Miongoni mwa wasomi mashuhuri wa siku zilizopita ambao wamesoma mambo haya kwa kina ni watu kama James G. Frazer (Folklore in the Old Testament) na William Wundt (Elements of Folk Psychology). Wundt, ambaye alijitahidi sana kupata sababu inayofaa ya asili huru ya hadithi mbalimbali za mafuriko (na ambaye hakuwa na upendo mkubwa kwa ushahidi wa kibiblia), alilazimika kukubali:

Kuhusu muunganiko wa vipengele vyote hivi(dunia kuangamizwa kwa maji, uokoaji wa mtu mmoja na mbegu ya wanyama kwa njia ya mashua, nk.), hata hivyo, tunaweza kusema bila kusita kwamba, haiwezi kuwa ilitokea mara mbili kwa uhuru” (1916, ukurasa 392, maelezo ya mabano katika asili).

Au, kama Dawson alivyohitimisha zaidi ya karne moja iliyopita:

[S]asa tunajua kwamba Mafuriko ya Nuhu si hadithi tu au mawazo ya mwanadamu wa zamani au fundisho la pekee la Maandiko ya Kiebrania. …[H]akuna tukio la kihistoria, la kale au la kisasa, linaloweza kuthibitishwa zaidi kama jambo la ukweli kuliko hili (1895, ukurasa 4).

MAREJELEO

Bancroft, H.H. (1883), Works: The Native Races of the Pacific Slope—Mythology (San Francisco, CA: A.L. Bancroft).

Clark, Harold W. (1968), Fossils, Flood and Fire (Escondido, CA: Outdoor Pictures).

Dawson, John William (1895), The Historical Deluge in Relation to Scientific Discovery (Chicago, IL: Revell).

Kearley, F. Furman (1979), “The Significance of the Genesis Flood,” Sound Doctrine, March/April.

Perloff, James (1999), Tornado in a Junkyard: The Relentless Myth of Darwinism (Arlington, MA: Refuge Books).

Rehwinkel, Alfred M. (1951), The Flood (St. Louis, MO: Concordia).

Roth, Ariel (1988), Origins: Linking Science and Scripture (Hagerstown, MD: Review and Herald Publishing).

Schoch, Robert M. (2003), Voyages of the Pyramid Builders (New York: Jeremy P. Parcher/Putnam).

Wundt, William (1916), Elements of Folk Psychology, trans. Edward L. Schaub (New York: Macmillan).

UZALISHAJI & MASHARTI: Tunayo furaha kutoa ruhusa ya makala hii kuzalishwa kwa sehemu au kwa ukamilifu, ili mradi masharti yetu yazingatiwe.

Masharti ya Uzalishaji→


Published

A copied sheet of paper

REPRODUCTION & DISCLAIMERS: We are happy to grant permission for this article to be reproduced in part or in its entirety, as long as our stipulations are observed.

Reproduction Stipulations→