Menu

Chagua Mungu Wa Chaguo Lako?

Dini ya Kikristo imekuwa chakula kwa fikra za “mila tofauti”(multiculture) na pia fikra za wenye nia mbili (pluralistic), ndani ya mila za Wamarekani. Dini imewekwa kufuatana na hizo hisia, ambazo raia wanayo haki ya kufanya uchaguzi wao, na “kufanya vitu vyao”. Yaani hiyo ni namna ya ki-Amerika. Hata hivyo nina haki zangu! Mtazamo wangu ni mzuri tu kama ule wa watu wengine. Bahati mbaya, hizi fujo za ubinafsi, hazimtayarishi mtu kujishusha kwa ajili ya Mungu. (Yakobo 4: 10). Badala yake inahamasisha tu kuendana na nafsi yako tu na dini yako, yaani dini  ambayo imeundwa kwa jinsi mtu anavyotamani tu. Paulo alirejea mtazamo huu kama “ibada za kujitungia” yaani kuabudu kwa mujibu wa mapenzi ya mtu (Wakolosai 2: 23)

Hali ya kidini katika karne ya kwanza, ilkuwa kwamba, watu walio wengi waliamini miungu wengi (Mfano Matendo 17: 16). Lakini kiuhalisia kulikuwa na Mungu mmoja (Waefeso 4: 6). Ukweli kwamba watu walitengeneza fafanuzi za mitego, kama vile vinyago, mahekalu n.k, na wakachukua dini zao kwa umakini mkubwa, haikubadilisha ukweli kwamba walikuwa wakijishughulisha katika “ibada za bure” na dini za uongo (Rejea Mathayo 15: 9; 2Petro 2: 1). Kuwaambia kuwa kulikuwa na Mungu mmoja , au kwamba mungu mmoja hakuwa mwema kama mwingine tu, haikuwa fundisho muhimu . Kiukweli fundisho la “Mungu mmoja” lilipokelewa, kama tishio halisi kwa wale wanaoamini miungu wengi kwa nyakati hizo na kama changamoto kali kwa afya ya dini za kifalme. Imani katika miungu wengi ilikuwa imepenya na kuenea kwenye jamii za karne ya kwanza, kiasi kwamba kupokea fundisho la “Mungu mmoja” ilikuwa haipokeleki kwa watu walio wengi.

Historia huwa inajirudia muda mwingi baadaye. Siku zetu hazina tofauti nay ale mazingira ya karne ya kwanza na mambo yake, wakati wa-Amerika kihistoria wamekataa fundisho a “miungu wengi” (Ingawa hata huu ukweli wa msingi unabadilika). Wazo la “Makanisa mengi” limepokelewa kwa kukumbatiwa kabisa, tabia zilizopo sasa ni “kuhudhuria Kanisani unalotaka” na kanisa moja ni zuri tu kama jingine, yako sawa. Lakini wazo la makanisa mengi, ni geni kwenye Agano Jipya, kama ilivyo kwa wazo la “miungu wengi”. Aya ile ile inayosisitiza Mungu mmoja tu (Waefeso 4: 6), inasisitiza pia “Kanisa moja tu” (Waefeso 4: 4; 1: 22, 23). Labda kwa kutokujua, kutoridhika, au kiburi, watu wamejiamlia wenyewe kutengeneza makanisa yao wenyewe, mafundisho ya kistaili, taasisi, ibada, na majina kutokana na mapenzi yao wenyewe. Baadhi hawaonekani kutambua kwamba, Yesu hakuacha mtu yeyote afanye kanisa lake (Mathayo 15: 9; 16: 18). Mafundisho ya uongo yote, walimu wa uongo na makanisa ya uongo vitakataliwa (Mathayo 15: 13).

Tusiwahamasishe watu “kujiunga na kanisa la chaguo lako” bali tuwasihi kukubali kwa kutii injili ya Kristo – kupitia imani, toba, na ubatizo wa maji (Matendo 2: 38) – ili kwamba waweze “kuongezwa” (Matendo 2: 47) kwenye Kanisa ambalo ni chaguo la Kristo mwnyewe (Mathayo 16: 18; Waefeso 5: 23).


Published

A copied sheet of paper

REPRODUCTION & DISCLAIMERS: We are happy to grant permission for this article to be reproduced in part or in its entirety, as long as our stipulations are observed.

Reproduction Stipulations→