Menu

Binadamu Siyo Wanyama

Pamoja na kupungua kwa maadili ya Kikristo ya Amerika kumekuja safu za imani zisizo na maana, za kigeni, na zisizo na mantiki. Mfano mmoja unaonekana katika jinsi Waamerika wamekuja kuweka thamani isiyofaa kwa wanyama. Mamilioni ya dola yametumiwa kwaajili ya  mambo ambayo huwafanya wanyama kuwa na thamani isiyo ya kawaida-kutoka pomboo, nyangumi, na kasa wa baharini, hadi ndege, dubu, na bundi wenye madoadoa. Minyororo ya maduka makubwa ya vifaa vya wanyama imeibuka kote nchini. Madaktari wa meno, wataalamu wa lishe ya wanyama-vipenzi, watunza wanyama vipenzi, hutoa huduma zao za bei ghali kwa watu ambao wanyama wao wa vipenzi wamekuwa “sehemu ya familia.” Uangalifu huu wote kwa wanyama unaweza kuonekana kuwa usiodhuru na kufurahisha watu wengi, lakini kuna hatari zisizofichika tunapokosa kupatanisha vipaumbele vyetu na vipaumbele vya Mungu. Hakika ni kweli kwamba wanadamu wanapaswa kuona jukumu linalofaa la kuundwa kwa wanyama na sio kuwafanyia ukatili na madhara yasiyo ya lazima (Mithali 12:10). Hata hivyo, kurudi kwenye akili ya Mungu huwezesha mtu kuwa na maoni yanayo faa kuhusu wanyama na umuhimu wao wa kadiri, ili asikazie kupita kiasi kile ambacho Mungu hakazii kupita kiasi. Kuwa na mtazamo huo ufaao kutawezesha mtu kutathmini ipasavyo mielekeo ya kitamaduni na “ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu” (Waefeso 4:14).

Ili kuona ni wapi kujitenga na maadili ya Kikristo kutaongoza watu, pitia tovuti ya “people for Ethical Treatment of Animals” (PETA). Fikiria kauli zifuatazo zinazopatikana kwenye tovuti:

Utunzaji wa kimaadili-kanuni bora-lazima ienee kwa viumbe vyote: wanyama watambaao, mamalia, samaki, wadudu, ndege, amfibia, na crustaceans. Ni lazima tuache mpaka wa kizamani na usio sahihi wa “binadamu,” ambao tunautumia kuhalalisha mauaji yanayoendelea ya mabilioni ya viumbe. Zaidi ya karne moja iliyopita, Charles Darwin alionyesha kuwa viumbe wote walikuwa na babu mmoja. Viumbe vyote vina shauku ya kuishi. Sisi sote tunasikia maumivu, furaha, huzuni, na raha. Sote tuna thamani wanyama si wetu kuwafanyia majaribio, kula, kuvaa, kutumia kwa burudani au matumizi mabaya kwa njia nyinginwe yoyote. Tunafanya kazi kwa bidii ili kujidanganya wenyewe na kila mmoja wetu ili kudumisha udanganyifu wa mpaka uhalisi unaomzunguka binadamu. Sisi sote ni wanyama. Wanadamu wana uwezo mdogo, ikiwa wapo, wa pekee-viumbe wengi wanaweza kujifunza lugha, kufurahia mahusiano magumu ya kijamii, kujinyima raha kwa manufaa ya wengine, kutumia zana, kuwazia, na kuota ndoto. Viumbe wengi hukumbuka habari, kucheza na marafiki, kufurahia urafiki kusengenya, na kuomboleza marehemu wao. Baadhi ya viumbe vina uwezo mkubwa zaidi ya wetu katika kuogelea, ustahimivu, mawasiliano, na kutambua matukio ya asili. Bado hatuelewi kikamilifu jinsi viumbe vyote hufikiri- au kile wanacho kifikiri-lakini kukataa ulimwengu wao wa akili kama chini ya maendeleo, busara, maadili, au akili kuliko yetu ni kosa wazi. Tunashikilia asili sawa ya mageuzi, tunaishi Dunia moja, na tunatawaliwa na sharia sawa za asili. Sisi sote ni sawa.

Maneno haya yana makosa mengi sana. Fikiria kuhusu haya maoni matano yafuatayo. Kwanza kabisa , ona kwamba mawazo hayo potofu yanajumuisha shambulio la ufafanuzi wa maana ya kuwa mwanadamu. Inafuata kabisa tofauti iliyowekwa na muumba ambaye “aliumba vitu vyote, na kwa mapenzi yake [ambaye] vinakuwako navyo vikaumbwa” (Ufunuo 4:11). Pengo lililopo kati ya wanadamu na wanyama ni kubwa na pana sana kwamba kwa mtu yeyote kuwachanganya wawili hao anapendekeza kutegemea hisia na upendeleo uliokithiri badala ya mantiki na sababu. Kwani, tofauti na wanyama wanadamu waliumbwa “kwa mfano wa Mungu” (Mwanzo 1:27). Hizi hapa ni sifa 10 zinazosaidia kufafanua maana ya kuwa “binadamu”-sifa ambazo wanyama hawawezi na hawatawahi kuwa nazo:

  1. Wanadamu wana uwezo wa kusema ambao ni tofauti na wanyama.
  2. Wanadamu wanaweza kuandika, kuboresha elimu yao, kukusanya ujuzi, na kuendeleza mafanikio ya zamani.
  3. Wanadamu ni wabunifu na wanausemi wa ubunifu.
  4. Wanadamu wana uwezo wa kiakili wa kuwaza na kufikiri unaopita akili za wanyama.
  5. Wanadamu wana uwezo wa hiari wa kufanya maamuzi ya busara.
  6. Wanadamu pekee ndio wana uwezo wa kuchagua kati ya mema na mabaya.
  7. Wanadamu wana dhamiri.
  8. Wanadamu wanaweza kupata hisia za moyo na uzoefu wa kihisia.
  9. Wanadamu peke yao wana mwelekeo wa kidini wa kipekee, wa asili, wenye tamaa na uwezo wa kuabudu.
  10. Wanadamu pekee ndio wanaobeba chapa ya kiroho ya Mungu kutokana na ukweli kwamba wana nafsi isiyoweza kufa.

Mambo mengi yanaweza kusemwa juu ya kila moja ya sifa hizi tofauti na udanganyifu ambao wakati mwingine hutengenezwa na hisia za wanyama. Hata hivyo, inaweza kuonyeshwa kwamba wanadamu hujitenga na wanyama katika urithi wao wa asili, uliojengeka wa sifa hizo za kiroho.

Pili, angalia kwamba agenda ya haki za wanyama imejikita katika mtazamo wa mageuzi wa Darwin. Ikiwa viumbe vyote na mimea ni makundi yaliyo badilishwa tu, basi moja siyo bora kuliko nyingine, zinatofautiana tu. Kwahiyo, waridi na nge ni za thamani na zinastahili kutunzwa kama mtoto mchanga au n’gombe. Mawazo haya yasiyo ya kawaida ni matokeo ya moja kwa moja ya kununua katika nadharia iliyobatilishwa kabisa ya mageuzi na kutupilia mbali uthibitisho mwingi katika mpangilio ulioumbwa wa muumba asiye wa kawaida ambaye amejidhihirisha kwa wanadamu kupitia maumbile na Neno lake lililoandikwa katika Biblia. Mara mtu anapokataa mtazamo wa ulimwengu wa Kikristo, uhuishaji unaaminika na hakuna mwisho wa hitimisho la ajabu, lisilo na mantiki ambalo litashinikizwa. Lakini ushahidi unapatikana ambao unathibitisha kwa uhakika ukweli wa Mungu wa Biblia, na uhalisi wa mawasiliano Yake kwa wanadamu kupitia Biblia. Ikiwa hivyo, hakuna myama yeyote Duniani-awe myama anayetambaa, mamalia (isipokuwa mwanadamu), samaki, wadudu, ndege, amfibia, au crustacean ni wa thamani kama binadamu. Akizungumza na watu wenye akili timamu ambao wangeweza kufuata mantiki hiyo, Yesu aliuliza: “Basi mwanadamu ana thamani gani kuliko kondoo?” (Mathayo 12:12). Wale ambao wamedanganywa na falsafa ya haki za wanyama wangekuwa hawajasadikishwa kabisa na sababu za Yesu. Lakini wale wanaoishi katika jamii inayotegemea kilimo wanaelewa kwa urahisi, na upatikanaji rahisi wa chakula na nguo, hivi kwamba wamewafukuza wapinzani wao kwa unafiki huku wakishiriki matokeo ya masharti ya wapinzani wao.

Tatu, wanyama waliotolewa na Mungu kwaajili ya chakula na matumizi mengine. Ikiwa Biblia ni ya asili isiyo ya kawaida (na inaweza kuthibitishwa kuwa hivyo), basi maelezo ya biblia kuhusu kusudi la wanyama ni ya kweli. Biblia huonyesha wazi uhusiano uliopo kati ya wanadamu na wanyama inaposema hivi kuhusu wanadamu: “Wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa juu ya nchi” (Mwanzo 1:26). Neno la Kiebrania la utawala (rahdah) linamaanisha kutawala. Neno linalotafsiriwa “kutiisha” (kahvash) humaanisha kutiisha kwa nguvu. Mtunga Zaburi alirudia maagizo hayo alipomsifu Mungu kwa kusema “umemtawaza juu ya kazi za mikono yako; umevitia vitu vyote chini ya miguu yake. Kondoo, na n’gombe wote pia; Naam, na wanyama wa kondeni; ndege wa angani, na samaki wa baharini; na kila kipitacho njia za baharini.” (Zaburi 8:6-8).

Mungu alikazia utawala wa wanadamu kwa maneno yenye nguvu hata zaidi baada ya Gharika: “Kila myama wa katika nchi atawaogopa ninyi na kuwahofu, na kila ndege wa angani: pamoja na vitu vyote vilivyo jaa katika ardhi, na samaki wote wa baharini; vimetiwa mikononi mwenu. Kila kiendacho kilicho hai kitakuwa chakula chenu, kama nilivyo wapa mboga za majani, kadhalika nawapeni hivi vyote.”(Mwanzo 9:2-3). Kizuizi pekee ambacho Mungu aliweka juu ya ulaji wa nyama ya mnyama ni kwamba damu ilitolewa kutoka kwa myama kabla ya kuliwa (Mwanzo 9:4; Mambo ya walawi 17:10-14; Kumbukumbu la Torati 12:16, 23-24; Samweli 14:32-34). Wanyama pia wanaweza kutumika kwa mavazi (Mwanzo 3:21). Ikiwa kwa kweli, Biblia ni neno la Mungu lililoongozwa na roho, basi wanyama si wanadamu.

Nne, katika sifa hizo ambapo wanyama ni bora kuliko wanadamu, sababu haitokani na mageuzi, wala ubora huo haumaanishi kugawana maana ya kuwa binadamu. Badala yake, Muumba aliwekeza viumbe vyake vyote kwa uwezo na ustadi tofauti ili kuvitayarisha kufanya kazi jinsi vilivyokusudiwa kufanya kazi. Tai wana macho makali kuliko wanadamu kutokana na ukweli kwamba waliundwa ili waweze kuona mawindo yao muhimu kutoka kwa urefu wa juu. Lakini wao si binadamu na hawatabadilika na kuwa binadamu.

Tano, inaeleza kwamba nukuu ya PETA inakubali kwamba wanadamu na wanyama “wanatawaliwa na sharia zilezile za asili.” Sheria kama hizi zinatoka wapi? Je, zilizotokana na mawe na uchafu? Kukiri kwamba sharia thabiti za asili zipo ni makubaliano kwamba mtunga sharia lazima awepo. Mtazamo wa mageuzi hauwezi kueleza ukweli huu kila mara au vya kutosha. Sheria zisizohamishika katika ulimwengu na Dunia zinatangaza ukweli wa Mungu wa Biblia (Zaburi 19:1 na kuendelea; Matendo 14: 17). Muumba huyo aliumba wanyama na wanadamu, lakini aliwaumba kwa njia tofauti sana. Wanadamu pekee ndio wameumbwa kwa mfano wake na watasimama mbele zake katika hukumu na kutoa hesabu kwaajili ya tabia zao. Wanyama hawataweza.

Jambo la kushangaza zaidi ni wito usiofaa wa matumizi ya “kanuni ya dhahabu” inarejelea moja kwa moja mwongozo uliotolewa na Yesu Kristo. Mtu anaweza kuwa na hakika kwamba Yesu hakuwa na wanyama akilini alipotangaza: “Na kama vile mnavyotaka watu wawatendee ninyi, ninyi nanyi watendeeni vivyo hivyo” (Luka 6:31). Ukweli ni kwamba, katikati yake, PETA inajigonga dhidi ya Ukristo na Mungu wa Biblia.

Hitimisho

Kabla ya watu wa haki za wanyama kuwahutubia wanadamu kuhusu madai yao ya unyama kwa wanyama, wangefanya vyema kutumia wakati wao kushughulikia “unyanyasaji” wa wanyama kwa wanyama wengine. Huo, pia, ungekuwa ufuatiliaji wa ubatili, wa kupitakiasi na wa kipuuzi, kwa kuwa myororo wa chakula uliumbwa na Mungu. Hata hivyo, angalau wangeacha kupoteza wakati, pesa, na jitihada za wale wanaowaandalia wanadamu chakula, dawa, mavazi, na manufaa mengine ambayo yanaondoa mateso na magonjwa, na kufanya maisha ya mwanadamu yaweze kuishi zaidi.

Rejea

1 PETA (2019), “What PETA REALLY Stands For,” https://www.peta.org/features/what-peta-really-stands-for/, italics in orig.

2 Taken from the following article which contains the research and facts that show the unbridgeable gap between humans and animals: Eric Lyons, et al. (2002), “In the ‘Image and Likeness of God’ [Part II],”              Reason & Revelation, 22[4]:25-31, https://apologeticspress.org/apPubPage.aspx?pub=1&issue=528.

3 Indeed, the PETA claim that “Charles Darwin showed that all beings had the same common ancestor” is completely false. Darwin proved no such thing. The scientific evidence is overwhelming that humans did not evolve from a non-human ancestor. See, for example, Jeff Miller (2014), “God and the Laws of Science: Genetics vs. Evolution [Part I&II],” Apologetics Press, https://apologeticspress.org/APContent.aspx?category=9&article=4779&topic=281.

4 For example, Hinduism, Buddhism, and all other forms of paganism.

5 See ApologeticsPress.org for extensive evidence.

6 (Harris, et al., 1980, 2:833; Gesenius, 1847, p. 758)

7 (Harris, 1:430)

Imechapishwa 28- Aprili- 2019

UZALISHAJI NA KANUSHO:Tuna furaha kutoa ruhusa ili Makala haya yanakilishwe kwa sehemu au kwa ukamilifu, mradi tu masharti yetu yazingatiwe.

Masharti ya uzalishaji


Published

A copied sheet of paper

REPRODUCTION & DISCLAIMERS: We are happy to grant permission for this article to be reproduced in part or in its entirety, as long as our stipulations are observed.

Reproduction Stipulations→