Akiolojia Na Agano Jipya
Wakati wowote kitabu kinadai kunukuu matukio ya kihistoria kwa usahihi kabisa, kwamba kitabu hicho kimsingi kinajifungua chenyewe kwa kiwango kikubwa cha ukosoaji. Kitabu kama hicho, kikidai hakina makosa katika uandishi wake wa kihistoria, hoja zinakuwa kali zaidi. Lakini hiyo itakuwa suala lingine, kwani ni wajibu wa kizazi hiki na kijacho kujua na kuelewa yaliyopita, na kusisitiza kwamba, historia ikijumuisha na nyakati muhimu sana, inanukuliwa na kulinganishwa kwa usahihi iwezekanavyo.
Agano jipya, halidai kwamba linawakilisha historia ya karne ya kwanza. Sio ki vile, ila ni kitabu cha historia tu. Hata hivyo kinadai, kwamba, ukweli wa kihistoria, unaohusishwa katika maandiko uko sahihi, bila mpaka wa makosa (2 Timotheo 3: 16, 17; Matendo 1: 1-3). Ni salama kusema kwamba kwa sababu ya madai haya yasiyo ya kawaida, Agano jipya limeshambuliwa kwa ukali kabisa, kuliko kitabu kingine kilichopo (labda isipokuwa kitabu dada, Agano la kale). Je matokeo ya mwisho ya uchunguzi huo imekuwa nini?
Matokeo makubwa kabisa ya uchunguzi huu makini ni mkusanyiko mkubwa wa ushahidi wa kiuchambuzi tena wa kushangaza ambao unathibitisha usahihi wa rejea mbalimbali za kihistoria katika Agano Jipya. Kama inavyoweza kusemwa kuhusu karibu kila makala juu ya uchambuzi na Biblia, kurasa hizi chache zifuatazo, zinazoelezea huu ushahidi uliochimbuliwa, unasugua tu sakafu ya ushahidi uliopo. Hata hivyo, uchunguzi wa somo hili unaonyesha kushangaza juu ya usahihi wa Biblia.
Maandishi ya kuchorongwa ya Pilato.
Wachache waliosoma maelezo ya Agano Jipya juu ya mashitaka ya Yesu wanaweza kusahau jina Pontio Pilato. Maelezo ya injili zote nne, yanarejelea, msisitizo wa kundi la Wayahudi, linalosimama kama kitu cha kukumbukwa katika maisha ya Yesu. Sio chini ya mara tatu, huyu ofisa wa Kirumi aliwaelezea, kwamba “Mimi sioni hatia yoyote kwake, (Yohana 18:38; 19: 4). Akitaka kuwatuliza Wayahudi hasira, hata hivyo Pilato aliosha mikono yake ikiwa ni kuwahakikishia rasmi, kwamba yeye hana hatia na damu ya Kristo, na halafu akamtoa, ili achapwe viboko na kusulubiwa.
Ni kitu gani kinaweza kukusanywa toka kwenye historia ya kawaida, isiyo ya kidini juu ya Pilato? Kwa karibu miaka 2,000, rejea pekee ya Pilato, ilionekana katika maandishi ya Josefu na Tacitus. Rekodi iliyoandikwa ya maisha yake, ilimuweka kama mtawala wa kirumi wa Yudea tangu 26 – 36 BK. Rekodi hiyo inaonyesha kwamba alikuwa anapenda mambo ya haraka haraka na mara kadhaa alikuwa mtu wa vurugu na mkali. Rekodi za Biblia mara kadhaa zinamtaja kwamba alimuua mgalilaya wakati akitoa dhabihu (Luka 13: 1). Mbali na rejea za msimu za Pilato katika rekodi zilizoandikwa, hata hivi hapakuwa na maelezo au mbao za mawe, zilizoelezea maisha yake.
Hali imeendelea kuwa hivyo mpaka mwaka 1961. Katika mwaka huo, Pilato alitoka katika umbile alilojulikana toka katika fasihi za zamani, akaja kwenye umbile ambalo linathibitishwa na wachimbuzi. Ofisa wa kirumi aliyeidhibiti Yudea nyakati za Yesu, uwezekano mkubwa ni kwamba makao yake makuu yalikuwa katika mji wa zamani wa Kaisaria, kama inavyoweza kuthibitishwa na rejea mbili; Josefu na shughuli za Pilato za siasa na za kijeshi katika mji huo (Finegan, 1992, ukurasa 128). Upo Kaisaria na pia ulikuwa na uwanja mkubwa wa michezo, ambao, kundi la wachimbuzi waliodhaminiwa toka Italia, walianza kuuchimbua mwaka 1959. Miaka miwili baadaye, katika mwaka 1961, watafiti hao waligundua mwamba-bapa (slab) wenye ukubwa wa miguu mitatu kwa miguu miwili, uliokuwa ukitumika katika ujenzi wa kituo kati ya kuruka hatua kwenye viti vya hapo uwanjani, kwa ajili ya wageni wa heshima (Angalia McRay, 1991, ukurasa 204). Maandishi ya Kilatini kwenye jiwe hilo, hata hivyo, yalithibitisha kuwa, mwanzo, haikukusudiwa kwa ajili ya ujenzi pale uwanjani. Juu ya jiwe watafiti walikuta maandishi yaliyobakia, yakiwa na jina la Pontio Pilato. Maandishi yote hayo hayasomeki, lakini kuhusu jina la Pilato, Finegan aliandika; “Jina Pontio Pilato ni jina lisilokosewa wala kuchanganywa, na lina umuhimu mkubwa kama maandishi ya zamani ya miambani kuhusu Pilato, aliyeongoza Yudea tangu 26 – 36, kwa mujibu wa tarehe zinazokubaliwa na wengi” (ukurasa 139). Kile ambacho maandishi hayo ya kwenye mawe yalisema hakijulikani hasa, lakini kuna makubaliano ya jumla kwamba mwanzoni mawe hayo yanawezakuwa yalitoka hekaluni, au katika mahekalu ya mtawala wa Kirumi Tiberiasi (Blaiklock, 1984, ukurasa wa 57). Kipande kidogo cha ushahidi wenye nguvu juu ya usahihi wa Agano Jipya, ungekuwa vigumu kuupata. Sasa likijulikana hasa kama “maelezo ya Pilato”, hili jiwe lenye ubapa, linaeleza kwamba Pilato alikuwa ofisa wa Kirumi aliyetawala Yudea, tena linatumia jina lake kamili, Pontio Pilato, kama linavyopatikana katika Luka 3: 1.
Mtawala Wa Thesalonike.
Akiandika kuhusu Wakristo wa Thesalonike ambao walilaumiwa kwa “kuupindua ulimwengu chini –juu” Luka aliandika kwamba, baadhi ya ndugu waliletwa mbele ya “watawala wa mji ule” (Matendo 17: 5, 6). Msemo huu “watawala wa mji” au kama matoleo mengine ya Biblia yanavyosema “mamlaka za mji” kwa kigiriki politarchas na linatokea tu, katika Matendo 17: 6, na 8. Kwa miaka mingi, wadadisi wa “Biblia kuwa na uvuvio” walimlaumu Luka kwa kutokuwa sahihi kihistoria, kwa sababu alitumia cheo politarchas kumaanisha maofisa wa mji wa Thesalonike, badala ya kutumia jina/ cheo kilichozoeleka, straeegoi (hakimu), au exousiais, (mamlaka). Ili kuunga mkono mashitaka yao, walionyesha kwamba, neno politarch, halipo popote katika fasihi ya Kigiriki, kama jina rasmi la cheo. Kwa hiyo wakasema Luka alikosea. Mtu anawezaje kurejea kwenye ofisi hiyo kama haikuwepo? Kuna yeyote aliyesikia au kusoma kuhusu politarch katika lugha ya Kigiriki? Hakuna yeyote, katika nyakati hizi, yaani hakuna mtu nyakati hizi aliyesikia mpaka ilipokutwa imerekodiwa katika miji mbalimbali ya Macedonia – jimbo ambalo Thesalonike ilikuwemo.
Katika mwaka 1960, Carl Schuleer, aliandika orodha ya maandishi ya kwenye mawe 32, yenye neno politarchas. Na karibu 19 kati ya 32, yalitoka Thesalonike, na angalau 3 kati ya hayo, yalikuwa ni ya karne ya kwanza (Angalia McRay 1991, ukurasa 295). Katika njia ya Egnatia, iliyopita katikati ya mji wa Thesalonike ya zamani, kuliwahi kuwepo mnara wa Kirumi, wenye njia katikati (Arch), ulioitwa “the Vardar gate”. Katika mwaka 1867, huo mnara, ulivunjwa, na kutumiwa katika kurekebisha kuta za mji zilizochakaa (ukurasa 295). Maandishi kwenye huo mnara, ambayo sasa yako katika makumbusho ya Uingereza yanahesabiwa kama ya muhimu sana unaposhughulikia neno politarchas. Haya maandishi, yanakadiriwa kuwa ya mwaka 30 – 143 BK, na yanaanza na neno “Katika nyakati za politarchas, …” (Finegan, 1959, ukurasa 352). Hivyo, mnara kwa kiasi kikubwa ulikuwa ukisimama wakati Luka alipokuwa akiandika nyaraka ya kihistoria iliyo julikana kama Matendo ya mitume. ,Na ukweli ni kwamba politarchas waliiongoza Thesalonike nyakati za kusafiri mtume Paulo, na sasa zinasimama bila kupingwa.
Sergio Paulo, Liwali Wa Cypus.
Kote katika safari za kimishenari za Paulo, yeye na wasafiri wenzake, walikutana na watu wenye hadhi tofauti tofauti – ikiwa ni pamoja na watawala wa Kirumi, wa eneo hilo, ambalo wamishenari walikuwa wanahubiri. Kama Luka alikuwa anaunganisha safari hizi, atakuwa alipata rejea za kutosha kwa watawala wa Kirumi bila kutaja majina maalumu wala vyeo. Lakini hicho sio kitu anachokiona mtu ndani ya kitabu cha Matendo, na kinyume chake, inaonekana Luka aliondoka zake, kuelezea miji maalum, sehemu, majina na vyeo. Kwa sababu ya hizi nakala za mashaka, tuna mazingira machache ambayo humo tuchunguze, kuaminika kwake kama mwanahistoria
Tukio moja kama hilo lipo katika Matendo 13, katika sura hiyo, Luka anaandika safari ya Paulo katika Seleucia, halafu Cyprus na Salamis, halafu Pafo. Katika Pafo, Paulo na wenzake, walikutana na watu wawili – Myahudi mwenye jina la Bar – Yesu, na mwenzake Sergio Paulo, mtu mwenye akili, liwali, akawaita Paulo na Barnaba ili kulisikia neno la Mungu (Matendo ya Mitume 13: 4-7). Hii rejea ya Sergio Paulus, inampatia mwanafunzi wa utafiti wa uchambuzi, aina mbili za vipimo vya usahihi wa Luka. Kwanza ni je, eneo la Cyprus na Pafo liliongozwa na Liwali nyakati za Paulo akifanya kazi pale? Na pili, je kumewahi kuwapo na Sergio Paulo?
Kwa miaka mingi, wenye mashaka na usahihi wa Luka walidai kwamba, eneo linalozunguka Cyprus, linaweza kuwa halikuongozwa na Maliwali. Kwa kuwa Cyprus lilikuwa ni jimbo la kifalme, lingekuwa chini ya umiliki wa mfalme na sio chini ya gavana (Unger, 1962, ukurasa 185, 186). Wakati ni ukweli kwamba Cyprus wakati fulani lilikuwa jimbo la kifalme, sio kweli kwamba, ilikuwa hivyo nyakati za kusafiri kwa Paulo pale. Kwa kweli, “katika mwaka 22 BK, Augusto alimuhamisha Seneta wa kirumi, na Cyprus ikawekwa chini ya uongozi wa liwali” (Free and Vos, 1992, ukurasa 269). Msomi wa Biblia F. F. Bruce aliongezea kwenye habari hii, alipoelezea kwamba, Cyprus ilifanywa kuwa jimbo la kifalme katika mwaka 27 BK, lakini Agusto, akaliweka chini ya Seneta miaka mitano baadaye, kwa kubadilishana na Dalmatia. Baada tu ya kupewa Seneta, Maliwali walitawala Cyprus, kama ilivyo katika majimbo mengine yaliyo chini ya Seneta (Bruce, 1990, ukurasa 295). Kama Thomas Eaves alivyosema;
Kama tunavyomgeukia mwandishi wa historia kwa kipindi hicho, Dia Cassius (Historia ya Rumi) na Strabo (Jiografia ya Strabo), tunajifunza kwamba kulikuwa na vipindi viwili vya historia ya Cyprus; kwanza, lilikuwa ni jimbo la kifalme likitawaliwa na Mmiliki, na baadaye katika mwaka 22 KK, likafanywa jimbo linaloongozwa na liwali, ilikuwa kati ya mwaka 40 – 50 BK, Paulo alipofanya safari yake ya Umishonari. Kama tunakubali historia nje ya kibiblia kwamba ni ya kweli, lazima tukubali pia historia ya Biblia, kwa sababu vyote vinakubaliana. (1980, ukurasa 234).
Kwa nyongeza juu ya ukweli unaofahamika, kwamba Cyprus ilikuja kuwa jimbo la seneti, wachimbuzi wamegundua fedha ya shaba toka katika eneo ambalo linarejea kwa maliwali wengine ambao hawakuwa wametolewa mpaka nyakati za Paulo. Fedha mojawapo kama hiyo, ambayo inaitwa kwa usahihi kabisa kama “Copper Proconsular Coin of Cyprus” ina picha ya Kaisari Klaudiasi na ina maandishi (anwani) ya “Arminius Proclus, Proconsul .. of Cyprus” (McClintock and Strong, 1968, 2: 627)
Ikiwa inavutia zaidi kuliko ukweli kwamba Luka alikuwa na cheo maalum kilichorekodiwa kwa usahihi, ni ukweli kwamba ushahidi umekuja kwenye mwanga, kwamba rekodi ya Segio Paulo, ni ukweli pia. Inafurahisha katika jambo hili, kwamba kuna maandishi kadhaa, ambayo huenda yanaweza kuendana na liwali, aliyerekodiwa na Luka.
Kamusi ya Biblia ya “international Standard” imerekodi maandishi ya zamani ambayo huenda yanaendana (Angalia Hughes 1986, 2: 728). Kwanza ; huko Soli, pwani ya kaskazini ya kisiswa cha Cyprus, maandishi yalichimbuliwa, ambayo yalimtaja Paulo, ambaye alikuwa liwali. Waandishi na wahariri wa kamusi hiyo, wanatetea kwamba, maandishi haya, kama ni mapema, basi yanaweza kuwa ya mwaka 50 BK, na kwa hiyo kwamba hayaendani na Paulo wa Matendo 13. Lakini wengine wameshawishika kwamba, huyu ni Paulo maarufu wa Matendo (Unger, 1962 ukurasa 185, 186; Angalia pia McGarvey, 2. 7). Kwa nyongeza ya upatikanaji huu, maandishi mengine ya Kilatini, yamegunduliwa ambayo yanarejea kwa “Lucius SergioPaulo, aliyekuwa “mmoja wa watunzaji wa mabenki ya Tiber nyakati za utawala wa Kludius.” Mchimbuzi maarufu, bwana Wiliam Ramsay alihoji kwamba mtu huyu baadaye alikuja kuwa liwali wa Cyplus, na anapaswa kuunganishwa na Matendo 13 (Hughes 2: 728). Mwisho, vipande vya maandishi ya kigiriki, vikitokea Kythraia, kaskazini mwa Cyprus, vimegunduliwa, vikimrejea Quintus, Sergio Paulo, kama liwali wa Cyprus wakati wa utawala wa Klaudius (Hughes 2: 728). Bila kujali ni yepi kati ya maandishi haya ya kuchoronga yanahusiana na Matendo 13, ushahidi unatupatia ufanano unaokubalika. Angalau watu kama wawili wanaoitwa Paulo walikuwa maliwali katika Cyprus, na angalau watu wawili tena wenye jina Sergio Paulo, walikuwa maofisa wakati wa utawala wa Klaudius. Usahihi wa Luka unatibitishwa kwa mara nyingine.
KUHUSU KIFO KWA NJIA YA KUSULUBIWA
Kwa karne kadhaa za historia, kusulubiwa imekuwa njia ya kifo yenye maumivu tena ya aibu sana, Kwa sababu ya aibu ya wazi inayounganishwa na kifo hicho, watawala wengi waliwasulubisha wale waliowapinga. Kwa historia, maelfu kadhaa wameuawa kwa njia hii ya kuchapwa viboko. Kwa ufupisho wa baadhi ya mifano ya kusulubu watu wengi kwa pamoja, John McRay alitoa maoni kwamba Alexander Jannaeus, alisulubisha Wayahudi 800 katika Yeruslem, Warumi walisulubisha watumwa 6,000, wakati wa uasi ulioongozwa na Spartacus na Yosefu aliona wayahudi “wengi” wakinyongwa huko Tekoe mwishoni mwa uasi wa kwanza (1991, ukurasa 389). Na bado, licha ya yaliyoandikwa wazi kuhusu kusulubisha, kama upo, ni ushahidi wa kuchimbua kidogo sana ambao umeshatolewa toka katika zile nchi takatifu kuhusiana na jambo hilo. Kuhusu watu wengi, mahali pengi, na matukio mengi yaliyorekodiwa katika Biblia, ukosefu wa huu ushahidi wa wazi ni kwa sababu ya kutengenezwa na wandishi wa Biblia, lakini ulikuwa tayari, badala ya kukosekana kwa habari za uchimbuzi.
Katika mwaka 1968, Vassilios Tzaferis, aligundua mabaki yasiyo na shaka ya mhanga wa kusulubiwa. Mifupa (skeleton) ya mhanga huyu iliwekwa katika kaburi la wengi (ossuary), ambalo lilikuwa ni sawa na yale yaliyotumiwa na Wayahudi katika nchi takatifu kati ya mwishoni mwa karne ya pili KK na kuanguka kwa Yerusalem mwaka 70 BK (McRay 1991, ukurasa 204). Kutoka katika maelezo ya mabaki ya mifupa ile ya mhanga, mtaalam wa mifupa na wataalam wengine wa afya kutoka chuo cha Afya Hadasa huko Yerusalem, walikuwa na uwezo wa kuamua kwamba mhanga huyo alikuwa mwanaume wa umri kati ya miaka 24 na 28, ambaye alikuwa kati ya futi 5 au 6 za urefu. Kufuatia maandishi ya kuchoronga kwenye kaburi lile jina lake linaoneka kuwa aliitwa “Yehohanan mwana wa Hagakol,” ingawa neno la mwisho la maandishi yale bado lina mashaka (Ukurasa 204). Kipande muhimu sana cha mifupa ya mhanga ni kile cha mfupa wa kisigino cha kulia. Katikati ya ncha ya ukucha na kisigino, vipande kadhaa vya kuni za mizeituni vilionekana vimelala. Randall Price, katika kitabu chake, ‘The stone Cry Out’ yaani mawe yanalia, anawaza kwamba, ukucha ulichimba na kuweka fundo katika miti ile ya mizeituni ambayo kwayo mtu huyu alisulubiwa, na hivyo kusababisha ukucha na kisigino kuondolewa pamoja, kwa ule ugumu wa kuondoa ukucha peke yake (1997, uk 307). [picha kamili ya rangi ya sehemu ya mfupa wa mguu, ikionyesha ukucha, inaweza kuonekana katika makala ya “Search for the sacred” iliyoandikwa na Jerry Adler na Anne Underwood, katika toleo Newsweek Magazine, la Agosti 30, 2004.
Kwa upande wa umuhimu wa ugunduzi huu, mwandishi Price ametupa ufupisho bora. Kwa miaka iliyopita, wasomi fulani waliamini kwamba, simulizi za kusulubiwa kwa Yesu zilikuwa na dosari, chache kati ya hizo ni, kwanza; Iliaminika kwamba, misumari haikutumika kumuwamba mhanga msalabani, ila kamba zilitumika badala yake kwa kusudi hili. Kukuta mfupa wa kisigino chenye urefu wa inchi kadhaa, kikiwa pamoja na vipande vya mti wa mzeituni, ni kiashiria cha ukweli kwamba, kisigino cha mhanga wa kusulubiwa vilishikamanishwa na msalaba kwakutumia misumari. Pili; Imeshauriwa kwamba wahanga wa kusulubiwa, hawakupewa maziko yenye heshima, baadhi ya wasomi wanaamini pia kwamba, maelezo ya maziko ya Yesu katika kaburi la Yusufu wa Arimathaya ilitengenezwa makusudi, kwani wahanga wa kusulubiwa walitupwa tu katika makaburi ya wengi, pamoja na wahalifu wengine. Maziko ya wahanga wa kusulubiwa waliogunduliwa na Tzaferis, yanathibitisha kwamba, angalau, katika matukio machache, wahanga wa kusulubiwa walipewa maziko rasmi ya kiyahudi (1997, uk 308-311; rejea Adler and Underwood, 2004, 144) .
SENSA YA KIRENIO.
Usahihi kabisa ambao kwao Luka aliripoti, vipengele vya kihistoria, umeandikwa tena na tena kwa karne nyingi na wachimbuzi na wasomi wa Biblia. Katika kila tukio, ambapo ushahidi wa uchimbuzi wa kutosha umeonekana wazi, Luka amethibitika kama mwandishi sahihi na tena makini. Wenye mashaka na wanaohoji, wameshindwa kuthibitisha hata makosa ya miaka au tofauti nyingine yoyote, ambayo kwayo kuponda jinsi waandishi wa Biblia wanavyodai kuongozwa na nguvu toka juu.
Hata hivyo, chunguza kigezo kilichotajwa hapo juu, kinachosimama kama msingi wa tathmini sahihi na isiyopendelea ya usahihi wa Luka: Pale ambapo ushahidi tosha wa kiuchimbuzi umeonekana wazi, wenye mashaka mara chache wanasawazisha madai dhidi ya Luka na waandishi wengine wa Biblia kwa misingi ya hoja kutoka kwenye kimya. Wanashindwa kutofautisha kupingana kwa kweli kwa upande mmoja na ushahidi usiotosha, ambao kwao kuja na hitimisho thabiti kwa upande mwingine. Madai ya kupingana au kukosa usahihi ndani ya Biblia sio halali na hivyo yasiyovumilika, katika maeneo hayo ambapo ushahidi wa kushirikiana kihistoria, ama haupo ama ni kidogo.
Kuhusu sheria hizi, zingatia maneno ya Luka yafuatayo;
Siku zile amri ilitoka kwa Kaisari Augusto ya kwamba, iandikwe orodha ya majina ya watu wote wa ulimwengu, orodha hii ndiyo ya kwanza iliyoandikwa hapo Kirenio alipokuwa liwali wa Shamu. (Luka 2: 1, 2)
Baadhi ya wasomi wamelaumu Luka kwa kufanya kosa, kwa msingi wa ukweli kwamba, historia inarekodi kwamba, Pablio sulpicio Kirenio, alikuwa Gavana wa Siria tangia mwaka 06 Bk – miaka kadhaa baada ya kuzaliwa Kristo. Ni kweli kwamba, mpaka wakati huo hakuna rekodi ya kihistoria iliyokuwa wazi, kuhakikisha u-Gavana au Sensa ya Kirenio kama inavyoonyeshwa na Luka, nyakati za kuzaliwa Kristo, na kabla ya kifo cha Herode katika mwka 04 KK. Kama mchimbuzi maarufu wa ki-Biblia G. Ernest Wright, wa shule ya Biblia ya, Chuo kikuu cha Havard, alivyokubali, “Hili tatizo la nyakati na matukio, halijawahi kutatuliwa” (1960, ukurasa 158).
Huu ukimya, katika habari ambazo bado zipo (ambao ungeruhusu uthibitisho wa kihistoria) hata hivyo, ushahidi wa kutosha haupo wa kutoa maelezo yanayokubalika kwa Luka kutaja, na hivyo kutoa madai ya kupishana yasiyojitosheleza. Akiwa mwanahistoria makini kama alivyokuwa, Luka alionyesha ufahamu wake kutofautisha Sensa ya jimbo wakati wa Kirenio kama Gavana tangu mwaka 06 BK (Matendo 5: 37). Kuhusu uzoefu wake huu, bila shaka asingechanganya sensa hii na ile iliyochukuliwa miaka kumi au zaidi kabla. Hivyo Luka aliona kwamba, ile sensa ya awali ilikuwa, naam, ilichukuliwa kwa amri ya Kaisari Augusto, wakati fulani kabla ya mwaka 04 KK. Alizuia hii sensa ya awali kwa kutumia maelezo prote egneto (“iliyofanyika kwanza”) – inayodhaniwa kuwa ile ya baadaye (rejea Nicoll, n.d. 1: 471). Kuhoji mamlaka ya haya madai, kwa sababu tu, hakuna rejea ya kipekee ambayo imeshaonekana, haikubaliki na ni kinyume na sheria. Hakuna anayehoji uhistoria wa sensa ya pili iliyochukuliwa na Kirenio mnamo mwaka 06 au 07 BK, licha ya ukweli kwamba mamlaka yote juu ya hili ni maandishi yaliyopatikana huko Venice. Bwana Wiliam Ramsey, anayeheshimika ki-dunia na anayetambulika kama mamlaka kwenye mambo hayo alisema, kama miaka zaidi ya mia moja iliyopita;
Tunapozingatia kwamba ni kwa ajali kiasi gani, ushahidi wa sensa ya pili, ulihitaji ushahidi wa sensa ya kwanza unaonekana kutoleta hoja dhidi ya kuaminika kwa kauli ya Luka (1897, ukurasa 386).
Na kwa nyongeza, vyanzo vya kihistoria vinaonyesha kwamba Kirenio alipendelewa na Augusto, na alikuwa mtumishi wa mfalme katika maeneo yanayozunguka Siria kabla ya hapo, na wakati ambao Kristo alizaliwa. Ni busara kuhitimisha kwamba Kirenio, anaweza kuwa aliteuliwa na Kaisari kufanya hiyo sensa kwa wakati huo na kwamba uwezo wao wa kufanya jambo hilo ulimfanya ateuliwe tena kwa sensa ya mwaka 06/07 BK (Angalia Archer, 1982, ukurasa 366). Chunguza pia kwamba Luka hakutumia neno legatus – ambalo ni cheo cha Gavana wa kirumi. Bali alitumia hegamon, ambalo lilitumika kwa mmiliki (gavano wa kiseneta), au Wakala wa kirumi, kama vile; Pontio Pilato, au kamishina wa kifalme (Angalia McGarvey and Pendleton, n.d, ukurasa 28). Baada ya kutoa ufupisho makini wa data za historia na za uchunguzi kuhusu suala hili, Finegan alihitimisha “Hivyo hali inayodhaniwa katika Luka 2: 3 inaonekana inakubalika kabisa” (1959. 2: 261). Naam inakubalika.
GALIO LIWALI WA AKAYA.
Matendo sura ya 18, inaanza na maelezo ya huduma ya Paulo katika mji wa Korintho, ni pale alipokutana na Akila na mke wake mwaminifu, Prisila, wote wakiwa wamefukuzwa toka Rumi, kwa amri ya Klaudio, na ambao matokeo yake, wamekuja kuishi Korintho. Kwa sababu walikuwa watengeneza mahema, kama vile, Paulo, Mtume huyu alikaa nao na akawa anafanya kazi kama “mhudumu mgeni”akishona mahema na kuhubiri injili, kama ilivyokuwa kwenye mahubiri ya Paulo, wayahudi wengi walikwazwa, na wakawa wanapingana na kazi yake. Kwa sababu ya upinzani huu, Mtume aliwaambia Wayahudi kwamba, tangu sasa na kuendelea nawageukia mataifa. Hayo aliyasema Paulo akienda kwenye nyumba ya mtu aliyeitwa Yusto, aliyeishi karibu kabisa na Sinagogi. Mara baada ya kutangaza kwenda kwa mataifa, Paulo alipata maono, katika hayo Mungu alimuelekeza kusema kwa ujasiri, kwa sababu hakuna mtu katika mji ule, atakayemshambulia. Akitiwa moyo na maono yale, Paulo aliendelea katika Korintho kwa mwaka na miezi sita, akifundisha neno la Mungu miongoni mwa watu.
Baada ya hiyo miezi 18 ya Paulo kukaa sana Korintho, upinzani kwenye mahubiri yake hatimaye uliibuka na kuwa fujo, na ikawa shida kisiasa Matendo 18: 12, 17 inaeleza;
Hata Galio alipokuwa liwali wa Akaya, Wayahudi wakamwinukia Paulo kwa nia moja, wakamleta mbele ya kiti cha hukumu, wakisema mtu huyu huwavuta watu, ili wamwabudu Mungu kinyume cha sheria. Na Paulo alipotaka kufunua kinywa chake, Galio akawaambia wayahudi, kama lingekuwa jambo la dhuluma au la hila mbaya, enyi wayahudi, ingekuwa haki mimi kuchukuliana nanyi. Bali ikiwa ni hoja juu ya maneno na majina na sheria yenu liangalieni ninyi wenyewe, maana mimi sitaki kuwa mwamuzi wa mambo hayo. Akawafukuza waondoke mbele ya kiti cha hukumu. Nao wote wakamshika Sosthene, mkuu wa Sinagogi, wakampiga mbele ya kiti cha hukumu, wala Galio hakuyaona mambo hayo kuwa ni kitu (18: 12- 17)
Kutokana na kifungu hiki cha maandiko, tunajifunza vitu kadhaa kuhusu Galio na hadhi yake. Chenye umuhimu mkubwa kabisa, ni ukweli kwamba Luka alirekodi kwamba Galio alikuwa Liwali wa Akaya. “Hapa tena Luka katika kurekodi taarifa maalum, kuhusu watawala wa kisiasa wa nyakati zake, aliwapa wasomaji wake, rejea inayoweza kuchunguzwa. Je Galio aliwahi kuwa Gavana wa Akaya?
Marianne Bonz, Mhariri mkuu, wa Havard Theological Review, aliwasha mwanga kwenye maandishi maarufu ya sasa kuhusu Galio, alielezea jinsi, mwaka 1905, mwanafunzi wa udaktari huko Paris, alikuwa akipitia pitia katika mkusanyiko wa maandishi, ambayo yalikusanywa katika mji wa Kigiriki wa Delphi. Katika maandishi haya mbalimbali, aliona vipande vine (4) tofauti ambavyo, vikiwekwa pamoja, vinaunda sehemu kubwa ya barua toka kwa mfalme Klaudio. Barua toka kwa mfalme iliandikwa, si kwa mwingine ila, Galio, Liwali wa Akaya (Bonz, 1998, ukurasa wa 8).
McRay, katika kutoa sehemu ya kigiriki ya maandiko hayo maarufu kwa sasa na kutoa herufi zinazokosekana katika sehemu za wazi za barua hiyo kuifanya istahili, aliitafasiri kama ifuatavyo;
Tiberio Klaudio Kaisari Augusto Germaniko, pontife Maximo, mwenye mamlaka ya mahakama kwa mara ya kumi na mbili, Mfalme mara 26…. Lukio Junio Galio, rafiki yangu na Liwali wa Akaya (1991, 226- 227).
Na wakati baadhi ya sehemu za maandishi hayo juu hayako wazi kabisa, jina la Galio na cheo chake katika Akaya, viko wazi na halali kabisa. Sio tu kwamba Luka alirekodi kwa usahihi jina la Galio, lakini aliandika vilevile cheo chake kisiasa kwa usahihi sawasawa.
Umuhimu wa maandishi ya Galio, unaenda ndani zaidi ya kuthibitisha usahihi wa Luka. Ugunduzi huu, unaonyesha jinsi utafiti unavyoweza kutupa uelewa mzuri wa simulizi za Biblia, na hasa katika eneo la matukio na miaka yake. Wasomi wengi wanaojihusisha na kusafiri na nyaraka za Mtume Paulo, watakiri kwamba, kushikamanisha tarehe maalum kwenye shughuli zake linabaki kuwa ni jukumu gumu. Maandishi haya ya Galio, hata hivyo yameongeza kipande kwenye kitendawili hiki cha matukio na miaka yake. Jack Finegan, katika kazi yake iliyoelezewa vyema, juu ya Matukio ya Biblia na miaka yake, aliyapa tarehe maandishi hayo kuwa mwaka 52 BK, na Uliwali wa Galio kuwa mapema mwaka 51BK, na Paulo kufika katika Korintho mwaka 49 au 50 BK. Finegan alieleza kuhusu hitimisho lake “Uamuzi huu wa muda alipofika Paulo huko Korintho, hivyo unatoa nanga muhimu kuhusu matukio na miaka yake, vya Paulo (1998, ukurasa 391-393).
NENO KUHUSU MAKABURI.
Kamusi inayohusu uchimbuzi wa nchi takatifu, inatoa maelezo bora ya makaburi (ossuaris) kwa ujumla wake. Mwandishi anaelezea kwamba Kaburi (Ossuary) ni boksi kama futi 2.5 urefu mara nyingi ikichongwa katika udongo au ikichorongwa mwambani, ikitumika kwanza kuzika mifupa ya watu baada ya nyama kuoza. Makaburi hayo kiukweli;
Ni maalumu kwa shughuli za kuzika huko Yerusalemu na maeneo yanayoizunguka nyakati za mwanzo za kipindi cha Warumi yaani kati ya mwaka 40 KK na mwaka 135 BK. Makaburi haya yanayopatikana katika eneo la makaburi la maherode katika Yeriko yanakadiriwa na Hachlil kwenye wakati finyu sana kati ya mwaka 10 – 68 BK (“Ossuary”, 2001, ukurasa 377).
Vifaa vya kaburi (mbao n.k) mara kadhaa vinakuwa na mapambo juu yake, na vingi vinakuwa na maandishi, ama ya kuchorongwa au ya kupaka (rangi), vikionyesha mifupa ile iliyo ndani ni ya nani.
Chenye faida ni ukweli kwamba, makaburi mengi yaliyogunduliwa mpaka sasa yana majina yale yale tunayoyaona katika maelezo ya Biblia. Na wakati hatuwezi kuwa na uhakika kwamba mifupa iliyomo mle kaburini ni ya watu hasa waliotajwa katika Biblia, kupatana kwa majina kunaonyesha kwamba waandishi wa Biblia angalau walitumia majina ambayo yalioana kwa usahihi kabisa na majina yaliyokuwa yakitumika nyakati Agano Jipya lilipoandikwa.
Tukishuka chini moja kwa moja toka mlima wa Mizeituni, ni eneo linalojulikana kama Dominus flevit, likivaa utamaduni kwamba hii ni sehemu ambayo “Bwana alilia juu ya Yerusalem” (Finegan 1992, ukurasa 171). Katika mwaka 1953 uchimbuzi ulianza katika eneo hili, na eneo kubwa la makaburi likagunduliwa, likiwa na kama maeneo ya kuzikia 500 yanayojulikana. Miongoni mwa maeneo haya mengi ya kuzikia, zaidi ya makaburi 120 yaligunduliwa, zaidi ya 40 kati ya hayo yakiwa na maandishi na michorongo. Miongoni mwa makaburi yaliyoandikwa, majina ni ya; Martha na Mariam yanatokea kwenye kaburi moja. Majina mengine yanayotokea kwenye makaburi hayo ni Yusufu, Yuda, Salome, Safira, Simioni, Yeshua (Yesu), Zakaria, Elieza, Yairo, Na Yohana (Finegan 1992 ukurasa 366, 371). Free na Vos, katika hoja zao kwa Rudolph Bultimann’s, “form Criticism” walitumia ushahidi wa kaburi kuweka wazi dosari chache katika wazo la Bultimann, waliandika
Baadhi ya wasomi mwanzo walishikilia kwamba, majina binafsi yaliyotumika katika injili, hasa katika Yohana, yalikuwa ya uongo, na yalichaguliwa kwa sababu ya maana zake, na sio kwamba yanarejea watu kihistoria. Uvumi kama huo hauna kithibitisho kwenye maandishi yale ya kwenye kaburi, ambayo yanatunza majina mengi ya kibiblia (1992 ukurasa 256)
Sambamba na hayo, Price alijadili makaburi kadhaa ambayo yalionekana kwa bahati mbaya mwaka 1990, wafanyakazi walipokuwa wanajenga, eneo la maji katika msitu wa amani huko Yerusalem. Kati ya makaburi ya miamba 12 yaliyogunduliwa, moja;
Lilikuwa limepambwa kabisa kwa urembo uliokatwa vizuri. Ni wazi lilikuwa la mtu tajiri, au mwenye cheo kikubwa, ambaye angeweza kugharamia boksi kama hilo. Juu ya boksi (sanduku) hilo kulikuwa na maandishi. Inasomeka mara mbili Qafa na Yehosef bin Qayafa (Kayafa, Yusufu mwana wa Kayafa). [1997 ukurasa 305].
Price alimuunganisha huyu Kayafa kwa yule aliyerekodiwa katika Biblia, kwa kutumia mistari miwili ya sababu; Moja; Kayafa katika rekodi za Biblia alikuwa mtu mashuhuri, kuhani mkuu maarufu, ambaye angeweza kuwa na uwezo kupata sanduku kama hilo bora kabisa. Pili; Wakati maelezo ya Agano jipya yanatoa jina moja tu la Kayafa, Yosefu anatoa jina lake kamili kama Yusufu aliyeitwa Kayafa, wa mbali za kuhani mkuu (1987 ukurasa 305). Chenye faida zaidi ni ukweli kwamba, makaburi yalikuwa na mifupa ya watu sita tofauti, mmoja wao akiwa ni mtu wa karibu miaka 60. Je hii ni mifupa ya Kayafa aliyerekodiwa katika Agano jipya? Hakuna anayeweza kuwa na uhakika. Ndivyo ilivyo pia, hata hivyo kwamba makaburi mengi yanakuta, kwa uchache sana, kuthibitisha kwamba Waandishi wa Agano jipya walitumia majina ambayo yalichukuliwa kwenye maandiko, wakati wa kipindi kile kile walichoandika.
Jambo la tahadhari linatakiwa kuhusu majaribio ya kuhakikisha muunganiko wa moja kwa moja kati ya tunachokiona katika makaburi (ossuary) haya na wahusika kwenye Biblia. Jaribio maarufu la namna hiyo, mpaka wakati huu, linatoka kwa kaburi la Yakobo, ambalo lilikamata macho na masikio ya ulimwengu mwaka 2002. Maandishi kwenye sanduku hilo la mifupa yalisomeka; “Yakobo, mwana wa Yusufu, ndugu wa Yesu”. Je hili ni sanduku lililobeba mifupa ya ndugu wa kimwili wa Yesu Kristo? Mwaka 2002, jibu lilibakia kuonekana. Katika makala fupi niliyoandika juu ya mada hii mwezi wa Desemba 2002, niliandika; “Kwa wakati huu hatuwezi kuhakikisha kidini kwa ushahidi wa hayo masanduku ya mifupa, au makaburi. (Butt, 2002). Kwa sasa, maandishi hayo, bado yanajikuta yako kwenye mijadala. Baada ya kuyaelezea maandishi hayo, kamati iliyoteuliwa na mamlaka ya mambo ya kale ya Israeli, iliyathibitisha maandishi hayo kuwa ni halisi. Kwa mujibu wa Eric Myers, msomi wa mambo ya kiyahudi katika chuo kikuu cha Duke, “Makubaliano makubwa ya wasomi ni kwamba, hayo maandishi sio halisi” (kama ilivyonukuliwa katika Adler and Underwood, 2004, 144). Hata hivyo, Harshel Shanks, mhariri anayeheshimika wa Biblical Archaeoloy Review, anasisitiza kwamba maandishi yale yanabaki kuwa ‘mali kale’ na huenda yakahusishwa na Yesu na Yakobo wa Biblia (Shanks, 2004; rejea Adler and Underwood, ukurasa 38)
Ikiwa maandishi yale ni halisi, au ikiwa sio halisi bado inabakia kuonekana. Bado, hata kama maandishi yale yanathibitisha mpaka leo, karibu karne ya kwanza, bado hayangeweza kuthibitisha kwamba, majina kama Yusufu, Yakobo na Yesu yalitumika wakati ule na kwa neo lile la ulimwengu, ambavyo, labda vingethibitisha kwamba waandishi wa Biblia walihusisha taarifa zinazokubaliana na matukio yanayotendeka kwa wakati walipoyatoa maandiko yao. Kama Andrew Overman, mkuu wa Classics, Chuo cha Makalesta, alisema “Hata kama Sanduku la mifupa la Yakobo ni halisi, halitoi habari mpya” (kama ilivyonukuliwa katika Adler and Underwood, ukurasa 39). Tunapowaangalia wachimbuzi, lazima tukumbuke kutoviuliza kuthibitisha sana. Nidhamu ina mipaka. Bado licha ya mipaka hiyo, inabaki kuwa ni kifaa chenye thamani, kinachoweza kutumika kutoa mwanga kwenye makala za Biblia. Kama Adler and Underwood waliyvosema, thamani ya uchimbuzi “inatoa muktadha kihistoria na kiakili, na mara kadhaa mwale wa kumulika taarifa muhimu” (ukurasa 39).
MATAIFA NA HEKALU.
Karibu na mwisho wa kitabu cha Matendo ya Mitume, mtume Paulo alikuwa akifanya kila jitihada kufika katika mji wa Yerusalem kwa wakati ili kusherehekea, sikukuu inayokuja ya Wayahudi. Alipofika Yerusalem, alikutana na Yakobo na baadhi ya viongozi wa kiyahudi na akaripoti “mambo hayo ambayo Mungu ameyafanya kati ya mataifa kupitia huduma yake” (Matendo 21: 19). Kwa kusikia ripoti ya Paulo, viongozi wa Kanisa, ambao ni wayahudi, walimshauri Paulo kuchukua watu fulani, ndani ya hekalu, ili kujitakasa pamoja na watu hao. Akiwa hekaluni, Wayahudi fulani toka Asia walimuona Paulo, na wakahamasisha watu kinyume chake wakisema;
Enyi wanaume wa Israeli, tusaidieni. Huyu ndiye mtu yule afundishaye watu wote kila mahali kinyume na taifa letu na Torati na mahali hapa. Tena zaidi ya haya, amewaingiza wayunani katika hekalu, akapatia unajisi mahala hapa patakatifu (Matendo 21: 28).
Katika aya inayofuata, ujumbe huu unahusisha ukweli kwamba watu wamemuona Trofimo mu-Efeso akiwa na Paulo huko mjini, na walidhani kwamba Paulo amemleta hekaluni (ingawa rekodi hazionyeshi kwamba yeyote hasa aliliona hili likitendeka).
Wakiitikia yale mashitaka kwamba Paulo amelinajisi hekalu kwa kuleta mataifa ndani, ujumbe ule unasema kwamba, “mji wote ukataharuki, watu wakakutanika mbio mbio, wakamkamata Paulo, wakamkokota, wakamtoa hekaluni, mara milango ikafungwa” (21: 30). Mstari unaofuata unaeleza wazi wazi nini kundi hili lenye fujo, lilipanga kumfanyia Paulo; “Na walipokuwa wakitafuta njia ya kumwua, habari zikamfikia jemadari wa kikosi kwamba Yerusalem imechafuka, mji mzima”. Chini ya sheria ipi kundi hili lilikuwa likifanya haya, pale lilipokusudia kumwua Paulo?
Jibu linalokubalika kwenye swali hili linakuja kwetu toka kwa wachimbuzi. Katika maelezo yake kuhusu hekalu la Yerusalem, Yusufu (Josephus) alielezea kwamba, maandishi fulani yalitenganisha sehemu ya hekalu ambayo mataifa wanaweza kuingia, na sehemu ambayo hawawezi kuingia. Maandishi haya, anasema Yusufu “yalimkataza mgeni yeyote kuingia, hata kwa maumivu ya kufa” (Antiquities, 15: 11: 5). Matokeo yaliyochapishwa mwaka 1871 na ndugu C.S. Clemont – Ganneau yanaleta picha katika muonekano safi. Karibu mita 50 toka mahali hasa pa hekalu, kipande cha jiwe chenye mistari saba ya maandishi ya kigiriki yaligunduliwa (Angalia Thompson, 1962, ukurasa 314). Finegan anatoa huo ujumbe wa kigiriki wote kabisa na ameutafasiri kama ifuatavyo;
Hakuna mgeni anayeruhusiwa kuingia katika uzio na eneo lenye uzio linalozunguka sehemu yote ya hekalu. Atakayekamatwa ajilaumu mwenyewe kwa kifo chake kitakachofuatia (1992, ukurasa 197).
Kwa nyongeza ya maandishi haya (ya kuchoronga), kipande kingine cha jiwe na kikaelezewa mwaka 1938. Kiligunduliwa karibu la lango la kaskazini la Yerusalemu (linajulikana pia kama lango la mtakatifu Stefano), kipande hiki cha nyongeza kilikuwa kifupi kuliko kile cha mwanzo, na kilikuwa na mistari sita badala ya saba. Maneno yaliyotunzwa kwa shemu, yalioana waziwazi na yale ya kwenye kipande cha awali. Finegan aliandika kuhusu maneno hayo yaliyotunzwa; “Kutokana na hayo inaweza kutokea kwamba maneno ya ujumbe ule wote yalifanana (isipokuwa out badala ya eautoo)…” Kama maandishi ya pembeni yanayofurahisha, Finegan alitaja kwamba, herufi za ujumbe wa pili, zilipakwa rangi nyekundu, na kwamba herufi zile bado zilibakia na muonekano wake wa asili (1992, ukurasa 197).
KORBANI
Katika matukio kadhaa, Mafarisayo na viongozi wengine wa kidini, walimwendea Yesu kwa hasira, kwa sababu yeye na wanafunzi wake walikuwa hawafanyi vile mafarisayo walivyodhani wangefanya. Mara nyingi viongozi wa dini, wametunga sheria au tamaduni, ambazo hazimo katika neno la Mungu, lakini hata hivyo lilichukuliwa kama liko sawasawa au hata kwa uzito zaidi ya sheria za Mungu. Katika Marko 7: 1 – 16, Biblia inarekodi kwamba Mafarisayo na viongozi wengine, waliona makosa kwa wanafunzi wa Yesu, kwa sababu wafuasi wa Yesu hawakunawa mikono yao kitamaduni kabla ya kula. Mafarisayo wakamwambia Yesu “Mbona wanafunzi wako hawaendi kwa kuyafuata mapokeo ya wazee, bali hula chakula kwa mikono najisi? (Marko 7: 5).
Kwa kusikia maswali hayo ya kushutumu, Yesu alianza kuwalaani wanaomshutumu. Yesu alifafanua kwamba wanaomuuliza mara kadhaa walitunza tamaduni zao pendwa, huku wakiacha amri za Mungu, ili kuweza kutunza tamaduni zenu (Marko 7: 9). Matokeo yake kwa kukataa kwao sheria ya Mungu, Kristo aliendelea kusema;
Maana Musa alisema, waheshimu baba yako na mama yako, na amtukanaye babaye na mamaye, kufa na afe. Bali ninyi husema, mtu akimwambia babaye au mamaye, Ni Korbani, yaani, wakfu, kitu changu chochote kikupasacho kufaidiwa nacho, huwa basi. Wala hamruhusu baada ya hayo, kumtendea neno babaye au mamaye. Huku mkilitangua neno la Mungu kwa mapokeo yenu mliyopokeana, tena mwafanya mambo mengi yaliyo sawasawa na hayo (Marko 7: 10 – 13).
Katika aya hizi, Yesu aliwakatalia Mafarisayo mifano yao isiyo ya ki-Mungu kuhusu tamadunu zao, na wakati huo huo alijumuisha rejea ambayo inaweza kuthibitishwa (na imeshathibitishwa) na ugunduzi wa wachimbuzi. Yesu alitaja neno Korbani, neno ambalo mwandishi wa simulizi za injili alidhani zinahitaji maelezo kidogo. Marko alilitafasiri kama “zawadi kwa Mungu” katika mjadala wa neno hili katika makala ya Kathleen na Leen Ritmeyer, neno linakuja katika mtazamo mkali. Waliandika kipande cha chombo cha jiwe, kilichogunduliwa karibu na ukuta wa kusini wa Hekalu. Kwenye kipande hicho, neno la kiebrania krbn, (korban – neno lile lile alilotumia Yesu katika Marko 7) limechorongwa (1992, ukurasa 41). Chenye faida zaidi ni ule ukweli kwamba maandishi yale yalijumuisha “ndege wawili waliochorwa kwa ubaya, bila heshima, waliotambuliwa kama njiwa” mwandishi anasema, chombo kile huenda “kilitumika sambamba na sadaka za kuteketeza, kusherehekea kuzaliwa mtoto” (Ritmeyer, 1992, ukurasa 41). Katika Luka 2: 24, tunasoma kuhusu Yusufu na Mariam, wakitoa njiwa wawili, walipompeleka mtoto Yesu, kumleta kwa Mungu. Kwa kuwa hawa ndege ndio walioruhusiwa kwa ajili ya baadhi ya sadaka za Hekaluni, wale waliowauza walijenga maduka ndani ya Hekalu. Kwa sababu ya vitendo visivyofaa vya wengi wa wafanyabiashara hao, waliangukia kwenye mashambulizi ya Yesu, alipolisafisha Hekalu na “akazipindua meza za wabadili fedha na viti vyao wauzao njiwa” (Marko 11: 15).
HITIMISHO.
Tena na tena, rejea za Biblia zinazoweza kukaguliwa, zinathibitisha kuwa ni sahihi kihistoria, katika kila kipengele. Baada ya mamia ya miaka ya uchunguzi mkali, yote, yaani, Agano la Kale na Agano Jipya yamethibitisha ‘uhalisi’ wake na ‘usahihi’ kila mara. Bwana Wiliam Ramsay, katika tathnia yake ya maandiko ya Luka katika Agano Jipya, aliandika;
Unaweza ukakandamiza maneno ya Luka kwa kiwango kilichozidi yale ya wanahistoria wengine, na yanastahimili tathimini kali sana na kushughulikiwa kwa ukali, ikiwa tu mtathimini huyo anajua somo na haendi nje ya mipaka ya sayansi na haki (1915, ukurasa 89).
Leo, karibu miaka mia moja, baada ya kuandikwa kauli hiyo mwanzo kabisa, kitu kile kile kinaweza kusemwa kwa uhakika zaidi wa maandiko ya Luka – na mwandishi mwingine wa Biblia. Karibu miaka 3, 000 iliyopita, mwimba Zaburi wa Israeli, katika kulielezea neno la Mungu, aliliweka vizuri zaidi aliposema “Jumla ya neno lako ni kweli” (Zaburi 119: 160).
REJEA
Adler, Jerry and Anne Underwood (2004), “Search for the Sacred,” Newsweek, 144[9]:37-41, August 30.
Archer, Gleason L. Jr. (1982), Encyclopedia of Bible Difficulties (Grand Rapids, MI: Zondervan).
Blaiklock, E.M. (1984), The Archaeology of the New Testament (Grand Rapids, MI: Zondervan), revised edition.
Bonz, Marianne (1998), “Recovering the Material World of the Early Christians,” [On-line], URL: http://www.pbs.org/wgbh/pages/frontline/shows/religion/maps/arch/re covering.html.
Bruce, F.F. (1990), The Book of Acts (Grand Rapids, MI: Eerdmans), third revised edition.
Butt, Kyle (2002), “James, Son of Joseph, Brother of Jesus,” [On-line], URL: https://www.apologeticspress.org/articles/495.
Eaves, Thomas F. (1980), “The Inspired Word,” Great Doctrines of the Bible, ed. M.H. Tucker (Knoxville, TN: East Tennessee School of Preaching).
Finegan, Jack (1959), Light from the Ancient Past (Princeton, NJ: Princeton University Press), second edition.
Finegan, Jack (1992), The Archeology of the New Testament (Princeton, NJ: Princeton University Press), revised edition.
Finegan, Jack (1998), Handbook of Biblical Chronology (Peabody, MA: Hendrickson).
Free, Joseph P. and Howard F. Vos (1992), Archaeology and Bible History (Grand Rapids, MI: Zondervan).
Hughes, J.J. (1986), “Paulus, Sergius,” International Standard Bible Encyclopedia, ed. Geoffrey W. Bromiley (Grand Rapids, MI: Eerdmans), revised edition.
Josephus, Flavius (1987 edition), Antiquities of the Jews, in The Life and Works of Flavius Josephus, transl. William Whiston (Peabody, MA: Hendrickson).
McClintock, John and James Strong (1968 reprint), “Cyprus,” Cyclopaedia of Biblical, Theological, and Ecclesiastical Literature (Grand Rapids, MI: Baker).
McGarvey, J.W. (no date), New Commentary on Acts of Apostles (Delight, AR: Gospel Light).
McGarvey, J.W. and Philip Y. Pendleton (no date), The Fourfold Gospel (Cincinnati, OH: The Standard Publishing Foundation).
McRay, John (1991), Archaeology and the New Testament (Grand Rapids, MI: Baker).
Nicoll, W. Robertson (no date), The Expositor’s Greek Testament (Grand Rapids, MI: Eerdmans).
“Ossuary” (2001), Archaeological Encyclopedia of the Holy Land, ed. Avraham Negev and Shimon Gibson (New York: Continuum).
Price, Randall (1997), The Stones Cry Out (Eugene, OR: Harvest House).
Ramsay, William M. (1897), St. Paul the Traveller and the Roman Citizen (Grand Rapids, MI: Baker, 1962 reprint).
Ramsay, William M. (1915), The Bearing of Recent Discovery on the Trustworthiness of the New Testament (Grand Rapids, MI: Baker, 1975 reprint).
Ritmeyer, Kathleen and Leen Ritmeyer (1992), “Reconstructing Herod’s Temple Mount in Jerusalem,” Archaeology and the Bible: Archaeology in the World of Herod, Jesus and Paul, ed. Hershel Shanks and Dan P. Cole (Washington, D.C.: Biblical Archaeology Review).
Shanks, Hershel (2004), “The Seventh Sample,” [On-line], URL: http://www.bib-arch.org/bswbbreakingseventh.html.
Thompson, J.A. (1962), The Bible and Archaeology (Grand Rapids, MI: Eerdmans).
Thompson, J.A. (1987), The Bible and Archaeology (Grand Rapids, MI: Eerdmans), third edition.
Unger, Merrill (1962), Archaeology and the New Testament (Grand Rapids, MI: Zondervan).
Wright, G. Ernest (1960), Biblical Archaeology (Philadelphia, PA: Westminster).
Imechapishwa tarehe 03 Oktoba 2004.
MASHARTI YA KUNAKILI; Tunayo furaha kutoa ruhusa kwa makala hii kunakiliwa, iwe ni kwa sehemu tu, au hata yote kabisa, ilimradi tu, vigezo na masharti vizingatiwe.
REPRODUCTION & DISCLAIMERS: We are happy to grant permission for this article to be reproduced in part or in its entirety, as long as our stipulations are observed.